Nyerere: Watanzania wasipoyapata mabadiliko ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM

ACHEBE

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
348
76


"WATANZANIA HAWA WANATAKA MABADILIKO, WASIPOYAPATA CCM WATAYATAFUTA NJE YA CCM" JK. NYERERE....."LAZIMA CCM TUWAPE WATANZANIA MABADILIKO WAYATAKAYO ILI TUENDELEE KUONGOZA" Nnauye (mtoto wa kuli).

NIMEKUTA KWENYE WALL YA NAPE YA FB, ANAYAAMINI HAYA?
 
Last edited by a moderator:
Hayo maneno kweli ni ya Mwl. Nyerere bt kitendo cha kuyakuta ktk wall ya Nape nadhan kaamua kupendezesha Facebook wall yake bt kiukwel sidhani km anayaamin hayo. Nape ajivue gamba, ajibu tuhuma zake zote au akiri yasemwayo tumwamini. USHAURI WANGU: NAPE TOA HIYO QUOTE, UNAMDHALILISHA MWL. Nyerere!
 
Mnafki huyo! na ikumbukwe tayari too late to catch the train na anajua ...mwl. Nyerere aliwambia watz wakikosa uongozi bora ccm watautafta nje ya ccm na watz wengi washaanza kuutafuta nje ya ccm na kurudi nyuma hapana, sababu ni moja tu haya mabadiliko wanayosema CCM hayana lengo la kutusaidia sisi watanzania bali yana lengo la wao kuendelea kututawala na kuendeleza umangi meza wao, kulindana na kujilimbikizia mali, tumeshawastukia hatudanganyiki tena! Washatudanganya sana kwa muda mrefu
 
Mwalimu Nyerere aliyasema haya alipokuwa akihutubia kwenye mkutano mkuu wa CCM mwaka 1995.
Alisema kuwa lazima mgombea yeyote wa urais awe ni yule ambaye atakuwa anakidhi matarajio ya Watanzania na si anayekidhi matarajio ya wachache wenye fedha zao.

Awe ni mtu anayechukia rushwa toka rohoni mwake.

Mtu anayeweza kuitoa Tanzania kutoka hapa ilipo kiuchumi na kuipeleka hatua mbele zaidi kiuchumi.

Anayetambua kuwa Tanzania ni maskini na kuwa nchi hii bado ni nchi ya wakulima na wafanyakazi.

Asiye kuwa mdini na mkabila.

Bila shaka kwa miaka hii hakuna kiongozi ndani ya CCM mwenye sifa hizi alizoziainisha Mwalimu Nyerere. Mi naona viongozi pekee waliobaki na sifa hizi alizozitaja Mwalimu wapo ndani ya CHADEMA pekee.

Na ukweli unabaki kuwa kwa kuwa viongozi wa CCM wameshindwa kutimiza yale yote aliyowaasa mwalimu basi yatupasa kuyatafuta mabadiliko hayo ndani ya CHADEMA mwaka 2015.

 
Last edited by a moderator:
Alyewakaa Nyerere wakati wa uhai wake ndo wameshika Tanzania.
Awe mtu anayechukia Rushwa kutoka Moyoni mwake. Hii inawashinda wengi sana ndani ya CCM.
 
Bravoooo!!!!
Nakupongeza kwa nukuu nzuri ya baba wa taifa na kuileta wakati muafaka.
Tatizo wenzetu wamesha kata fuse zote hakuna kinacho ingia wala kutoka kichwani, akili yao yote iko kusaka urais kusudi watengeneze mitandao yao ya kifisadi kama dhaifu anavyofanya. Cdm kaza kamba ukombozi wa nchi yetu uko mikononi mwenu!!!
 
CCM lazima mtambue wananchi wanataka mabadilko ambayo yameshindwa kupatikana ndani ya ccm kwa hiyo ni muda muafaka wa kuyatafuta nje ya ccm lazima mkubali ukweli nchi hii mmeifanya kama shamba la bibi kila mtu anafanya anavyotaka yeye kama maswala ya rushwa imekuwa ndo sera ya chama tawala sekta zote ni rushwa mpaka hospitali mgonjwa anaweza kufa kwa kukosa panadol kwa sababu ya madaktari kutaka rushwa kama huna basi maisha yako yanakuwa hatari.

Hakuna sekta ambayo inaendeshwa bila rushwa uozo kila mahali bado CCM mna ndoto za kuendelea kutawala tena mnapoteza muda wenu miaka 50 ya uwongo na dhuluma imeisha wananchi wameshaelimika kwa sasa wanajua pumba na mchele siyo wale wa kuwadaa ni kanga au kofia tena bado mnaendelea kuchezea pesa zetu kwenye bunge la katiba wakati uwezekano wa kupata katiba mpya hamna inatia uchungu sana

Vijana wenzetu muda wa kuogopa umeisha tujiandae kwa maandamo ya nchi nzima kupinga unajisi unaoendelea kule bungeni kwa pamoja tutafanikiwa kuwaondoa hawa wahuni wa CCM kule bungeni. UKAWA ni sumu ya kuuwa ccm na vibaraka wake wote

View attachment 185811
 
Mkuuu hata me nakuunga mkono sana!Zaidi hua nakumbuka sana maneno ya P.Kagame aliposema kama angepata nafasi ndogo tu ya kuisimamia bandari ya Dar angeweza kuifanya Tz kama ulaya. Najiuliza ameitamani bandari tu, je, tunazo rasirilimali ngapi ndani ya nchi hii?Kwanin watu wachache waifanye nchi yetu kama shamba la bibi? Ni nani anayeujua uchungu wa kukatwa kodi kwenye mshahara wake kila mwezi huku deni la taifa linakua kila siku? Kwa mtu mwenye kuguswa na hili anaweza hata kutamani hata asiishi Tz.
 
Hii speech ya mwalimu kwa nini haiwekwi ili wananchi wamsikilize vizuri mwalimu hasa kipindi hiki cha muungano wa vyama 4 vya siasa? Naomba kujua kwa nini hii speech TBCCCM na na ITV YETU YA TAIFA hawatuoneshi!
 
Hii hotuba uwapime na Maraisi waliopita baada yke utaiona ilivyowagusa ukimtazama Kikwete kwa kweli hatuba hii inaonyesha wazi failure ya Mheshimiwa Kikwete hasa hapo panapogusia rushwa ,ameshindwa.
 
Wakuu nimesikiliza hotuba nyingi za baba wa taifa hasa kupitia chombo cha habari cha taifa tbc pamoja Na mikutano ya ccm pale dodoma ambako wana bango Lao maarufu limeandikwa 'bila ccm madhubuti......' Lakini cha ajabu hii kauli ya Mwl.kwamba watanzania wasipopata mabadiliko kutoka cc
m watayatafute kwengine sijawahi kusikia tbc au ccm wakiionesha hadharani. Je Ni kwanini? naomba mnisaidie jamani.
 
Hotuba za Mwalimu bado ziko valid sana mpaka leo hii, huyu mtu alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuona mbali.

"Watanzania wanataka mabadiliko na wasipoyaona wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM."


 
Last edited by a moderator:
Maendeleo tumeyakosa CCM kwa majangili,tutayatafuta CHADEMA kwa wazalendo!!

Rest in hell CCM!
 
Hii ni kauli ya baba wa taifa aliotoa mwaka 1995 katika hotuba yake ya kumpta mgombe uraisi kupitia CCM.

Moja ya mambo alioyataja katika hotuba yake hiyo ya mwaka 1995 ni pale aliposema watanzania wamechoshwa na rushwa iliyokithiri serikalini.

Hii ni kauli inayoishi mpaka leo.

Ninachofurahi ni kuona kauli hii ikitimia kwa vitendo hasa baada ya sakata la Escrow kwa watanzania kutafuta mabadiliko nje ya CCM kwa kuiadhibu CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita hivi karibuni.

Ni matumani yangu kuwa kauli hii itaendelea kutimia zaidi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Juhudi za CCM kupambana na rushwa ni ndogo mno na kibaya zaidi ni kuwa vita hiyo inaangalia sura hivyo ni lazima CCM itaanguka tu kutokana na kukithiri kwa rushwa.

Kikwete na serikali yake ndio wa kulaumiwa kwa kufumbia macho rushwa kubwa hasa kwa doublestandard ya kushughulikia baadhi ya watuhumiwa wa rushwa.
 
Hahaahahaha Halafu kuna mtu anajifananisha na Nyerere... Mmghh
 
"....Watanzania wanataka mabadiliko...Wasipoyaona...Wasipoyapata ndani ya CCM; watayatafuta nje ya CCM...."

".....Lakini inatakiwa ukiulizwa swali...huyu atatusaidia kupiga vita rushwa jibu litoke ndani ya roho yako....."

Je ni wakati muafaka wa kuyatafuta mabadiliko hayo nje ya CCM...??

https://www.youtube.com/watch?v=GAEpisZ3Cuk
 
Back
Top Bottom