Nyerere: Ili nchi iendelee inahitaji Watu, Ardhi, Siasa safi na Uongozi bora

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,542
141,351
Nasoma moja ya vitabu vilivyoandikwa na hayati Julius Kambarage Nyerere, kwa kweli vimejaa hekima na busara.

Naipima Tanzania na vigezo vya maendeleo alivyoainisha Mwalimu Nyerere kwamba ni watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.

Bado sijajua Tanzania tunakosa nini katika hivyo vinne!

Je, kuna tofauti kati ya mtu na binadamu?

Nawasalimu kwa jina la JMT!
 
Kwa bahati mbaya sisi tumejaliwa ardhi na watu pekee. Huko kwingine ni upuuzi mtupu.
 
Tunakosa capital mkuu, hata kama ardhi yetu ina dhahabu na almasi kama mchanga, tunahitaji capital ili kunufaika na hizo rasilimali.

Lakini pia, siasa na uongozi kwa sasa tuna mapungufu makubwa sana. Connection kati ya uongozi na watu imekufa kabisa, kwa hiyo huwezi kufanya chochote.

Uongozi haupo tena kwa kunufaisha watu, na hivyo watu hawana mwamko wa kuendeleza nchi, bali kuangalia nchi inawezaje kuwaendeleza wao, iwe kwa kuiba au namna yoyote ya ufisadi. Ndio maana watu wanaiba hadi alama za ishara za barabarani, ili mradi tu waiibie nchi kitu fulani.
 
Kati ya hivyo vitu tatizo kubwa la Tanzania ni uongozi na siasa safi huwezi kuwa na viongozi wanaochaguliwa kwa ukabila,ukanda urafiki undugu bila sifa za kielimu ukatarajia maendeleo.

Siasa huwezi kuwa na siasa za kuuana, kufungana, kuzuia vyama visifanye siasa, kutumia dola kutisha wapinzani kuchafua chaguzi kuiba kura ukatarajia maendeleo
 
Tatizo kubwa la Tanzania kuliko yote, ni kikosa uongozi wenye uwezo na ulio bora. Ukikosa uongozi, hayo matatu ualiyobakia, hayana msaada wowote.
 
Back
Top Bottom