Nyerere na Kikwete mababa wa Kisiwa cha Pemba

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,992
Katika maraisi ambao unaoweza sema ni mababa wa kisiwa cha Pemba ni Nyerere na Kikwete.Hawa watu waliwapenda mno watu wa kule japo hawapendeki.Wakati Karume alipokuwa akiwavurumusha wapemba wakati wa mapinduzi na baada ya mapinduzi Nyerere aliwapa hifadhi Tanzania bara na kuingia muungano na Zanzibar ili kuwawezesha wapemba wasije kumalizwa na majambia Zanzibar waishi popote Tanzania bara.

Wapemba wengi wakanusurika, maisha yao yakanusurika na biashara zao zikanusurika kwa kupewa nafasi za kuishi bara.Nyerere pia ndiye alijitosa kuwalea wapemba kisiasa .Ndiye aliyelea Wapemba kisiasa kama akina Abdulhaman Babu,salim ahmed Salim, Seif shariff Hamad nk ambao watu kama akina Karume na sheikh Thabit Kombo walikuwa hawawataki.Nyerere akawalea wee hadi basi.

Shukrani waliyomlipa nyerere ni nini? Wapemba akina Mohamed Said na wasomi kama akina Professor Haroub Othman na Akina Seif sharif Hammad nk walianza kuuponda muungano na kumponda Nyerere waziwazi kwa maandishi,matamshi na vituko vya kisiasa

Mtu mwingine ambaye ni Baba wa Kisiwa cha Pemba ni Kikwete.Allipokuwa katika kampeni za uraisi aliahidi kulimaliza tatizo la kisiasa zanzibar.Kweli aliposhika akasema kuwa Wazanzibari wasiwe watumwa wa historia akahangaika mpaka akafanikisha kwa mara ya kwanza kupatikana Raisi Mpemba ambaye ni Dk Shein na Makamo wa rais Mpemba Seif Sharif hamad.Haikuwa kazi rahisi kwake lakini alifanikisha.Lakini pamoja na juhudi zake zote hizo bado hawana shukrani hao wapemba wamekuwa wakimlaani kuwa ndiye chanzo cha mgogoro wa Zanzibar!

Mimi kwa maoni yangu nadhani wana laana za baba zao Nyerere na Kikwete ambao wameshindwa kuwaheshimu ndio maana mambo yao mengi hayaendi vizuri.

Ni vizuri wawe na siku ya kuwaenzi baba zao Nyerere na Kikwete badala ya kuwatukana kila wakati wanachuma laana
 
Me hayo mengine sina uhakika nayo nahis nilikuwa mdogo kipindi hicho ila kwa sasa lililo mbele yetu nililolishuhudia ni utawala wa kimabavu uliofanywa na ccm waziwazi hilo ndio naweza kusimulia kizazi changu
Mlaaniwe ma ccm
 
Katika maraisi ambao unaoweza sema ni mababa wa kisiwa cha Pemba ni Nyerere na Kikwete.Hawa watu waliwapenda mno watu wa kule japo hawapendeki.Wakati Karume alipokuwa akiwavurumusha wapemba wakati wa mapinduzi na baada ya mapinduzi Nyerere aliwapa hifadhi Tanzania bara na kuingia muungano na Zanzibar ili kuwawezesha wapemba wasije kumalizwa na majambia Zanzibar waishi popote Tanzania bara.

Wapemba wengi wakanusurika, maisha yao yakanusurika na biashara zao zikanusurika kwa kupewa nafasi za kuishi bara.Nyerere pia ndiye alijitosa kuwalea wapemba kisiasa .Ndiye aliyelea Wapemba kisiasa kama akina Abdulhaman Babu,salim ahmed Salim, Seif shariff Hamad nk ambao watu kama akina Karume na sheikh Thabit Kombo walikuwa hawawataki.Nyerere akawalea wee hadi basi.

Shukrani waliyomlipa nyerere ni nini? Wapemba akina Mohamed Said na wasomi kama akina Professor Haroub Othman na Akina Seif sharif Hammad nk walianza kuuponda muungano na kumponda Nyerere waziwazi kwa maandishi,matamshi na vituko vya kisiasa

Mtu mwingine ambaye ni Baba wa Kisiwa cha Pemba ni Kikwete.Allipokuwa katika kampeni za uraisi aliahidi kulimaliza tatizo la kisiasa zanzibar.Kweli aliposhika akasema kuwa Wazanzibari wasiwe watumwa wa historia akahangaika mpaka akafanikisha kwa mara ya kwanza kupatikana Raisi Mpemba ambaye ni Dk Shein na Makamo wa rais Mpemba Seif Sharif hamad.Haikuwa kazi rahisi kwake lakini alifanikisha.Lakini pamoja na juhudi zake zote hizo bado hawana shukrani hao wapemba wamekuwa wakimlaani kuwa ndiye chanzo cha mgogoro wa Zanzibar!

Mimi kwa maoni yangu nadhani wana laana za baba zao Nyerere na Kikwete ambao wameshindwa kuwaheshimu ndio maana mambo yao mengi hayaendi vizuri.

Ni vizuri wawe na siku ya kuwaenzi baba zao Nyerere na Kikwete badala ya kuwatukana kila wakati wanachuma laana
tatizo sugu sio upemba na uunguja. naogopa hata kutaja. kuwa na historia ya mtumwa ni balaa ndio maana hata chotara roho haitulii akikuona mwafrika unajidai mtwana.
 
halafu wanasema historia haina sehemu katika matatizo yanayoikumba zanzibar. hili ni kosa kubwa. kuwapa ushindi walioshinda uchaguzi linaweza kuwa suluhisho lakini kwa hali ilivyo litaambatana na gharama kubwa. tusubiri tuone.
 
Tatizo la wengi kama siyo baadhi humu Tunapenda "KUJUUMUISHA/KUJUMLISHA" Kimaadili unapotoa rai yako UJUWE SIYO WOTE !!!

@Kmbwembe
YEHODAYA Yapo ya kweli na yapo ya kuzusha..... JUST LET US BE FAIR !!!
 
tatizo sugu sio upemba na uunguja. naogopa hata kutaja. kuwa na historia ya mtumwa ni balaa ndio maana hata chotara roho haitulii akikuona mwafrika unajidai mtwana.
Sasa ndugu yangu nawe roho yako haijatulia kwa kuwa Umeanza kwa UCHOTARA !! tujifunze kuwasilisha hoja !!
 
Pole, usilolijua ni usiku wa kiza. Nilidhani mtoa mada angeliona kusema kuwa "' eti mambo ya Wzanzibari hayaendi vizuri !" unajidanganya. Elewa kuwa kwa uwiano, mzanzibari ana maisha mazuri zaidi ukulinganisha na Mtanganyika mmoja mmoja.

1 Nyerere kwetu ndio chanzo cha kuiangamiza Zanzibar. Alikuwa chanzo cha kukisambaratisha chama cha wazanzibari asilia SHIRAZI ASSOCIATION na kutengeneza chama ASP ambacho kilipoteza mahaba na mvuto kwa wazanzibari tokea ukolioni. Shirazi Association kilipomeguka ndio kikazaa ZPPP ambacho kilifanya UKAWA na chama cha ZNP kukiangusha chama cha ASP
2. Kikwete sio alioleta muafaka Zanzibar. Msanii hawezi kuleta jambo adhimu na ya kukumbukwa milele. Walioleta mwafaka Zanzibar ni Karume na Seif Sherif, Kwa ufupi ni wazanzibari wenyewe!
3.Wagombea wote wa Urais wa JMT kupitia CCM hawajawahi hata mara moja kupata kura zaidi ya mgombea wa Urais wa JMT kutoka upinzani.
4 Wapemba kimaumbile ni watu wenye akili sana na wanajua kuzitumia hasa panapo majuha

KWETU SISI WOTE HAO NI MAJANGA TUi
 
Mtowa mada sipendi kutumia lugha Kali kumbuka tu wapemba hawapo Tanganyika tu Mpemba yupo kila mahali katika dunia yetu ni watu makini wanajielewa na hawakubali kuyumbishwa na sijambo zuri kukubali kila kitu hatakama hakina maslah Na moja ya sifa ya Mpemba haogopi MTU akikwambia SEBU ujuwe sebu kweli
 
Pole, usilolijua ni usiku wa kiza. Nilidhani mtoa mada angeliona kusema kuwa "' eti mambo ya Wzanzibari hayaendi vizuri !" unajidanganya. Elewa kuwa kwa uwiano, mzanzibari ana maisha mazuri zaidi ukulinganisha na Mtanganyika mmoja mmoja.

1 Nyerere kwetu ndio chanzo cha kuiangamiza Zanzibar. Alikuwa chanzo cha kukisambaratisha chama cha wazanzibari asilia SHIRAZI ASSOCIATION na kutengeneza chama ASP ambacho kilipoteza mahaba na mvuto kwa wazanzibari tokea ukolioni. Shirazi Association kilipomeguka ndio kikazaa ZPPP ambacho kilifanya UKAWA na chama cha ZNP kukiangusha chama cha ASP
2. Kikwete sio alioleta muafaka Zanzibar. Msanii hawezi kuleta jambo adhimu na ya kukumbukwa milele. Walioleta mwafaka Zanzibar ni Karume na Seif Sherif, Kwa ufupi ni wazanzibari wenyewe!
3.Wagombea wote wa Urais wa JMT kupitia CCM hawajawahi hata mara moja kupata kura zaidi ya mgombea wa Urais wa JMT kutoka upinzani.
4 Wapemba kimaumbile ni watu wenye akili sana na wanajua kuzitumia hasa panapo majuha

KWETU SISI WOTE HAO NI MAJANGA TUi

Mkuu kama walioleta muwafaka Zanzibar ni wazanzibar wenyewe kwa nini sasa hivi anaombwa Mh .Magufuli aingile kati?
 
Back
Top Bottom