Mhere Mwita
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 235
- 1,275
Nimefuatilia sakata la CAG Prof Mussa Assad na spika wa Bunge Ndugai Juu ya Neno dhaifu nimeona spika Ndugai anatumiwa na Mafisadi ili kuziba hoja ya wizi wa pesa za wananchi.
Mfano mzuri Spika Ndugai hakuitaka serikali ituambie wananchi ni wapi ilipo Trillion 1.5 ambao ilikuwa ikafika trillion 2.4 mwaka 2016/2017 na Leo Imefika Trillioni 4. Ndugai hataki tujue Lugumi Enterprise amepiga Sh. 604 Milioni. #CAGReport ya Serikali Kuu Uk. 304:
Tshs 604,390,244 kwa kile kilichoelezwa ni mafunzo ya wataalamu 30 zimetolewa Serikalini kupitia Jeshi la Polisi na kupokelewa na Lugumi Enterprise lakini hakuna mafunzo yaliofanyika.
Kwenye Mamlaka ya Rufaa za koda kuna mashauri ambayo yana jumla ya Trillion 382.6 sawa na 1200% ya Bajeti ya Nchi kwa maana hiyo Ndugai anatengeneza Mgogoro ili ufichwe Uozo.
Kama neno Udhaifu ni tusi mbona mwalimu Nyerere alimuita Rais Mwinyi ni dhaifu ukiangalia kwenye kitabu cha Mwl Nyerere cha Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania cha Mwaka 1994 ukurasa wa 66 Mwl aliandika hivi Nanukuu "Rais Mwinyi ni mtu mwema na mpole lakini ni kiongozi dhaifu; na upole wake na udhaifu wake unatumiwa na watu ambao sio wema" kwa hiyo Nyerere alimkashfu Rais Mwinyi.
Spika Ndugai Acha kutumika kuficha uozo neno dhaifu aliwezi kusababisha pesa za walipa kodi zipotee, sisi watanzania tunataka kujua pesa zetu ziko wapi.
Sent using Jamii Forums mobile app