Nyie baby daddies mnatutesa sana hamjui tu. Mwenzenu niko njia panda sielewi

Status
Not open for further replies.
Haikua bahati mbaya tulipanga kupata mtoto but ikatokea tu hataki tena na akataka nitoe kitendo cha kukataa kutoa hapo ndo imekua vita adi leo
Wewe unakubali vipi kuzaa na mwanaume ambaye hata hajulikani kwenu wala hajajitambulisha......?!

Ni vipi ikaja kutokea mwanaume unae pata nae mtoto kumbe anatoka kimahusiano na ndugu yako mwingine na wameshazaa wakashindwana.....

Watoto wa kike sijui akili gani mnatumia now days.....
 
Wewe msichana washukuru hata wazazi wako kwa kukupokea na mtoto wako. Hakuna kitu kinachomuuma mzazi; kama ambavyo mzazi anajinyimakwa ajili ya mtoto wake kusoma, only kwa huyo mtoto kurudi na degree zake mbili. Afu kama haitoshi muhusika wa degree ameingia mitini, automatically unawaongezea majukumu mengine wazazi wako. Narudia tena washukuru sana, hayo manyanyaso madogo madogo sio kwa sababu hawakupendi wewe na mtoto wako nope; ni uchungu tu kwamba wewe huwaonei huruma unawaongezea majukumu kwa sababu ya starehe zako.

Huo uhuru wa wewe kutoka na kuingia nyumbani kwenu kadri unavyojisikia wewe, unautaka wa kazi gani? Wanakunyima kutoka kufanya mambo yako ya msingi au una hamu ya kwenda kutafuta mtoto mwingine huko? Tulia nyumbani wewe, uhuru ukizidi kwa mtoto wa kike una gharama kubwa sana.

Huyo mume wa mtu achana naye, huyo baby daddy wako achana naye pia; focus yako iwe mtoto wako na kutafuta kazi. Kazi peke yake ndiyo itakufanya utoke hapo nyumbani, ukapambane huko nje kwa ajili ya mwanao. Huyo mtoto wa kwanza umemzaa bila utaratibu, sasa kurupuka ulete mimba ya 2 kwa wazazi wako. Hayo maumivu em nenda hospital nako.

Afu huyo baby daddy wako bado unamtaka au? Yaani leo hii uolewe eti aje akunyang'anye mtoto; anaanzia wapi kwanza, na hizo nguvu anazitolea wapi? Sasa wewe ukipata mwanaume serious usiolewe naye, endelea kuogopa fujo za baba mtoto ambaye hata kwenu hatambuliki

Jamani hawa watoto tuwazae kwa utaratibu, tunawatesa sana. Itokee tu sababu ya msingi ya mtoto kulelewa na mzazi moja, sio kwa sababu ya tamaa na upumbavu wetu. Imagine mtoto akiita tu baba anavyoshambuliwa, bado hajapata akili akaanza kuona wenzie na baba zao afu yeye baba mwenyewe hata kujitambulisha hataki. God forbid hapo umedondoka ghafla, after years mtoto anaanza kujitokeza kwenye mitandao "namtafuta baba yangu, niliambiwaga anaitwa fulani". Sio sawa
Well said darling
 
Kwanza pole sana.Pili hongera kwa kukuza mtoto hadi hapo ingawa ulikuwa unasoma.

**Mwambie mzazi mwenzio amkatie bima ya afya mtoto.

**Nenda kwa wazazi wake au muajiri wake (kama kaajiriwa)aweke kimaandishi kuwa kila mwisho wa mwezi shilingi ngapi atakupa ya mtoto.

**Jishushe kwa ba mtoto mpigie panapokuwa na ulazima.

**Tafuta yaya wa mtoto katafute pesa.

**Jiheshimu mtaani wasikuone umeshindikana.

**Shiriki kwenye shughuli za kijamii misiba,sherehe na jichanganye uonekane.

Jitunze. Utaolewa tu.
 
Kwanza nikupongeze kwa kuwa mama na pili nikwambie tu kuwa Huwa nina washangaa sana wanawake wanaojiona Single Mother's,hivi mbona hiyo ni bahati mimi naona? usiuchukie u single Mother,utaona faida yake ukipambana mwanao akaja akawa na maisha yake "uta enjoy sana" hakuna raha kama kula mkate wa slace 24 peke yako..(sijui kama unanielewa)

Turudi kwenye mada sasa,nisikie bibie pole kwa misukosuko unayopitia hapo home ni misukosuko hiyo hiyo ilinifanya nikaondoka nyumbani kwetu miaka hiyo bila kuaga mtu (nilichoka asee) kwahyo naelewa sana unapta ktk kipindi gani.

chakufanya mimi siwezi kukushauri eti sjui vumili,hao n wazazi,sijui uliwaumiza,nk nk mimi ni mmoja ya wale wanao amini "Hata wazazi wanakosea" wao si malaika,kwahiyo solution ya wewe kutulia na kuepuka hyo misuko suko ya home ni wewe kuondoka.

Unaondokaje?! (Akili kichwani mwako) Huyo baba anaejipendekeza kwako,hilo jitu zima La saba failure namuita la saba failure kwasababu mtu mzima mwenye akili huwezi muonyesha mwanamke unaempenda kwa dhati Ka nyumba na kagari eti ili akukubalie,shenzi kbsa (jitu zima hovyo hilo) sasa kwasababu na wewe humpendi ni vzuri "umenifurahisha" hapo.

Njia ya kutoka ni lazima awe huyo kenge maji,kwasasa sijui kama una kamchepuko zaidi ya hilo small dadie,sio ukubali enda olewa kwasasa sahau maswala za Kuolewa "futa kabisa huko kichwani" sahau maswala ya kuishi na mwanaume "futa kabisa huko kichwani" ila mtumie huyo dingi kupata Pesa ya kuondokea hapo home.

Mwambie kama kweli anakupenda akupe hela ufungue biashara,uweze jisimamia mwenyewe,mwambie haupo tyr akuoe ukawe goli kipa,mwambie kuna leo na kesho akifa nani atasimamia familia? mwambie kama kweli ana upendo wa dhati kwako,akupe mkwanja ufungue biashara yako mwenyewe.

Then' ukipewa pesa Hama hapo Home,tena swala la kuhama hapo home mshirikishe huyo mzee mwambie unataka kwenda kupanga ila ndio akupe pesa ukapange (usije fanya makosa ya kuruhusu ajue unapoenda kupanga) wewe kazi yako iwe n kumpgia picha ya chumba ukipata,picha za godoro ulilonunua kwa pesa yake,nk nk yani info zote zimfikie kupitia picha.

Usiende kupanga kama hajakupa hela ya biashara,kwahyo hela ya biashara kwanza kisha kodi baadae...Ukifanikisha yote hayo akayafanya kwako nadhani swala la kuhama home utakua umelimaliza na biashara utakua nayo,hapo umepga ndege wawili kwa jiwe 1.

Kuhusu maumivu ya tumbo,usidanganywe sijui kuzaa sijui mafyoko fyoko gani Tumia dawa hizo hizo kunywa dawa ya kila mzizi wa mmea ulioota juu ya ardhi yani,usidanganyike eti na wanaosema uzae,ni Uongoooooo hiyo ya kuzaa si ya kila mtu Unaweza ukazaaa na maumivu yakawepo au yakaondoka ni betting unafanya.

sasa yanini ubetie maisha yako,meza mizizi hadi ya muwashawasha ikibidi ilimradi hayo maumivu yatoke..Ona future yako na zaidi Ona future ya mwanao usiongeze mzigo mwingine wakati ulionao tu unakutoa jasho.

Mwisho nikwambie tu kitu kimoja Tafuta sehemu mtoto wako atapata upendo wa kila anaemzunguka na kama hakuna n bora uishi nae mwenyewe,mpende na mthamini mwanao Teseka sasa kwa ajili yake kama iliandikwa uteseke kwa ajili ya huyo mtoto Kubali mama sio dhambi,Usichezee tena future yako na zaidi usije hta siku 1 ukamuona huyo mtoto ni mzigoo N bahati na ana sababu kwann wewe n mama yake.

Mimi n mzee wa kuandika,pole kwa kusoma risala langu n refu ila lahitaji roho ngumu kulitekeleza,na kweli uwe umedhamiria.
Mkuu mawili..... Ulilelewa na mama pekee yake au unaishi na baba mpole na mama mtata......

You sound so Beta in between the lines.
 
Ushauri wangu anza kupata kwanza pa kuanzia. Fanya juhudi uwe na cha kufanya,iwe biashara au kazi yoyote kwa uchache, isiyopungua laki 150 kwa mwezi. Mbananishe huyo njemba iwe kwa kumbembeleza au njia yoyote,akupe mtaji,wa biashara utakayofikiria. Kisha fuata ondoka nyumbani kapange. Usifikirie kuoelewa tena itokee tu kwa bahati,na huyo mtu lazima uwe umemchunguza sana. Shida mnayopitia nyie wadada wa siku hizi ni wengi kufikiria maisha yenu yote lazima uolewe. Waoaji siku hizi hawapo. Lazima mjiandae kwa hilo. Huyo mbaba anaekumendea ksbb humpendi achana nae tu. Ukipata tu cha kufanya hasa biashara hiyo itakuwa njia ya kutoka home. Nazijua madhira unayopitia. Kuna familia nyingi hizi za kimasikini binti akizalia nyumbani anapata tabu sana. Njia ni kufanya biashara itakayokufanya uwe na kipato cha kukutosha ukichanganya na sapot ya mzazi mwenzio,mbele itajulikanaga,kwa sasa anzia hapo kwanza.
Sasa wewe badala ya kumshauri vema mwenzako unaanza kumfundisha kukurupuka kama pofu aliekurupushwa na simba....

Nani amekudanganya kuwa wanaume waowaji hawapo?! Kama hiyo ni kweli hivi umefuatilia idadi ya ndoa zinazosajiriwa makanisani na misikitini. Je umetazama bookings za kumbi za starehe.....

Jibu ni moja na very simple. Wambili havai moja..... Wewe sio marriage material so usidhanie kila mtu yupo kama wewe....

Secondly, naomba nikwambie, kwenye mahusiano kuna zaidi ya kutafuta maisha. Kama wewe unahisi kuwa na biashara, kipato na sehemu ya kuishi basi maisha umeyapatia then kafanye tafiti tena.....

Kila mtu anahitaji mwenzake wa kumuamini na wa kuwa nae kila siku na kila mahala atakapohitaji uwepo wake.

Wewe unampotosha mwenzako kama as if maisha ni vita.... Sasa unaishi ili iweje kama una mtazamo hasi kiasi hiki?!
 
Haikua bahati mbaya tulipanga kupata mtoto but ikatokea tu hataki tena na akataka nitoe kitendo cha kukataa kutoa hapo ndo imekua vita adi leo
Hakuwa na time na wewe alikuwa anataka kupita tu so ikabidi akuongopee na wewe ukajaa mazima Matokeo yake ndio hayo
 
Sijasoma yote ila nimejitahidi kusoma mpaka pale ulipoanza kumfundisha utapeli huyu dada nikaanza kukosa interest za kumalizia kusoma na kweli nikaamua kuacha. Hivi unajua ni maumivu kiasi gani atamsababishia huyo mwanaume kama atachukua ushauri wako? Ulishawahi kuliwa hela na mwanamke unayempenda na yeye alikuaminisha anakupenda? Yeye kama ataweza kutoboa bila kufanya utapeli wa kimapenzi hapo sawa ila asithubutu kuwatumia wanaume kama daraja kufika anakotaka, yatamtokea puani. Ushauri kama baba wa mwanae hajaoa afanye kila awezalo arudiane naye. Tatizo huyu demu anaonekana jeuri, kwa maelezo yake anaonekana ni pasua kichwa. Mwanamke anayeweza kuchambana na mwanaume huyo ni kichwa maji. Huyu demu ni wale wanaojifanya wanayaweza maisha bila usaidizi wa wazazi wenzao hivyo huwa wajeuri balaa, huwa hawataki kujishusha, hawaambiliki anaweza hata kukublock mkikwaruzana.
Upo sahihi kabisa.
 
maisha hayana formula...
kuna wanaume wanawapenda wanawake wenye mimba,
wengine wanawapenda wenye watoto,
wengine wanawapenda wasiozaa kabisa,
wengine wanawapenda wanawake bikra,
wengine wanawapenda wanawake malaya,
nk
nk
nk
Wengine wanawapenda wanawake wajane........ndivyo maisha yalivyo mkuu
 
Mbona mpendwa unachapia Sana au chuo gani rishe?kuludi?najua r na l huwasumbua wengu but kwako kwa kurudia Mara nyingi inaonyesha Kuna something serious going on
 
Pole sana kwa changamoto na hongera kwa kuwa mama.

Sasa baby daddy aje kwenu kujitambulishaje wakati hamna hata mahusiano? Kwamba "wazazi mimi ndio nimezaa na binti yenu"? Kama hakuja enzi hizo asije wala usimuombe aje.

Huyo dingi anataka tu kukunjunja, na kishaona una shida zako basi anakutongoza kipare kukuonesha picha ya gari, mpotezee.

Hauna mpango wa kutafutana kazi? Kujikwamua kwa namna yeyote?
 
Pole sana kwa changamoto na hongera kwa kuwa mama.

Sasa baby daddy aje kwenu kujitambulishaje wakati hamna hata mahusiano? Kwamba "wazazi mimi ndio nimezaa na binti yenu"? Kama hakuja enzi hizo asije wala usimuombe aje.

Huyo dingi anataka tu kukunjunja, na kishaona una shida zako basi anakutongoza kipare kukuonesha picha ya gari, mpotezee.

Hauna mpango wa kutafutana kazi? Kujikwamua kwa namna yeyote?
Ninayo biashara ninacho kiwanja ila tu kwa sababu nimezaa na mtoto hana baba wanaona siwezi jisimamia na naogopa kuondoka kwa shari wao ndio ndugu zangu kwa shida na raha naweza leta kiburi yakinshinda ntaludi wapi?
 
Ninayo biashara ninacho kiwanja ila tu kwa sababu nimezaa na mtoto hana baba wanaona siwezi jisimamia na naogopa kuondoka kwa shari wao ndio ndugu zangu kwa shida na raha naweza leta kiburi yakinshinda ntaludi wapi?
Mtoto hana baba umemzaaje, ana baba ila baba yake hamna uhusiano.

Mbona unajichukulia negative sanaaa, unajitesa bure tu.
 
Sasa wewe badala ya kumshauri vema mwenzako unaanza kumfundisha kukurupuka kama pofu aliekurupushwa na simba....

Nani amekudanganya kuwa wanaume waowaji hawapo?! Kama hiyo ni kweli hivi umefuatilia idadi ya ndoa zinazosajiriwa makanisani na misikitini. Je umetazama bookings za kumbi za starehe.....

Jibu ni moja na very simple. Wambili havai moja..... Wewe sio marriage material so usidhanie kila mtu yupo kama wewe....

Secondly, naomba nikwambie, kwenye mahusiano kuna zaidi ya kutafuta maisha. Kama wewe unahisi kuwa na biashara, kipato na sehemu ya kuishi basi maisha umeyapatia then kafanye tafiti tena.....

Kila mtu anahitaji mwenzake wa kumuamini na wa kuwa nae kila siku na kila mahala atakapohitaji uwepo wake.

Wewe unampotosha mwenzako kama as if maisha ni vita.... Sasa unaishi ili iweje kama una mtazamo hasi kiasi hiki?!
Wewe mjibu huyo mtoa mada,usinifokee mimi.

Yeye ndie atachambua hoja gani nzuri za kufuatwa,sio kukanusha kilicholetwa na wengine.

Kwani wewe nani amekuchagua kuwa unajua kuliko wengine? Kiasi kwamba hoja zako ndio sahihi?. Ukimjibu mleta tred utakuwa umefanya la maana,yeye ndio ataamua kufuatana na stuation za aliko.
Hakuna mahala nimekuambia maisha ni ugomvi au akagombane na mtu. Nilichomaanisha,sawa ataingia kwenye mahusiano lakini yenye tija,yeye akiwa huru sio kama mnavyowaonea wanawake ksbb ya utofauti wa kipato.
Tatu nimekuambia waoaji hawapo,hiyo huwa nawafundisha mabinti zangu pia. Sababu ni kwamba wanawake wengi wanajisikia ovyo sana akifikisha miaka 30 hajaolewa. Na ni kweli kwa kipindi hiki,wengi hawajaolewa,wapo nyumbani tu. Sasa kama mupo waoaji kwa nini wasichana ni wengi sana hawajaolewa,tofauti na ilivyo kuwa zamani?.
Kwa hiyo kumfundisha hivyo kuwa waoaji hawapo ila ikitokea hivyo ni bahati,kuna maana kwamba yeye mwenyewe binti awe strong kwanza yeye mwenyewe sio lazima kumsubiria mwanaume tu,si lazima kusubiri tu kuolewa bila kufanya juhudi zozote za yeye kujikwamua kimaisha.
Ndio hivyo wengi wanaosubiri kuolewa wengi wanaishia kuzalishwa nyumbani,na wengi wakizalishwa nyumbani wanaishia kugombana tu na wazazi wao.
Lakini je unafikiri akijimudu kwanza kimaisha,hata akizalishwa nyumbani unafikiri kutakuwa na shida sana kwa wazazi wake?. Ksbb anamudu kila kitu pale home.
Wewe ndie unataka kumdanganya asubiri tu mahusiano yasiyo na maana yoyote. Ndio maana mpaka sasa aliemzalisha anampelekesha tu anavyotaka. Sababu kuu huyo binti hana uwezo anasubiri kuolewa na kunyanyaswa kihisia,kama unavyomshauri
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom