Nyerere ndio alisababisha Rushwa, Umaskini, Ufisadi Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere ndio alisababisha Rushwa, Umaskini, Ufisadi Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, Dec 14, 2011.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Enough with romantization of Mwalimu.

  99% ya watawala wetu leo wote walilelewa na mwalimu hivyo ni uzao wake

  kwa hiyo its fair to say matatizo yetu yalianza toka enzi zake na sasa wanaendelea kuruthishana kama ambavyo CCM wanawapitisha watoto wao kuchukua na nafasi na CHADEMA akina mtei kuwaandaa akina Mbowe kututawala

  Mimi naona Mwalimu ndio cause ya matatizo yetu yote haya

  hakutaka accountability wala transparency kwa hiyo wanasiasa wetu wa leo wanaendeleza yale yale ya mwalimu.

  Kama hamuamini Tazama Cabinet imejaa akina nani na wametokea wapi? Mtu kama Mathias Chikawe tazama profile yake utaelewa naongelea nini
   
 2. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Watanzania ni watu wa kulalamika sana Nyerere ameacha uraisi lini! 1984 ni miaka 27 iliyopita! Je kwa miaka 27 iliyopita. Vilevile ilikuwa ni wakati wa Cold War!. Kuna nchi nyingi duniani zilikuwa na matataizo makubwa sana kuliko sisi Tanzania.

  Toka wakati huo tumegundua Gold kwa wingi, Gas kwa wingi, Miasaada imeongezeka, technologia imeongezeka, elimu ya Watanzania imeongezeka. Je ni kwanini tunamlaamu nyerere wakati tumekuwa na miaka 27 ya kurekebisha.

  Rwanda miaka michache tu walikuwa wanauana sasa unchumi wao unakuwa! hatuwezi kulaaumu historia. Kuna watu wengi sana wanarudisha nyuma Tanzania. Mfano je ni kwanini Watanzania hawana umeme ni kwasababu ya Nyerere!, kusumbuliwa kwenye vibali vya viwnja....wakulaamu ni viongozi wetu wa sasa hivi
   
 3. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,255
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Ilikuwa haina haja ya kuanzisha thread mpya... Mbona hii kitu sio kigeni ulichopost, tafuta thread husika uchangie... Naona kuna kampeni za kumponda sana Nyerere kipindi hichi...
   
 4. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,943
  Trophy Points: 280
  Ni kweli, angeenda kuchangia ile ya "Nyerere alikua kiongozi mbovu"
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ni kweli... pia aliyaambukiza mataifa Aidi ya 35 duniani gonjwa baya la ufisadi eh?
   
 6. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,943
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nashangazwa sana, ina maana tukikubaliana na wewe kwamba mwalimu was this or that, basi ndo mafisadi watafungwa?
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Dec 14, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,732
  Trophy Points: 280

  .........Rushwa wachukue wengine wa kulaumiwa ni Mwalimu!!!! Mikataba ya kifisadi wasaini akina Mkapa na Kikwete wa kulaumiwa ni Mwalimu!!!! Ukistaajabu ya Malaria Sugu utayaona ya Chuki Athumani!!!! Dah!!!!.........
   
 8. nimie

  nimie JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hapo kwenye bluu:

  Ukijaribu kuangalia sana utaona majority ya wanaomponda Mwl Nyerere ni watu wenye mawazo mgando, watu wanaokwepa responsibility, ni watu ambao wangependa kufanyiwa na si kufanya.
  Nimesikia jana Radio 5 kuwa wananchi wa kijiji kimoja huko Simanjilo, katika kujadili ile slogan ya Tumethubutu, Tumeweza na Tunasonga mbele wamesema katika maraisi wote waliotawala Tanzania, ni Mwl Nyerere tu alithamini na kutunza maliasiri za nchi, wenzie wote wamekuja kufuja na kuuza kwa bei ya kutupa hizo mali alizowatunzia mwenzao.
   
 9. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #9
  Dec 14, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  to understand the present we must unmask the past, to plan for the future we must plan from today.

  Viongozi wengi leo ni wale waliofanya kazi chini ya nyerere ni yeye ndie alietakiwa kupanga katiba bora, ni yeye ndie alitakiwa kupanga misingi ya sheria bora, ni yeye ndie alitakiwa kupanga misingi ya kupata viongozi bora, ni yeye ndie aliewanyima wazee wetu elimu ya kujuwa ya kuwa CCM ni chama kibovu ni yeye ndie leo tunapigania katiba bora baada ya muundo wa vyama vingi ni yeye ndio leo anatufanya tuseme mambo lazima yabadilike ni ubishi usiokuwa na maana kusema kwamba huyu bwana alitukosea sana watanzanina.
   
 10. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #10
  Dec 14, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mtatukana sana ila Hakuna kama nyerere nchi hii.
   
 11. t

  toby ziegler Senior Member

  #11
  Dec 14, 2011
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  acheni kuwa too sensitive

  kuna threads za nyerere zaidi ya 20 humu

  lakini mkiona thread imeanzishwa kumlaumu kwa madhila tuliyonayo leo maana kuwa defensive
   
 12. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #12
  Dec 14, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  hii mada ingeondolewa na kupelekwa kuunganishwa na ile mada nyingine. Haina uzito wa kujitegemea
   
 13. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #13
  Dec 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,155
  Trophy Points: 280
  Nyerere ni Rais ambae ametuletea maendeleo makubwa sana ya kiuchumi, kaondoka katuwacha shule zetu ni bora katika Afrika. Katuwachia barabara bora katika Afrika, katuwachia wasomi bora katika Afrika, katuwachia huduma za afya bora katika Afrika, nani anaebisha?
   
 14. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #14
  Dec 14, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  unataka kuniambia ujerumani inaendelea na udikteta kama urithi kutoka kwa adolf hitler?hawa kina slaa hawakuwepo wakati wa jkn?
   
 15. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #15
  Dec 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,155
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja yako 110% hakuna kama Nyerere nchi hii.
   
 16. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #16
  Dec 14, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  well, kwako wewe wenzako, maendeleo ni km za barabara za lami, majengo ya vyumba vya madarasa na majengo ya hospitali.
  Bahati mbaya sana maendeleo ya matumizi ni maendeleo hovyo zaidi duniani. Actually, ni maendeleo ya 'nyani'.......unatumia tu.
  Nyerere aliacha vitu gani kwa ajili ya uchumi?? Aliacha viwanda, sio viwanda vya ice cream na maji, bali viwanda vikubwa tu kwa ajili ya kuzalisha bidhaa na kuprocess raw material ili kuipandisha bei. Leo hii hakuna kiwanda cha maana zaidi ya viwanda vya ice cream.

  Unakumbuka viwanda vya 'machine tools'? Unakumbuka vilikuwa vingapi tanzania? Wakati huo ukitaka spare ya tractor ambayo haipo dukani, unaenda machine tools na wanafanya fabrication, unaondoka na spare yako.......leo hii unataka tujisifu kwa 'maendeleo ya used spares'??
  Nyerere ndo aaliwaambia mfilisi viwanda, then mviuze kama scraper??

  Maendeleo ya nyani sio maendeleo.
  Ukitaka meza, usipotaka tema, hata sisimizi watakula.
   
 17. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #17
  Dec 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,155
  Trophy Points: 280
  Unajuwa Nyerere alikuta hii nchi inanuka rushwa, yeye ndio akakomesha rushwa.

  Unajuwa hii nchi alipokabidhiwa Nyerere alikuwa imejaa magendo kila kona, Nyerere ndio alikomesha.

  Unajuwa hii nchi Nyerere aliikuta ni maskini wa kutupwa, yeye ndio akaifanya nchi tajiri.

  Unajuwa hii nchi Nyerere aliikuta haina hata chakula, watu wanashinda na njaa, yeye ndio akafanya watu wakawa wanapata kula kwa wingi tu.

  Unajuwa Nyerere alikuta hii nchi watu hawajuwi kulima, wanakuja wa Malawi kulima, yeye ndio akawafundisha kilimo bora vijiji vya ujamaa.

  Unajuwa Nyerere alikuja alikuta hii nchi barabara hazipitiki, ukitaka kwenda Mwanza mpaka upite Kenya, yeye ndiyo akzitengeneza barabara za zikawa zinapitika.

  Unajuwa Nyerere alilikuta hili jiji la Dar linanuka kwa uchafu, yeye ndio akalisafisha na likawa safi.

  Ni mengi tu, tutakumbushana mema ya Nyerere kila tunapoendelea...
   
 18. Losomich

  Losomich JF-Expert Member

  #18
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  To some extense naweza kukubaliana na wewe. Isipokuwa your too late for more than 27 years kula hoja hii katika public arena. Ni sawa na mtu anayehukumu mzuka. Let him alone to rest in peace!!! RIP MWL JK NYERERE-WE WILL REMEMBER YOU ALWAYS FOR ALL GOOD YOU HAVE DONE FOR TZ!!!
   
 19. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #19
  Dec 14, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  unajua mungu muumba wetu hutumia vitendo kuongea na binadamu au mdomo wa mtu mwenginewe kukushauli. Hizi kauli za kumpinga nyerere na kumchambua sana past perfomance zake ,zinatokana na kitendo cha Baraza la maaskofu cha kutaka kumfanya Nyerere kuwa ni mtakatifu. Hii itaendea sana mpaka iko siku litakuja lipuka siri la nguvu ambalo litamwacha kila mtu mdomo wazi.

  Naomba baraza la maaskofu wafikirie sana kitendo chao hicho cha kumtakatifuza baba wa taifa. hilo ni ombi langu tuu kwa AMECEA!
   
 20. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #20
  Dec 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,155
  Trophy Points: 280
  Mbona sikuelewi? Mimi nakuambia Nyerere kawacha mazuri tu, alikuta nchi haina kiwanda alipoondoka yeye vimejaa viwanda na vinafanya kazi. Vya machine tools, vya nguo, vya matrekta, oohh tena Tanzania tulikuwa tunazalisha Matrekta bora duniani, yanaitwa Velmet, hivyo vyote ni viwanda alivyoacha Nyerere vinazalisha kwa wingi sana. Kaacha uchumi uko juu sana, tuna akiba kibao benki. hatuna madeni wala hatuhitaji msaada. Nani anaesema Nyerere hajafanya kitu?
   
Loading...