Nyerere Hakuwa na mapungufu, alikuwa Kiongozi Mbovu!

Nimeongea na Waislamu wengi, kusema kweli hakuna anayemsema vizuri Nyerere pamoja na mazuri yake mengi na pia hakuna anayemsema vibaya Kikwete pamoja na mabaya yake mengi! Piga, ua, garagaza hapa issue kuu ni UDINI! Kwa upande wa Wakristo wamekuwa critical hata kuwaita akina Mkapa, Lowassa, Chenge, etc MAFISADI! Laiti kama Mkapa, Lowassa, Chenge, etc wangekuwa Waislamu ungeona sarakasi nyiingi za Waislamu za kuwasafisha! Anyway, asikudanganye mtu, major issue hapa ni UDINI, period! Ndio maana Waislamu bila haya wanadiriki kuwatetea mafisadi wa Ikulu MWINYI na SITI MWINYI, simply kwa kuwa alikwapua mafungu ya Ikulu kuwajengea misikiti! Fuatilieni mijadala ya Waislamu humu mtajua ninasema nini, maana mawajua kwa matendo yao!
Yaaniwewe umemaliza umemaliza. Tatizo kubwa ni udini unapelekea watu kujustify hata kitu cha uongo kabisa, hatakituykilichowazi. Mi naona MwlNyerere alichokosea ni kutaifisha Shule za Mission na kuwafanya hawa wasome baaaaasi.
 
Mwalimu alipoingia Madarakani alikuwa na wahandisi watatu tu,wataalamu wengine wachache sana! akajenga viwanda vya Nguo vingi na akaanzisha mashirika ya umma kibao,nikiwa mdogo nimekua nasikia mashirika kibao ya umma,viwanda nk,vitu hivyo alianzisha Nyerere aliye anza na wahandisi watatu tu.usitake kutudanganya hapa Nyerere alituachia mambo mengi ya msingi kabisa ambayo waliomfuata walipaswa kuyaendeleza! na hata yeye hakuwa malaika yale mabaya wangeyaacha.

Matokeo yake wameharibu mambo ya msingi kabisa ya taifa hili,walianza na Azimio la Arusha,wakauza mashirika yote,sasa madini yote yanakwenda wengine tumebaki kuwa watazamaji halafu unasema alikuwa kiongozi mbovu,ulitaka atufanyie kama Mobutu? Nchi sasa inaongozwa na watu binafsi wenye nguvu za pesa na masikini hatuna chetu ndiyo maana tunamlilia nyerere!

Hii ni kweli kabisa despite kuwa na wasomi wachache, resources chache alifanya makubwa sana. Hebu tembelea MorogoroViwandani ushuhudie.Mimi naamni kunajuhudi za makusudi kabisa za kupotosha ukweli. Mungu wangu Tanzania sijui tunaenda wapi. Hivbi sasa naomba uniorodheshee hata vitu 3 tu vizuri. Au uhuru wa Kuuza unga??????? Kuua Tembo? Kujenga matabaka? kukumbatia udini?? Nyerere angekumbatia udini sdijui kama wengine hata wangejua dunia inaendeleaje. Kunagenge la watu limetumwakupotosha.
Naomba kueleweka si kwamba hakuna alichokosealakini kumpima binadamu tunalinganisha mapungufu na mazuri . Nyerere alituliliana nasi mpaka kesho tutamlilia tena sana tu. Na kwa watu wa kipato cha chini enzi za mwalimu Elimuingewainua hebu niambioe sasa watainukia wapo, iwapopArdhi tu waliyorithi iko kwenye hati hati????
 
Asante sana mtoa mada kwa kuzidi kuwaelimisha WaTZ hasa wale wasiotaka kusikia mabaya ya Nyerere. Kwa kweli huyu mtu atabeba dhima kubwa sana mbele ya Mungu na Watanzania kwa ujumla kutokana na madhila aliyotuachia. Pamoja na hayo uliyoyasema mzee huyu alifanya utumbo ufuatao:

1. Alitumia fedha zetu nyingi kwenye harakati za ukombozi kusini mwa Afrika pasina kuwa na mkakati wowote wa namna nchi yetu itakavyonufaika na uhuru wa hizo nchi. Matokeo yake rasilimali zetu zimetumika, tumebaki masikini wa kutupwa na hao tuliowasaidia hawaonekani kuthamini mchango.

2. Alijifanya anapigania umoja wa Afrika kumbe ndio kwanza alikuwa anapanda mbegu za utengano kwa bara hili. Kumbuka huyu jamaa alipeleka msaada kule Biafra kuwasaidia waasi kujitenga na serikali ya Nigeria mwaka 1967.

3. Kwa uswahiba wake na Obote akaitumbukiza nchi yetu kwenye vita na Uganda mwaka 1978-1979. Watu waache ushabiki na kujitahidi kusoma vyanzo mbalimbali ili kujua chanzo halisi cha vita vya Kagera. Tuangalie namna Mwalimu alivyokuwa anawaunga mkono waasi wa Uganda na kufadhili harakati zao dhidi ya Amin. Uadui huu wa Mwalimu dhidi ya Amin ndio uliotutumbiza vitani. Uchumi wetu umeanguka, kumbuka tulitumia takriban dola milioni mia tano (USD 500,000,000) kugharamia vita hivyo (Soma: Structural Adjustment Programmes for Southern Africa by Mwanza)

4. Aliharibu elimu yetu kwa kutuingiza mkenge kwenye UPE na ESR.

5. Alikuwa diktekta mkubwa aliyetesa watu bila ya hatia (Soma: Ludovick S. Mwijage: The Dark Side of Nyerere's Legacy)

6. Sera mbovu za uchumi kama zile za Azimio la Arusha zimechangia kwa kiasi kikubwa madhila tuliyo nayo hivi leo.

7. Anahusika na vifo vingi vya watu wasio na hatia wakati wa utekelezaji wa sera ya vijiji vya ujamaa. Kumbuka maelfu ya Watanzania walipoteza maisha yao kwa kuliwa na wanyama wakali na magonjwa.

Ha Ha Ha . Uongozi wa sasa umetuweka Ahersa naona!!!
 
Alliopo amewavua wangapi?????? tunabeba viongozi wabovu kwa kuwa tu ni maswaiba au ndugu Shame on you!! Uzuri effect ya kiongozi unaemtetea itakupata hata wewe! Madawa ya kulevya, ufisadi, name it. Angalau wkt wa Mwalimu kulikuwa na haki. Ukiwa na akili utasoma mpaka mwisho wa upeo wako? Je Haki hiyo bado Ipo????? au upendeleo tu kwa kwenda mbele??????
Fuatilia ukitaka kujua ni mara ngapi.
 
JAmani Salaam,

Mimi ni mgeni humu jamvini, sijakuja kuazima jamvi, bali nimekuja kukaa, mtu ambae ameni "inspire" ni Faiza Foxy, sijui kama ni mke au Mme, ila nimependa sana jinsi anavojua kuwadadavua wale wanaojifanya wasomi na wenye dharau za hali ya juu, ..nakuvulia kilemba FAiza Foxy,

Ama kuhusu Nyerere! Jamani asiwaongopee mtu, huyu bwana alikuwa ni mtu mbaya tena jesusi nambari moja! mtu huyu si wa kumsifia hata kidogo, huyu ndie alosababisha mpaka uchumi wa Tanzania leo umfikia hapa ulipo, yeye ndio alodumaza watu wa dini fulani mpaka leo nimesoma comments nyingi sana humu nasikitishwa kuona either wasilamu au uislamu unadhalilishwa katika Tanzania hii lakini wamesahau kuwa sababu kubwa ni Nyerere!

Nyerere alitaifisha majumba mengi sana ya Waislamu ili kuwadhoofisha wasiendelee kwa sababu ya kulitumikia kanisa, alitaifisha shule japo zilikuwepo za katoliki lakini nyingi zilikuwa za agha khan, aliwadhoofisha waislamu kwa kumtumia benjamin mkapa wakati ule akiwa mtangazaji na alihakikisha anawagawa waislamu na pande mbili, waislmu jina na waislamu wenye imani ya kweli, akawachagua kina songambele na kawawa ambao hawana uchungu wa uislmu akawafanya ndio eti wakuu wa kiislamu nchini angalia vizazi vya watu hawa wawili kama kweli waliku ni waislmu safi leo tusingeshuhudia kizazi chao kilivo. \

Someni histoai, someni kitabu cha "the dark side of Mwl Nyerere" muone ubaya wa huyu mtu na vipi ameukandamiza uislamu kwa kutmia kanisa.

Ametulisha unga wa njano back in late 1970s huyu kwa kuingia katika vita ambayo si yake na ukisoma ukweli ilikuwa kumpinga amini kwa sababu alikuwa tu anataka kuendeleza uislamu pale Uganda, kwa sababu kanisa halikutaka haya basi akaingia katika vita isiyo yake! huyu mtu mbaya sana ! akaongopa kuwa iddi amini dikteta ilhali yeye ndio dikteta mkubwa sana ! ukweli hamuujua , iddi amini hakuwa dikteta bali nyerere alikuwa akilitumikia kanisa baada ya kuona Amini anataka kuliingiza taifa ya Uganda katika usilamu na ndio maana leo Uganda kuna Qaadhi na wamejiunga na OIC, nyerere ana madhambi mengi sana huyu ! na WALLAHi ataungua mtoto huyu mpaka siku ya kufufuliwa kwetu !

Kwahiyo Amini ndio mzuri, ha ha ha. Sasa ndugu zake ndio hawakumtaka ila wewe ndio unamtaka sanabu tu kuendeleza uislamu at any cost!
 
He simply failed in all aspects, may it be politically, economically or socially. For more than 23 Years, what was he doing? leaving us the poorer of the poorest.
Haya hao wawili waliofuatia wametupeleka wapi kwamiaka karibu 20???? Hahaha hata Socially shame on you, kwa hiyo hao wawili socially wametupeleka wapi? Politically wametupeleka wapi?
 
@everbody

Nilikuwa nafikiri anataka kusema nyerere alikuwa kiongozi mbovu bahati aka over stay 24 yrs

Viongozi waliofuata ilibidi wasafishe uchafu mwingi uliolundikana, ikiwemo tabia chafu (kutowajibika, rushwa ) iliyojengeka miaka 24yrs kwa civil servants wa taifa..wakajikuta wanamaliza miaka 20yrs kufanya hivyo..

Kwa hiyo 24-20 =4 inafact sisi kama nchi nafikiri tumefanya kazi miaka minne kutokana na historia hii..

Nafikiri hiyo ndio LINK

KAKA hii hesabu kali nimeipenda,, sina comment....
 
UJAMAA ndio umetufikisha hapa tulipo,, huwezi kuongoza ujamaa kama wewe sio katili, huwezi kuwa mjamaa kama una dini.

mifano ya viongozi WAJAMAA,, ni MAO, LENIN, MUSSOLIN, huku ndiko ujamaa ulikofanikiwa na aina ya viongozi walikuwa makatili kupindukia, (huwezi fananisha na NYERERE). NAKUBALIANA NA MTOA MAADA, NYERERE AMETUFIKISHA HAPA TULIPO (UMASIKINI).
 
Nyerere ndio BABA wa taifa hili.Hatatokea mwingine.Watakuja marais wengine watapita na tutawasahau.
 
Usitishe watu kwamba kuna kitu kikubwa sana kwenye uongozi wa nyerere..

embu eleza moja moja basi tuelewe kuliko maneno matupu..

Mkuu Topical tofauti kubwa ya Nyerere na Viongozi waliomfuata ni kwamba NYERERE ALIKUWA KIONGOZI WA WATU na Hawa wengine ni watawala wa Watu.Hii ndiyo tofauti kubwa na wakati huohuo yeye akiwa Ndugu ya watu hawa ni waheshimiwa na watukufu.
 
Watajiumauma tu hapa na
kutetea ujinga lakini hawawezi kukupa jibu la maana hata chembe, walitoe
wapi?

Ningeshangaa kama usingetupia nene, hata hivyo naunga mkono yaliyosemwa. Kitendo cha kuchukia makabira yenye upeo na upana wa mawazo kama wanyakyusa, wachaga na wahaya ndicho chanzo cha haya yote.
 
Nimeongea na Waislamu wengi, kusema kweli hakuna anayemsema vizuri Nyerere pamoja na mazuri yake mengi na pia hakuna anayemsema vibaya Kikwete pamoja na mabaya yake mengi! Piga, ua, garagaza hapa issue kuu ni UDINI! Kwa upande wa Wakristo wamekuwa critical hata kuwaita akina Mkapa, Lowassa, Chenge, etc MAFISADI! Laiti kama Mkapa, Lowassa, Chenge, etc wangekuwa Waislamu ungeona sarakasi nyiingi za Waislamu za kuwasafisha! Anyway, asikudanganye mtu, major issue hapa ni UDINI, period! Ndio maana Waislamu bila haya wanadiriki kuwatetea mafisadi wa Ikulu MWINYI na SITI MWINYI, simply kwa kuwa alikwapua mafungu ya Ikulu kuwajengea misikiti! Fuatilieni mijadala ya Waislamu humu mtajua ninasema nini, maana mawajua kwa matendo yao!
Kwa hoja zako hizi basi wewe ni mtu unayepaswa kupuuzwa!
 
Hawakumbuki umaskini uliokuwepo alipowatoa babu zetu ktk ukoloni... mlitaka ashushiwe utajiri awape?! Amejitahidi ili japo na wewe umekuta rasilimali, sivyo ungesoma ktk history tu.
 
Yaaniwewe umemaliza umemaliza. Tatizo kubwa ni udini unapelekea watu kujustify hata kitu cha uongo kabisa, hatakituykilichowazi. Mi naona MwlNyerere alichokosea ni kutaifisha Shule za Mission na kuwafanya hawa wasome baaaaasi.
Ni moja ya hoja chakavu kabisa kupata kutolewa kwenye mada hii!! Udini upo wapi? Niliyosema ambayo si kweli ni yapi? Aliyekuambia kwamba shule zote ambazo alitaifisha zilikuwa ni za Mission(bila shaka ukitaka kumaanisha za Kikristo) ni nani? Jadili hoja badala ya kuleta hoja zisizo na maana.
 
Duh...
Nyerere ameondoka ameacha viwanda vya pamba, nguo, viatu, cement, mbolea, majembe, sabuni, magari (Nyumbu), baisikeli (swala) - waliofuata wameviua vyote....
Nyerere aliacha nyumba za watumishi wa umma, aliacha UDA inafanya kazi, aliacha Kampuni za mabasi ya taifa (KAMATA), aliacha mabasi ya Umma (Railways corporation), aliacha bandari zenye meli Nyasa, Victoria, Tanganyika etc, aliacha reli ya uhuru na reli ya kati vikifanya kazi.....waliofuata wamgawana na kuviua. UDA ndo hiyo inaenda kwa Mr. Smile huku tukikenua meno kama mazuzu....
Nyerere alijenga hospitali za rufaa Mbeya, Meta, Muhimbili, Tanga etc,... waliofuata wamezifanya majina tu. hawajaendeleza , wala hawajajenga mpya,,.....tulivyo mazuzu tunawasifia kina mwinyi, Mkapa, na Kikwete...jamani!
Nyerere alituachia Serengeti, aliacha mahoteli ya taifa Lake nchi nzima (TAHI), leo hii mahoteli hayo wamegawana "wenzetu"......Loliondo wamemegewa waarabu, Hoteli zote zimeuzwa kwa bei ya kugawana...bado watanzania tunashangili....eh?
Nyerere aliacha Bank ya NBC, ilikuwa the strongest and largest Bank in Africa, Shirika la Bima la Taifa lilikuwa kubwa kabisa Africa nzima, alituachia General tyre East Africa, alituachi viwanda vya tumbaku na sigara, viwanda vyetu vya bia......waliofuata wamewapa makaburu , walewale tuliokuwa tunawapiga vita Africa Kusini....Watanzania bado tunakenua meno wakati genge la wahuni likigawana mali na kuwagawia wakoloni wetu.....
Nyerere alituachia viwanda vya kuprocess diamond....leo tunapeleka almasi ghafi nje....hivi tuna laana gani jamani?
Nyerere aliachia madaraka miaka 28 iliyopita, bado tunapiga kelele kumhusu yeye? Hawa walioongoza nchi hii kwa karibu miaka 30 wamefanya nini zaidi ya kutupokonya hata haki ya kupata elimu ili walau tukahemee huko nje baada ya wao kugawana nchi......
Watanzania , bila kujali itikadi zetu tuseme basi. Tuungane tuwatimue Mwinyi, Mkapa, Kikwete na vibaraka wao wote tulinde heshima ya nchi hii...Tafadhari sana , hakuna cha Mangula, wala, Mkapa, wala Mwinyi wala Kikwete, wala Lowasa wala Malechela watakaweza kututoa hapa. Wote wameharibu, na wako radhi tuuwane ili walinde uchafu wao. Ni wakati wa kuwafurusha wote , turudi kwenye misingi ya Nyerere. No matter what , Nyerere remains the greatest Leader Tanzania, and Africa had. To hell with Mandela ....Nyrerere ni wa kipekee na hakuna anayeweza kufuta historia yake kamwe!!!
 
Hakika umesema ndg yangu , Nyerere aliacha mashamba ya Nafco kama Kapunga na Mbarali rice farm pia kule hanan'g lakini wakubwa wameuziana kwa bei ya kutupa, hata wananchi walipotaka wanunue bado waliwakatalia, Prof. Tibaijuka majuzi aliwaahidi kuwarudishia wananchi sehemu ya shamba la Kapunga baadae amegeuka lakini najua amelazimishwa na wakubwa ambao ndio waliojiuzia kwa mgongo wa mwekezaji. Lakini iko siku ardhi yetu itarudi tu ,gesi mmemwambia Mengi hawana mitaji na ardhi yet nayo hatuna majembe? Siku yaja hizo nyumba za masaki na Oyster bay mlizogawana
 
Back
Top Bottom