Nyerere, Nkurumah na Lumumba ndio marais bora – Askofu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
MWALIMU Julius Nyerere wa Tanzania, Nkwame Nkuruma wa Ghana na Patrice Lumumba kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) ni miongoni mwa marais wa kipekee waadilifu Afrika,anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo imetolewa jana na Dk. Barnabas Mtokambali, Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Asembless of God (TAG) wakati wa mahubiri ya uzinduzi na uwekaji jiwe la msingi wa Kanisa la Jerusalem Christian Centra (JCC) Tanzania Assembile of God lililopo Nkuhungu mjini Dodoma.

Askofu Mtokambali amesema, kwa muda mrefu viongozi hao katika Bara la Afrika akiwemo Nelson Mandela wa Afrika Kusini ndio waliweza kuongoza nchi zao kwa uaminifu na bila kuutukuza wizi na ulaghai.

Dk. Mtokambali akihubiri kanisani hapo kwa lengo la kusisitiza uaminifu kwa viongozi amesema, ni vyema wakaiga mifano ya viongozi hao ambao waliongoza nchi zao kwa uaminifu mkubwa katika maeneo yao katika kipindi chao.

Licha ya kuwataja viongozi hao amesema kwa sasa Mungu ameiona nchi ya Tanzania kwa kuipatia Rais John Magufuli kuiongoza nchi ambayo ilikuwa inanuka uozo mkubwa na ufisadi wa kutosha.

Amesema, kitendo cha Rais Magufuli kupata nafasi hiyo ya urais kwa sasa anaweza kuongeza idadi ya viongozi waaminifu kufikia wane.

Amesema, kwa kipindi kirefu Tanzania imekuwa ikiongozwa na watu ambao siyo waaminifu ambao walipenda kujilimbikizia mali bila kujali kuwa, wapo watu ambao wanataabika kwa umasikini walionao.

“Katika eneo hili tumeweza kuwa na marais watatu tu ambao waliweza kuweka historia ya kuongoza kwa uaminifu waliobaki wote walikuwa ni wezi na wanyang’anyi kwa kupenda kujilimbikizia mali bila kujali shida za wananchi.

“Hata kwa Tanzania kwa kipindi kirefu tumekuwa na viongozi ambao hawakuwa na haja ya kuwa sikiliza watu wanyonge.

“Rais Magufuli amekuwa mwaminifu mtetezi wa wanyonge na kuhakikisha anasimamia kile ambacho anaona kitakuwa ni haki kwa Watanzania wengi huku akiwashukia vigogo ambao walikuwa wakijilimbikizia mali,” amesema Askofu Mtokambali.
 
Usipende kutumia Kitwanga ndio uje huku
Badala ya kujibu hoja za Askofu wenu unahangaika na mimi msome kiduchu kiongozi wenu wa Kanisa.

"Rais Magufuli amekuwa mwaminifu mtetezi wa wanyonge na kuhakikisha anasimamia kile ambacho anaona kitakuwa ni haki kwa Watanzania wengi huku akiwashukia vigogo ambao walikuwa wakijilimbikizia mali,” amesema Askofu Mtokambali."

Umemkubali baba Askofu?
 
Haya maneno bahati nzuri kaongea Askofu.

Yangesemwa na Sheikh angetukanwa humu daah!!..

Haya kaongea Askofu msomi siyo mnywa kahawa.

Teh teh teh!! Nipo kipembeni nimejibanza nasubiri majibu
 
Mkapa. Namkubsli hata kama alijilimbikizia mali baadhi ya watu wanavyodai.
 
Badala ya kujibu hoja za Askofu wenu unahangaika na mimi msome kiduchu kiongozi wenu wa Kanisa.

"Rais Magufuli amekuwa mwaminifu mtetezi wa wanyonge na kuhakikisha anasimamia kile ambacho anaona kitakuwa ni haki kwa Watanzania wengi huku akiwashukia vigogo ambao walikuwa wakijilimbikizia mali,” amesema Askofu Mtokambali."

Umemkubali baba Askofu?
Wacha hicho utumiachi kijana ungemwelewa kwanza Askofu
 
MWALIMU Julius Nyerere wa Tanzania, Nkwame Nkuruma wa Ghana na Patrice Lumumba kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) ni miongoni mwa marais wa kipekee waadilifu Afrika,anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo imetolewa jana na Dk. Barnabas Mtokambali, Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Asembless of God (TAG) wakati wa mahubiri ya uzinduzi na uwekaji jiwe la msingi wa Kanisa la Jerusalem Christian Centra (JCC) Tanzania Assembile of God lililopo Nkuhungu mjini Dodoma.

Askofu Mtokambali amesema, kwa muda mrefu viongozi hao katika Bara la Afrika akiwemo Nelson Mandela wa Afrika Kusini ndio waliweza kuongoza nchi zao kwa uaminifu na bila kuutukuza wizi na ulaghai.

Dk. Mtokambali akihubiri kanisani hapo kwa lengo la kusisitiza uaminifu kwa viongozi amesema, ni vyema wakaiga mifano ya viongozi hao ambao waliongoza nchi zao kwa uaminifu mkubwa katika maeneo yao katika kipindi chao.

Licha ya kuwataja viongozi hao amesema kwa sasa Mungu ameiona nchi ya Tanzania kwa kuipatia Rais John Magufuli kuiongoza nchi ambayo ilikuwa inanuka uozo mkubwa na ufisadi wa kutosha.

Amesema, kitendo cha Rais Magufuli kupata nafasi hiyo ya urais kwa sasa anaweza kuongeza idadi ya viongozi waaminifu kufikia wane.

Amesema, kwa kipindi kirefu Tanzania imekuwa ikiongozwa na watu ambao siyo waaminifu ambao walipenda kujilimbikizia mali bila kujali kuwa, wapo watu ambao wanataabika kwa umasikini walionao.

“Katika eneo hili tumeweza kuwa na marais watatu tu ambao waliweza kuweka historia ya kuongoza kwa uaminifu waliobaki wote walikuwa ni wezi na wanyang’anyi kwa kupenda kujilimbikizia mali bila kujali shida za wananchi.

“Hata kwa Tanzania kwa kipindi kirefu tumekuwa na viongozi ambao hawakuwa na haja ya kuwa sikiliza watu wanyonge.

“Rais Magufuli amekuwa mwaminifu mtetezi wa wanyonge na kuhakikisha anasimamia kile ambacho anaona kitakuwa ni haki kwa Watanzania wengi huku akiwashukia vigogo ambao walikuwa wakijilimbikizia mali,” amesema Askofu Mtokambali.
Askofu alimpa nani uaskofu huo! self proclaimed bishops!
 
Viongozi hawa wa dini wangrkuwa wakati wa yesu angeshauri wafungiwe Jiwe LA kusaga na watupwe baharini.

Hawana tofauti na kasuku kwa kuimba bila kufikiri. Mbaya zaidi siku hizi wamekwenda shule lakini hawaelimiki. Sio wakweli wamejaa unafiki kwa kushindwa kusimamia kweli. Labda kwa sababu nao huchaguliwa baada ya kufanya kampeni kama wafanya siasa.

Kwanini hawawezi sema mabaya ya watawala wakiwa madarakani ambako huishia kusifia kwa kila aina ya maneno lakini wakitoka madarakani wanawalaumu?
 
MWALIMU Julius Nyerere wa Tanzania, Nkwame Nkuruma wa Ghana na Patrice Lumumba kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) ni miongoni mwa marais wa kipekee waadilifu Afrika,anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo imetolewa jana na Dk. Barnabas Mtokambali, Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Asembless of God (TAG) wakati wa mahubiri ya uzinduzi na uwekaji jiwe la msingi wa Kanisa la Jerusalem Christian Centra (JCC) Tanzania Assembile of God lililopo Nkuhungu mjini Dodoma.

Askofu Mtokambali amesema, kwa muda mrefu viongozi hao katika Bara la Afrika akiwemo Nelson Mandela wa Afrika Kusini ndio waliweza kuongoza nchi zao kwa uaminifu na bila kuutukuza wizi na ulaghai.

Dk. Mtokambali akihubiri kanisani hapo kwa lengo la kusisitiza uaminifu kwa viongozi amesema, ni vyema wakaiga mifano ya viongozi hao ambao waliongoza nchi zao kwa uaminifu mkubwa katika maeneo yao katika kipindi chao.

Licha ya kuwataja viongozi hao amesema kwa sasa Mungu ameiona nchi ya Tanzania kwa kuipatia Rais John Magufuli kuiongoza nchi ambayo ilikuwa inanuka uozo mkubwa na ufisadi wa kutosha.

Amesema, kitendo cha Rais Magufuli kupata nafasi hiyo ya urais kwa sasa anaweza kuongeza idadi ya viongozi waaminifu kufikia wane.

Amesema, kwa kipindi kirefu Tanzania imekuwa ikiongozwa na watu ambao siyo waaminifu ambao walipenda kujilimbikizia mali bila kujali kuwa, wapo watu ambao wanataabika kwa umasikini walionao.

“Katika eneo hili tumeweza kuwa na marais watatu tu ambao waliweza kuweka historia ya kuongoza kwa uaminifu waliobaki wote walikuwa ni wezi na wanyang’anyi kwa kupenda kujilimbikizia mali bila kujali shida za wananchi.

“Hata kwa Tanzania kwa kipindi kirefu tumekuwa na viongozi ambao hawakuwa na haja ya kuwa sikiliza watu wanyonge.

“Rais Magufuli amekuwa mwaminifu mtetezi wa wanyonge na kuhakikisha anasimamia kile ambacho anaona kitakuwa ni haki kwa Watanzania wengi huku akiwashukia vigogo ambao walikuwa wakijilimbikizia mali,” amesema Askofu Mtokambali.
Hivi Lumumba alikuwa Rais wa nchi gani au naota?
 
Back
Top Bottom