VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Kila nikitafakari kilichofanyika kwenye muungano bado nakosa jibu. Nilijiunga CCM mwaka 1980 nikiwa mwaka wa mwisho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Wakati huo,CCM ilikuwa chini ya Uenyekiti wa Baba wa Taifa,Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Mambo ya Nyerere bado siyaelewielewi.
Mwaka 1964,nikiwa na umri wa kutosha lakini wa ujana,nilishuhudia Muungano huu wa sasa. Nilishuhudia kuchanganywa udongo wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Udongo huo ukaua nchi husika. Ukazaa nchi moja: Tanzania. Ilikuwa ni tarehe 26/4/1964,miezi mitatu baada ya mapinduzi ya Zanzibar.
Usanii
Nyerere aliiua kabisa Tanganyika na kuiacha Zanzibar ndani ya Tanzania. Tanganyika ikabatizwa jina la Tanzania Bara. Kemia aliyotumia Nyerere ndiyo inayonichanganya. Muungano huu ulikuwa wa namna gani ikiwa nchi sasa zimekuwa tatu huku moja ikiwa imekufa? Yaani, Tanganyika+Zanzibar=Tanzania + Tanzania Bara+Zanzibar.Ukitaka kuziona nchi hizi tatu ni rahisi. Fuatailia Challenge kule Uganda halafu subiria michuano ya kombe la dunia au mataifa ya Afrika. Utaziona timu za Tanzania Bara,Zanzibar na Tanzania.Pia,angalia Serikali zilizopo.Kuna Wizara za Tanzania,zipo za Zanzibar na pia za Tanzania Bara. Kwa mfano,kuna Wizara ya Miundombinu ya Tanzania Bara na ile ya Zanzibar.Hakuana ya Tanzania.
Kemia gani hii jamani? Huu si usanii uliotukuka uliofanywa na mzalendo wetu Nyerere? Nini kilitokea hapa? Huwa kichwa kinaniuma