Nyie mlioolewa muwe na msimamo na ndoa zenu mtakuja kusabisha mauaji hivi hivi

Redpanther

JF-Expert Member
Feb 23, 2019
2,813
3,766
Habari gani wanajamvi.

Ngoja niende moja kwa moja kwenye mada, leo mida ya saa 10 jioni nikiwa maeneo fulani nimetulia napunga upepo akawa amepita mdada na mkaka wametangulizana basi mie nikawa nimevunga kama sijaona nikaendelea na mambo yangu wakapita.

Baadae tena sijui nini hii, nimekuja maeneo ya home kitaa kwangu dukani kwa Mangi nimesimama nasubiri huduma mara paap mtoto huyu hapa, nikamcheki naye akawa kama ananiangalia nikageuza uelekeo wa macho yangu na kuelekeza dukani huku moyo unanidunda kwa haraka haraka nikahisi kama nimekosea kumtizama cha kushangaza demu si akanisalimia Mambo .. nikamjibu poa basi namimi nikaona isiwe shida nikamuuliza vipi yule broo ulikuwa naye mnatembea wote barabarani mnatembea ndo shemeji nini au Kaka ? Akasema shemeji yako basi nikakohoa ile kichokozi.

Basi nikamwambia hongera, demu akaniuliza kwani vipi alfu kitu kama anataka sijui nimuombe namba ila roho inaniambia “Acha ujinga we mbwa utakufaa”.! Manzi akawa kama anasubiri nimwambie naomba namba yaani dizaini fulani ana Subiri nimwambie nipe namba yake maana akawa anaregeza jicho

Mie nikawa nataka kumwambia nipe namba yako si jamaa aliyekuwa naye akafika akamwambia “Mbona humalizi tu twende bhana “ kwa sauti fulani ya ukali. Sasa nikauliza kwa mangi kuhusu huyo demu mangi akaniambia Bwashee huyo ni mke wa mtu ila sema tu huyo demu anaonekana “Cha wote “

Sasa hapo huyo mwanamke si kidogo aniingize kwenye bifu na mwana kama jamaa lingenikuta naoewa namba
 
😆😆😆😆😆 wataalamu wa saikolojia utawajua tu!!! Yan ukimsalimia tu anajua shida yako ni nini.😄😄😄😄😄😄😄😄
 
Mahusiano yenyewe ya siku hizi mnaishi kwa wasiwasi kama mnachemsha maziwa.

Yaani kama ubalozi wa marekani huruhusiwi kupiga picha
 
Back
Top Bottom