Nyerere katika kuwabeba wahindi na matokeo yake kwa Mtanzania wa sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere katika kuwabeba wahindi na matokeo yake kwa Mtanzania wa sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jagermaster, Dec 30, 2011.

 1. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [FONT=&amp] Nimekuwa muumini mkubwa wa Mwalimu Nyerere baba wa Taifa hili kwenye mambo mengi aliyofanya Tanzania wakati wa utawala wake. Kama mtanzania mweusi wa Taifa la Tanganyika naomba tu nilikili kuwa katika vitu ambavyo Mwalimu aliboronga katika utawala wake, ama kwa makusudi kabisa au kwa wivu wake ni hili kukataa kuwanyima uraia watu wa jamii ya kihindi, Pakstani na South Asians baada ya uhuru, aumuzi ambao ulikuwa ukipingwa vikali na chama cha ANC ambacho kabla ya Uhuru kilikuwa na slogan ya Africa for Africans.[/FONT]

  Ndugu zangu kwa wale Political Scientists, Sociologists, Lawyers, Economist n.k Napenda kuwakumbusha Theories za Structural Functionalism ambazo hasa msingi wake ilikuwa ni kujenga matabaka katika jamii na kila tabaka likiwa na kazi zake za kufanya katika jamii. Utaratibu huu ulitumika sana kwenye makoloni na kwa Upande wa Tanganyika kulikuwa na matabaka matatu, ya Wazungu (Rulers), Waasia (Busnessman and assistants in white collar jobs) na weusi (vibarua). Utaratibu huu pia ulitumika kwa nchi za Uganda, na Kenya kwa ukanda wa Africa Mashariki. Kwa upande wa Zanzibar waliamua kuretain waarabu kama tabaka la kati. Kama tunavyojua nchini Rwanda na Burundi Wabeligili waliwatumia watu wa jamii wa kitutsi kama tabaka la kati ili kuweza kufanikisha mambo yao

  Mwandishi Erik W. Larson katika makala yake ya mwaka 2007 yenye kichwa cha makala NATION-STATES CONFRONT THE GLOBAL: Discourses of Indigenous Rights in Fiji and Tanzania akielezea jinsi gani Tanzania na Fiji zinavyotekeza maazimio ya Umoja wa Mataifa katika tafsiri tofauti na ilivyokusudiwa na UN, anaeleza wazi mgogoro uliokuwepo Tanganyika wakati wa harakati za Uhuru , pale ambapo Wahindi na jamii nyingine ya watu wa Asia alivyokuwa ikionyesha dharau, kejeli kwa watu weusi kuwa waafrica hawazi kujitawala.
  Baada ya Uhuru kulikuwa na vyama vingi, kama ANC vilivyokuwa vikishauri kuwa kazi ya kuondoa tabaka la wazungu ilikuwa ya ya kwanza sasa kilichokuwa kikifuata ni kuondoa pia tabaka la Waasia. Nyerere hakukulibali kabisa wazo lile na hapo ndipo ninapomlaani Nyerere na kuona alikuwa mpenda sifa, na madaraka wala hakuenda kukomboa tabaka la weusi wa Tanyanyika. Akijua wazi kuwa wahindi walikuwa waki-ocuppy tabaka la wafanyabiashara, akaleta policy kuwa Tanganyika ni nchi ya wakulima na wafanyakazi kwa maana nyingine badala ya serikali kuanza kujenga tabaka la wafanyabiashara weusi baada ya uhuru Nyerere alichofanya ni kuhubiri na kujenga Taifa la wakulima na wafanyanya kazi, huku akiacha jamii ya watu wa asia wajiimarisha kwenye biashara na weusi wakiwa maskini wa kutupwa. Kuna watu wengi walimpinga kwa hili, hata jaribio la mapinduzi la mwaka 1964 linaelezewa kuwa ndio sababu hasa iliyosababisha mapinduzi yale, kwani waafrika wengi walichukia kitendo kile kama kinavyoeleza kipande hiki cha Aminzade(2000) "Julius Nyerere's 1964 declaration that Africanization was dead and that Asians and Europeans would be allowed to join TANU generated intense protest, including an abortive military uprising, the repression of which temporarily put an end to the public debate over racial issues. Individuals and political parties advocating racial nationalism fell victim to laws instituting a single-party state and restricting freedom of association and assembly".

  Hii hali ilikuwa tofauti kabisa kwa nchi za Uganda na Kenya. Hawa walifanya effort za wazi kabisa kuhahakisha tabaka la hawa cockroach linaondoka. Kenya waliwapa wakati mgumu sana kupata uraia na Uganda waliwatimua kabisa. Nchi hizi zemeweza kujenga tabaka la middle class weusi wa kutosha licha ya mapungu ya kikabila ambayo yapo lakini kuna weusi wengi ambao wanaweza ajiri weusi wenzao. Angalia Tanzania ya sasa kila kitu kimeshikwa na Wahindi na waarabu, sio biashara ya mafuta, viwanda, mahotel, mpaka tender za serikali. Watanzania weusi tumekuwa vibarua tu katika nchi yetu, opportunity zote mpaka ufundi mchundo sasa unachukuliwa na waasia na waarabu, weusi tunapeana sumu wenyewe kwa wenyewe, wengine wanasema tupo kama senene ndani ya chupa, hatupumui hatutoki, wale walibahatika kureplace tabaka la wazungu nao wako busy kujiweka sawa ili wabaki kwenye tabaka hilo pamoja vitukuu vyao, nao pia wanashirikiana na tabaka la watu jamii ya ki-Asia katika kufadhiri hizo wanaita kampeni ambazo wanagawa vi tshirt na kanga kwa akina mama weusi vijijini na kuwasahau mpaka baada ya miaka mitano, nchi imegeuka jina inaitwa bongo, hakuna mtu anastuka kuwa hili jina baya au zuri kwa nchi.

  Watu tulilishwa sumu na Nyerereism, wala hatuoni mbele wala Nyuma mtu akitetea haki za watu weusi kama Mtikila huwa wanachekwa, (sijui huko wapi huyu mzee maskini, mzee nae kaona ale kivyake). Iddi Simba aliwahi anzisha mambo ya uzawa alienda kubanwa huko wanakoita kikao cha NEC naye kimya sasa. Lakini tutake tusitake hili swala Nyerere alifanya makosa makubwa, hata yeyé waatalamu wa mambo wanasema aligundua makosa na mpaka alifikilia Azimio la Arusha. Lakini mtu mzima hakupenda ona naye aonekane anakosea akaamua kula ganzi na ndio sasa tunaumia. Inasigitisha sana Nyerere alikuwa kinara katika mapinduzi ya Zanzibar katika kung'oa utawala wa waarabu ila hakuweza ona kama Wahindi ndani ya Tanganyika ni tatizo mpaka anaenda kaburini. Sasa aanza kuamini kuwa mwalimu wala hakuwachukia waarabu ndani Zanzibar bali aliuchukia uislam na kuona utawala wa sultani ni kitisho kwa ukatoliki katika ukanda huu.

  Ukiwa Dar es Salaam kwa mwananchi wa kawaida kwa siku lazima utumie bidhaa ya jamaa mmoja anaitwa Azam, lakini ukijaribu kuuliza ni vijana wangapi wanafanya kazi kwa azam atleast wamejenga nyumba za kuishi atleast yenye standard flan, ni almost hakuna. Kitu kama kama hiki kwa nchi ambazo nimewahi ishi kwa uzoefu wangu ni lazima kungekuwa na watu middle class ambao wanafanya kazi huko kweye viwanda vya juice, unga, ice cream. Ukiuliza unaambiwa wapo lakini si weusi.

  Kwa kuwa weusi wa Tanganyika wamekuwa ni vibarua wa muda mrefu sasa imefikia hatua tunaogopa shirikisho la ajira la Africa Mashariki. Hili kweli kabisa kwa kuwa watu ndani ya Tanganyika tumekuwa vibarua katika nchi yetu kwa muda mrefu. Yatupasa kuvuta pumzi kabla hatujajichanya na wakenya lasivyo hata ile subordínate position tuliyonayo kwa wahindi sasa itachukuliwa kiulaini sana Wakenya pamoja na Waganda.
  Ningependa kusema Nyerere alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kutuungasha watu weusi kuwa kama kabila moja lakini hakufanikiwa kuaanzisha middle class baina ya watu weusi na badala yake aliacha ngedere wale mahindi shambani huku watu weusi wanapiga jembe vijijini, aliacha wahindi watambe kwa biashara, huku ikiwa marufuku kwa watu weusi kufanya hivyo. Hakika alirithi utaratibu wa wazungu na pia inaoneysha wazi alikuwa na wivu hakupenda aonekane mtu mweusi ana hela Tanzania, tena mbaya zaidi akiwa na hela zaidi yake. Ni wazi kabisa aliona bora mhindi aonekane ana hela na anatumikisha watu weusi, hakupenda ona mwafrika anaajili mwafrika mwenzake, alipretend aonekane kuwa yeye ni Marxist huku ikijulikana wazi kuwa hakuwahi kuwa Marxist, aliweza tu kutumia Marxism katika kukandamiza mtu mweusi asimwajiri mweusi mwenzake,uku ikiwa halali kwa mhindi kuajiri mtu mweusi, wala hakuweza tambua kuwa communism iliyohusudiwa Russia na China iliwahusu watu wa race moja na wala hakutambua kuwa wahindi waliletwa na wakoloni. Mpaka sasa ametuacha vibarua ndani ya nchi yetu tukiendelea kutumikia wahindi viwandani miaka hamsini ya uhuru, ameacha wakati mgumu sana kwa marais walimfuatia maana tayari walishabanwa na sheria za kimataifa kibao.Hili swala ni kama taboo kwa Tanzania, ukiliongelea kwenye public unaonekana muasi, watawala weusi wameamua kufumba macho vibarua weusi wanapata shida na wala hakuna Chama cha Siasa kinacholizungumza kwa wazi na kuona kama ni tatizo. Debate zimediverge kwenye mambo ya udini,muungano na shirikisho la Afrika Mashariki, lakini kirusi kinachoangamiza watu weusi tangu Uhuru ndani ya Tanzania hakiongelewi. Mimi kuanzia mwaka 2012 naahidi kutumia elimu yangu katika kuandika jinsi gani TABAKA LA WAASIA "RAIA WA TANZANIA" WANAVYOIRUDISHA NYUMA TANZANIA TOKA UHURU NA KIPI KIFANYIKE ILI KUNUSURU RAIA WEUSI.
  [FONT=&amp]
  Ndugu zangu mabadiliko yanaanzia kwako, usione uko upo kwenye kiti cha kuzunguka na kiyoyozi au uko kwenye gari umefunga vioo unawaona watanzania wako nje ya mageti ya viwanda vya wahindi wakisubiri kuitwa ndani kama itakuwa bahati yao kwa siku hiyo, ukafikiri wewe umesalimika. Usione Zimbabwe mpaka leo wanasumbuka kuling'oa tabaka la settlers ndani ya nchi yako wewe wajiona uko salama. Tena afadhari ya Zimbabwe kwani mpaka hii makala inaandikwa tayari kuna malalamiko kuwa watu wa jamii ya Asia wanazidi kuingia Tanzania kwa kutumia procedure dhaifu za Uhamiaji. Hao watu wanaingia wala hawaonekani wanayoondoka, ikiwa na maana wapo na wanazidi kujazana. Tabaka hili halina mpango wowote kwa maendeleo ya Tanzania bali kuvuna chochote watakachoona mbele yao wakitumia njia nyeupe ambayo Nyerere aliwatangenezea tangu Uhu
  ru [/FONT]
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Lakini mpaka leo Tanzania ni nchi ya wakulima na wafanyikazi.
   
 3. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ikiwa na maana na wahindi pia ni wakulima na ni wafanyakazi. This is ridiculous!
   
 4. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wasomi kama Shivji pamoja na kuandika vitabu vingi na maaruku kama Class Struggle in Tanzania, hajawahi andika kuhusu race struggle in Tanzania na jinsi gani mfumo uliopo unavyowabeba wahindi kwa kuwa na yeye ni Mhindi. Waafrika amkeni tusilishwe pumba tu muda wote,
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hapana. Sijasema hivyo. Majority ya Waafrika unaowatetea ni wakulima na wafanyikazi na Nyerere alilitambua hilo. Hivi percentage ya wahindi Tanzania populationwise ni kiasi gani?
   
 6. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  There are currently over 90,000 people of Indian origin in Tanzania. Many of them are traders and they control a sizeable portion of the Tanzanian economy. Indians have a long history in Tanzania starting with the arrival of Gujarati traders in the 19th century. They came to gradually control the trade in Zanzibar. Many of the buildings constructed then still remain in Stone Town, the focal trading point on the island.
  Post independence, the leadership of Julius Nyerere ensure peaceful transition and equal representation for all Tanzanian people, thus escaping the conflicted path taken by Kenya and Uganda.
  Still some Indians migrated overseas to the United Kingdom, United States and Canada. Some have achieved great prominence, most notably the late Freddie Mercury (born Farouk Bulsara into the Parsi community of Stone Town, who reached fame as the lead singer of the rock group Queen).
   
 7. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wahindi ndio washika vikoba wa viongozi wetu, hakuna kiongozi hata mmoja anaemwamini mtu mweusi mwenzake, pesa zote za ufisadi uliotukuka tangu enzi za Mwalimu na Karume walikabidhiwa wahindi au waarabu ili kiongozi asionekane nazo, kwa hiyo wahindi ni muhimu sana tanzania watusaidie viongozi wetu waonekane watumishi safi kumbe kila mmoja ana chake kwa muhindi.
   
 8. k

  komredi ngosha JF-Expert Member

  #8
  Dec 30, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 381
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hua inaniuma sana kila siku jioni nikipita pale mtaa wa kisutu kwenda kupanda gari posta kuelekea nyumbani Tandika kwa walalahoi. Jamaa wanafaidi nchi balaa. Na kinachosikitisha zaidi, licha ya kupata faida kubwa hawana mpango na maendeleo ya Tz wanaenda kujenga na kuendeleza nchi yao hapa ni pa kuchumia tu.

  niliwahi kusikia story kua wahindi wageni hua wanakuja nchini na kufadhiliwa chakula na malazi pamoja na pesa kwa muda flani. Muhindi mgeni atafungua akaunti benki halafu kila siku asb atapeleka pesa na kuitoa mchana kwa muda wa miezi 6 au zaidi. Baada ya hapo, akiwa tayari ameshapewa jengo la biashara ataenda benki na kuomba mkopo kwa kigezo cha kua na ofisi na biashara inayomwezesha kuingiza na kutoa pesa benki kwa kiasi kikubwa kila siku. Then atapewa mkopo wa kufa mtu!

  kuna muhindi mmoja alikua anatudharau wa Tz kua alipokuja wakati bado mgeni alianza kuvaa mashati ya kijani na suruali nyeusi. Uhamiaji na police hawakumgusa kuhusu kibali

  #wewe nenda India uone utakavyopokelewa.
  Ukitaka kujua wanavyofaidi, nenda South Beach au sehemu nyingine nzuri ya kula raha uone utofauti au tembelea mtaa wa kisutu saa 1 usiku

  wahindi ndio sumu ktk nchi hii
   
 9. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #9
  Dec 30, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,554
  Trophy Points: 280
  Viongozi wetu wanaogopa wasibaniwe kwenda Appolo! Lakini wakumbuke wanakwenda kama wateja wengine tu,wanatumia pesa.tumechoshwa na wimbi hili la kutisha la wahindi tena wadanganyifu wakisaidiwa na uhamiaji! wahindi wamewaweka kiganjani Uhamiaji wakati mwingine wakisaidiwa na Viongozi wazito sababu ni washirika wenzao kibiashara! Serikali isipochukua hatua sasa kwa kubadili mfumo wa kutoa vibali na kuanza rasmi ukaguzi wa vibali vilivyotolewa maofisi yote na kwenye makazi yao Kariakoo,upanga na mnazi mmoja wajue wanaandaa chuki za wazi za Watanzania kwa wahamiaji hawa haramu! Kila siku wanakamatwa wasomalia sababu hawana cha kuhonga na si tishio kwa ajira kama hawa wahindi! Ndio wahindi wanawekeza sana Tz lakini isiwe sababu ya kujaza kihuni wenzao na kuajiri wabongo wachache kuzugia tena wengi vibarua tu! Tunataka hatua za haraka!
   
 10. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #10
  Dec 30, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,554
  Trophy Points: 280
  Lema wewe ni waziri kivuli wa mambo ya ndani chukua hatua,anza na uhamiaji,pameoza pale! Hawa waasia ndio wakwepa kodi mabingwa kiujanjaujanja! Asilimia kubwa ya makampuni yao kila mwaka ni hasara tu!
   
 11. F

  Fahari MJ JF-Expert Member

  #11
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 425
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe unawaita "wahindi" na unachambua kuwa nyeree aliwabeba. kuna wengine hao unawaita wahindi kitendo cha shule zao kutaifishwa kuna watu humu wamendika unyanyasaji wa nyerere kwa "waislam" na alivyodumaza maendelo ya waislam. hapo wanatumia mifano ya shule za aghakhan. Utaawaambiaje watu hao
   
 12. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #12
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  sera za kikatili za Adolph hitler, zaingia tanzania kilaini! mtoa mada hajajifunza kwa nini german ilipoteza usafu mwamba wa dunia kwa kutumia sera za uzawa. waliwatimua wayahudi wote na wengine milion sita kuuwawa . hili liliwacost wajerumani kumpoteza mwanasayansi Alberto Aistein ambaya alikuwa myahudi aliyekimbilia marekani na kutengeneza bomu liliwapa usafu mwamba wa dunia marekani.

  kero ya wahindi tanzania naijua, lakini kinachotakiwa ni katiba yetu sisi ambayo ikiwa kali hata hao waliopo kizamiaji watajikuta ni vibarua ndani ya chi ya watu weusi. siku zote raisi akiwa ana sauti kubwa kuliko katiba, nchi haiheshimiki kamwe na huisha kuibiwa mali na wageni. tiweka kifungu cha kuwa raisi lazima shitaki mara baada ya kumaliza muda wake, adhabu ya kifo kwa wala rushwa na wahujumu uchumi, matatizo ya uhamiaji na tabia yao ya kuomba rushwa itatoweka mara moja.

  halafu mwamndishi kajichafua mwenyewe aliposema nyerere alikuwa na chuki na uislamu na kuupenda ukatoliki. sasa maada hii imekujaje na hili swala la uzawa?
  mwisho. lazima ujue kuwa dar es salaam, haikujengwa na mkoloni bali ni mhindi. unajua hilo? sehemu zote tanznaia alipata kukaa mhindi ni bomba kijadi, ila ambazo mhindi hakukaa ni debe tupu. Ona Songea, singida, lindi na mtwara ni ziii kabisaa. Ona mbeya, mwanza , arusha, Dar na tanga. hivyo hawa wahindi nao wana faida zao kuliko hata swala lako la uzawa.

  halafu ukija katika shule , agakhan kajenga sana shule tanzania . kwa kifupi sera zako za chuki na uzawa hapa si mahali pake.
   
 13. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #13
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,435
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Kwa taarifa uchumi wa tz uko mikononi mwa wahindi, ndio walikuwa CCM damu sasa wanapima upepo na kuanza kusuport upinzani ili maslahi yao yasipotee.
  Biashara ya retail na whole sale kwa bidhaa zote muhimu iko mikononi mwao except pombe kutokana na imani zao.
  Sukari, mafuta ya kula, sabuni, viberiti, chumvi, maziwa, pads, toilet papers n.k bidhaa zenye turnover iko mikononi kwao na marufuku mswahili kutia mikono mpaka ngazi ya retail.
  Ndio maana id amin aliwafukuza ili uchumi uwe mikononi kwa wazawa bongo tunajaza thread jf lakini wazalishaji wahindi, wasambazaji wahindi sie ni wachuuzi tu
   
 14. W

  WildCard JF-Expert Member

  #14
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  NHC ya sasa na kabla ya hapo kulikuwa na Msajili wa Majumba ziliundwa na nyumba alizotaifisha Mwalimu kwa WAHINDI. Nyumba hizi zingekuwa za Wachagga, Wakurya, Wanyakyusa, Wahehe,...., ingekuwaje? Kumbuka pia ni nyumba hizi walijenga kwa jitihada zao na mbaya zaidi hawakufidiwa.
  Wahindi waliondoka kwenye UTUMISHI wa UMMA miaka mingi iliyopita pia. Wakabaki wanasiasa wachache akina Amir Jamal waadilifu kwelikweli kuliko wazawa wenu wengi.
   
 15. kingadvisor

  kingadvisor Senior Member

  #15
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda ni-commend kidogo

  1.Kuhusu Nyerere kuita nchi ya wakulima na wafanyakazi ilikuwa ni slogan ya kisiasa ya kuungwa mkono apate kura maana ndio walikuwa wengi hakuhitaji kura za wafanyabiashara walikuwa wachache na kura zao hakuziona za maana.Siasa kushinda unalenga walio wengi wakukubali.Njia hii ilitumika nchi nyingi tu ambako kuanzia URUSI,CHINA,CUBA,ULAYA MASHARIKI N.K na zilifanya waliotumia slogan hiyo wakachukua nchi na Nyerere aliitumia nchi akaipata na akaendelea nayo hadi alipoondoka hakuna aliyemmudu kumtoa.Sasa hivi ndio viongozi wengi wanatishiwa nyau na wafanyabiashara hadi kuyumba maamuzi but stilll wakulima na wafanyakazi ndio wengi kiasi kuwa wanakosa tabaka maalum la kuwaunga mkono.Wanasiasa wa sasa wanaelea hewani Si CCM si CHADEMA,si CUF n.k hawana tabaka maalum la kuwa-support kama wakati wa Nyerere.Ndio maana kuna myumbo wa kisiasa ambao si afya sana kwa ustawi na utulivu wa Nchi.Nchi huongozwa na matabaka lakini unatafuta tabaka ambalo ni majority na popular na linakubalika.Ndio maana enzi za mwalimu viongozi walitoka tabaka la wakulima na wafanyakazi wakiwemo watoto wao akiwamo mtoto wa mkulima waziri mkuu PINDA.Wafanyabiashara walikuwa out of equation ndio maana watoto wengi wa wakulima na wafanyakazi ndio wamefurika maofisi ya serikali na mashirika ya umma na wahindi hawapo!!!! Nyerere alikuwa akiliendeleza na kulipa ajira tabaka hilo alilokuwa akitawala nalo.Wakulima na wafanyakazi saa hii baada ya ubepari kuanza kuingia wameanza kulia kilio cha ngedere.Ubinafsishaji,Globalization,uwekezeji etc ni maneno tu lakini ni mapinduzi ya kijeshi ya kupindua tabaka la wakulima na wafanyakazi na vizazi vyao ni kulitimua madarakani na kuweka wafanyabiashara na vizazi vyao madarakani.Tanzania tuko kwenye process ya kupindiluliwa ndio maana hadi sasa baadhi ya viongozi hawaishi kupiga magoti kwa wafanyabiashara.

  2.Kuhusu wahindi kutotimuliwa au kubanwa baada ya uhuru ni kuwa nchi hii ilikuwa inatawaliwa na wazungu na wahindi walitawala kupitia mlango wa nyuma wa biashara na vyeo serikalini.Tuipopata uhuru nchi ikajikuta haina watawala wasomi sababu wazungu walitimka.Tukabaki na wahindi wasomi wachache serikalini ,majeshini na mashirika ya umma .Serikali haikuwatimua hawa wahindi waliokuweko sababu bado walikuwa tegemeo.Wakaachwa lakini wengi wao walikuwa kifanya kazi kwa shingo upande sababu hawajazoea kutumwa na mweusi kwa hiyo kazi nyingi walifanya chini ya kiwango Nyerere akazira hakutaka tena kuwaajiri wengine pamoja na kuwa vijana wa kihindi wasomi waliosomea India na UK walikuwepo akaamua asomeshe watu wake bure apate wataalamu wake watoto wa wakulima na wafanyakazi.

  Pia hakuwatimua wafanyabiashara wa kihindi wala kuwabana kwa kuwa ndio walikuwa wenye biashara kubwa na walipa kodi enzi hizo.Serikali yake ilihitaji kodi ijiendeshe hakukuwa na ruzuku kutoka Uingereza tena sasa kama angewatoa ingesumbua waafrika weusi walikuwa hoi si wakulima si wafanyakazi akawaacha waendelee kumlipa kodi ajenge nchi.Lakini wakati huo akisomesha weusi hadi kuwa maprofesa wa biashara ili washike biashara baadaye.Lakini kama waliishia kuwa maprofesa wa biashara bila kuwa na biashara si tatizo la Nyerere ni lao binafsi.

  Kuhusu kuwawezesha wafanyabiashara weusi Tanzania wakati wa Nyerere hata baadhi ya maraisi waliofuata ilijitahidi.Mfano kulikuwa wakati makampuni ya kiswahili yalikuwa yakiomba na kupewa tenda serikalini au mashirika ya umma walikuwa wakipewa pesa kabla ya kuanza kazi Ili kuwawezesha wafanyabiashara walalahoi wafanye ile kazi hiyo waliyoshinda tenda.Kilichokuwa kikitoa wanazila hizo pesa,wanalewa kwenye mabaa na tenda hawazitekezi kabisa au wakitekeleza wanazifanya chini ya kiwango cha hovyo kabisa.Ule ulikuwa uwezeshaji wa weusi ila wali-abuse serikali ikaona inakula hasara ikautupilia mbali mpango huo na kuamua kuwa acha watu washindane tu na walipwe wakishaleta vitu sasa hapo ndipo kilio cha uzawa feki ndipo kinakuja ohh tuwezeshwe ! muwezeshwe mara ngapii? Hapo sasa ndipo wahindi wakarudi tena kwa nguvu baada ya mifumo ya tenda kubadilika.Cha msingi ni kuwa tabaka la wafanyabiashara weusi laweza kuingia sokoni na wako wanaofanya vizuri.Kinachotakiwa ni wawe waaminifu.Uaminifu ukiwepo serikali itawapa matenda,mabenki yatawakopesha n.k riba hata kwenye mabenki ni kubwa si kwa sababu tu ya gharama lakini sehemu kubwa wenyewe milango ya nyuma wanasema risk ya kukopesha wafanyabiashara weusi Tanzania ni kubwa mno hivyo lazima uweke Ile risk element kwenye Interest rate ndio maana ziko juu sana.Gharama za ufuatiliji nazo ziko juu mtu analkwambia ana nyumba analeta hati ya dhamana na picha ya nyumba ukisema twende tukaione anaanza kiswahili mara ilikuwepo hapa mara pale ila sasa haipo imechukuliwa na mafuriko uongo kibao.Kukosa uaminifu ni tatizo ndio maana kama utaendelea tutarajie wahindi kuendelea kushika biashara milele Tanzania.

  Kuhusu Idd Simba kuwawezesha weusi nadhani ni uongo Idd Simba alitaka kujiwezesha mwenyewe ndio maana alitimuliwa uwaziri sababu ya ile kashfa ya sukari alitaka weusi wapewe mianya akijilenga na akajilenga kweli wakamtimua.NEC iachwe si kweli Idd Simba ana uchungu na weusi wazawa.

  kingadvisor@yahoo.com
   
 16. M

  Mzee Kijana JF-Expert Member

  #16
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 748
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 80
  Kaka Shivji mwenyewe gabachori unategemea ataandika nn kuhusu Wahindi wenzake? Ni sawa na kesi ya kenge ukampa mamba. Hata hivyo nakubaliana na mengi uliyosema na kuna ukweli wa kutosha tu. Nyerere kwa kweli ni chanzo cha matatizo mengi ya Watanzania. Watu wamezungumza sana humu JF kuhusu maovu ya huyu mzee lkn kuna watu kama wamelishwa kasumba. Wao na Nyerere, Nyerere na wao!
   
 17. n

  ng'wabuki Member

  #17
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jana kulikuwa na makala kwenye raia mwema, wahindi wanataka kuwekeza kwenye makaa ya mawe na tayari huko kwao wanatmbulika ni wakwepa kodi, kamishna wa nishati na madini anaifagilia huyu nae ni nyerere?

  Pili RA nae kapigiwa kampeni za ubunge na mwenyekiti wake kuwa ni mchapakazi hajawahi kuona, je huyu jk nae ni nyerere?

  Acha kufikiria kwa kutumia miguu wewe
   
 18. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #18
  Dec 30, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Inawezekana ni kweli kuwa Amir Jamal alisepa na koba la Mwalim!
   
 19. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #19
  Dec 30, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45

  Amir Jamal muadilifu? Kwa nini alipostaaf alikimbilia Canada?
   
 20. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #20
  Dec 30, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Lazima viongozi wetu wakubali kuwa waasia wamewazidi ujanja wazawa na waweke mikakati ya makusudi ya kuwainua wazawa wa nchi hii vinginevyo kuna siku hii nchi itatawaliwa na wahindi na ndio utakuwa mwisho wetu.
   
Loading...