Nyerere: Siku moja Watanzania watalirudia Azimio la Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere: Siku moja Watanzania watalirudia Azimio la Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sheba, Sep 1, 2012.

 1. S

  Sheba JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 210
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kumepambazuka, nauona mwanzo wa safari mpya, safari ya kurejea kwenye njia itupelekayo kule kwenye nchi yetu ya ahadi, nchi yenye kujitegemea, ambayo watu wake hawapishani sana kimapato, wote wana haki sawa, wanashiriki katika ujenzi na ulinzi wa taifa lao na wanapatiwa hifadhi na kinga dhidi ya uhuru wao kupitia sheria na mahakama zinazotoa haki. Nchi ambayo watu wake wanaishi kijamaa(Sio maxism) na ambayo viongozi wanasimamiwa na miiko. Nchi hiyo ni nchi ya agano, agano lililokuwa likiitwa Azimio la Arusha ambalo lilibeba maudhui ya 'Ahadi za Mwana TANU" , ahadi ambazo zimeunda taifa lisilo na ukabila, udini na lenye amani. Agano ambalo viongozi waliamua kulipuuzia na kuja na Agano la Zanzibar ambalo hatuna mashaka kuwa sasa limeshindwa.

  Hakuna shaka kuwa watanzania wote wanayo manung'uniko juu ya namna mambo yanavyokwenda. Manung'uniko yao ni ya msingi, wau hawaridhiki na namna wanavyoongozwa, namna viongozi wanavyopotoka, namna tusivyoheshimiana na namna rasilimali za umma zinavyotumika vibaya. Lawanma zinaelekezwa kila upande, baadhi wanalaumu rika, wengine wanalaumu dini, wengine wanalaumu ukanda na wengine wanalaumu vyama, alimradi kila mtu nchini anatafuta mchawi.

  Ukiangalia kwa makini, manung'uniko yote yanatokana na taifa kukosa mwongozo sawa na abiria ndani ya jahazi ambalo limepoteza dira. Ukiangalia mjadala wa katiba na maoni ya vyama vya siasa, asasi za kiraia na wananchi kwa ujumla unapata picha kuwa agenda ya nchi ni moja na wala hakuna chama chenye sera tofauti. CCM na CHADEMA ukiwafuatilia hawana tofauti za kisera bali ni kwenye dira tu. Vivyo hivyo, hata makundi ndani ya CCM hayatofautiani kisera bali Dira tu. Hili linanilazimu kuhitimisha kuwa ipo dira moja iliyo kuu kuliko vyama vyetu, dini zetu na makabila yetu, nayo ni Azimio la Arusha.

  Wakati sasa umefika kwa wasomi wenu, viongozi wetu na wananchi yetu kurejea kwenye msingi, tulisome upya Azimio la Arusha, tulihuishe kulingana na nyakati tulizonalo sasa kwani huko ndio jibu letu lilipo. Azimio la Arusha limetutoa mbali na mambo makubwa ambayo taifa hili iliyafanya yaliongozwa na Azimio la Arusha ikiwemo ushindi wetu dhidi ya Nduli Idd Amini, ujenzi wa viwanda, kuelimisha watanzania wote na kumuwezesha mtoto wa mkulima yoyote kuwa kiongozi wa ngazi yoyote tofauti na sasa ambako mfumo wa kimangi umeanza kujitokeza.


  Mwalimu Nyerere wakati anahojiwa kuhusu Azimio la Arusha baada ya kutoka madarakani alisema kuwa haoni tatizo juu ya Azimio lile, analisoma kila leo na anatembea na biblia na Azimio lile tu, ingawa kuliongelea kwa sasa (wakati huo) ni sawa na kuwa mwendawazimu, yeye yuko tayari kunyamaza maana muhimu kwake ni Tanzania, akahitmisha kwa kusema, anaamini watanzania iko siku watalirudia Azimio.

  Je, maneno haya hayajtimia? Je, hatupo hapa tulipo kwa kutelekeza misingi ya Azimio hilo? Je, mzimu wake haututafuni? Hakika hatujachelewa. Waswahili husema, "Mwenda tezi na Omo marejeo ngamani"
   
Loading...