Sibonike
JF-Expert Member
- Dec 23, 2010
- 17,294
- 18,027
Siku chache zilizopita, Rais mstaafu, Jakaya Kikwete amezindua taasisi yake. Kabla yake, Rais mstaafu Benjamin Mkapa aliwahi kuzindua yak wake na kabla yake Baba wa taifa Mwl Nyerere alizindua ya kwake pia.
Malengo ya taasisi zote hizo yanafanana kwa kiasi kikubwa – utawala, bora na huduma za jamii kama afya na elimu.
Najiuliza kama taasisi zote hizo zinaweza kuwa na kazi za kutosha ili ziendelee kuwepo. Natambua haki ya kila Rais mstaafu kufungua taasisi yake. Hivi taasisi ya Mwl Nyerere ikiongozwa na mzee Butiku inafanya kazi gani siku hizi? Je ya Mkapa nayo? Kwa upya wake, bila shaka taasisi ya Kikwete itakuwa busy hizi siku za mwanzo. Miaka mitano au kumi ijayo itakuwa vipi na hasa kama Rais Pombe atakuja kufungua ya kwake?
Kwa minajili hiyo hiyo, tunaweza kujiuliza ile NGO ya Anna Mkapa imefia wapi? Nayo WAMA ya Salma Kikwete ipo kimya siku hizi.
Hivi lazima kila Rais mstaafu awe na taasisi yake? Mzee Mwinyi hakuwahi kufungua taasisi yake lakini ushauri na busara zake kwenye siasa za Tanzania na kimataifa ni taasisi tosha!