Nyerere na Kawawa

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,769
2,000
Siku moja Mwalimu alienda London na Waziri Mkuu wake Mzee Kawawa, Malkia akawafanyia State Banquet. Waandishi wa habari walikuwemo ndani ya ukumbi kumhoji Mwalimu juu ya mambo mbali mbali kuhusu jinsi atakavyoiendesha nchi hii changa Tanganyika. Muda wote huu mlo unaendelea na kwa kuwa wote walikaza macho kumsikiliza Mwalimu Mzee kawawa akatumia mwanya huo kuweka mfukoni uma mbili na vijiko viwili na visu viwili vyote vikiwa ni vya dhahabu. Wakati huo Mwalimu alikuwa anamuona.
Katika hotuba yake akagusia mila na desturi za kiafrika hususan mazingaombwe akasema:
"Kwetu Afrika kuna watu mbali mbali wa utaalamu asilia", akaomba msaidizi mmoja amletee uma mbili, vijiko viwili na visu viwili. Akaendelea Hivi vijiko nilivyo navyo mfukoni ninaweza nikaviweka mfukoni mwangu halafu mkavikuta kwa Kawawa. Akaviweka halafu akasema "Kawawa toa vijiko vyote".
Kawawa akatoa automatically Mwalimu akawa amehamisha vijiko toka kwa Kawawa kwenda kwake, Kawawa akakaa kimya. Akarudi navyo nyumbani.

LOL
 

Mtaalam

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
1,320
1,250
hahahahaaaaa...vitu kama hivi ni muhimu sana kurelax mbavu zetu after kukerwa na mengi...senx bubu
 

Shukuru

JF-Expert Member
Sep 3, 2007
749
0
ha ha ha ha, kwanza hii unaweza kuinipa in media form? kwi kwi kwi..

Sipati picha baadae hisabu ya vijiko na umma kwa ma-store keeper!


Oooops ni Kesi kubwa!!
 

Kithuku

JF-Expert Member
Nov 19, 2006
1,398
1,250
Tulipokuwa shule kulikuwa na hadithi nyingi za masikhara zikiwahusu Nyerere na Kawawa, na hasa Kawawa alitaniwa zaidi. Wakati wa mapumziko shuleni katika kupiga soga watu walikuwa wanapeana zamu kusimulia vituko vya Nyerere na Kawawa.

Iko hadithi moja wanamtania Kawawa eti alikwenda Ulaya akiwa amefuatana na viongozi wenzie miaka hiyo, Michael Kamaliza, Bibi Titi Mohamed na wengineo. Basi wanadai wakati wa kuwatambulisha akasema "This is Mr Ka-finish and this is Mrs Breast...."
 

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
4,220
2,000
wadau hivi ile habari kwamba Nyerere(RIP) alimwambia Kawawa(RIP) afunike kikombe kwenye mkutano aliokuwa akihutubia huko nje ya nchi zilikuwa za kweli? mara nyingi nimekuwa nikijiuliza hili.
 

Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,293
1,250
wadau hivi ile habari kwamba Nyerere(RIP) alimwambia Kawawa(RIP) afunike kikombe kwenye mkutano aliokuwa akihutubia huko nje ya nchi zilikuwa za kweli? mara nyingi nimekuwa nikijiuliza hili.

Pumba!
 

Chimunguru

JF-Expert Member
May 3, 2009
10,649
2,000
Ulikuwa utani ule. Kweli SImba wa Vita alitaniwa sana enzi zile hahahahhhahaha
 

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
6,802
2,000
Jamani mnalikumbuka hili? Je lilikuwa na ukweli wowote? Nauliza tu, na kama kuna anajua zaidi atujulishe.
 

superfisadi

JF-Expert Member
May 22, 2009
553
195
mm nilikuwa nadhani kweli nilishangaa nilipokuja kubaini kawawa alienda shule ,uongo unasambaa kwa kasi kuliko ukweli
 

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,037
2,000
Ina maana wa2 wamesemaga uwongo kivile? Na ukizingatia enzi hiyo wa2 walikuwa makini kutowasema viongozi wao vibaya si kama kizazi hiki cha leo wasio na hekima. Kwa kweli mi nasema hiyo ilikuwa kwa true na ukizingatia Kawawa ana elimu ya darasa la pili ya ukoloni miaka ya 1948-49 ni elimu fupi sana. Kwa hyo thread ya jamaa ni ya ukweli.
 

mashikolomageni

JF-Expert Member
Jan 5, 2010
1,568
1,250
Kawawa hakuishia darasa la 2, ukisoma historia vizuri kawawa amesoma Tabora huko alikuwa shule ya Sekondari alikuwa anazungumza kiingereza vizuri. Hizo zilikuwa story za vijiweni tu
 

Bobo Ashanti

Member
Nov 4, 2010
49
0
Kawawa hakuishia darasa la 2, ukisoma historia vizuri kawawa amesoma Tabora huko alikuwa shule ya Sekondari alikuwa anazungumza kiingereza vizuri. Hizo zilikuwa story za vijiweni tu
Na watu wengi walimchukulia mzee Kawawa kuwa hajasoma kutokana na ile character aliyoigiza katika sinema ya 'muhogo mchungu' enzi za 19kweusi akiwa mwajiriwa wa idara ya ustawi wa jamii.Hata hicho kituko kilikuzwa kutokana na dhana kuwa hakufuta umande.Kumbuka mzee Kawawa alikuwa muasisi wa chama cha wafanyakazi Tanganyika.
 

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,321
2,000
kamuulizeni vita!hata wengine humu babu zenu hawakwenda skul,cha msingi walitukwamua kwenye ukoloni wether thewere educated or not!!
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
61,089
2,000
Hayo mambo kama yalitokea ulaya, ni nani mmbeya aliyekuja kuvujisha siri huku nyumbani
 

mzee74

JF-Expert Member
Sep 17, 2011
11,078
2,000
Ilitokea safari moja Nyerere alienda ughaibuni na Kawawa na kufika huko wakakirimiwa kwa kahawa.Walikunywa pamoja hadi ikatokea Nyerere kutosheka akaamua kufunika kikombe isipokuwa Kawawa utaratibu wa kufunika kikombe yeye hakuujua hivyo akawa anaweka mezani kikombe kinajazwa tena naye kwa aibu aliendelea...
kunywa hadi Nyerere alipomwambia Kawawa funika kikombe!Watakuuwa😁


Wakati wa kulala kila mtu chumba chake Kawawa kaingia chumbani hakuona kitanda akalala sakafuni.Asubuhi Nyerere akaja kumtazama na kumuuliza ulilala wapi na yeye akamwambia sakafuni! Nyerere akabofya ukutani kikatokea kitanda.Kawawa akabaki kushangaa!😁
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom