Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Mswahili,
Kama uko karibu hivyo na Jumbe mwulize juu ya zile fedha alizompa Ghadafi mwaka 1975 na kama alinunua suti ngapi Washington D.C kwa kutumia hizo fedha. Utakuwa umeshajibu dukuduku za DrWho
 
mswahili said:
Mugishagwe
Masuala ya waraka nimeahidi kumpatia Mkandara kama atataka. humu sitauweka naogopa maisha yangu kukatwishwa. wewe umesema Usalama wa Taifa kuna watu wa seminary za kanisa na huko jeshini unafahamu wazi wako watu wa sehemu gani?
Mkandara nadhani si ndugu yetu kama unavyolazimisha wewe na yeye.
maana sehemu ya kutukana kajitoa ' Amesema nyie waislamu mik.... yenu' angesema yetu.
Father Mbiku yupo pale na nina majina ya WAkristu walioingizwa pale wakiwa na division 3.
pia nina orodha ya wanafunzi zaidi ya miaka 300 ambao mwaka juzi waliomba kuingia kama Private sponsorship lakini ukiwa mkristu basi unapewa goverment sponsorship.
ninao majina ya watu waliopewa Goverment sponsorship na mzee Mkono kwa ukristu wao.
ninao hata waraka wa muungano ambapo umefichwa na Nyerere ila hapa si mahala pake kama nilivyosema hapo juu.
nakupa home work.
ilikuwaje nyerere awa support Biafra? ambao walijitenga na serikali halali? jibu Ukristu wa Nyerere ndio uliomsukuma kufanya hayo.
jiulize Iddi Amin na nguvu iliyotumika kumshambulia ilikuwa nini? kisa nyerere alitaka ukristu utawale Africa ndio maana hata Gaddaf akawa ana msaidia Idd Amin kwani vilikuwa vita vya kidini.
pia hutakiwi kumshambilia mtu hadi ndani mwake Nyerere alipeleka jeshi hadi katikati ya Uganda.tumeingizwa kwenye vita kumsaidia mkatoliki obote.
huyu ndio mwalimu aliyetuwekea usiku hadi bongo haijulikani kwenye ramani ya dunia. kisa udini+ukabila


Mswahili wewe mtu wa ajabu kweli kweli; du! sikujua kuwa kuna watu wanaweza kuongea utumbo hivi. Yaani wakati Amini anachukua ile sehemu ya Kagera pale na kutamba kuwa ameiteka kwa rekodi ya dakika 24, wewe unasema hiyo ilikuwa ni sawa tu, Nyerere alitakiwa anyamaze na kumwacha Amini amege sehemu ya nchi yetu kimabavu hivi hivi tu. Yaani eti kitendo cha Nyerere kupigania kukomboa sehemu hiyo ya nchi wewe uliona ni kutaka kuendeleza ukatoliki Afrika.

Kama ungekuwa unajua historia kuwa support ya Nyerere huko Biafra ilikuwa inatokana na personal friendship kati yake na Col Ojukwu ambaye alikuwa amesaidia kutuliza mapinduzi ya 1964 hivi wakati jeshi la kwanza limeasi hapa Tanzania usingeingiza dini hapa. Col Ojukwu alikaa Dar es Salaam kwa muda wa karibu mwaka mzima akiongoza majeshi ya commonwealth yaliyokuja kulinda amani Tanzania baada ya maasi hayo. Kwa vile Nigeria ilikuwa kati ya nchi za kwanza kwanza kufanya mapinduzi ya kijeshi, jambo ambalo Nyerere hakuwa anakubaliana nalo kwa vile lilikuwa pia linagusa yeye binafsi kama rais ambaye angeweza kupinduliwa, ndiyo maana alisimama upande wa wale wanaopinga viongozi walioongoza mapinduzi ya kijeshi, in that case Col Ojukwu. Kwa jumla Nyerere hakuwa na uhusiano mwema na viongozi wote walioingia madarakani kwa kupindua kijeshi.

Mbona Kati ya marafiki wakubwa wa Nyerere wakati huo alikuwa Gamal Abdel Nasser wa Misri, je na yeye alikuwa makatoliki? Alhaji Abubablar Tafawa Balewa wa Nigeria (mpaka leo kuna barabara pale Mwanza inaitwa mtaa wa Balewa karibu na kitua cha basi nafikiri), je naye alikuwa mkatoliki? Ahmed Sekou Toure wa Guinea alikuwa swahiba mkubwa sana wa Nyerer, je naye alikuwa mkatoliki (Kuna hospitali pale Mwanza inaitwa hospitali ya Seketure kwa hesima yake )

Sidhani kama una uhakika na ulichoandika, inawezekana una sababu nyingine. Ninajua kuna grupu la waislamu hapa ambalo halitaki kusikia jina la Nyerere na wanafanya kila jitihada kutaka lifutike kabisa katika kumbukumbu za Tanzania. Ni haki yao kufanya hivyo, lakini siyo kufanya hivyo kwa kupindisha historia ili kukidhi matakwa ya chuki hiyo.
 
Ujinga huu... waacheni.
Ni Nyerere pekee kiongozi wa Afrika aliyekataa katakata hadi anaondoka madarakani kuitambua serikali ya Isreail hali waarabu wote wa Afrika ikiwa ni pamoja na Eygpt walikuja kuweka mkataba lakini Nyerere alikataa katakata.
Kaingia Mwinyi muislaam kitu cha kwanza ni kuitambua Israel ili tupate misaada kisha mnamtukana sana Nyerere kuwa aliwachukia waislaam. Kawapa chombo muhimu sana Bakwata na serikali kugharamia watu kwenda Hijja bureee! waswahili nyie mkaanza kuwatoza watu rushwa kupata nafasi.
Kichuguu umezungumzia Mwanza,
Unajua hapo zamani Mwanza Secondary ilikuwa ikiitwa AghaKhan, mshikaji hakuna mswahili wahindi watupu!. Mzizima palikuwa hakuna mswahili ila kwa mwenye kujulikana hakuna cha division 1 wala 2, huingii hapo ng'oo. Acha mbali shule za kiktristu ambazo ndizo wanapenda kuzishambulia. Kaingia Nyerere tumeweza kusoma shule hizo tena Bureee!imekuwa nongwa kwa mswahili anataka umpe hadi mkeo ati sababu wanaosema sana ni wale waliofaidika na Ulevi wa wahindi na waarabu.
Ujinga mtupu
Nadhani hili lilikuwa pungufu la Nyerere angewaacha kama walivyo washenzi wote wasiokuwa na shukurani..
Mswahili,
Nasubiri huo waraka wa Jumbe nitumie barua pepe kama unaogopa kiasi hicho. Box langu tupuuu!
 
Jizaledo said:
Mswahili,

Ukienda mbali kughorodhesha Nyerere alivyofadhiliwa na Waislamu itaonekana kama unawasimanga hawa ndugu zetu. Mimi nisingependa uende huko, si vizuri. Pia siafikiani nawe kuyaleta majina ya akina Magufuli hapa kwani zaidi ya wao kuwa wakristo si dhani ni mahali pa kuwajadili kwenye mada hii. Ukifanya hivyo utaonekana unamkaba shingo kila ambaye ni mkristo. Waachie wao wafanye hilo wewe usiwajoin.

Of Course, Nyerere alipoanza harakati za Ukombozi alipata support kubwa kutoka kwa waislamu, hakuna alieyepindisha hiyo historia; ndio waliokuwa wengi pale Dar es Salaam. In fact ukiwaambia waislamu hao waliofanya kazi kwa karibu sana na Nyerere watasuta uwongo huu wa udini. Nenda kamwulize Mzee Kawawa ambaye ndiye mwislamu pekee aliyefanya kazi kwa karibu sana na Nyerere wakati wa uhai wake wote katika Serikali na katika TANU/CCM. Inasikitisha kuwa Hayati Mzee Thabit Kombo naye kwa sasa hivi hayupo kujibu baadhi ya uzushi huu.
 
mswahili said:
Kichuguu
Kawawa hana tofauti na Mkandara.
Jasusi
Nitafuatilia habari kamili.

Kwa hiyo Kawawa siyo muislamu, au na yeye alipigania kuendeleza ukatoliki.

Wahenga walisema mwizi huwa haamini watu wengine kwa vile anadhani nao ni wezi. Kwa kadri wewe na wenzako mnavyodhani kuwa kila asiyekuwa musialamu basi anachukia waislamu ndiyo hivyo hivyo mlivyo, yaani wewe pamoja na grup lako mnachukia watu wote wasio wasiokuwa waislamu, ambayo ndiyo filosofi ya al-qaeda na taliban wote. Yule jamaa aliyebadilisha dini pale Afghanistan kwa hiari yake mwenyewe, wao wakasema achinjwe! tabia ya ajabu kabisa.

Watu wenye mawazo kama nyinyi mngekuwa madarakani pale Tanzania tungepata hali ile ile ya Sudan; nchi nzima ingelazimishwa kuwa waislamu na kufuata SHARIA. Watu wenye heshima zao kitaifa kama Kawawa, Thabit Kombo na hata marehemu Omar Juma leo mnasema wao hawakuwa waislamu kwa vile walipigania haki kwa watu wote badala ya kupigania haki kwa waislamu tu. Kwenu nyinyi watu wenye haki zaidi ni waislamu tu, yaani watu wa dini nyingine zote ni kama wanyama tu. Huu ni wendawazimu kabisa.
 
ninawasilisha sehemu ya tamko la serikali ya Tanzania kuhusu kuiunga mkono Biafra, pamoja na sababu za kufanya hivyo. Tamko hilo lilitolewa 1968 na C.Y.Mgonja, aliyekuwa waziri wa mambo ya nje.
The world has taken it upon itself to utter many ill-informed criticisms of the Jews of Europe for going to their deaths without any concerted struggle. But out of sympathy for the suffering of these people, and in recognition of the world's failure to take action at the appropriate time, the United Nations established the State of Israel in territory which had belonged to the Arabs for thousands of years. It was felt that only by the establishment of a Jewish homeland, and Jewish national state, could Jews be expected to live in the world under conditions of human security. Tanzania has recognised the State of Israel and will continue to do so because of its belief that every people must have some place in the world where they are not liable to be rejected by their fellow citizens.

But the Biafrans have now suffered the same kind of rejection within their state that the Jews of Germany experienced. Fortunately they already had a homeland. They have retreated to it for their own protection, and for the same reason - after all other efforts had failed - they have declared it to be an independent state.

In the light of these circumstances, Tanzania feels obliged to recognise the setback to African Unity which has occurred.

We therefore recognise the State of Biafra as an independent sovereign entity, and as a member of the community of nations. Only by this act of recognition can we remain true to our conviction that the purpose of society and of all political organisation, is the service of man.

hotuba nzima inapatikana hapa. hoja zilizojengwa ni nzito na hakuna UDINI hapo. http://www.biafraland.com/biafra_recognized_by_tanzania.htm

Unajua kuna kikundi cha Waislamu wa Tanzania waliamua kusoma hitma kwa heshima ya Iddi Amin Dada. Kitendo hicho kinasikitisha ukizingatia kwamba kimefanywa na Watanzania wenzetu. Kikundi hicho ndiyo kinaleta madai kwamba vita ya kumuondoa Nduli Amini ilikuwa ya kidini.

Jamani, Gadaffi alikuja kumuomba radhi Nyerere na Watanzani kwamba alipotoshwa na Iddi Amini kuhusu ugomvi wake na Tanzania. Sijui ni kwanini watu wanaendeleza hoja hii hata baada ya kukanwa na wahusika wake wakuu.

Hoja ya kudai Uhuru, pamoja na kwamba waasisi wake wengi walikuwa ni waislamu, haikuwa hoja ya KIDINI au UDINI. Ilikuwa ni hoja ya KITAIFA. Hoja ile ilitaka kurejesha heshima ya MWAFRIKA ndani ya nchi yake.

Kwamba hakuna Kanisa lililounga mkono waziwazi hoja ya kudai Uhuru, si suala gumu kueleweka. Mkoloni alikuwa Mkristo, kuna ugumu ktk hilo? Pamoja na hayo kulikuwa na mbinu za chinichini za Wamisionari/Kanisa kumuunga mkono Mwalimu na Tanu katika kudai Uhuru.

Ziko taarifa kwamba wamisionari wa Maryknoll walikuwa wakimsaidia Mwalimu kifedha wakati wa harakati zile. Ziko fununu kwamba alipokuwa UNO Mwalimu alifikia katika misheni ya Maryknoll.

Pamoja na hayo hiyo siyo hoja ya msingi. Waislamu wenyewe waliojitoa mhanga kuanzisha harakati za Uhuru walimkataa kila aliyejaribu kuziteka nyara harakati zile na kuzipa sura za Kidini--Uislamu. Waislamu walimkataa Mtemvu alipotaka kuleta Udini katika kudai Uhuru.

Kinachonishangaza mimi ni kwanini Waislamu wa miaka ya 1980/1990/2000 wadai harakati zile zilikuwa za dini yao, wakati waasisi wenyewe, wengi wao wakiwa Waislamu, walishakataa kuhusishwa na UDINI? Kwanini?
 
Kwa kusaidia tu hapa harakati ama mchakato mzima wa kutaka kumpa Mwalimu Utakatifu umeanzishwa na kanisa Katoliki Jimbo la Musoma kushirikiana na shile hilo la wa Merryknoll na rafiki mkubwa wa Mwalimu Fr.Art Wille hadi sasa anakusanya mambo mbali mbali mazuri ya Mwalimu kujaribu kuona kama kuna uwezekano wa kumfanya Mtakatifu . Baada ya mkoloni Kanisa lilikuja kwa kasi kuleta maendeleo kwa Watanzania wote na Mwalimu alipo ona waislam walibaki nyuma akaamua kuchukua mali za wakristo na kuwapa waislam na wasio kuwa na dini kwa manufaa ya Tanzania na watanzanai wote hadi sasa .
 
jokaKuu,
Good questions. But I bet you won't get a straight answer from the likes of Mswahili and Jizalendo.
 
Mswahili,
Umekwisha bob, hapa maji marefu na chunusi mbaya sana!... ngoma nzito hii huiwezi, wee kaa pembeni wanaume tuvute uradi...
 
JOKA KUU,
Lini Gaddaf alikuja kuomba msamaha kwa Nyerere? naomba uthibitisho.
Harakati za uhuru zilikuwa za waislam ndio maana utaona masheikh wameacha kazi na kufanya kazi ya kuzunguuka nchi nzima hata kabla ya mikutano ya Taa hata Tanu ilikuwa kwanza inaanza dua toka kwa sheikh haikutokea dua au misa toka kwa mchungaji. unataka nini ujue kama ilkuwa ni harakati za waislam, ambao wame sacrifice kwa ajili ya maanufa ya nchi na huo udini wangekuwa nao wasingemtanguliza Nyerere na kumuachia madaraka kwani lengo lao ni kuikomboa nchi.
wewe unajifanya unajua rekodi tizama picha za mikutano ya Tanu kwenye harakati za uhuru ni vibaraghasia na mabaibui tu. wenzetu mlikuwa kanisani kuwafurahisha wakoloni. na kama kuuliwa au kunyongwa waislam walikuwa tayari ili nchi yao ipate uhuru wa kweli.
unasema kuna fununu mwalimu alipokuwa UNO hapa hatuzungumzii fununu bali fact.
hata chuo kikuu cha Dar-es-salaam waislam walitoa michango mingi na mikubwa ili wananchi wanaufaike lakini leo akina Father Mbiku wanatufanya second- class citizen.mfano mzuri Bi Tatu alitoa mchango wa shiling mia tano huku mkristu pekee Nyerere alitoa mia mbili. leo tunaambiwa na akina Mlalahoi hatujui thamani ya elimu.fuatilieni michango ya ujenzi wa Udsm.
kuna mtu kaleta uongo wa Afghanstan kuwa uislam ni ukatili kwanini usimuulize Yvonne Ridley ambaye alikuwa mwandishi mwanadamizi wa The Independent huyu alikamatwa na Taliban alipoona ukweli na tabia nzuri za waislam akaamua kusilimu mtafuteni kwenye Google atakwambieni kama waislam ni wanyama au laa.
Hao waliomsomea Hitima Idd Amin hawana kosa wamefanya jambo la busara sana kwani ni muislam mwenzetu. huko kuna watu wanataka kumfanya mtatifu mtu aliyewabagua watu kwa kila hali kidini na kikabila na ameua na kuwatia vilema watu wengi tu. kaenda kuanzisha vita dhidi ya uganda ili kumfurahisha Mkatoliki mwenzake Obote.
Mugishgwe
katuachia uovu wa udini ambao bado mnaundeleza.
 
mswahili said:
JOKA KUU,
Lini Gaddaf alikuja kuomba msamaha kwa Nyerere? naomba uthibitisho.
Harakati za uhuru zilikuwa za waislam ndio maana utaona masheikh wameacha kazi na kufanya kazi ya kuzunguuka nchi nzima hata kabla ya mikutano ya Taa hata Tanu ilikuwa kwanza inaanza dua toka kwa sheikh haikutokea dua au misa toka kwa mchungaji. unataka nini ujue kama ilkuwa ni harakati za waislam, ambao wame sacrifice kwa ajili ya maanufa ya nchi na huo udini wangekuwa nao wasingemtanguliza Nyerere na kumuachia madaraka kwani lengo lao ni kuikomboa nchi.
wewe unajifanya unajua rekodi tizama picha za mikutano ya Tanu kwenye harakati za uhuru ni vibaraghasia na mabaibui tu. wenzetu mlikuwa kanisani kuwafurahisha wakoloni. na kama kuuliwa au kunyongwa waislam walikuwa tayari ili nchi yao ipate uhuru wa kweli.
unasema kuna fununu mwalimu alipokuwa UNO hapa hatuzungumzii fununu bali fact.
hata chuo kikuu cha Dar-es-salaam waislam walitoa michango mingi na mikubwa ili wananchi wanaufaike lakini leo akina Father Mbiku wanatufanya second- class citizen.mfano mzuri Bi Tatu alitoa mchango wa shiling mia tano huku mkristu pekee Nyerere alitoa mia mbili. leo tunaambiwa na akina Mlalahoi hatujui thamani ya elimu.fuatilieni michango ya ujenzi wa Udsm.
kuna mtu kaleta uongo wa Afghanstan kuwa uislam ni ukatili kwanini usimuulize Yvonne Ridley ambaye alikuwa mwandishi mwanadamizi wa The Independent huyu alikamatwa na Taliban alipoona ukweli na tabia nzuri za waislam akaamua kusilimu mtafuteni kwenye Google atakwambieni kama waislam ni wanyama au laa.
Hao waliomsomea Hitima Idd Amin hawana kosa wamefanya jambo la busara sana kwani ni muislam mwenzetu. huko kuna watu wanataka kumfanya mtatifu mtu aliyewabagua watu kwa kila hali kidini na kikabila na ameua na kuwatia vilema watu wengi tu. kaenda kuanzisha vita dhidi ya uganda ili kumfurahisha Mkatoliki mwenzake Obote.
Mugishgwe
katuachia uovu wa udini ambao bado mnaundeleza.

Wewe Mswahili nenda kalale,

Kwamba hujui kuwa Gadaffi alimwomba randhi Nyerere na kutamka kuwa alifanya makosa sana kumsaidia Amin kuishambulia Tanzania. Tafuta paper hii usome mwenyewe:

Oye Ogunbadejo "Qaddafi and Africa's International Relations"
Journal of Modern African Studies, Vol. 24, No. 1 (Mar., 1986), pp. 33-68.


Kwamba kati ya Amini na Nyerere unasema afadhali Amin kwa sababu alikuwa "mwislamu mwenzetu." Huu ndio uwendawazimu kabisa.

Kwamba watu wote waliochinjwa na kurekodiwa kwenye na video zilizosambazwa wewe hukuziona! tena jamaa walikuwa eti wanaomba dua kabla ya kumchinga binadamu mwenzao!! Ukitaka video mimi nitakufauti u-tube.com zipo nyingu tu.

Kwamba huyu jamaa aliyekuwa amehukumiwa kuchinjwa eti kwa sababu alibadili dini na kuwa mkriso wewe unseam ni uwongo. Jamaa aliponyeshwa na serikali ya merakani iliyoamua kuweka shinikizo. Angalia hapa ..http://www.cnn.com/2006/WORLD/asiapcf/03/22/afghan.christian/index.html

Sidhani kama wewe na group lako hapa mnaopiga kampeini za kuanzisha chuki za kidini mna nia njema na jambo lolote. Nimekuwe nasikia kuwa kuna kada fulani wa kiislamu kazi yao ni kutafuta visababu vya uongo na ukweli ili kuchochea violence za kidini lakini nilikuwa bado sijakumbana nao kikamilifu; Mswahili wewe ndiwe wa kwanza kwangu.

Pamoja na kuwa mimi nimekulia katikati ya dini ya kiislamu pale Tabora ambako tulikuwa tumezungukwa na waislamu mtaa mzima, hakukuwa na kada wa namna yako hata mmoja, na hata pale Dar sikuwahi kukumbana na kada wa level yako. Wewe katika mambo haya ya kipuuzi ni moto wa kuotea mbali kabisa; ni wa kuogopa kama ukoma!
 
mswahili,
nafikiri hujanielewa kidogo. ni kweli harakati za uhuru zilianzishwa na zilikuwa na msisimko zaidi miongoni mwa waislamu. pamoja na hayo harakati hizo hazikuwa na mtizamo wa Kidini kama ambavyo nyinyi wakereketwa wa siku hizi mnavyotaka tuamini.

madai yangu ni kwamba, wazee, waasisi wale, hawakuwa na UDINI kama huu tunaoushudia toka kwako. historia inaonyesha kwamba watu waliokuwa na mwenendo kama wako, mfano. Zuberi Mtemvu, walikataliwa, na hawakupewa nafasi, na waislamu waasisi wa harakati za uhuru.

Gadaffi alimpa Nyerere siku 7 awe ameondoa majeshi ya Tanzania ndani ya Uganda. Majibu ya Tanzania ilikuwa kuwasambaratisha askari wa Libya pale Lukaya. Kilichofuatia ni Gadaffi kuondoa majeshi yake, na kutafuta SULUHU ya kurudishiwa askari wake waliotekwa na majeshi yetu.

Unataka ushahidi gani? Nikafukue maiti za Walibya Lukaya? Nini kilichomtoa Gadaffi Uganda? Mateka wale walirudishwa baada ya Libya/Gadaffi, kuamua kuacha uhasimu na serikali ya Tanzania.

Binafsi siamini kama Nyerere anastahili nafasi ya Utakatifu. Vilevile waliomsomea dua Iddi Amini walilenga katika kuwatukana askari wetu waliopigana vita vya Kagera.

Mwisho, wamisionari wa Maryknoll walimsaidia Nyerere kwa namna mbalimbali wakati wa harakati za Uhuru. Kauli mbiu ya uhuru iliungwa mkono na wananchi wote wa Tanzania, bila kujali imani zao za kidini, au kabila. Ukweli huo unathibitishwa na mapokezi aliyokuwa akiyapata Nyerere kila alipotembelea, pamoja na matambiko ya KIMILA aliyokuwa akifanyiwa.

Matambiko yaliyokuwa yakifanywa siyo Uislamu, ni MILA, ni JADI, ni UAFRIKA.
 
JokaKuu,
Labda kukumbushia tu, kwa kuunga mkono hoja yako kuhusu Gadafi, labda Mswahili anaweza kutuambia ni kwa nini Amin alifukuzwa kutoka Libya, akakimbilia Saudi Arabia ambako mauti ilimkuta?
 
Ukipinga Mwalimu kuwa hastahili utakatifu lazima ujue unacho kipinga . Kuna watu wana kusanya data ili kufanya maamuzi baadaye lakini data pekee hazitoshi tunangoja miujiza . Tayari kuna ushahidi wa tu kuhiji Butiama na wamepona . Hilo hutakubali lakini ndiyo mwanzo wa miujiza . Mtu yule alikufa Tanzania ikatikisika na maeneo ya wazanaki tuliona mambo ya ajabu . Hii ni ishara kwamba Mtawala alikuwa kaaga Dunia na si kawaida ile .

Unapinga kwanza wewe nani ? Muislam upinge kwa kelele za aina yako nani atakusukiliza ? Kwanza anza kupinga ukatili wa waislam huko Iraq, Sudan, Afghanstan nk . Wapeni wanawake wa kiislam haki zao heshumi maisha huru kabla hujaanza kuingilia mambo ya Kanisa katoliki . Lile lina mizizi mizito kiroho na kisiasa .

Umeona mwenyewe alipokufa Papa ulijionea na hata alipokuja TZ hata waislam waliishiwa nguvu .

Pole sana na mimi nasema kama unapinga JKN kuwa Saint fika Jimboni Musoma toa hoja zako with evidence . Makatoliki yameenda shule yatakusikiliza na kuchukua maamuzi si kama akina Taleban kaka
 
Joka kuu
Amin hakufukuzwa Libya. ila Saudia walimuomba na wakampa heshima kubwa. hata fungu alilokuwa anapewa ni dola laki 2 kwa mwaka. Libya hawakuwa na pesa hizo.
acheni kumzulia Amin.shujaa wetu
 
Kumbe wewe ni Mganda ? Maana Amin was a living devil Ugandan leader.Anakuwa shujaa wako kivipi ? Kuna akina Mkwawa hapa , shujaa Nyerere, Patrice Lumumba nk na hata Amina naye ? Ama ni shujaa wa Waislam ? lakini kwa ushujaa upi hata wa kuwafanya nyie waiskam kumkumbuka ?
 
Mswahili,
Amin alifukuzwa Libya na Gadafi baada ya Gadafi kugundua huyo Mwislamu mwenzake anabughia pombe. Ndipo Saudi Arabia wakampa hifadhi. Gadafi naye ana mafuta. Asingekosa fedha za kumtunza. Wewe utamwombaje mgeni wa mwenzako ahamie kwako? Inaeleweka?
 
Back
Top Bottom