Nyerere, mshahara wa Rais na kipato cha mwezi cha mwananchi

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,986
1,282
"Mshahara wangu ni Shilingi elfu tano kwa mwezi. Shilingi elfu tano katika nchi masikini. Masikini anayepata shilingi mia mbili tu kwa mwezi itamchukua miaka 25 kufikia kiwango cha mshahara wangu kwa mwezi. Ndiyo, nakubaliana na nyinyi kwamba tunalipana (viongozi) mishahara mikubwa mno, na nitahakikisha mishahara hii tunayolipana inarekebishwa." - See more at: Raia Mwema - Mishahara ya Pinda, Kikwete inajadilika, tusihofu kuijadili!

Wakati Nyerere alikuwa na fikra hizo kipindi ambacho uchumi wetu ulikuwa mzuri ukilinganisha sasa, lakini viongozi wetu wasasa povu zinawatoka kwaajili ya posho na kujiongezea mishahara pamoja na kwamba hali ya maisha ya mtanzania ambaye ndiye mbeba gharama hizo ni duni kupita kiasi.

Nashukuru tuna chama chenye kuona haja ya kushusha mishahara ya viongozi wa kisiasa na kuondoa posho za kuketi kikao ambacho ni sehemu ya kazi ambayo kwayo viongozi wa kisiasa hupata mishahara yao. Safi sana CHADEMA, niko na imani ikichukua Dola hichi kitakuwa kitu cha kwanza, na itakuwa vizuri sana vyama vingine vikiiga hili.

Njano5.

0655345394
 
Ndugu yangu Njano, wazalendo wa nchii wamebaki wachache sana, mishahara yenyewe wanadai ni siri, wakati waajiri wao ni Wananchi!! Nyerere alikuwa na guts za kutaja mshahara kwa kuwa alikuwa mzalendo na pia alikuwa anajua waajiri wake ni Wananchi!
 
sijui unachoongea kama kinatekelezeka #lema week zilizopita alilia lia mishahara ya wabunge iongezeke,wawe na maslahi makubwa,BORA HATA SHIBUDA AMBAYE ALILIKAA SUALA LA KUKANA SITTING ALLOWANCE MAPEMA.............TUKAMUONA MSALITI,LAKINI CHAKUSHANGAZA WABUNGE WA CDM WALIFUATA NYAYO ZAKE KIMYA KIMYA KWA KUCHUKUA POSHO ZAO
 
suala hili si la wabunge wa chadema, suala hili ni la chama na kiukweli ni SERA. Kukosea kwa Rema si sababu ya kubeza sera hii nzuri ya CHADEMA. Lema si CHADEMA ila Lema ni mwanaCHADEMA na kamanda.
 
suala hili si la wabunge wa chadema, suala hili ni la chama na kiukweli ni SERA. Kukosea kwa Rema si sababu ya kubeza sera hii nzuri ya CHADEMA. Lema si CHADEMA ila Lema ni mwanaCHADEMA na kamanda.

bora ulipokubali kama lema alikosea,safi sana huo ndo uungwana wa kujenga hoja
 
Je huo mshahara aliokuwa anaoupata Nyerere ambao ulikuwa mkubwa kuliko wa Kikwete aliurekebisha au aliishia kusema tu?
 
bora ulipokubali kama lema alikosea,safi sana huo ndo uungwana wa kujenga hoja

Lema hajakosea, jifunzeni kumwelewa mpigania haki za binaadamu huyu mkapate kujua baadhi ya mbinu mnaweza kuzitumia mkiweza kuzitafsiri.

Eleweni kuwa budget ya hizo posho ishatengwa kisheria, hukosei kuichukua, kwa kuwa ukiiacha itarejeshwa kimya kimya hazina ambako inaweza isifike, wakapewa akina Mwigulu Nchemba wakanunulie mabom china waje kuwalipua.

kwahiyo kwa kuwa ni haki ya kisheria kuchukua hizo posho kwa sasa, ni heri Lema achukue ili ajaze mafuta kwenye gari lake achanje mbuga kuwafikia wapiga kura awape elimu ya uraia.

Tunapigania sheria ibatilishe posho!!!!
 
CCM ni ukoo wa panya--babu mwizi, baba mwizi, watoto wezi, wajukuu wezi, vitukuu wezi, vilembwe wezi na vining'ina wezi!
 
Lema hajakosea, jifunzeni kumwelewa mpigania haki za binaadamu huyu mkapate kujua baadhi ya mbinu mnaweza kuzitumia mkiweza kuzitafsiri.

Eleweni kuwa budget ya hizo posho ishatengwa kisheria, hukosei kuichukua, kwa kuwa ukiiacha itarejeshwa kimya kimya hazina ambako inaweza isifike, wakapewa akina Mwigulu Nchemba wakanunulie mabom china waje kuwalipua.

kwahiyo kwa kuwa ni haki ya kisheria kuchukua hizo posho kwa sasa, ni heri Lema achukue ili ajaze mafuta kwenye gari lake achanje mbuga kuwafikia wapiga kura awape elimu ya uraia.

Tunapigania sheria ibatilishe posho!!!!

kaka usijaribu kutetea hilo,,,Rema alisema hawezi kuishi maisha ya kimaskini kwa kuwatetea maskini, atapokea posho huku akitetea maisha bora kwa watz, huu ndio utetez wa Rema ambao unakiuka misingi mkuu wa sera yenyewe. Rema anaona mshahara na posho anayoipata ndogo, huu ni upuuzi wa kupingwa, kama anataka kujiongezea posho aanze kuongeza maslahi ya wananchi,,,aanze kwanza kuwashawishi hao wangunge wenziwe wakubali kubadili huo mfumo akifanikiwa ndio aweze kujiongezea posho na yeye.
 
sijui unachoongea kama kinatekelezeka #lema week zilizopita alilia lia mishahara ya wabunge iongezeke,wawe na maslahi makubwa,BORA HATA SHIBUDA AMBAYE ALILIKAA SUALA LA KUKANA SITTING ALLOWANCE MAPEMA.............TUKAMUONA MSALITI,LAKINI CHAKUSHANGAZA WABUNGE WA CDM WALIFUATA NYAYO ZAKE KIMYA KIMYA KWA KUCHUKUA POSHO ZAO

hivi lema si ni cdm?

sasa mbona anashabikia ujinga?

ama kweli cdm imeharibikiwa jamani!
 
Acha kuchanganya udhaifu wa Mwanachama na utendaji wa taasisi nzima kwa ujumla wake.

mbona hujarudi kujibu hili :
quote_icon.png
By appriciator
Je huo mshahara aliokuwa anaoupata Nyerere ambao ulikuwa mkubwa kuliko wa Kikwete aliurekebisha au aliishia kusema tu?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom