Nyie Amkeni, uchumi wa Kati: TZ inatengeneza Magari!

Hivi tunashindwa nini kuanzisha foundry, kiwanda cha kukunjia mabati, rim na matairi? Cha waya East african cables dhumuni lake lilikuwa kuunda nyaya za aina zote zikiwemo za magari! Sielewi tunafeli wapi!

Kwa teknolojia ilipofikia kutengeneza gari ni kama keki tu! Sijui tunakwama wapi
 
Hapa sio kutoa kejeli kwa ugunduzi uliofanyika busara kuhoji system nzima ya hili gari ina Advantage ipi kutokana na technology ya magari sasa bongo, just thinking mfumo mzima unaweza kua wa umeme hii ni big achievement kuendeleza hii innovation.
 
Uchumi wa viwanda, TZ tunatengeneza magari

View attachment 1793036
Hapo ni chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT) na hao ni wanafunzi wa mechanical engineering wanafany project ili waweze kugraduate lkin ndio hivyo pesa hawana mana hapo serikali inaweza ikakupa laki moja ya kufanyia project au usipewe kabisa na hizo project zinahitaji pesa ili ufanye kitu cha uhakika mana kutengeneza kifaa chochote cha ubunifu kitaalamu na kwa ufanisi huwa kuna changamoto nyingi sana so inakula sana pesa na muda. Mtu unajikuta una ideas nyingi lakin resources na funds za kufankisha hilo ndio mtihani kwahy hapo kinachobakia ni kuokotezaokoteza mabati ili tu umalize project.Hao wananikumbusha kipindi na mimi nafanya project yangu aisee project ilinimalizia pesa zangu zote mpaka ikawa sasa nashinda njaa najibana ili nipate pesa nikanunue vifaaa yani mpaka project naimliza nilikonda hatar kwa sulubu niliyopitia,sasa kwa staili hiyo usitegemee mtu aunde project ya kibabe ni ngumu sana
 
Uchumi wa viwanda, TZ tunatengeneza magari

View attachment 1793036
This is stupidity of highest level. Kweli kabisa unadhani na wao wanaona hicho no kitu kabisa???

COSTECH inafanya kazi gani? Hawa wangeongezewa pesa ya study yao wangecome up with a better version. Ukimwambia mtaalamu kwamba hiyo ndio pilot version dah 😃

I appreciate the efforts Ila workdone=0 sorry
 
Hilo gari au wameunganisha siso.
mkuu hiyo ni project ya chuo ambayo kila mwanafunzi wa uhandisi huwezi maliza chuo mpk ufanye project kwahiyo hapo hawajaungaunga tu, hapo kuna mahesabu mengi tu yamefanyika mana kila hatua unayoifikia lazima uende ukapresent mbele ya jopo la malectures wa chuo na hapo utafanya presentation ya project yako kitaalamu pia utaulizwa maswali ya kitaalamu na inabid ujibu kwa ufanisi ndio project yako ipitishwe ,so hapo calculations nyingi zinazohusiana na design ya gari zimefanyika hapo calculations kama za aerodynamics, vehicle dynamics,vehicle stability ,strength of materials etc zote wamefanya sema tatizo ni kwamba pesa hawana ndio mana hilo gari linaonekana la kuungaunga, Sisi wenyewe tumetokea hukohuko kwahiyo tanaelewa sana hayo mambo na najua msoto wanaoupitia hapo kwa sasa,polen sana vijana
 
Hivi tunashindwa nini kuanzisha foundry, kiwanda cha kukunjia mabati, rim na matairi? Cha waya East african cables dhumuni lake lilikuwa kuunda nyaya za aina zote zikiwemo za magari! Sielewi tunafeli wapi!

Kwa teknolojia ilipofikia kutengeneza gari ni kama keki tu! Sijui tunakwama wapi
Wazo zuri, lakini waulize wamiliki wa viwanda vya bidhaa mbalimbali gharama za uzalishaji bongo ziko juu sana.

Tumekwama kwenye mambo mengi ikiwemo policies na necessities kama umeme.
 
Hivi tunashindwa nini kuanzisha foundry, kiwanda cha kukunjia mabati, rim na matairi? Cha waya East african cables dhumuni lake lilikuwa kuunda nyaya za aina zote zikiwemo za magari! Sielewi tunafeli wapi!

Kwa teknolojia ilipofikia kutengeneza gari ni kama keki tu! Sijui tunakwama wapi
Viongozi wanawaza kupiga tu. Hivi hii serikali Ina mpango wowote angalau in the next twenty years? Bunge la Sabufa nduguyai haliwazi hii nchi itakuwa wapi 2041. Mle ndani Ni kudemka, kumsema Mbowe na upinzani wa Simba na watoto wa mjini Dar es Salaam Young Africans.
 
Back
Top Bottom