Nyerere na kipindi cha ujenzi mkuu,kikwete na kipindi cha kushika kasi kwa ubomoaji mkuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere na kipindi cha ujenzi mkuu,kikwete na kipindi cha kushika kasi kwa ubomoaji mkuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mapple, Jun 6, 2012.

 1. m

  mapple New Member

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ebu tuvipitie vipindi Tanzania ilivyopitia na kisha tuangalie kama kuna matumaini 2015
  MWALIMU NYERERE-Kipindi hiki kilitawaliwa na ujengaji wa misingi na falsafa ya nchi.Hiki kipindi ndicho kilikuwa na maendeleo makubwa kupita vyote vitakavyofuata(Relatively).Kwa mwaka 1977 serikali ya mwalimu iliweza kuandikisha watoto wanaotakiwa kwenda shule kwa zaidi ya asilimia 97(ikumbukwe pato la taifa lilikuwa linategemea kilimo tu).Ni katika kipindi hiki idadi ya watu wasiojua kusoma ilishuka ukilinganisha na sasa hivi.Elimu ilikuwa bure,afya bure na kila mwananchi alikuwa na imani na serikali yake.Gap kati ya maskini na tajiri lilikuwa dogo sana.

  Mwalimu alikuwa ni kiongozi mwenye nia thabiti,mzalendo na aliyetamani kuiona nchi yake inaendelea.Pamoja na kuwa falsafa yake ya azimio la Arusha ilikuwa ni safi na bado itaendelea kuwa safi lakini viongozi wenzake hawakuielewa ama kama walielewa basi kwa makusudi hawakutaka kuiamini , kwani ilikuwa inawabana wao. Azimio la Arusha likabakia kuwa la kwake na sio la wananchi wala viongozi wenzake na mwishoe likaanguka.


  Kipindi cha nyerere kilikuwa ni kipindi cha ujenzi
  .Makosa ya nyerere ni kile kitu wanafalsafa wanakiita Betsheba syndrome (Makosa ambayo yanafanywa na viongozi bila kuwa na dhamira ovu) .


  MWINYI
  -Hiki ni kipindi ambacho mi nakiita ni kipindi cha maandalizi ya ubomoaji mkuu.Serikali ya wakati huu ilijazwa na viongozi waliokuwa katika awamu ya kwanza.Wengi wao walikuwa ni amateur katika siasa,diplomasia na katika mambo ya uchumi.Baada ya mwalimu kungÂ’atuka na kuwaachia ilikuwa ni sawa sawa na kunyofoa sterling kwenye gari lililoko kwenye mteremko.


  Hiki ni kipindi ambapo serikali iliicha nchi ipigwe na mawimbi ya mabadiriko toka nje bila kuweka kingo za kuzuia.Viongozi waliokuwepo walianza kutumia nafasi zao kujiendeleza wao binafsi na kusomesha watoto wao nje ya nchi.Ni katika kipindi hiki miiko ya uongozi ilikufa na tamaa ya uroho wa madaraka ikajengeka kwenye mioyo ya viongozi.Kila kitu kilikuwa ruksa,wizi ruksa,rushwa ruksa,ubadhirifu wa mali ya umma ruksa.Kwa kifupi matatizo yote ya nchi yetu chimbuko lake ni kipindi hiki.


  MKAPA
  -Mkapa alilirithi nchi ambayo tayari ilikuwa imeanza kubomoka.Katika kipindi hiki dunia ilikuwa inapitia mabadiriko makubwa ya kisayansi na kisiasa na ambayo yalikuwa yanakwenda kwa kasi ya ajabu.Kipindi hiki Tanzania ilikuwa inahitaji kiongozi mwenye fikra na maono makubwa ya kuweza kukabiliana na changamoto hizi.Mkapa alikuwa na kila kitu katika hayo ingawa alikuwa aaminiki kwa wananchi.


  Kipindi cha Mkapa Tanzania ilishuhudia mabadiriko makubwa ya sera za uchumi,hasa katika swala la ubinafsishaji.Kwa mtu yoyote atakubaliana na mimi Ubinafsishaji katika kipindi hiki ulikuwa ni lazima.Lakini jinsi gani ulivyofanywa linabaki kuwa swali la mjadala ambalo linauzunguka uongozi wa mkapa.Kwa wale wanaopinga sera za ubinafsishaji wanafanya kosa kusahau kuwa mashirika mengi ya umma yalikufa kibudu wakati wa kipindi cha Mwinyi.Kwa hiyo ni dhambi kusema hakukuwa na haja ya kubinafsha kwani katika kipindi cha nyerere mashirika haya yalikuwa yanafanya vizuri,ni kweli yalikuwa yanafanya vizuri lakini je katika kipindi cha mwinyi?


  Mazuri ya Mkapa ni kuwa katika kipindi chake hali ya maisha ilikuwa nafuu.,bei ya vitu muhimu zilikuwa chini,Ujenzi wa miundo mbinu ilianza kujengwa kwa wingi,kodi ya kichwa ikafutwa,MEM,MES,TASAF vilianzishwa (ambavyo kama vingeendeshwa vizuri vingekuwa chachu ya maendeleo makubwa)


  Mabovu ya mkapa ni yeye mwenyewe kujihusisha na biashara wakati bado yuko ikulu na kushindwa kudhibiti ufisadi ambao ulikuwa unatendeka wenda kwa yeye kujua ama pasipokujua,Haya ni makosa yanayomgharimu na kufunika mazuri yake.Mkapa alikuwa ni kiongozi bora aliyeweza kukabili vyema mabadiriko makubwa ya dunia kwa ufanisi mkubwa.Mkapa alikuwa na kila kitu cha kumfanya aweze kukumbukwa lakini alijisahau akatumia kipaji chake chini ya kiwango,alikuwa amekirimiwa mengi na watanzania walihitaji mengi kutoka kwake, ambayo akuyatoa.Hili analijua na si kwamba hajutii makosa yake tatizo ni mgumu kukubali na hiyo ni hulka yake.


  Kwa fikra zangu mkapa anauweo wa kuwa kiongozi wa taifa lolote la ulaya,kipindi chake mi nakiiita kipindi cha Marekebisho makuu japo yana kasoro zake.


  KIKWETE
  -Kikwete aliingia madarakani huku watanzania wakiwa na imani kubwa kwake zaidi ya viongozi wote waliotangulia.Angeweza kutumia ushawishi wake kuwaongoza wananchi katika mabadiriko makubwa kabisa kuwahi kutokea, kama angekuwa na maono ya kimaendeleo.


  Kikwete ni Kati ya viongozi ambao wanatamani kuwa viongozi lakini hawajui kwa nini wanataka kuwa viongozi au watafanya nini wakiwa viongozi.Bahati mbaya afrika imejaa viongozi wa namna hii.Hawa ni sawa na mtu mwenye hamu ya kusafiri ila hajui wapi anatakiwa kwenda.


  Serikali ya kikwete imejazwa na watu wasio na fikra za kutatua matatizo,wengi wao ni watu wenye tabia kufunika moto kwa blanketi ilimradi usionekane.Na kwa kuwa uwezo wao wa kupambana na changamoto za dunia hii ni haba wamekuwa ni mabingwa wa kutoa visingizio kila pale mambo yanapokwenda mlama.


  Kwa sasa hali ya kiuchumi ni mbovu,mfumuko wa bei unatisha,huduma za afya ni duni,Elimu inashuka kila kukicha,vyuoni idadi ya wanaozidi kukosa mikopo inaongezeka na hata wale wanaopata fedha zinachelewa.Bahati mbaya hakuna jitihada zozote zinazoonekana za kutatua kero zinazoonekana.Wengi wetu tunaendelea kuamini kuwa hata vurugu zilizotokea Zanzibar zinasababishwa na muungano ama udini mimi siamini hivyo.Katika dunia hii chanzo cha matatizo yote ni hali ngumu ya uchumi.Kunapokuwa na hali ngumu ya kiuchumi ndipo vikundi vya kidini na kikabila vinazuka na kuona vinaonewa.


  Kipindi cha kikwete mimi nakiita ni kipindi cha kushika kasi kwa Ubomoaji mkuu.Na ni lazima jambo Fulani lifanyike kuzuia kasi hii ambayo italidondosha kabisa taifa na kulitupa katika umasikini wa kutupwa


  JE KUNA MATUMAINI 2015 NDANI YA CCM?


  Jawabu ni rahisi na linapatikana kwa kuangalia wanaokibeba ccm kwa sasa na wale wanaopigiwa chapuo kugombea uraisi.

  Je Samweli Sita,Mwakyembe,Magufuli,Lowasa,Membe na wengine wanauwezo wa kupambana na changamoto za dunia hii inayobadirika kwa kasi,Jibu langu ni hapana,wote hao hakuna hata moja aliyeonyesha kuwa ana uwezo wa kupambana na dunia inayohitaji kutumia ubongo zaidi katika kuleta maendeleo.I hold a soft center kwa Magufuli ingawa najua Tanzania ya sasa inahitaji mtu zaidi yake ila nahusifu utumishi wake uliotukuka.Ukitazama ndani ya CCM hakuna kiongozi hata moja katika utumishi wake ameshafanya mambo kimapinduzi wote fikra zao ni zile zile,wanatumia fikra hizo hizo katika kutatua matatizo yale yale yaliowashinda awali


  Kwa kifupi hakuna tumaini ndani ya CCM, sio wenyewe wala watoto wao (kina makamba,riziwani,nnauye,malisa, malechela n.k)wanaorithishwa chama wanaweza kubadirisha yanayotokea.Kwani na wao wamerithi fikra zisizoweza kutatua matatizo jaribu kuangalia kwa kina utabaini

  Swali ni je Mkapa anaweza kuwa mtu atakayeiokoa CCM na Tanzania Kwa ujumla 2015 au labda kuna mwingine?
   
Loading...