Nyerere na Kawawa wangeanza ufisadi 1961 leo mafisadi wangekuta nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere na Kawawa wangeanza ufisadi 1961 leo mafisadi wangekuta nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sulphadoxine, Dec 30, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  TANGANYIKA na hatimaye Tanzania bara kama inavyojulikana sasa ni sehemu ya nchi za ambayo ilitawaliwa na wakoloni, baadhi kwa muda mfupi na wengine wakiitawala kwa muda mrefu.

  Wakoloni wa awali walikuwa Wareno hawa kwa kiwango fulani wanahesabiwa kuwa walikuwa wapita njia kwani waliweka vituo wakiwa safari kwenda Mashariki ya mbali.

  Hatimaye walikuwa Waarabu ambao sio kwamba tu walitawala hususani ukanda wa pwani bali pia walijihusisha na biashara ya utumwa, jambo linalodhihirishwa na sehemu za kihistoria za Bagamoyo (Bwagamoyo) na Zanzibar ambako lilikuwepo soko kuu la watumwa.

  Baada ya hapo, kufuatia mkutano wa nchi za Ulaya uliofanyika Berlin himaya mbalimbali za Ulaya ziliigawa Afrika katika vipande vipande na kipande kilichotajwa kuwa ni Tanganyika kiliangukia mikononi mwa Wajerumani.

  Kuanguka au kushindwa kwa Ujerumani kwenye Vita Kuu ya Pili ya Dunia kulizifanya himaya ilizokuwa inazitawala kuangukia mikononi mwa Waingereza na hivyo ndivyo ilikuwa kwa Tanganyika kutawaliwa na Waingereza.

  Kila mkoloni alikuja na lengo lake lakini manufaa ya kiuchumi yalikuwa ndio kipaumbele cha kila mkoloni. Leo hii Waafrika tunaposoma historia iliyoandikwa na wakoloni hao tunajiona kama binadamu wa kiwango cha chini zaidi katika dunia hii.

  Wasomi wa Kiafrika katika fani ya historia baadhi wamejitahidi kuiandika historia ya Mwafrika kuanzia enzi za himaya, kutawaliwa na kupambana kupatikana kwa uhuru.

  Wanahistoria kama Profesa Adu Boahen, aliichambua historia kwenye ukanda wa Afrika Magharibi na hilo linajibainisha kwenye kitabu chake “Topics History of West Africa” na Dk. Walter Rodney ambaye kupitia kitabu chake cha “How Europe Underdeveloped Africa” anabainisha mengi yaliyofanywa na watawala wa kikoloni katika kurudisha maendeleo ya bara hili nyuma.

  Haiyumkiniki kwamba wapo wanahistoria wanaoendelea kufanya tafiti mbalimbali ili kuiweka kwenye mkondo sahihi zaidi na kuibua mengi zaidi yasiyopotosha kama ilivyokuwa na historia iliyoandikwa na wakoloni kuhusu Afrika na Mwafrika mwenyewe.

  Pamoja na kuwepo upotoshaji mkubwa wa historia iliyoandikwa na wakoloni wa Ulaya, kitu kimoja kinaonekana wazi leo hii katika Bara la Afrika. Ukweli huo ni kwamba Mwafrika mweusi hususan viongozi wengi wa siasa hawajalifanyia mema Bara la Afrika katika kipindi cha miaka 50 iliyopita toka Ghana, nchi ya kwanza Afrika kupata uhuru wa bendera mwaka 1957.

  Lakini hii haina maana kwamba hakuna viongozi weusi waliofanyia mema nchi zao au kujitahidi kufanya mema. Wapo akina Kwame Nkrumah wa Ghana, Patrice Lumumba wa Congo Kinshasa, Julius Nyerere wa Tanzania, na Kenneth Kaunda

  Viongozi hawa wema walikuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi wakati walipopata madaraka miaka ya mwishoni mwa 1950 na mwanzoni mwa 1960. Afrika bado ilikuwa na wakoloni wakongwe, katika nchi kadhaa baadhi ya walowezi kama ilivyokuwa Zimbabwe na Afrika Kusini walishajitangazia uhuru. Walikumbana pia na vikwazo mbalimbali toka nje ya Afrika na hususani kutoka kwa nchi zilizokuwa zinanufaika na makoloni.

  Lakini jambo muhimu kwa viongozi waliotangulia lilikuwa ni ukombozi wa kisiasa na kiuchumi kwa Mwafrika mweusi. Umuhimu wa kuleta ukombozi wa kiuchumi kwa Mwafrika haupo tena kwa viongozi wengi wa Afrika hivi sasa. Wengi wanahubiri maneno mazuri sana ya kuleta faraja kwa raia lakini maneno yao ni kinyume kabisa na matendo yao.

  Mfano halisi ni tatizo la ufisadi hapa Tanzania. Hakuna Mtanzania makini asiyekumbuka jinsi uchaguzi wa Rais na Wabunge ulivyokuwa na ushindani mkubwa mwaka 1995. Mfumo wa vyama vingi uliorudishwa rasmi 1992 ulileta upinzani mkubwa kwa chama tawala-CCM.

  Viongozi wa CCM walipata shida kubwa kumnadi mgombea urais wa CCM Oktoba 1995, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, kwani ilibidi Mwalimu Julius Nyerere asaidie kampeni za uchaguzi wa rais ili Mkapa asishindwe na wapinzani wake wakati huo, Augustino Mrema, John Cheyo na Ibrahim Lipumba.

  Mwalimu alisema anampigia kampeni Mkapa kwa sababu anamfahamu kama ni mtu "safi”. Naye Mkapa akiwa ni mwanafunzi wa sekondari wa Mwalimu Nyerere, alijua fika jinsi ya kucheza karata zake vizuri ili afike ngazi za juu za uongozi. Awali alikuwa muumini mkuu wa Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea iliyoasisiswa na Mwalimu Nyerere. Alikuwa kundi la watekelezaji mahiri wa siasa hiyo kwa kupiga propaganda kali huko Ulaya Kaskazini, Asia na Marekani akiwa balozi na hata awali akiwa mhariri wa gazeti la The Nationalist.

  Hata alipokuwa anatafuta kuteuliwa na CCM kugombea urais, Mkapa alikuwa na wapenzi wachache sana ndani ya CCM lakini alitumia vizuri karata zake kwa Mwalimu Nyerere hadi akaaminika na kuitwa "Mr. Clean”.

  Alipoteuliwa kugombea urais, Mkapa alifanya kampeni zake kwa ahadi za kupambana na rushwa bila woga akiwa rais. Na kwa hakika alipoapishwa tu Oktoba 2005, Mkapa alianza kutangaza mali zake kama mfano wa kuzuia tamaa za viongozi kujitajirisha. Alifuatiwa na viongozi wengine wakiwemo mawaziri, wakuu wa mikoa, makatibu wakuu wa wizara, wabunge na kadhalika. Polepole Mkapa alianza kupata umaarufu na kujiimarisha madarakani kwa kuunda Tume ya Kutathmni Kero za Rushwa chini ya Jaji Joseph Warioba mwaka 1996. Hatua hiyo ilitanguliwa na zoezi la kutangaza mali ambapo Mkapa alikuwa kinara.

  Hatimaye Serikali ya Mkapa ilipeleka mswada katika Bunge kuunda sheria ya Usalama wa Taifa mwaka 1996. Wakati huo alishatoa takrima kwa maofisa waandamizi wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) na Idara ya Usalama wa Taifa kwa njia ya mikopo ya kununua magari ya kifahari. Hiyo ilikuwa mbinu ya kujipatia umaarufu katika vyombo vya ulinzi na usalama.

  Mkapa aliendelea kujijenga kwa wafadhili wa nje kwa kuanza kukusanya kodi na kulipa madeni na kukataza kabisa Benki Kuu kuchapisha sarafu au noti zenye picha yake. Taarifa za Benki ya Dunia zinaonesha kwamba katika kipindi cha miaka 10 (1995-2005), Serikali ya Tanzania ilipewa mikopo zaidi ya misaada. Uhodari na uaminifu alioonesha Rais Mstaafu Benjamin Mkapa katika kulipa madeni ya nje ulikuwa ni kivutio kikubwa kilichowatia moyo wa ‘huruma’ wafadhili (wakopeshaji) wengi kukubali kutoa mikopo mingine.

  Katika kipindi hiki (1995-2005) serikali ilinunua magari mengi sana ya kifahari (Toyota Land Cruser VX au “mashangingi”) kwa mapato ya kodi kuliko kipindi chochote cha utawala toka nchi kupata uhuru. “Shangingi” moja linauzwa zaidi ya shilingi milioni 60.

  Lakini ung’ang’anizi wa ununuzi wa mashangingi hayo umekuwa unaendelea hadi sasa na hata kuingia kwa wabunge ambao wamepewa kwa mikopo yakiwa yamepanda bei hadi kufikia milioni 80/- hadi 90/-.

  Hata hivyo, linapokuja suala la vyombo vya usafiri kwa kina mama wajawazito zinatolewa ambulance za Bajaj ambazo kama ni kwenye mazingira ya vijijini ambapo miundombinu ya barabara ni mibovu haiyumkiniki kiumbe kinachotarajiwa kuzaliwa kinaweza kisivute pumzi ya dunia hii.

  Matumizi haya yaliambatana na kuibuka kwa majumba ya kifahari mbali na yale ya umma kama PPF Tower, Mafuta House, NSSF Nyerere Tower, NIC Ubungo Plaza, NSSF Water Front, Millenium Tower, PPF House, na BoT Twin-Tower pia yapo ya watu binafsi, bnaadhi wakiwa viongozi serikali ambayo vyanzo vya mapato yao ni vigumu kuvielewa ndio kwanza yalishamiri.

  Hapa ndipo viongozi wetu walianza kuwapa kisogo maskini walipakodi waliowachagua na kujiingiza kwenye taswira inayofana na viongozi wa nchi zilizoendelea.

  Yaliyojitokeza ni pamoja na ununuzi wa rada ambayo imekuja kubainisha kuwa kuna rushwa iliyotembea kwenye ununuzi wake ambayo imekuwa ikipambanuliwa kama ‘vijisenti’.

  Katika mazingira mengine likaja suala la ununuzi wa ndege ya rais hii hakuna aliyewahi kusema kama inatembea au imepelekwa wapi. Lakini pamoja na hali hiyo ununuzi wake ni sawa lakini kilichosikitisha ni kauli iliyotolewa na Waziri wa Fedha wakati huo, Basil Mramba, akitetea ununuzi wa ndege hiyo akisema kuwa lazima inunuliwe ikibidi hata wananchi waliokuwa wanakabiliwa na uhaba wa chakula waendelee kutaabika kwa kula nyasi.

  Hata hivyo, ni kwenye mazingira hayo pia wawekezaji kwenye sekta ya madini waliendelewa kupewa maeneo yenye madini kwa kutoa mirahaba ya asilimia 3.0 tu kwa serikali.

  Baadaye ukaja ukwapuaji wa fedha kutoka kwenye akaunti ya malipo ya nje (EPA) ambapo bilioni 133/- zilichukuliwa kwa njia ya kughushi.

  Katika mazingira haya na hususani baada ya kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika ni lazima kutafakari na kujiuliza maswali mengi ambayo ni, “Kama Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Rashid Kawawa wangeanza ufisadi wa kiwango hicho Tanganyika ilipopata uhuru 1961, na kuendelea nao hadi walipostaafu baada ya miaka 24 (1985), je, leo hii kuna mtu na hususani mafisadi angekuta chochote cha kuiba?

  Lipo jambo ambalo wengi wanafikriria kuwa Mwalimu alikuwa hazijui rasilimali hizi dhana ambayo ni potofu kwani madini yanayochimbwa sasa Mwalimu Nyerere na Mzee Kawawa walikuwa na habari nayo toka 1961 lakini wakayaacha salama na mengine kuyalinda kwa kutumia majeshi. Je, wangeanza kuyachimba wakati huo tungekuwa na migodi inayoneemesha watu wachache leo hii?

  Tutafakari kwamba tunapotapanya urithi tulioachiwa si kujitafutia laana. Je, vizazi vijavyo havitalazimika kufukua makaburi yetu baada ya kukuta mashimo yaliachw ana wachimbaji ili kuangalia mbongo zetu zilikuwaje hadi kuachia utajiri wa nchi kufadiwa na watu wachache? Lakini tukiutumia vizuri raslimali zetu hizi, kwa kuzisimamia vizuri hata kuanzia sasa kwa sababu hatujachelewa sana, bila shaka miaka 50 ijayo ya Tanzania itakuwa ni ya neema na baraka tele.
   
 2. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Nyerere na Kawawa hawakuwa wajanja kama akina Kikwete
   
 3. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,019
  Trophy Points: 280
  Nchi haifilisiki, hata waibe vipi na msitulazimishe kuamini nyerere na kawawa ndio walikuwa hawapigi hela.
  Mbona kawawa ana mijumba kibao na wake wengi na watoto kibao? Nyerere alijijenga mwenyewe ili mumtukuze kwa gharama za serikali.
  Mbona walikuta nchi masikini wamekufa wameiacha masikini.
   
 4. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Ujanja kwa tafasiri ya kibongo ni 'wizi'.... Nyerere na nduguye Kawawa walikuwa na fursa hiyo tena kipindi hicho watz walikuwa wamelala fofofo, leo pamoja na kuelevuka kwetu tunawaacha wakora wakipora kila kilicho mbele yao.

  Tumerogwa....
   
 5. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Utawajua tu makuwadi... Estate moja tu ya Mkapa inakusanya utajiri wote alokuwa nao Mzee Kawawa pamoja na ukoo wake.

  Kama ni wakili umeitwa kuwatetea waporaji wa mali za wanyonge inabidi uwe na akili ya mwendawazimu kujenga utetezi huo.
   
 6. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hizi zako ndio akili za shule za kata. Kusema nchi haifilisiki ni mtindio wa ufahamu na ni kichekesho. Kwa taarifa yako, Tembo wakiuawa na pembe zake kuuzwa nje hao tembo baada ya muda fulani watatoweka. Madini yanayochimbwa ardhini mwetu, sio mihogo kusema yatachipua na kukua tena. Kuzorota kwa huduma za jamii kunaimarisha umaskini na ujinga na nchi inarudi nyuma au kukua kwa kasi ndogo isiyoendana na kasi ya ukuaji wa uchumi wa dunia na hivyo tunaachwa nyuma. (Kwa taarifa yako, TANZANIATE tuliokuwa tunajivunia sasa inaelekea ukingoni)

  Unaposema Nyerere alijijenga unamaanisha nini? Nyumba iliyopo Butiama si nyumba ya kutisha ambayo tuseme wewe ukikazana utashindwa kujenga kwa miaka 15. Na hata hivyo alijengewa na JWTZ ili atoke kwenye kile kinyumba chake cha awali. Angekuwa na akili finyu kama tunaowaona, ungekuta amewaweka madarakani wanawe, lkn hakufanya hivyo.

  Kuikuta nchi maskini na kuiacha maskini si maana yake kuwa waliiba. (Sijui kama umeenda shule angalau kidogo ndugu yangu). Hawakuiacha nchi maskini kwani waliiacha ikiwa na deposit ya madini kila kona. Hawa waliopo ndio wataiacha na mashimo baada ya Barrick kuchukua madini na kutuachia 3% yetu.

  Na kuhusu Kawawa, ningekuomba uwe na nidhamu na huyo mzee. Kwangu mimi, Kawawa ndio mfano wa Mwanadamu Mwenye Dini. Hapa unasema mijumba, lkn umejiuliza kama ilikuwa nje ya uwezo wake kiuchumi kuijenga? Baada ya kumaliza kazi ya siasa alianza kulima zake uyoga na kufuga vikuku, mfn mzuri kwa hawa waliopo ambao ukiondoa siasa hawana kingine wananchojua ndio maana wameamua kuwa wezi.

  Kwa kifupi huna POINT zaidi ya kutumwa na mafisadi. Nyerere na Kawawa, safi sana!


  Ya kwake mwenyewe.jpg
  Hii ndiyo Nyumba ya Nyerere ya Butiama akiwa Rais kati ya Miaka ya 60 na 80

  Aliyojengewa na CCM.jpg
  Hii alijengewa na CCM lkn hakuwa akiitumia mpk

  Aliyojengewa na JWTZ.jpg
  Alipojengewa hii na JWTZ baada ya vita vya kagera.
   
 7. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,019
  Trophy Points: 280
  Point nchi haifilisiki, inahita weledi kidogo kudadavua. Nyerere na Kawawa pia si wakubali mie mgonga nyundo wote hawanisaidii ila ukweli utabaki kuwa ukweli.
  Wengine tulikuwepo wakati wao na hakuna nafuu yeyote
   
 8. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #8
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Punguza jazba.
   
 9. g

  germstone jnr Member

  #9
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kwa kweli si haki kusema Mwl. na Kawawa hawakuifanyia hii nchi kitu.Wale wangekuwa na level ya ufisadi hata robo ya waliopo leo,mengi tunayoyaona leo ya kawaida yasingekuwepo.Kwa nia na matendo walijielekeza kupiga vita maadui wao wa ujinga,maradhi na umaskini.hata kama walitumia njia ambayo leo 2nafikiri sio sahihi ya ujamaa na kujitegemea.WATU WALISOMESHWA BILA KUJALI UMRI, NA NI KTK KIPINDI CHA TZ ILIFIKIA KIWANGO CHA JUU CHA KUJUA KUSOMA NA KUANDIKA,tukiongoza barani Afrika,viwanda 2livyogawa kwa wawekezaji uchwara waliovigeuza magodauni ili bidhaa zao za nje zisipate ushindani vingi walijenga wao,migodi ya umeme wa maji walijenga wao,kwenye madini Mwl. hakuwa tayari kupata kidogo na wageni kufaidika zaidi,akataka tujiandae kwanza leo 2nakula 3%! yetu na tunaona swafi!Hawa wazee wangeifisadisha TANGANYIKA tangu awali leo 2ngekuwa taabani zaidi.
   
 10. c

  comte JF-Expert Member

  #10
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 866
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 80
  kumbe hata mitambo ya richmond yetu
   
Loading...