Elections 2010 Nyerere

mdaumie

Member
May 12, 2008
77
1
wana JF mnaonaje mimi nikimtuhumu nyerere hafai kuitwa BABA wa Taifa .

Maana yeye hakuunga mkono wapinzani na suala la kuunda Katiba mpya
 
wana JF mnaonaje mimi nikimtuhumu nyerere hafai kuitwa BABA wa Taifa .

Maana yeye hakuunga mkono wapinzani na suala la kuunda Katiba mpya
Be visionary...!
Tunasonga mbele sio kuangalia kunako nyuma!
Usitupotezee broda!
Tunajadili Kauli ya Dr Slaa KESHO!
 
Utakuwa Umedata, yeye ndiye alikubali ujio wa vyama vingi licha ya watanzania wengi kupinga
 
wana jf mnaonaje mimi nikimtuhumu nyerere hafai kuitwa baba wa taifa .

Maana yeye hakuunga mkono wapinzani na suala la kuunda katiba mpya

review historia vizuri kabla ya kuhamaki kutoa maamuzi. Hicho kilikuwa kichwa a.k.a mtambo mkubwa
he deserves to be a father of the nation.i respect that man
 
Kumtuhumu Nyerere itakuwa Makosa kutokana na alama za nyakati za wakati ule.
Nyerer alikuwa anakazi ya kukuza demokrasia ndani ya mfumo wa chama kimoja kwanza (mono party system),
Ni Nyerer huyu ndiye aliyekubali kuanzishwa kwa multi-party democracy in 1992.

Hivyo kazi yake ilikuwa nzuri kwa wakati wake.
 
wana JF mnaonaje mimi nikimtuhumu nyerere hafai kuitwa BABA wa Taifa .

Maana yeye hakuunga mkono wapinzani na suala la kuunda Katiba mpya
Angalia wewe utakamatwa muda si mrefu, kashifu wote lakini siyo BABA WA TAIFA yeye ndo aliyeleta vyama vingi hapa nchini.
 
Ni mtazamo tu, hujui ni kwanini anaitwa baba wa taifa? Best unataka vita tu na sisi wabongo, sasa asiitwe baba wa taifa na hiki cheo tumpe nani, Kikwete?
 
utakuwa hujafikiria sn!naomba usome hii meseji ya mwalimu:

Ingawa alikuwa mwanzilishi wa CCM, kwa nia njema ya kuendeleza mapinduzi katika nchi yetu, miaka ilivyozidi kwenda Mwalimu Nyerere alishuhudia jinsi CCM ilivyobadilika na kuwa mzigo kwake na pia tishio kwa usalama wa Taifa.

Mwaka 1993 Mwalimu alichapisha kitabu kiitwacho Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (Harare: Zimbabwe Publishing House, 1993). Pamoja na mambo mengine katika kitabu hiki, Mwalimu alisema kuwa kuna kansa katika uongozi wa CCM. Nanukuu baadhi ya maneno yake:

Chama cha Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake, hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake, mazoea ya watu, na ubovu wa Vyama vya Upinzani, kinaweza kuchaguliwa na Watanzania, pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu wanaweza wakachoka, wakasema, "potelea mbali:" wakachagua Chama cho chote, ilimradi tu watokane na kansa ya uongozi wa CCM. Hainifurahishi kuyasema haya, lakini uhai wa Nchi yetu unataka yasemwe. (Ukurasa 61)

Mwalimu hakuishia hapo, bali aliongezea namna hii:

Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona Chama kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa Vyama Vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata Chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM; au ambacho kingekilazimisha Chama cha Mapinduzi kusafisha uongozi wake, kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao. Lakini bado sijakiona Chama makini cha upinzani; na wala dalili zo zote za kuondoa kansa ya uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama cha Mapinduzi, Chama hiki kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini hili si jambo la kutarajia bila hofu na wasi wasi! (Ukurasa 66)

Ni wa-Tanzania wangapi wenye utamaduni wa kusoma vitabu? Ni wangapi wanaosoma vitabu vya Mwalimu Nyerere?
(SOURCE:hapakwetu.blogspot.com)
 
Nanukuu baadhi ya maneno yake:

Chama cha Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake, hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake, mazoea ya watu, na ubovu wa Vyama vya Upinzani, kinaweza kuchaguliwa na Watanzania, pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu wanaweza wakachoka, wakasema, "potelea mbali:" wakachagua Chama cho chote, ilimradi tu watokane na kansa ya uongozi wa CCM. Hainifurahishi kuyasema haya, lakini uhai wa Nchi yetu unataka yasemwe. (Ukurasa 61)

Mwalimu hakuishia hapo, bali aliongezea namna hii:

Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona Chama kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa Vyama Vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata Chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM; au ambacho kingekilazimisha Chama cha Mapinduzi kusafisha uongozi wake, kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao. Lakini bado sijakiona Chama makini cha upinzani; na wala dalili zo zote za kuondoa kansa ya uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama cha Mapinduzi, Chama hiki kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini hili si jambo la kutarajia bila hofu na wasi wasi! (Ukurasa 66)

Wakati umefika wa CCM kuona kwamba maneno ya JK Nyere yanaelekea kutimia maana kansa ya CCM imekuwa so malignant and metastatic kiasi kwamba viungo vyote vya mwili vimeathirika. Kupoteza nafasi nyingi kwa wabunge na mawaziri wa CCM ni dalili tosha kwamba watanzania sasa wanaweza kuwa na chama kizuri cha kuiondoa CCMM madarakani ifilie mbali na kansa yake.

Wana CCM kazi kwenu na watanzania kazi kwetu!
 
wana JF mnaonaje mimi nikimtuhumu nyerere hafai kuitwa BABA wa Taifa .

Maana yeye hakuunga mkono wapinzani na suala la kuunda Katiba mpya[/QUOT

80% ya watanzania walisema wanataka mfumo wa chama kimoja na 20% walisema wanataka mfumo wa vyama vingi. Yule mzee kwa uwezo wa akili aliokua nao akaona hawa 20% ndo wananchi wangu walioelimika kwa wakati huo akaamua kuruhusu mfumo wa vyama vingi. Hawa waliobaki ndo hamna kitu kabisa
 
Sipendi mijadala inayomhusu Mwalimu, iwe iwavyo kama Mwanadamu yeyote anayo mazuri yake Basi ni vema tukayachukua hayo pia yale yalio kinyume yapo, kwa kuwa ametangulia mbele za haki ni vema kusamehe na kusahau. Na siku zote WANADAMU huhesabu mabaya na kuyasahau MEMA. KWA KWELI ALIIFANYIA KAZI NCHI HII. NA ANAKUMBUKWA KWA HILO> FUUUULSTOP>
 
Back
Top Bottom