Nyerere, Mwinyi, Mkapa and Kikwete: Leadership Styles and A Lesson to Learn!

Nina wasiwasi na upeo wako wa kufikiri.Hata kama kweli umelipwa kupandikiza udini nchini,unafikiri ni sahihi?Unaonekana upo tayari kutetea ujinga mradi tu mwenye huo ujinga ni dini moja wa wewe.Na upo tayari kupingana na busara yoyote ati kwa kuwa busara hiyo inatoka kwa m2 mwenye dini tofauti na wewe!Kusema kwamba JK alijibu vizuri hilo swali umeonyesha wewe ni mtu wa aina gani.Inaonekana hata ungekuwa wewe umeulizwa hivyo ungeboronga zaidi kuliko hata unaemtetea.Ungesema umeona mito na mabonde kwa akili yako nilivyokusoma.Kama raisi na mgombea anayetetea kiti na ambaye ameshakuwepo madarakani miaka mitano,kwa lile jibu alienda kinyume na mantiki ya swali.Umesema nimefeli shule lakini kutambua swali linataka nini wala haliitaji shahada ya BA.Economics!That's why mwenye elimu hiyo hakulitendea haki swali,hata mimi 'niliyefeli nisingejibu shalow vile'.Iweke akili yako huru usibanwe na udini ndipo utakapoweza kutoa hoja ambazo haziko biased na udini.

Hivi jamaa ni Mchumi, aliahidi kazi kwa watz za kufungua vizibo vya bia. Tehe tehe! Anatwanga safari kwenda kuomba vyandarua in exchange of bars of gold. Kazi kweli kweli
 
kwa hiyo Kikwete amefanya mauaji madogo madogo kama ya Arusha? Toa ushahidi wa kuhusu Mkapa

wewe ndio zuzu kweli kweli, yaani hujui Mauaji aliyoyafanya zanzibar? vikosi vya wajeshi vilitoka bara kwenda kuua, yaani umenikera kiasi kwamba ungekuwa karibu yangu ungechezea kichapo. wewe unasema mauaji ya Arusha mbona husemi kabla ya mauaji akina slaa walihamasisha nini?
 
Nadhani hii mada inakusudia watu watoe maoni yao kuhusu nani ni bogus president ever kati ya hao wanne na si kujadiliana. Kwa mtazamo wangu Kikwete ndio the worst president, kwanza kwa muda mfupi tu aliokaa ofisini (ukilinganisha na wenzake) tumeshuhudia maisha yakizidii kuwa magumu, ufisadi umeeongezeka, ameshindwa kuwawajibisha watendaji wabovu (e.g Hussein Mwinyi kwenye scandal ya Mbagala na Gongo la Mboto), hana vision wala vision katika uongozi wake decisions nyingi anafanya kwa msukumo wa CHADEMA, ameshindwa kujivua gamba wakati yeye ni gamba nambari moja, aliingizwa madarakani kwa ufisadi wa fedha za EPA uliokuwa ukiratibiwa na EL na RA ingawa sasa anawageuka wenzake, amefanya CCM kuwa chama cha kisultani (refer kampeni za uchaguzi mwaka jana, position ya Rizwani UV-CCM na uingizwaji wa Nape Nnauye na January Makamba). Hapa ni miaka mitano tu je atakapomaliza miaka kumi itakuwaje? Kikwete is the bogus president ever on earth!!!!
 
Nimeshindwa kuweka jedwali zuri.

Uzalendo: Nyerere, Mkapa, Mwinyi, Kikwete
Ufisadi: Kikwete, Mkapa, Mwinyi, nyerere
Udictator: Nyerere, Mkapa, Mwinyi, Kikwete
Ubepari: Mkapa, Mwinyi, Kikwete, Nyerere
Utajiri: Mkapa, Mwinyi, Kikwete, Nyerere
Ufalsafa: Nyerere, Mkapa, mwinyi, Kikwete
Matumizi: Kikwete, Mwinyi, Mkapa, Nyerere
Vita na Ubabe: Nyerere, Mkapa, Mwinyi, Kikwete

Kwakweli hawa ni binaadamu wa kawaida, na wana mazuri na mapungufu.:whoo:

Ubarikiwe Sanga
 
Fredrick Sanga

Kati ya vigezo hivyo ufisadi na matumizi mabaya ni vitu vinavyomgusa mtanzania wa kawaida ktk maisha ya kila siku kwani vinasababisha hazina kukauka na upandaji bei wa bidhaa kwa kushuka thamani ya sh. na vile vile ukosefu wa huduma muhimu kwa jamii. Hivyo utasoma mwenyewe nani ni the worst.
 
Last edited by a moderator:
Viongozi wote ni wazuri ndio maana wamekuwa Marais, Hata wewe ukipewa Ikulu utatizamwa kwa mitizamo tofauti. Kuwa na mali ni moja wapo ya kiongozi yeyote barani Africa. Kwani wote huwa wanafanya mazuri tu? Hata mabaya pia huwa tunayafanya ili tuweze kuimarika zaidi.
kiongozi kuwa na mali(pesa nyingi)sio tatizo kaka,tatizo ni namna amezipata na hata Kama utasema analipwa mshahara kwani hana matumizi binafsi?,Pili kiongozi Kama Raisi kukubali kirahisi kutowachukulia hatua baadhi ya viongozi wezi anaoshirikiana nao tumtafsiri vp?Wewe mwenyewe shahidi RICHMOND to DOWANS,IPTL,KAGODA,EPA,SONGASI,malipo ya wafanyakazi hewa(bilion 48),,,,,,,malizia
 
Kati ya vigezo hivyo ufisadi na matumizi mabaya ni vitu vinavyomgusa mtanzania wa kawaida ktk maisha ya kila siku kwani vinasababisha hazina kukauka na upandaji bei wa bidhaa kwa kushuka thamani ya sh. na vile vile ukosefu wa huduma muhimu kwa jamii. Hivyo utasoma mwenyewe nani ni the worst.

Unajua tungesaidiana kutengeneza jedwali zuri zaidi na kuvipa uzito vigezo na mwisho tukawa na weighted matrix. Tungepata mtazamoa mzuri. Hivi ni vigezo vichache tu.
 
EPA, Richmond + Dowans, IPTL, TICTS, TRL, Madini, TUCTA, Udini etc
HE! wewe inaelekea huwezi hata kufikiri tu!Hayo ma EPA,RICHMOND+DOWANS.IPTL,TICTS,TRL,MADINI,TUCTA,UDINI etc yalianzia wakati wa mkapaa ila hayakusikika kwasababu ya udikteta wa mkp,kumbuka,hakuruhusu vyombo vya habari kuhoji wala kutangaza habari zozote zilizoihusu serikali na viongozi wake.Nyerere was the worst president of all.Alitawala WAJINGA WENGI,na WASOMI WACHACHE waliotoka ktk Taasisi za dini ambazo yeye alitoa mchanga mkubwa! badala ya kujenga mfumo wa elimu wa serikali aliyoiongoza!Toka UHURU hadi kufa kwake Chuo kimoja tu! tena chenye wanafunzi wasiozidi elfu kumi!Kwa ushahidi soma kitabu kiitwacho KANISA KATOLIKI NA SIASA YA TANZANIA BARA-1953 hadi 1985. Mwandishi Dr. C.SIVALON M.M.
Nawasilisha
 
Kama ulitegemea kila mtu atajibu "zidumu" baada ya wito wa zidumu fikra mwenyekiti ,sio hapa. Makala iliuliza nani rais mbaya katika marais waliyowahi kutawala na mpaka aliyepo sasa ...Kwahiyo hata (dikteta) Nyerere hata salimika. Kweli ni dhambi kumsema vibaya marehemu. Lakini vilie vile hatuta watendea haki wale wote walio uwawa, teswa na katika utawala wake. Mambo yanayotokea nchi za kiarabu sasa hivi ,ilikua tufanye sisi miaka ile . Lakini kama kawaida yetu bado usingizi mnono. Hawa ambao wako katika madaraka hivi sasa bado wanaitumia "advantage" hio.

Takashi, majibu yangu uliyoyatolea ufafanuzi niliyatoa specifically kwa mwanaJF kwa ID Nduguyangu ambaye alitoa somo la historia juu ya maisha yalivyokuwa magumu wakati wa uongozi wa Mwl. Nyerere. Kimsingi katika hoja yake kulikuwa na kila dalili ya kumlaumu Mwl kwa kile alichokiita udikteta. naomba upokee intro hiyo.

Sasa hii hoja yako kwama "Mambo yanayotokea nchi za kiarabu sasa hivi ,ilikua tufanye sisi miaka ile " naomba nikupe ufafanuzi huu: Tume ya Late Judge Francis Nyalali iliyozunguka nchi nzima kupata maoni ya wananchi juu ya uwepo au la wa vyama vingi vya siasa, ilitoa matokeo yaliyoweka bayana kuwa takriban 80% ya watanzania walioshiriki kwenye utoaji wa maoni walisema waziwazi wanataka mfumo wa chama kimoja uendelee. only 20% walisema wangependelea mfumo wa vyama vingi! Kwa taratibu za kidemokrasia basi ilitakiwa iwe hivyo - mfumo wa chama kimoja maana wengi wape. Lakini wote tunakumbuka kuwa ni Mwl aliyewashawishi viongozi wenzanke ndani ya chama (ccm) na hata serikali kufuata maoni ya wachache 20% na kubadili mfumo wa chama kimoja ili kuruhu vyama vingi.

Kinachotekea kwenye nchi za kiarabu ni umma unataka demokrasia pana inayowapa wananchi uhuru wa kuchagua watu wanaowata kwa maana ya kuwa na "multiple choice in the ballot paper" kwa maneno mengine vyama vingi. Na niseme tu kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa siasa dalili za matatizo ya leo kwenye nchi hizi zimekuwepo kwa muda lakini wakubwa wakawa wanazizima. Kila kitu kina mwisho sasa umma umechoka wanataka mabadiliko. Sasa,tukirudi kwenye hoja yako ni kwamba Nyerere aliona yaliyotokea Tunisia takribani miaka 20 iliyopita, aliona Misri, na aliona Yemen, still counting na ndio maana akashauri maoni ya 20% yachukuliwe badala ya 80%. Hii ndio equation tunaweza kuuita 'Pro-active + Vision". Tanzania tumeingia kwenye mfumo wa vyama vingi kiulani kabisa tofauti na nchi nyingi Africa. That's the kind of leadership tunakata kwamba viongozi wetu wanakuwa na 'maono' (vision) na sio kuongoza nchi kwa mtindo wa zima moto.

Kuhusu mauaji na mateso kwa watu naomba nikuachie hilo wewe maana unaonekana kulijua kivyako ila niseme tu hata sasa watu wanakufa kwa kukosa huduma za matibabu - hospitali zetu hazina dawa. Sijui unaweza kutuambia ni kwani hazina dawa hizi hospitali zetu?
 
Utakatifu wa Nyerere haupatikani kwa njia hizi.
Nitachangia kuhusu 9 na 10 tu.Nyerere mwenyewe alikuwa mhujumu uchumi wa kujadiliana naye angetoka wapi?.Wakati wananchi wanakula chakula cha farasi wa Marekani yeye alitoa kibali kwa kanisa kuagizia wanachotaka kutoka nje.Huu si uhujumu tu bali mauji ya kimbari kabisa.
Makosa ya mtoto mmoja wa raisi au mke wa raisi hata ikiwa ni kasoro havilingani na kutaifisha mali za waislamu chini ya EAMWS na kuzitapanya alivyopenda.Mabiliioni ya fedha!.Akishitakiwa Nyerere in absentia kwa hili wala si kosa.

Ami, hakuna mahali popote nimeandika 'Utakatifu' wa Mwl. Nyerere naomba usome tena kwa makini. Mwl. Nyerere alikuwa binadamu, alikuwa na mapungufu? - yes, alikuwa na mazuri? yes. Hata yeye mwenyewe alikiri haya kwamba wakati wa utawala wake yako mema alifanya na mabaya. Huo ndio ubinadamu. Majibu yako kwenye red tafsiri yake ni ni kwamba unatueleza kuwa wakati wa Mwl Nyerere Wakristu walikuwa wanakula chakula kizuri tena toka nje ya nchi! ila kwa wasio-kuwa Wakristu walikuwa wanakula chakula cha farasi wa Marekani na matokeo yake kulikuwa na vifo vingi mithili ya mauaji ya kimbari! Labda utufanunulie haya:

1.Hicho chakula cha farasi wa marekani kinaitwaje na kililetwa na nani? (maana ni cha farasi wa marekani sio Tanzania)
2. Kwa familia ambazo zilikuwa zimechanganyika yaani baba ni mwislam na mama ni mkristo & vice-vesra mlo ulitolewa kwa mtiririko huo? yaani baba anakula chakula cha farasi huku mama anakula mlo mzuri ulioagizwa nje ya nchi?
3. Ni watu wangapi walikufa (mauaji ya kimbari si idadi ndogo) kutokana na 'uhujumu' huu wa Mwl Nyerere wa watu kula aina ya chakula kulingana na imani zao?
4. Kuna mali , shule, hospitali - zozote za wakristu zilitaishwa wakati wa Mwl. Nyerere.

Mwisho, haipendezi mtu mzima kueneza majungu!. Si heshma!
 
Kwenye mdahalo kipindi kile cha uchaguzi, alishindwa kujibu swali "....unawaachia watz regacy gani, ambayo wakukumbuke nayo"
Akasema wanaikumbuke kama niliwatoa hapa na kuwapeleka pale...
Jamani JK ni maandazi kabisa huyu jamaa, atlesat Ben alikuwa anatupeleka shimoni kwa misingi ya kuua "kujitegemea kwa taifa" lakini huyu hata hajui anatupeleka wapi.

chonde chonde chonde, siyo "regacy" ni legacy!!!! kwamba utaacha alama gani ambayo itakumbukwa kwa uzuri/mchango
 
Takashi, majibu yangu uliyoyatolea ufafanuzi niliyatoa specifically kwa mwanaJF kwa ID Nduguyangu ambaye alitoa somo la historia juu ya maisha yalivyokuwa magumu wakati wa uongozi wa Mwl. Nyerere. Kimsingi katika hoja yake kulikuwa na kila dalili ya kumlaumu Mwl kwa kile alichokiita udikteta. naomba upokee intro hiyo.

Sasa hii hoja yako kwama "Mambo yanayotokea nchi za kiarabu sasa hivi ,ilikua tufanye sisi miaka ile " naomba nikupe ufafanuzi huu: Tume ya Late Judge Francis Nyalali iliyozunguka nchi nzima kupata maoni ya wananchi juu ya uwepo au la wa vyama vingi vya siasa, ilitoa matokeo yaliyoweka bayana kuwa takriban 80% ya watanzania walioshiriki kwenye utoaji wa maoni walisema waziwazi wanataka mfumo wa chama kimoja uendelee. only 20% walisema wangependelea mfumo wa vyama vingi! Kwa taratibu za kidemokrasia basi ilitakiwa iwe hivyo - mfumo wa chama kimoja maana wengi wape. Lakini wote tunakumbuka kuwa ni Mwl aliyewashawishi viongozi wenzanke ndani ya chama (ccm) na hata serikali kufuata maoni ya wachache 20% na kubadili mfumo wa chama kimoja ili kuruhu vyama vingi.

Kinachotekea kwenye nchi za kiarabu ni umma unataka demokrasia pana inayowapa wananchi uhuru wa kuchagua watu wanaowata kwa maana ya kuwa na "multiple choice in the ballot paper" kwa maneno mengine vyama vingi. Na niseme tu kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa siasa dalili za matatizo ya leo kwenye nchi hizi zimekuwepo kwa muda lakini wakubwa wakawa wanazizima. Kila kitu kina mwisho sasa umma umechoka wanataka mabadiliko. Sasa,tukirudi kwenye hoja yako ni kwamba Nyerere aliona yaliyotokea Tunisia takribani miaka 20 iliyopita, aliona Misri, na aliona Yemen, still counting na ndio maana akashauri maoni ya 20% yachukuliwe badala ya 80%. Hii ndio equation tunaweza kuuita 'Pro-active + Vision". Tanzania tumeingia kwenye mfumo wa vyama vingi kiulani kabisa tofauti na nchi nyingi Africa. That's the kind of leadership tunakata kwamba viongozi wetu wanakuwa na 'maono' (vision) na sio kuongoza nchi kwa mtindo wa zima moto.

Kuhusu mauaji na mateso kwa watu naomba nikuachie hilo wewe maana unaonekana kulijua kivyako ila niseme tu hata sasa watu wanakufa kwa kukosa huduma za matibabu - hospitali zetu hazina dawa. Sijui unaweza kutuambia ni kwani hazina dawa hizi hospitali zetu?

Mkuu Mwalimu alikuwa kweli ana vision maana ni baada ya kuona upepo ulioanza Ulaya Mashariki, hautabakisha kitu na ndio akawa hivyo pro-active.

Kuhusu hio kura ya maoni (kama ni ya kuaminika kweli), 80% ya Watanzania walitaka mfumo wa Chama kimoja. Jee walisema hicho kimoja kiwe CCM? Mimi sikuliona suala hilo kwa bahati mbaya.
 
Nadhani kikwete anaonewa sana.yapo mapungufu yake bt na haki yake apewe.kama ni ufisadi hakuna raisi alokuwa fisadi kama mkapa.alichukua kila kitu kikawa mali yake nanyi mkanyamaza kimya.mkapa kasababisha kwa mara ya kwanza nchi kutoa wakimbizi.naomba niambiwe kwa data ni upi udini wa kikwete?sio tukurupuke kusema mambo yasiyo na mashiko.nyerere kawaweka watu ndani kizuizini bila makosa wala kufunguliwa kesi.huo si ubabe?au hamjawahi kusikia habari hz?toweni uamuzi wa haki sio kuongozwa na hisia.

Usituletee maneno yasiyo na kichwa wala miguu hapa. Hizo data zinazoonyesha kuwa Mwl. Nyerere alikuwa anawaweka watu kizuizini bila makosa umeziokota wapi!!! Ninachojua ni kuwa Mwl. Nyerere hakuwa chizi kiasi cha kufanya upuuzi unaouzungumzia hapa. Kama huna cha kuandika bora uendelee na vijiwe vyenu vya kahawa.
 
Takashi, majibu yangu uliyoyatolea ufafanuzi niliyatoa specifically kwa mwanaJF kwa ID Nduguyangu ambaye alitoa somo la historia juu ya maisha yalivyokuwa magumu wakati wa uongozi wa Mwl. Nyerere. Kimsingi katika hoja yake kulikuwa na kila dalili ya kumlaumu Mwl kwa kile alichokiita udikteta. naomba upokee intro hiyo.

Sasa hii hoja yako kwama "Mambo yanayotokea nchi za kiarabu sasa hivi ,ilikua tufanye sisi miaka ile " naomba nikupe ufafanuzi huu: Tume ya Late Judge Francis Nyalali iliyozunguka nchi nzima kupata maoni ya wananchi juu ya uwepo au la wa vyama vingi vya siasa, ilitoa matokeo yaliyoweka bayana kuwa takriban 80% ya watanzania walioshiriki kwenye utoaji wa maoni walisema waziwazi wanataka mfumo wa chama kimoja uendelee. only 20% walisema wangependelea mfumo wa vyama vingi! Kwa taratibu za kidemokrasia basi ilitakiwa iwe hivyo - mfumo wa chama kimoja maana wengi wape. Lakini wote tunakumbuka kuwa ni Mwl aliyewashawishi viongozi wenzanke ndani ya chama (ccm) na hata serikali kufuata maoni ya wachache 20% na kubadili mfumo wa chama kimoja ili kuruhu vyama vingi.

Kinachotekea kwenye nchi za kiarabu ni umma unataka demokrasia pana inayowapa wananchi uhuru wa kuchagua watu wanaowata kwa maana ya kuwa na "multiple choice in the ballot paper" kwa maneno mengine vyama vingi. Na niseme tu kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa siasa dalili za matatizo ya leo kwenye nchi hizi zimekuwepo kwa muda lakini wakubwa wakawa wanazizima. Kila kitu kina mwisho sasa umma umechoka wanataka mabadiliko. Sasa,tukirudi kwenye hoja yako ni kwamba Nyerere aliona yaliyotokea Tunisia takribani miaka 20 iliyopita, aliona Misri, na aliona Yemen, still counting na ndio maana akashauri maoni ya 20% yachukuliwe badala ya 80%. Hii ndio equation tunaweza kuuita 'Pro-active + Vision". Tanzania tumeingia kwenye mfumo wa vyama vingi kiulani kabisa tofauti na nchi nyingi Africa. That's the kind of leadership tunakata kwamba viongozi wetu wanakuwa na 'maono' (vision) na sio kuongoza nchi kwa mtindo wa zima moto.

Kuhusu mauaji na mateso kwa watu naomba nikuachie hilo wewe maana unaonekana kulijua kivyako ila niseme tu hata sasa watu wanakufa kwa kukosa huduma za matibabu - hospitali zetu hazina dawa. Sijui unaweza kutuambia ni kwani hazina dawa hizi hospitali zetu?

Asante Mkuu FJM.... Nilivyo elewa mimi kuhusu chanzo cha hii Makala ni kutaja ubaya wa marais wetu waliyowahi na ambae yuko madarakani. Kwahiyo mimi mchango wangu ulikua hivyo kuelezea mabaya ...Lakini haina maana kama hakuna mazuri ya yule Mzee. Tafauti yangu mimi na wewe ni kuwa wewe umechagua mazuri yake na mimi nimechagua mabaya yake.
Kila siku tunasikia sifa zake kama vile alikua malaika, au mtakatifu fulani. Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi Tanzania, Kule Zanzibar CUF walishida .Lakini Nyerere yeye ndio aliyezuwia ushindi wa CUF na kuwapa CCM. Alitoa mfano mbaya sana ndio hadi sasa vyama vya upinzani vinaendelea kunyimwa ushindi wa kihalali. Mimi sio CUF wala sina chama chochote. Ila tu uelewe kama yeye ndio alikua "BABA" hakupaswa afanye vile.
 
Mr. Ahadi Nyingi, aliyetoa speach iliyo sisimua na yenye matumaini baada ya uchaguzi lakini akabaki anacheka cheka kwa kushindwa kuyashughulikia aliyo ya ahidi, akaacha mafisadi wakiongoza nchi huku yeye akila misele ya ughaibuni huyo ndo Rais Mbovu kuliko wote East and Central Africa siyo Bongo tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom