Nyerere katuharibu watanganganyika sera ya umoja,amani na upendo vinatufanya kuwa watumwa wa haki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere katuharibu watanganganyika sera ya umoja,amani na upendo vinatufanya kuwa watumwa wa haki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, Apr 12, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hizi kauli za Watanganyika kuwa eti ni kisiwa cha amani, wapole, wakarimu,wasikivu imetufanya tunyang'anywe haki zetu za msingi ndani ya nchi yetu pendwa Tanganyika. Hivi kweli Watanganyika ni lini tulishakusanyana kuitetea nchi yetu kama wafanyavyo wa ng'ambo ya Pili juu ya nchi yao hata kwa mambo ya kipuuzi hivi sisi tumelogwa.

  Kuna wazee wanadai amani ni kila kitu hizi kauli zinanikera sana amani gani tuliyonayo wakati hakuna haki ndani ya nchi hii. Pesa na matumizi mabaya ya madaraka kwa walionacho dhidi ya sisi walipa kodi zaidi ya mara mbili. Mshahara wangu kodi wanakata na ninapoenda kununua vitu nalipa tena kodi.

  NATAMANI NCHI HII TUNGEIKOMBOA KWA MTUTU WA BUNDUKI TOKA KWA MKOLONI TUNGEHESHIMIANA.
  Kwa maana hata kama mtu ukipewa kitu uthamani wake unakuwa dhaifu dhidi ya kile ulichokitolea jasho.

  Hivi inaingia akilini Wazanzibar 1,500,000 watawale mchakato wa katiba kushinda watanganyika Milioni 42 tuliopo bara?

  NYERERE KATUHARIBU natamani tupigane heshima irudi ndani na nje ya nchi yangu Tanganyika


  Mniwie radhi kwa niliowaudhi
   
 2. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tunaria tunaria watz, tunamlilia baba wa taifa mw nyerere
  Fimbo imetuponyoka hatuna pa kukimbilia, baba wa taifa ametutoka..
  Mw. Nyyerereeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 3. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tunaria tunaria watz, tunamlilia baba wa taifa mw nyerere
  Fimbo imetuponyoka hatuna pa kukimbilia, baba wa taifa ametutoka..
  Mw. Nyerereeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  sera hizo zimefanya 95%ya uchumi wetu kushikiliwa na watu wachache wasiozidi 100 MENGI aliwataja 10
   
 5. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu... ni methali iliyosheheni ukweli mwingi kisayansi na kisanaa. Umoja ukitumiwa vyema unaleta ushindi katika nyanja za maendeleo, teknologia, elimu, ustaarabu na mengineyo mengi. Lakini ukitumiwa kipumbavhu kama hivi ilivyo sasa kwakweli ni kama ujinga fulani hivi.

  Mimi nionavyo ni kuwa umoja una masharti yake, yakitimizwa unadumu, na yakikiukwa unatoweka. Umoja unataka haki, heshima, uzalendo, upendano, na demokrasia ....

  Mambo hayo yalikosekana Rwanda wakauwana.. Somalia, wanaendelea, Libya, Syria, Mali, Zimbabwe, Kenya, Misri, Burundi, Yemen, .....
   
 6. E

  EL HOMBRE Member

  #6
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nyerere alifanya vema ila watanzania tunapaswa kujifunza suala la ujasiri wa kudai haki linatoka moyoni mwa mtu siyo la kufundishwa kwa ninachowaasa ndugu zangu siku za kusubiri zimekwisha tuamke tuikomboe nchi yetu sote tuwe wamoja tushikamane kwa nguvu ya uma tutafanikiwa
   
 7. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #7
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Tulidanganywa tume ya katiba kuapishwa mwisho wa mwezi mara ghafla kumbe wameshaitana ikulu walio na taarifa ni spika wa bunge na gazeti la uhuru kuna nini hapo
   
 8. S

  SAIDALI Member

  #8
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hamia somalia , kama hupendi amani, kwanza jiulize wewe una inafaida gani na tz.
   
Loading...