Nyerere Hakuwa na mapungufu, alikuwa Kiongozi Mbovu!

A government is an instrument of oppression (Prof. Chamungwana UDSM-RIP). Nyerere was heading the government and therefore he oppressed many! How comes that he is to be a Saint?
Unajuwa vigezo vya kuitwa mtakatifu! Kama ni mapungufu basi hata Mungu kuumba wengine weusi na wengine weupe, au vilema na wengine wafupi na wengine warefu alikosea, maana yangu kila kitu kilichofanyika wakati wake kilikuwa sahihi! Mnamsema hayo sasa kwa sababu kuna vitu vya kupigia mfano fananisheni na zama hizi mtuambie kama hamuoni chochote!
 
Mleta mada msimvunje sana moyo swali lake lina mantiki, jambo ambalo tunaweza kuliepuka ni kumlaumu moja kwa moja lakini tunaweza kuchukua nafasi hiyo kujifunza kutofanya makosa aliyofanya. Ni kawaida ya sisi watu weusi kutotaja makosa ya mtu aliyekufa, hili naona ni utamaduni mbaya unaotunyima watu nafasi ya kujifunza. Mtu anakufa kwa ukimwi watu tunaishia kusema bwana ametwaa! ametwaa kwa namna gani hatutaki kusema matokeo yake watu wanaendelea kufa.

Sasa basi kwa kuchangia kidogo kwa mleta mada ni kweli Nyerere alifanya mambo mengi mazuri mojawapo ni kutusaidia sisi watoto wa maskini anglau kupata elimu bure. Lakini pia kuna mambo ambayo yalimshinda mojawapo ikiwa ni uchumi. uchumi wa kijamaa ni mfumo ambao haumfanyi binadamu kujituma ili kazi yake iwe na tija (efficiency). mkiwa na kitu kinaitwa chetu ni tofauti na kusema changu. Mungu amemuumba binadamu kiumbe kinachotaka kulimbikiza mali kwa hiyo kama kiongozi unatakiwa binadamu umuache na tabia yake ya asili alimbikize mali awezavyo lakini uhakikishe analipa kodi stahili. Hili ndilo walilofanya watu wa magharibi - Private ownership of means of production.

Hata wachina tunaowasifia leo mtawala mmojawapo aitwaye Deng Xiaoping aliona mfumo wa ujamaa wa Karl Max and Lenin wa Urusi hautawapeleka mbali, akaruhusu private ownership kwa watu wake matokeo yake leo tunayaona kila siku tunawasifia kwa hatua waliyopiga lakini hatujiulizi wamefikaje huko.

Ya kuchangia ninayo mengi lakini acha niishie hapa.
Mkuu umenena vyema, lakini tunapaswa kujiuliza pia, Je, upi ni ukomo wa hiyo asili ya binadamu kupenda kujilimbikizia mali? Na ni wapi ukomo huo ulifanikiwa kumfunga binadamu na kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi, chini ya hiyo Private ownership?

Muhimu pia kujiuliza upya, Je, Ubinafsi ndio Asili pekee ya binadamu kiasi kupaswa ku-shape kila aina ya mfumo Wetu?

Je, kuna binadamu anayeweza kuishi mwenyewe pasi kufungamana na mwingine? Kama hayupo, je mahusiano ya mtu na mtu katika kufungamana kwao yanaweza kulindwa na Ubinafsi?
Mungu wetu Anaita sasa!
 
N
Unajuwa vigezo vya kuitwa mtakatifu! Kama ni mapungufu basi hata Mungu kuumba wengine weusi na wengine weupe, au vilema na wengine wafupi na wengine warefu alikosea, maana yangu kila kitu kilichofanyika wakati wake kilikuwa sahihi! Mnamsema hayo sasa kwa sababu kuna vitu vya kupigia mfano fananisheni na zama hizi mtuambie kama hamuoni chochote!
Nakataa utakatifu, lakini ni mfano wa kuigwa na haujawahi tokea na labda hautatokea. Anastahili sifa zote, tena zote narudia tena zote ila UTAKATIFU!
 
Mkuu umenena vyema, lakini tunapaswa kujiuliza pia, Je, upi ni ukomo wa hiyo asili ya binadamu kupenda kujilimbikizia mali? Na ni wapi ukomo huo ulifanikiwa kumfunga binadamu na kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi, chini ya hiyo Private ownership?

Muhimu pia kujiuliza upya, Je, Ubinafsi ndio Asili pekee ya binadamu kiasi kupaswa ku-shape kila aina ya mfumo Wetu?

Je, kuna binadamu anayeweza kuishi mwenyewe pasi kufungamana na mwingine? Kama hayupo, je mahusiano ya mtu na mtu katika kufungamana kwao yanaweza kulindwa na Ubinafsi?
Mungu wetu Anaita sasa!

Hulka ya binadamu kupenda kujilimbikizi mali haina ukomo, hulka si rahisi kuiacha, tabia ni rahisi binadamu kuiacha lakini si hulka, hulka ni tabia ya mtu kuzaliwa nayo. Kwa maana hiyo basi ktk kutaka kulimbikiza mali huyu mtu anatafuta fursa usiku na mchana, kwa kufanya hivyo anatafuta usaidizi wa watu wengine ili aweze kufikia lengo lake, kwa maneno mengine anabuni ajira za watu wengine na wenyewe wanaanza kufurahia juhudi za huyu mlimbikiza mali.

Kwa juhudi hizi za mlimbikiza mali serikali inapata mapato zaidi kwa kuwa analipa kodi mbalimbali kadri anavyopata. Kwa hiyo mafungamano yataendelea kuwapo maana wanategemeana.
 
Mkuu nafikiri labda nimeshindwa kuuliza namna ya kueleweka haraka... Tunaposema HULKA ni wazi tunahusisha Matamanio na matendo yake mtu, niliposema Ukomo nilimaanisha, nini ni kifungo cha Matamanio ya binadamu? Nini kina-guarantee zao la hulka zake mtu kuwa Furaha kwa jirani zake na si maumivu na unyonyaji na unyonge? Na wapi hicho kifungo kimefanya kazi hiyo? Ni wapi huko ubinafsi umeleta furaha kwa wengine? Anaita sasa.
 
Ngoja tuongee kwa lugha nyepesi, mimi nikifanya kwa bidii nikawa tajili nakuwa nimekunyonya wapi wewe ambaye unalala bila kufanya kazi? kuwa kwangu maskini hakukufanyi wewe kuwa tajili and vise versa.

Hulka ya mlimbikiza mali inakuwa furaha kwa wengine kwa kuwa atawapa ajira kwa sababu hataweza kufanya kila kitu yeye mwenyewe kwa kuwa katika process ya ulimbikizaji inahitaji watu wengine wamsaidie.
 
Mkuu nimependa analysisi yako, zikiletwa mada za kufikirisha kama hizi wabongo wengi hatupendi, Hicho kitabu hapo juu najua itakuwa ngumu kukipata lkn je unaweza kudadavua kidogo kwa ufupi nini kiliongelea?

Kujadili mambo ya mabaya ya watu waliokufa sisi waafrika tunaona ni uchuro lakini ni namna ya kureflect mkaona ni wapi yalifanyika makosa ili msiyarudie tena. Angalia serikali ya sasa hivi inachofanya, inarudi kule mkapa alikoitoa kutoka kufanya biashara kwenda kuwa mwezeshaji kutunga sera zitakazowezesha sekta binafsi kuendesha uchumi. Sasa hivi serikali inaona private sekta ni enermy of the state, wanataka kila kitu kifanywe na serikali. Moja ya sababu ya hili ni kutojifunza kutokana na historia. Wanasema huyu mtu ana nia njema but we have to evaluate the consequences of implementing the 19th centrury type of socialism.
Mkuu ktabu kina mengi ambayo sio tu dunia bali wachina walipaswa kutokukisoma maana kingefanya nchi isitawalike.
Kiliandikwa kwa siri kwa mujibu wa vyanzo vya kimagharibi. Baada ya Waziri mkuu Zhao Ziyang Kuwa upande wa Wanafunzi waliokuwa wanaandamana na kupinga amri ya Serikali ya kusambaratisha waandamanaji wote kwa jeshi na vifaru, Na yeye alionekana katikati ya waandamanaji na kutoa speech ya kuwasihi waondoke wasije wakakumbana na mkono wa dola aliishia kifungo maisha yake yote hadi anakufa January 2005. Mauji ya waandamanaji hao wengi wakiwa wanafunzi yanajulikana kama Tiananmen Square Massacre.
Alijirekodi kwa siri akiwa kifungoni juu ya baadhi ya vitu alivyoona haviko sawa, Hakuruhusiwa kuonekana public, wala chapisho lake lolote kuonekana china. Hata mazishi yake yalikuwa sio ya kitaifa maana serikali iliogopa kama angeachiwa huru au aongee hata dakika mbili alikuwa ni mtu mwenye ushawishi wa hali ya juu na china yote ingekuwa vipande vipande.
West wanampenda maana alikuwa na element za kidemocracy.
Unaweza kusoma story yake Wikipedea, Au baadhi ya insights zake kwenye mitandao zikijadiliwa. Hata kwenye siasa za marekani juzi Trump alikuwa anatumia mifano kama ya Hiyo Massacre ili kujustfy baadhi ya maamuzi yake.

PAMOJA NA YOTE MZEE HUYU MIMI NAMKUBALI KWA JINSI ALIVYOUSUKA UCHUMI WA CHINA. Utamsikia Deng Xioping huyu hasikiki lakini huyu jamaa ndi founder wa EPZ, Special Exporting Coaster Cities na Chinese international trade archtect alikuwa kichwa balaa. Binafsi ni miongoni mwa wachina ninaowakubali sana sambambamba na Deng Xioping.
51fqsa-ubiL._SX327_BO1,204,203,200_.jpg

Hiki kinaelezea migogoro na zengwe kwenye chama cha kichina CCP. Alipotoa wazo la kutumbua watoto wa vigogo waliokuwa na Mali nyingi huku wazee wao wakiwa bado kwenye ngazi za juu. hapo ndipo alipoanzia kusakamwa na kufanyiwa fitna. Nimejaribu kuelezea kwa juu juu maana hata mimi najifunza bado kutoka kwa watu hawa wazito duniani.
 
Mkuu nakushukuru sana kwa historia hiyo, inawezekana mimi nilikuwa nikimsifu sana Deng Xiaoping kumbe kulikuwa na wengine ambao ni unsung heros. Thank you very much i appreciate for taking your precious time to educate me.
 
Umejitahidi kuyabainisha...ILA KUIBA KURA kwa kweli ni jambo la kishenzi kabisa yeye kama muasisi uchaguzi wa zanzibar 1995

Wengi wenu mnaomkashifu Nyerere asingewalazimisha baba zenu shule msingejua hata kuandika majina yenu.Pima kiwango cha mahali unapotoka na mwamko wa elimu wakati wa Mwalimu na baada ya utawala wake kuondoka.Ni kipindi cha Mwalimu tu kiwango cha waliojua kusoma na kuandika kilipokuwa juu kuliko wakati wowote.Fuatilia taarifaa za UNICEF.

Wapo jirani zetu mnaodhani wametuzidi sintaitaja jina nchi yao ila tafuta habari utapata ardhi yao inamilikiwa kwa Zaidi ya 50% na familia zisizozidi 10% ya raia wake. kwenu wengine hii ni misingi mizuri iliyoachwa kwangu huu ni wendawazimu.

Ni Tanzania tu usiyoweza kuilinganisha na nchi yeyote inayotuzunguka unapoweza kuwakuta raia wake wanaongea bila kubaguana kwa makabila wala dini zao,japo kuna wapuuzi wachache wanataka kuanzisha ligi hiyo.Nitajie nchi moja inayotuzidi kwa kuheshimiana iliyo jirani nasi niungane na ninyi.

Ni Nyerere peke yake ambaye watoto wake walisoma shule wanazosoma anaowaongoza/watawala.Nitajieni kashfa moja ya watoto wa Mwalimu iliyoathiri maslahi ya nchi.Wana kasoro zinazoathiri mambo yao tu si kuathiri maslahiya Taifa maana hakuwapa upenyo wa uhuni kwa cheo chake.

Ninayajua mapungufu mengi yaliyoiathiri nchi,napima chanzo cha mapungufu hayo na nia yake.Mizani inanionyesha mema yake yalikuwa mengi kuliko maovu.Mimi ni Mkristo,mktaba mmoja wa hovyo alioufunga na baadaye akaukiri ni kuikana Imani kwa kujiunga na miungu mingine kwa kuruka mnyama aliyetolewa sadaka kwa mizimu.

Alianzisha vijiji vya ujamaa bila maandalizi mazuri iliniumiza binafsi kwa kuchukua sehemu ya mashamba yetu ila tija yake ilikuwa kubwa.Shule ya Msingi niliyosoma ilikuwa umbali wa km 8 kutoka nyumbani wadogo zangu walisoma shule iliyo umbali wa km 1 kwa wengine hili si kitu kwangu ni jambo kubwa.

BWM tunayemsifu alipewa nafasi aliyopata kwa shinikizo na ushawishi wa Mwalimu.Ameuza mali nyingi zilizoanzishwa na kutunzwa na Mwalimu na uchumi ukatengamaa.Mimi pia nimerithi mali nyingi zilizoachwa na baba yangu na sijazalisha kuliko alizoziacha,sijioni kuwa ni bora kuliko yeye bali dhaifu kuliko yeye.
Tunamlinganisha Mwalimu na viongozi aliowasomesha ili hali yeye alisaidiwa na wataalamu wengi waliokuwa na uwezo wa kusoma na kuandika tu. Orodheni Watanganyika na baadaye Watanzania waliokuwa na digrii moja kuanzia 1961-1971 nitanyamaza.
 
huwezi sema eti baada ya miaka 50 nchi ya tatu duniani kwa kuomba omba na umasikini
na yeye Nyerere alitawala nusu ya miaka hiyo 50 halafu useme Nyerere was the best leader Afrika

that is insult to people with brain........
Huwezi kulinganisha mazingira na wakati aliotawala Nyerere na mazingira katika utawala huu... ni vitu viwili tofauti. Nyerere alitengeneza misingi ya utawala na maendeleo ya nchi hii (alikuwa katika wakati mgumu zaidi), waliofuata waliendelea kwa kile alichokiacha. Hivyo basi si sahihi kumlaumu Mwalimu!! Mafanikio mengi tunayoyaona leo ni kutokana na misingi aliyoiweka Nyerere!!
 
Tens ni kiongozi hovyo,kabakia kwenye hotuba tu,hivi jiuluze kiongozi mwadilifu aliyewezaje kutawala kwa katiba mbovu,hovyo yenye kila viashiria vya kifalme na kidicteta,ndiye chanzo cha umaskini wetu wa Leo,aliiweka serikali kiganjani,ndivo ilivyo Leo kila anakuwa raid anafuata anaweka nchi kiganjani,
 
Ngoja tuongee kwa lugha nyepesi, mimi nikifanya kwa bidii nikawa tajili nakuwa nimekunyonya wapi wewe ambaye unalala bila kufanya kazi? kuwa kwangu maskini hakukufanyi wewe kuwa tajili and vise versa.

Hulka ya mlimbikiza mali inakuwa furaha kwa wengine kwa kuwa atawapa ajira kwa sababu hataweza kufanya kila kitu yeye mwenyewe kwa kuwa katika process ya ulimbikizaji inahitaji watu wengine wamsaidie.
Bidii zako chini ya Ubinafsi wako zinawezaje kukufanya tajiri pasipo kumuathiri mwingine? Kama unataka tutangulize Ubinafsi, ni nini kitanizuia nisitoe ujira mdogo kwa waajiriwa wangu ili niongeze Faida? Na kama nitafanya hivyo, ujira mdogo unawezaje kuwa Furaha kwao?

Ni wapi huko tunakoweza shuhudia, Furaha ya mlimbikizaji mali imetoa furaha kwa wamzungukao pasi na maumivu, unyonge na unyonyaji?
 
Ni wazi kuwa hakuna shughuli nzuri ikakosa kasoro,hakuna binadamu aliyekamilika bali ni Mungu pekee ambaye hana mapungufu.

Katika maisha yangu kwa kiasi kikubwa wachambuzi wanaopata nafasi ya kumchambua Mwalimu Nyerere,hueleza mambo mazuri tu.

Katika majukwaa,mihadhara,mahojiano,mikutano na kadhalika. Kipindi cha nyuma sikuwa najiuliza sana kawa Baba wa Taifa angeweza kuwa na mapungufu katika utendaji wake.

Kama mnavyofahamu binadamu anafikiri kulingana na mazingira na taarifa anazopata. Kwa kipindi hiki ninajiona kuishi katika jamii ya kuhoji hususani ninapokuwa humu JF. Kwa muktadha huo nimepatwa na maswali kwamba ina maana Nyerere hakuna na mapungufu? Mbona hayasemwi sana ili kusaidia kujisahihisha.

Katika hotuba yake moja nimaskia akisema yapo mabaya waliyofanya katika serikali yake akaomba wasamehewe na yasiigwe. Ni yapi hayo?

Inaonekana kama ni dhambi Fulani hivi kueleza mapungufu ya Nyerere. Nakumbuka kipindi cha katiba mpya Mh.Tundu Lissu aliwahi kuainisha mapungufu ya Mwalimu(ingawa kwa kutumia baadhi ya lugha Kali) lakini ikawa kama mtu aliyemtukana Mungu. Kwa nini iwe hivyo?

Hata katika jamii nimejidhirisha kwamba jicho la kumtazama Mwalimu ni kama linataka kuwa na imani za kidini. Kuna baadhi ya Waislam hubeza sana "mazuri" ya Mwalimu. Na ni mara chache sana kukuta mkirsto ana anapiga matendo ya Mwalimu...Kwa nini iko hivi?

Katika kuelekea maadhimisho ya Tanzania bila Mwalimu,tunaomba wana historia mtu elimu vijana wenu,yapi yalikuwa mapungufu ya uongozi wa Mwalimu?

FaizaFoxy, Nguruvi3 barafu, paschal Mayalla Matola Mohamed Said Yericko Nyerere nk
 
Chipungahelo (huyu anayesughulikia miss Tz) akiwa anahojiwa katika kipindi cha Mkasi akasema.

"Siku hizi maisha yamebadilika, enzi hizo (za Nyerere) tumenunua Beetle (Mgongo wa Chura) lakini tukiwa tunarudi nyumbani unaipaki mitaa miwili nyuma, unashuka unarudi nyumbani kwa miguu. Tuliogopa tukionekana tuna gari tutaulizwa tumelitoa wapi"
 
Back
Top Bottom