Nyerere na TANU walidai uhuru mkoloni hawakuwapa uhaini lakini Mbowe na CHADEMA kudai katiba mpya wamepewa kesi ya ugaidi

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Hayati BABA wa TAIFA na TANU yake Walidai UHURU wa NCHI kutoka kwa Watawala wa KIKOLONI Watawala ambao Walikuwa ni KATILI na Wangeweza kumkamata na Kumpa KESI ya UHAINI lakini HAWAKUFANYA hivyo baada ya kujua ni HAKI yake na CHAMA chake Kudai UHURU.

Leo Freeman Mbowe na CHADEMA wanawapigania Wananchi kupata KATIBA MPYA KATIBA waliyoipendekeza Wananchi Chini ya TUME ya JAJI Warioba Mchakato ambao Ulianzishwa na RAIS MSTAAFU Jakaya Kikwete Lakini leo hii MBOWE na Wenzake Wamefunguliwa MASHTAKA ya UGAIDI kwa ili WASIDAI KATIBA MPYA

Najiuliza kama Mkoloni alijua ni HAKI ya NYERERE na CHAMA chake KUDAI UHURU wa WATANGANYIKA na HAWAKUMKAMATA kwanini WATAWALA mnamkamata MBOWE wakati KUDAI KATIBA MPYA kwa WANANCHI ni HAKI yake kama Mwananchi?

WATAWALA muachieni MBOWE na WENZAKE waendelee KUDAI KATIBA MPYA kwa Ajili ya WANANCHI
WANANCHI TUNATAKA "KATIBA MPYA"
KATIBA Iliyopo WANANCHI Hatukushirikishwa

20211217_073047.jpg
 
Bora ya mkoloni mweupe alituletea maendeleo makubwa kuliko mkoloni mweusi katuletea vilio
 
Back
Top Bottom