Nyerere kulisoma Azimio la Arusha kwa miaka 28! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere kulisoma Azimio la Arusha kwa miaka 28!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kieleweke, Apr 23, 2011.

 1. K

  Kieleweke Member

  #1
  Apr 23, 2011
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa maneno yake mwenyewe mwaka 1995, Julius Nyerere alitamka kwamba anatembea na vitabu viwili yaani BIBLIA na AZIMIO LA ARUSHA.

  Biblia hakuitunga hivyo ana mengi ya kujifunza kilichomo. Lakini kuna siku Pius Msekwa aliweka wazi kwamba Azimio la Arusha ni kitabu alichokiandika Julius Nyerere kwa mkono wake. Azimio likatinga mtaani mwaka 1967.

  Hapa linakuja swali langu hasa kwa wana-saikolojia. Iweje kitabu ulichokitunga miaka 28 iliyopita, kikasomwa na wengi halafu usibanduke nacho mkononi, yaani kila wakati uwe unakipitia kama vile unafanya research?

  Nisaidieni kuelewa?
   
 2. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kitabu hicho kilikuwa sawa na Biblia katika utendaji kazi wake. Kiongozi mzuri ni yule anayetunga sheria au sera na kuzitekeleza kwa vitendo kama alivyofanya yeye kwenye azimio la Arusha. Ili uweze kutekeleza yale yaliyo kwenye sheria au sera, huna budi kukaa na kitabu au waraka wa sera hizo kila unapokuwa ukifanya kazi ili ukitumie kama mwongozo (terms of references) na kuhakiki kama hauendi nje na yale uliyokusudia. hii ni tofauti kabisa na viongozi wa sasa ambao utakuta anapitisha sheria kwa mbwembwe za kila aina lakini mara tu baada ya kuipitisha yeye huyohuyo anakuwa wa kwanza kwenda kinyume na sheria hiyo. Haya yote ni matokeo ya kupitisha sheria bila kujua misingi ya sheria hiyo na pia inatokana na viongozi hao kutokurejea sheria husika kabla ya kufanya jambo.
   
 3. p

  profkobayashi JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 224
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  the man was an idiot

  dead people dont count
   
 4. K

  Kieleweke Member

  #4
  Apr 23, 2011
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Silas Haki, Hujanisoma. Sheria unazosema zinatungwa na watu mbalimbali ksiha zinapitishwa na wabunge wasiopungua 60.

  Umekubaliana na mimi kuwa Azimio ni article aliyotunga na kuiandika yeye mwenyewe kama Julius kama alivyoandika article nyingi tu.

  Unapoandika article kila kitu kiko kichwani maana ndiko ilikotoka.
   
 5. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Usijidanganye hivyo ndugu yangu, kichwa cha mwanadamu siyo kompyuta na hata kompyuta yenyewe wakati mwingine hushindwa kuweka kumbukumbu sawasawa. Kutunga kitu au kuandika kitabu haimaanishi kuwa yote uliyoyaandika yatakaa kichwani mwako. Mpaka leo hii ulishafanya mambo mangapi na ulishayasahau? Mimi nimeshaandika articles kadhaa lakini haimaanishi kuwa ukiniuliza kuna kitu gani ukifungua ukurasa fulani wa article nitakujibu kirahisi. Pia kumbuka kuwa Nyerere alikuwa msimamizi mkuu wa sheria au sera hiyo na hivyo ili aweze kuwakosoa waliokuwa wanatenda kinyume na sera hiyo ilimpasa awe na kitabu ili aweze kurejea pale anapomwadhibu mkosaji. Kumbuka hata mahakama pamoja na kujua kuwa unasitahili kufungwa pale unapotenda kosa huwa inarejea sheria zilizopo mezani ili ku-justify the case. Epuka kufanya maamuzi pasipo kuwa na supporting evidence or terms of references when working for the public offices.
   
 6. K

  Kieleweke Member

  #6
  Apr 23, 2011
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kauli ya yeye kutembea na kitabu kile aliitoa mwaka 1995 akiwa na miaka 10 ameshastaafu, na kukiwa na miaka mitatu tangu Azimio la Arusha lilipopinduliwa na Azimo la Zanzibar.

  Labda kama una hamu tukusikie ukihadithia utendaji wa Mwalimu kuhusiana na Azimio, wakati hoja yangu ni yeye kutembea na kijitabu kile wakati yeye mwenyewe alishakiri unaweza kuendesha nchi bila Azimio ambalo lilishapigwa teke miaka kadhaa nyuma.
   
 7. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Uwe muelewa na mtu wa tafakari; Uwemakini unapochukua sehemu ya kauli ya mtu na kuifanyia uchambuzi ... Uhakikishe kuwa unasoma na kupitia hoja nzima kabla ya kujadili sehemu ya hoja yenyewe!!

  1. Unakubali kuwa alikuwa anatembea na biblia wakati wote .... unaelwa nini hapa... Nani alishamuona akitembea na Biblia wakati wote? elewa kuwa hapa anasisitiz aimani yake juu ya Biblia na sio kwamba alikuwa anaishikilia siku nzima na kupita nayo mtaa hadi mtaa ...!!!

  2. Kasikilize hotuba yote aliyoitoa na kutoa matamshi hayo ... alimaanisha kuwa alikuwa muumini wa Azimo la Arusha ... alimaanisha kuwa ni kitu ambacho alikuwa hawezi kukitupa na kukiacha... ni kitu kiko moyoni kwake.... ni kitu alichokuwa anakiamini ... na haoni sababu ya kupuuziwa. Kusema anatembea nacho ilikuwa ni swala la kuonyesha msisitizo....

  3. Ni vema unapoamua kuchukua sehemu ya kauli za watu ...uhakikishe umepitia ... hoja nzima ndipo uanze kuziungumiza...otherwise you will miss a lot of what you wish to express!!
   
 8. K

  Kieleweke Member

  #8
  Apr 23, 2011
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Mbinu nzuri ya watu wanaoshindwa hoja kwanza ni kuwahadaa watu kwamba jambo linalozumgumziwa halina tafsiri ile, kana kwamba kilichotamkwa ni kitendawili au msamiati au methali inayohitaji tafsiri.

  Ukifaulu hapo basi unajua ushindi wa kukwepa hoja unakaribi maana mleta hoja akishakubali kuuingia mtego wa tafsiri unajua wazi tafsiri ziko hata milioni basi huko mtalumbana huko kwamba ipi ni tafsiri bora lakini binafsi unakuwa umefaulu kuhamisha mjadala.

  Hotuba ya tamko lile inasemwa kila mara hata mtoto wa miaka 9 imemkaa kichwani.

  Leteni hoja mtushawishi tuwaunge mkono. Yeye mwenyewe Nyerere asilimia 90 ya majibu yake yalijaa hoja na si kulikwepa swali kwa kulibambikia jambo tafsiri.

  Sijakata tamaa. Bado nasubiri kuna watu watanijibu swali langu kuliko nyinyi ambao sasa mnaumba hoja ambazo hata Mwalimu mwenyewe akifufuka anawashangaa mnavyomtetea.
   
 9. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  nadhani kauli yake ya kutembea na vitabu hivi haimaanishi anavipitia kama unavyotaka kutuaminisha!
   
 10. m

  matunge JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  down down and and down....
   
 11. K

  Kieleweke Member

  #11
  Apr 23, 2011
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna anayeaminishwa. Nyerere hakuwa mtunga mafumbo au vitendawili na htouba zake zilikuwa public. Lete majibu tuelimike au waachie wenye vichwa vyenye majibu!
   
 12. A

  Adili JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 2,012
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  Mtukane mwenye uwezo wa kujitetea.
   
 13. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Azimio Jipya ametoa jibu zuri sana na linaloeweka hata kwa mtu ambaye hakwenda darasani kabisa. Ukiona mpaka hapo hujaelewa ujue wewe ni kilaza wa kutupwa kabisa.
   
 14. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  NADHANI HALIANZA HIVYO BAADA YA AZIMIO LA ZANZIBAR.

  Na sababu ya kutembea nacho ni kuwa alikuwa HAELEWI ni vipi WATU,wakane AZIMIO LA ARUSHA, kwahiyo alikuwa anakipitia HAJIRIDHISHE KAMA KWELI KULIKUWA NA SABABU YA KUFANYA HIVYO.
   
 15. T

  The Possible New Member

  #15
  Jul 16, 2015
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  He was trying to find what is wrong with Arusha declaration mpaka wameleta Azimio la Zanzibar,ndo maana aliongeza kauli kwamba huwa analipitia halafu haoni tatizo...
   
Loading...