Nyerere, Magufuli na Polepole: Mashujaa pekee wa CCM katika enzi za siasa za vyama vingi

Ni wazi CCM wanaamini kukosoana wenyewe ni kosa la jinai na hasa kumkosoa mwenyekiti ni dhambi isiyovumika!!

Vyama upinzani wanayo hii pia, Ila kwakuwa mada inawaangazia hao mashujaa watatu, ndipo nimeitaja CCM!

Ndani ya CCM usikosoe serikali hadharani
Watakushughulikia kungali kweupe!
Hii desturi si njema kwa afya ya Taifa, na hii inatokana na desturi ya kuthamini chama kuliko Taifa.

Hadi Sasa, kumbukumbu zangu zinaniambia, ni watatu wamethubutu kukiuka huo mwiko na kuonekana mashujaa, wakaamua waziwazi kusema wanaCCM wanakosea katika hili au lile

Kukosoa watendaji wa serikali ukiwa ndani ya CCM, ni ujasiri mkubwa!

Tunaomba Wana CCM tubadilike,
Uhai wa chama ni uwajibikaji Bora wa watendaji wetu.

Tujisahihishe

Hio nayo ni sehemu ya kumuenzi Mwl Nyerere!
Acha tena acha huo ujinga wa kumfananisha nyerere na takataka kama polepole

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Ni Nyerere yupi unamtaja hapa? Ni Steve Nyerere au ile sanamu alichonga KIGWANGALA ? Dogo kama ni baba wa Taifa JK Nyerere nakushauri nenda kafanye utafiti kwanza ili umuelewe. Wacha kumfananisha na huo UJINGA wa Chato

Ungeeleza utofauti wa Nyerere, baba wa Taifa, na huyo unayemwita UJINGA wa Chato, hoja yako ingekuwa na mashiko, la wewe ndiye huyo, au?
 
Unamkosea heshima JK Nyerere kwa kumfananisha na vitu vya ajabu.
Nyerere alitoa maoni yake pia kipindi cha uongozi wa Mstaafu mzee mwinyi ,kila mtanzania ana haki ya kimsingi ya kutoa maoni yake juu ya Taifa letu Polepole yupo sahihi kikatiba kwa mfano madudu ya bandarini kuhusu mikataba mibovu ya mabilioni ya watanzania maskini ulitaka watu wakae kimya huku wachache wachache wasiowaaminifu wakinufaika huku kundi kubwa la wahitimu vijana hawanà ajira
 
huyu huyu polepole jamaa alikuwa anatembea na hela kwenye mabegi ndani ya ma-vieteeee kununua wapinzani - kweli? kweli ?
 
Ungeeleza utofauti wa Nyerere, baba wa Taifa, na huyo unayemwita UJINGA wa Chato, hoja yako ingekuwa na mashiko, la wewe ndiye huyo, au?
Mbona mambo yako wazi tu, tumia simu yako ku google umjue Nyerere. Ila kwa ufupi nitakupa machache hapa;
1. Utawala wa Sheria, kamwe Nyerere hajawahi kuingilia Uhuru Mahakama pamoja na kuwa alitawala kwenye mfumo wa Chama Kimoja

2. Kupendelea Maendeleo Wilaya yake, Nyerere aliangalia Tanzania nzima kwa uzito ulio sawa katika miaka 25 aliyotawala hata barabara lami Butiama ilikuwa haijajengwa mpaka alipotoka. Huyu miaka 3 tu kapeleka Airport, Mbuga ya wanyama, Hospitai ya Rufaa

3. Kuua wakosoaji, Nyerere hakuwaua japo aliwaweka kizuizini kwa wakati fulani. Magufuli alimuua Ben Saanane, Azory Gwanda, na alishambulia Tundu Lissu kwa risasi

4. Kubambikiza wakosoaji kesi, wakosoaji kama akina Eric Kabendera, Tito Magoti, Mdude Chadema nk

5. Kuwanyanga'anya fedha matajiri , kama akina James Rgemalira kwa kisingizio cha Plea Bargaining

6. Ufujaji au Ufisadi. Magufuli kwa miaka 4 CAG aligundua kuwa fedha zipatzo Tsh 2.4 Trilioni hazijulikani ziko wapi

7. Vyama vya upinzani, Nyerere ndiye mwasisi wa vyama vingi na aliviunga mkono. Huyu aliendesha utawala wa KIDKTETA na hakupenda vyama vya upinzani kabisa

8. Magufuli alitumia Imani yake ya Kikatoliki kujijenga kisiasa ndiyo maana akawa anahutubia pale St Peters. Nyerere alisali tu nakuondoka
 
ni Kama enzi zileee,mpinzani wa kweli atatoka ccm,kichwa kimoja,kinachachafya vichwa mia tatu na point,vya bungeni,ujue ni mtu mmoja tu anatosha kusababisha reforms serikalini .wait &see.kwa Sasa tz Kuna spirit 2,ambazo zinanguvu hapa tz ,mwal. Plus jpm.
 
Taifa linapokuwa na ukosefu wa mashujaa
Hadi wagonjwa wa akili nao wanaitwa mashujaa
Magulegacy; Huo ndio ugonjwa mkubwa wa wakati huu. Kama YEYE mwenyewe alivyokuwa na bidii ya kuyajaza na kuyainua matakataka(Bashite, Sabaya........), waathirika nao wanakimbizana mpaka majalalani kuokoteza hata wachawi halafu wayaite 'mashujaa'.
 
Ni Nyerere yupi unamtaja hapa? Ni Steve Nyerere au ile sanamu alichonga KIGWANGALA ?

Dogo Weakman kama ni baba wa Taifa JK Nyerere nakushauri nenda kafanye utafiti kwanza ili umuelewe. Wacha kumfananisha na huo UJINGA wa Chato

Atakuwa yule Nyerere aliyewekwa madarakani na waingereza baada kupinduliwa ? na kuwa kibaraka wao , kwa kuivamia na kuitesa Zanzibar mpaka leo ?
 
Mbona mambo yako wazi tu, tumia simu yako ku google umjue Nyerere. Ila kwa ufupi nitakupa machache hapa;
1. Utawala wa Sheria, kamwe Nyerere hajawahi kuingilia Uhuru Mahakama pamoja na kuwa alitawala kwenye mfumo wa Chama Kimoja

2. Kupendelea Maendeleo Wilaya yake, Nyerere aliangalia Tanzania nzima kwa uzito ulio sawa katika miaka 25 aliyotawala hata barabara lami Butiama ilikuwa haijajengwa mpaka alipotoka. Huyu miaka 3 tu kapeleka Airport, Mbuga ya wanyama, Hospitai ya Rufaa

3. Kuua wakosoaji, Nyerere hakuwaua japo aliwaweka kizuizini kwa wakati fulani. Magufuli alimuua Ben Saanane, Azory Gwanda, na alishambulia Tundu Lissu kwa risasi

4. Kubambikiza wakosoaji kesi, wakosoaji kama akina Eric Kabendera, Tito Magoti, Mdude Chadema nk

5. Kuwanyanga'anya fedha matajiri , kama akina James Rgemalira kwa kisingizio cha Plea Bargaining

6. Ufujaji au Ufisadi. Magufuli kwa miaka 4 CAG aligundua kuwa fedha zipatzo Tsh 2.4 Trilioni hazijulikani ziko wapi

7. Vyama vya upinzani, Nyerere ndiye mwasisi wa vyama vingi na aliviunga mkono. Huyu aliendesha utawala wa KIDKTETA na hakupenda vyama vya upinzani kabisa

8. Magufuli alitumia Imani yake ya Kikatoliki kujijenga kisiasa ndiyo maana akawa anahutubia pale St Peters. Nyerere alisali tu nakuondoka
AMEN, AMEN.
 
Itikadi zao zinafanana kwa maana ni wajamaaa,but kwa kizazi cha sasa itikadi zao ni mfu.
Ni wajamaaa kwa maneno na sio kwa matendo.
 
Nyerere alitoa maoni yake pia kipindi cha uongozi wa Mstaafu mzee mwinyi ,kila mtanzania ana haki ya kimsingi ya kutoa maoni yake juu ya Taifa letu Polepole yupo sahihi kikatiba kwa mfano madudu ya bandarini kuhusu mikataba mibovu ya mabilioni ya watanzania maskini ulitaka watu wakae kimya huku wachache wachache wasiowaaminifu wakinufaika huku kundi kubwa la wahitimu vijana hawanà ajira
Pole ndugu,
Hivi ni lini Polepole alikubali Rais (wake)Magufuli akosolewe. Maoni ya waliyokuwa na mitazamo tofauti kuhusu makinikia yalipotoshwa kwa makusudi mazima na huyuhuyu Chakubanga. Wakaitwa wasaliti,wakakamatwa kiholela, wakawindwa, wakabambikiwa kesi na kutiwa ulemavu kwa vipigo. Nadhani yeye haswa ndie "......alitaka watu wakae kimya huku wachache wasiowaaminifu wakinufaika huku kundi kubwa la wahitimu vijana hawana ajira...". AMEN
 
Back
Top Bottom