Nyerere Hakuwa na mapungufu, alikuwa Kiongozi Mbovu!

Hata ulivyopost inaonyesha unafiki na prejudice ya hali ya juu! on "NYERERE 'HAKUWA NA MAPUNGUFU' LAKINI ALIKUWA KIONGOZI MBOVU" Unakubaliana na lipi kati hizi contadicting statements?! mnafiki mkubwa. UDINI unauleta wewe kwa ujinga wa kujemga hoja! Unaposema waislamu hawakuwa/hawana na chuki na Nyerere una maana gani? tumeona threads nyingi sana hum nyingi zikionyesha kuwa waislamu walitafuta/pigania uhuru wa tanganyika Nyerere akawadhulumu haki ya kuongoza. Eti vile nyerere alianzisha mfumo Kristo Crazy ****** bila yeye wote nyie wala msingekuwa na lolote kwa wamisionari waliokuja kuhamasisha madrasa na Ilimu Ahera.
Kwa kipindi kile "Nyerere was the greatest but also a human being"

Kama mapungufu na ubovu kwako ni ki2 kimoja then u have long way to go!
 
NYERERE ni nyerere, mwinyi ni mwinyi, mkapa ni mkapa, jk ni jk....tz inazidi kufa masikini na kuzalisha mafisadi na wananchi mazoba.
 
wakati wa nyerere at least tulikua tunaexport agricultural products na per capita ilikua $700 wakati wa 1970's sasa per capita ni $900 lakini haijakua in real terms..elimu ya kucram haikuwepo, nyerere anastaafu barabara hazikuzidi km 1000, waliofuata wamejenga km1500 tena wakiwa wanakusanya kodi kubwa zaidi...

Nyerere alitusaidia kuwa na usawa kiasi fulani kutokana na ujamaa pamoja na kua ufanisi na ubadhirifu ulikuepo... je angerushusu ubepari kama Kenya huu usawa ungetoka wapi? tungeanza kutengeneza akina Rostam, Mkapa na Lowassa mwaka 1960 leo tungekua wapi?

hawa "wawekezaji" uchwara si wangekua wamechukua ardhi yetu yote pamoja na wanasiasa na wewe na mimi kumiliki ardhi si ingekua ndoto? Mazuri ya Nyerere alijitahidi kufanya nchi isitawaliwe na kakikundi ka watu-wafanyabiashara au wanasiasa au watu wa kabila fulani kwa hiyo alijenga misingi ambayo wewe leo unaweza kumiliki kakipande chako cha ardhi, unaweza kufungua kabiashara kako pamoja na kua inakua vigumu kila siku ziendazo kutokana na ufisadi kuharibu mazingira ya ushindani wa kibiashara, unaweza kuingia kwenye siasa, unaweza kuishi mahali popote na bado kikubwa una matumaini na Tanzania.
 
Angalau ume include figures.
 
NasDaz, What a great RANT!!! Well may be Nyerere was not a perfect leader, now tell us how well off we have become since his departure. Could it be that bad leadership is ingrained in our Tanzanian fabric? Each incoming leader builds on what was left by his predecessors. In our case we seem to demolish what was left by the last leader. You can't blame that on Nyerere. Can you?
 
Humu ndani, kuna watu wakiona Hayati Julius Nyerere, the First Preisdent wa URT anasemwa vibaya basi wanakuja juu!! Kinachonikera mimi, ni wengi wao kuhusisha na imani za dini! Kwamba, mtu akisema ubaya wa Nyerere, na hasa mtu huyo akihisiwa ni Mwislamu, basi hoja ya wapofu wa hoja watachukulia ukosoaji huo ni chuki ya waislamu dhidi ya Nyerere!! Hivi ni lini Waislamu wamepata kuwa na chuki na mwalimu?! Sasa haya mambo kwamba mtu akitaja mabovu ya Mwalimu basi ni chuki za waislamu dhidi ya mwalimu yanatoka wapi?! Binafsi, am muslim, na kama utaniambia nikutajie my favorite president sitasita kumtaja Julius Nyerere. lakini pamoja na yote hayo, kama nitaambiwa nitaje top two poorest presidents ever happaned in our history, basi Nyerere ni mmoja wapo, akiwa sambamba na mwinyi! Binafsi, nikimwangalia Nyerere, ni eneo moja peke yake ambalo linaweza kumweka kama best leader! hakuwa corrupt leader ingawaje serikali yake ilikuwa very corrupt government!! Na wala si kweli kwamba Nyerere alikuwa mkali kwa corrupt leaders, vinginevyo nchi hii Mwinyi asingeikuta alipoikuta! Sana sana ki2 ambacho labda Nyerere aliweza kuzuia ni kutokuwa na State House corrupt leaders...lakini ukitoka hapo, wengi walikuwa corrupts!Serikali ya Nyerere ilijaa watendaji ambao walikosa kabisa uwajibikaji na ndio maana Mwinyi alikuja na kitu kilichojulikana kama Fagio La Chuma! Kwanini awe na fagi la chuma wakati uwajibikaji ulikuwapo?! Serikali isiyo corrupt, haiwezi kuwa na irresponsible leaders. Ni kweli, Nyerere hakuwa corrupt leader, lakini aliendesha corrupt government na anayebisha aniambie kwanini viwanda vyote vilifia mikononi mwake!!Ni kweli JK ni goi goi! hata Nyerere alikuwa ni goi goi kupita kiasi!! hakuwa mkali kama tunavyoaminishwa watu ambao hatukuwa na ufahamu wakati wa utawala wake. Nyerer alikuwa mkali kwa wapinzani wake wa kisiasa, and not otherwise!! Kama alikuwa mkali kweli, umasikini tulionao ulitokea wapi?! Aliwafanya nini waliokuwa wanaharibu mali za umma zaidi ya kuwahamisha?! kama sio ugoi goi tuite nini hii?!Kulikuwa na miradi kadhaa ambayo ilianzishwa wakati wa utawala wake, na vilevile ilikufa hata kabla haijafika kokote....sasa kama sio ubadhirifu huo tuite nini?! Siwezi kumsifia kiongozi aliye msafi yeye pekee na familia yake wakati serikali yake imejaa watu irresponsible!!Amekaa Ikulu more than 20 years lakini ametoka akiwa ameachwa barabara zimejaa mahandaki kila mahali!! Bahati mbaya sana, sehemu ambazo zilikuwa na corrupt leaders toka kwenye serikali yake ndio sehemu pekee ambazo angalau zilikuwa na barabara nzuri kidogo! Sehemu ambazo walitoka honest leaders kama yeye, ndizo zikabaki balaa tupu!!! Hiyo ndio sababu kuu iliyofanya mikoa ya kusini kuwa hoe hae zaidi kwani viongozi wake wengi walikuwa honest kama yeye...hawa ni pamoja na akina Kawawa na Nnauye! Hivyo, umaskini wa kusini haukusababishwa na Nyerere kama Nyerere, bali ulisababishwa na irresponsible central government ambayo ugawaji wa keki ya taifa haukuwa the same! ilitegemea sana sehemu husika ana power gani serikalini and how corrupt s/he is!!!Nyerere ameondoka akiwa ameacha vyuo vikuu viwili tu, UDSM na SUA na kuishia tu ktk kujenga vyuo vya kati ambavyo hata hivyo navyo productivity yake ilikuwa chini. Chuo pekee cha kati ambacho kilikuwa kinatoa elimu ya maana labda ni Mzumbe peke yake....na sababu kuu ni kwavile kilikuwa more political! Tena hata nina mashaka kama kweli kilikuwa kinatoa elimu ya maana!! tangu lini katibu wa nini sijui mwenye miaka 45++ akaweza kuhimili mikiki mikiki ya elimu ya juu?! Tunaambiwa enzi zake elimu ilikuwa na ubora kuliko sasa!! na hii ndio tabia ya wazee....kwamba kila ki2 chao kilikuwa bora!!! Huo ubora ulisaidia nini basi katika kutatua matatizo ya uchumi wa nchi hii?! Sana sana hao tunaoambiwa walikuwa wasomi wakati wa elimu bora ndio hao hao waliogeuka kuwa corrupts wasio na haya wakati wa Mwinyi.....bisheni!!! Kama ni kweli wakati huo elimu ilikuwa bora basi vilevile ilisaidia kuzalisha BEST CORRUPT LEADERS!!! Serkali corrupt haiwezi kuwa na jeuri ya kujenga vyuo vikuu vya kutiosha kwavile haina fedha.....kutokuwa na fedha ni dalili ya serikali corrupt!!!MATATIZO ya umeme tuliyonayo hivi sasa source yake ilikuwa enzi za mwalimu!!! Serikali ya Mwalimu haiku-forecast mahitaji ya umeme over the next 50 years!! Ni kweli, wakati wa Nyerere, haukuwa wa mgao! Sasa mgao ungetoka wapi wakati nyumba zenyewe za umeme zilikuwa chache?! Mgao ungetoka wapi wakati hakukuwa na uzalishaji mkubwa wa kuhitaji matumizi ya umeme?! Mgao ungetoka wapi wakati hata kumiliki radio ilikuwa ni anasa?! Kwahiyo, si kwamba ni uongozi bora wa Nyerere ambao ulifanya nchi isiwe na mgao/upungufu wa umeme, bali hiyo ilikuwa ni matokeo ya serikali mbovu!Tunaambiwa huduma za jamii zilikuwa bure! Huduma gani za jamii?! hizo za kufuata zahanati kilometa 50 na shule ya msingi kilometa 10?! Dar es salaam yote hii aliacha shule saba tu za sekondari (za serikali, ambazo hata hivyo hakujenga yeye)-Jangwani, Azania, Tambaza, Forodhani, Kisutu na Kibasila!!! Nani atakayethubutu kusema kwamba shule hizo zilikuwa zinakidhi mahitaji ya elimu ya sekondari jijini? Huko mikoani ndo ilikuwa balaa tupu, unaweza kukuta mkoa mzima una shule moja au mbili za serkali.....bado tunaambiwa huduma za jamii zilikuwa bure! Ni serikali gani ingeshindwa kuhudumia shule chache kama hizo?!Ubovu wa serikali ya Nyerere ni mwingi kuliko uzuri wake, otherwise, wale wanaoona kwamba mgtu akisema basi ana chuki za kidini (styupid thinking) basi anitajie hapa mazuri yaliyofanywa na serikali yake ambayo natarajia yawe mengi kuliko mabovu!wapo watakaosema kwamba Nyerere amewezesha nchi hii kuwa na amani! Kwani aliichukuwa wakati nchi haina amani?! Sifa kama hizo anatastahili kupewa Kagame aliyechukua nchi baada ya mauaji ya kutisha nchini mwake! Anyway, waliosoma historia wanisaidie kunitajia ni vita gani vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimepata kupiganwa Tanganyika katika karne ya 19! Kama hakuna au zilikuwa si za kutisha sana, basi inawezekana Watanganyika hatuna silika ya kupigana tangu zama hizo!!Hivyo basi, mtu anavyotaja ubovu wa Nyerere inakuwa ni ujinga uliepitiliza kusema kwamba ni chuki binafsi...Na inakuwa sio ujinga, bali ni upumbavu mtu akisema ni chuki za kidini! Nyerere kama Nyerere alikuwa was a very good person BUT NOT A GOOD LEADER! He was a good person who was a poor leader! Kutokana na hayo, sipati kigumumizi hata chembe kusema wazi kwamba SI KWAMBA NYERERE ALIKUWA NA MAPUNGUFU, BALI ALIKUWA KIONGOZI MBOVU! Ukweli wenyewe ndio huo, ukiona mgumu kuumeza, chukua maji ushushie!Anayekataa, atoe data za mazuri yake kama kiongozi yenyewe manufaa kwa Tanzania!
Mkuu NasDaz, pole sana kwa kuandika habari ndefu inayakinzana kwa hoja zako mwenyewe. Lakini pia kwangu imenipa ugumu kuelewa, hoja yako hasa imelalia wapi. Katika udini au katika ubovu wa uongozi wa hayati Mwl, Nyerere?Niandike tu machache kuhusu kukinzana kwa hoja;Unasema Mwl. alikuwa kiongozi mbovu, lakini wewe huyo huyo unasema tena Mwl. alikuwa my favorite president!!!??? Sielewi!!!Halafu kama aliweza kuwadhibiti State house corrupt (leaders!!!???) officials, kwa nini unasema alishindwa kuwadhibiti walio chini ya hao?, Walikuwa na nguvu kuliko wa ikulu? Sikuelewi!!!Kuhusu vyuo vikuu. Vingi ya unavyovisifia leo hii, havikujengwa na hao unaowasifia bali vilijengwa kipindi cha Mwl. na vilikuwa vinatoa vyeti vya hadi diploma na diploma ya juu. Waliofuata baada yake wamevibadilisha na kuviita vyuo vikuu, lakini baada ya kupata waalimu wenye sifa na ambao hapo awali walisoma bure enzi za Mwl. Kwa hiyo kipindi cha Mwl. watu hao (wanafunzi enzi hizo na waalimu kwa sasa) walikuwa bado hawana sifa ya kuwa waalimu wa vyuo vikuu.Kuhusu umeme, zaidi ya Kihansi ni kinu gani kingine cha kufua umeme ambacho si cha kifisadi kimejengwa na awamu zilizofuata?Labda niishie hapo mkuu, great thinkers wengine wataendeleza kuhusu ubora na mazuri ya mwalimu. Umeandika kwa jazba na si kwa tafakuri.
 
Humu ndani, kuna watu wakiona Hayati Julius Nyerere, the First Preisdent wa URT anasemwa vibaya basi wanakuja juu!! Kinachonikera mimi, ni wengi wao kuhusisha na imani za dini! Kwamba, mtu akisema ubaya wa Nyerere, na hasa mtu huyo akihisiwa ni Mwislamu, basi hoja ya wapofu wa hoja watachukulia ukosoaji huo ni chuki ya waislamu dhidi ya Nyerere!! Hivi ni lini Waislamu wamepata kuwa na chuki na mwalimu?! Sasa haya mambo kwamba mtu akitaja mabovu ya Mwalimu basi ni chuki za waislamu dhidi ya mwalimu yanatoka wapi?! Binafsi, am muslim, na kama utaniambia nikutajie my favorite president sitasita kumtaja Julius Nyerere. lakini pamoja na yote hayo, kama nitaambiwa nitaje top two poorest presidents ever happaned in our history, basi Nyerere ni mmoja wapo, akiwa sambamba na mwinyi! Binafsi, nikimwangalia Nyerere, ni eneo moja peke yake ambalo linaweza kumweka kama best leader! hakuwa corrupt leader ingawaje serikali yake ilikuwa very corrupt government!! Na wala si kweli kwamba Nyerere alikuwa mkali kwa corrupt leaders, vinginevyo nchi hii Mwinyi asingeikuta alipoikuta! Sana sana ki2 ambacho labda Nyerere aliweza kuzuia ni kutokuwa na State House corrupt leaders...lakini ukitoka hapo, wengi walikuwa corrupts!

Serikali ya Nyerere ilijaa watendaji ambao walikosa kabisa uwajibikaji na ndio maana Mwinyi alikuja na kitu kilichojulikana kama Fagio La Chuma! Kwanini awe na fagi la chuma wakati uwajibikaji ulikuwapo?! Serikali isiyo corrupt, haiwezi kuwa na irresponsible leaders. Ni kweli, Nyerere hakuwa corrupt leader, lakini aliendesha corrupt government na anayebisha aniambie kwanini viwanda vyote vilifia mikononi mwake!!

Ni kweli JK ni goi goi! hata Nyerere alikuwa ni goi goi kupita kiasi!! hakuwa mkali kama tunavyoaminishwa watu ambao hatukuwa na ufahamu wakati wa utawala wake. Nyerer alikuwa mkali kwa wapinzani wake wa kisiasa, and not otherwise!! Kama alikuwa mkali kweli, umasikini tulionao ulitokea wapi?! Aliwafanya nini waliokuwa wanaharibu mali za umma zaidi ya kuwahamisha?! kama sio ugoi goi tuite nini hii?!

Kulikuwa na miradi kadhaa ambayo ilianzishwa wakati wa utawala wake, na vilevile ilikufa hata kabla haijafika kokote....sasa kama sio ubadhirifu huo tuite nini?! Siwezi kumsifia kiongozi aliye msafi yeye pekee na familia yake wakati serikali yake imejaa watu irresponsible!!

Amekaa Ikulu more than 20 years lakini ametoka akiwa ameachwa barabara zimejaa mahandaki kila mahali!! Bahati mbaya sana, sehemu ambazo zilikuwa na corrupt leaders toka kwenye serikali yake ndio sehemu pekee ambazo angalau zilikuwa na barabara nzuri kidogo! Sehemu ambazo walitoka honest leaders kama yeye, ndizo zikabaki balaa tupu!!! Hiyo ndio sababu kuu iliyofanya mikoa ya kusini kuwa hoe hae zaidi kwani viongozi wake wengi walikuwa honest kama yeye...hawa ni pamoja na akina Kawawa na Nnauye! Hivyo, umaskini wa kusini haukusababishwa na Nyerere kama Nyerere, bali ulisababishwa na irresponsible central government ambayo ugawaji wa keki ya taifa haukuwa the same! ilitegemea sana sehemu husika ana power gani serikalini and how corrupt s/he is!!!

Nyerere ameondoka akiwa ameacha vyuo vikuu viwili tu, UDSM na SUA na kuishia tu ktk kujenga vyuo vya kati ambavyo hata hivyo navyo productivity yake ilikuwa chini. Chuo pekee cha kati ambacho kilikuwa kinatoa elimu ya maana labda ni Mzumbe peke yake....na sababu kuu ni kwavile kilikuwa more political! Tena hata nina mashaka kama kweli kilikuwa kinatoa elimu ya maana!! tangu lini katibu wa nini sijui mwenye miaka 45++ akaweza kuhimili mikiki mikiki ya elimu ya juu?! Tunaambiwa enzi zake elimu ilikuwa na ubora kuliko sasa!! na hii ndio tabia ya wazee....kwamba kila ki2 chao kilikuwa bora!!! Huo ubora ulisaidia nini basi katika kutatua matatizo ya uchumi wa nchi hii?! Sana sana hao tunaoambiwa walikuwa wasomi wakati wa elimu bora ndio hao hao waliogeuka kuwa corrupts wasio na haya wakati wa Mwinyi.....bisheni!!! Kama ni kweli wakati huo elimu ilikuwa bora basi vilevile ilisaidia kuzalisha BEST CORRUPT LEADERS!!! Serkali corrupt haiwezi kuwa na jeuri ya kujenga vyuo vikuu vya kutiosha kwavile haina fedha.....kutokuwa na fedha ni dalili ya serikali corrupt!!!
MATATIZO ya umeme tuliyonayo hivi sasa source yake ilikuwa enzi za mwalimu!!! Serikali ya Mwalimu haiku-forecast mahitaji ya umeme over the next 50 years!! Ni kweli, wakati wa Nyerere, haukuwa wa mgao! Sasa mgao ungetoka wapi wakati nyumba zenyewe za umeme zilikuwa chache?! Mgao ungetoka wapi wakati hakukuwa na uzalishaji mkubwa wa kuhitaji matumizi ya umeme?! Mgao ungetoka wapi wakati hata kumiliki radio ilikuwa ni anasa?! Kwahiyo, si kwamba ni uongozi bora wa Nyerere ambao ulifanya nchi isiwe na mgao/upungufu wa umeme, bali hiyo ilikuwa ni matokeo ya serikali mbovu!

Tunaambiwa huduma za jamii zilikuwa bure! Huduma gani za jamii?! hizo za kufuata zahanati kilometa 50 na shule ya msingi kilometa 10?! Dar es salaam yote hii aliacha shule saba tu za sekondari (za serikali, ambazo hata hivyo hakujenga yeye)-Jangwani, Azania, Tambaza, Forodhani, Kisutu na Kibasila!!! Nani atakayethubutu kusema kwamba shule hizo zilikuwa zinakidhi mahitaji ya elimu ya sekondari jijini? Huko mikoani ndo ilikuwa balaa tupu, unaweza kukuta mkoa mzima una shule moja au mbili za serkali.....bado tunaambiwa huduma za jamii zilikuwa bure! Ni serikali gani ingeshindwa kuhudumia shule chache kama hizo?!

Ubovu wa serikali ya Nyerere ni mwingi kuliko uzuri wake, otherwise, wale wanaoona kwamba mgtu akisema basi ana chuki za kidini (styupid thinking) basi anitajie hapa mazuri yaliyofanywa na serikali yake ambayo natarajia yawe mengi kuliko mabovu!

wapo watakaosema kwamba Nyerere amewezesha nchi hii kuwa na amani! Kwani aliichukuwa wakati nchi haina amani?! Sifa kama hizo anatastahili kupewa Kagame aliyechukua nchi baada ya mauaji ya kutisha nchini mwake! Anyway, waliosoma historia wanisaidie kunitajia ni vita gani vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimepata kupiganwa Tanganyika katika karne ya 19! Kama hakuna au zilikuwa si za kutisha sana, basi inawezekana Watanganyika hatuna silika ya kupigana tangu zama hizo!!

Hivyo basi, mtu anavyotaja ubovu wa Nyerere inakuwa ni ujinga uliepitiliza kusema kwamba ni chuki binafsi...Na inakuwa sio ujinga, bali ni upumbavu mtu akisema ni chuki za kidini! Nyerere kama Nyerere alikuwa was a very good person BUT NOT A GOOD LEADER! He was a good person who was a poor leader! Kutokana na hayo, sipati kigumumizi hata chembe kusema wazi kwamba SI KWAMBA NYERERE ALIKUWA NA MAPUNGUFU, BALI ALIKUWA KIONGOZI MBOVU! Ukweli wenyewe ndio huo, ukiona mgumu kuumeza, chukua maji ushushie!

Anayekataa, atoe data za mazuri yake kama kiongozi yenyewe manufaa kwa Tanzania!

hii ni FACT - kama mtu ana tatizo na FACT - BASI YEYE BINAFSI NI TATIZO
 
Tatizo kubwa la threads nyingi humu jamvini kuhusu Nyerere ni pale mapungufu ya wakati wa utawala ule wa awamu ya kwanza yanatumika kujustfy uzembe, wizi, ufisadi na kukosekana uwajibikaji wa serikali zilizofuata. Lakini dimensions na vigezo vinakuwa jumla jumla tu. Mfano mtu anasema JK ameleta zahanati nyingi kuliko raisi mwingine yeyote, lakini ukichallenge kwamba mbona hamna wauguzi wala madawa inaletwa hoja wakati wa Nyerere zilikuwa ngapi???????

1. Lakini kama watu wangekuwa wanafahamu mfano enzi zile kila shule ya sekondari ilikuwa na zahanati yenye qualified medical assistants, madawa yalikuwepo na hiyo ilisaidia sana kuelimisha watu kuondokana na imanai za kichawi ambazo walitoka nazo makwao kabla ya kuja shule. Leo hii hata shule hizo zinazotoza mamilioni zina zahanati au hata first aider?

2. Enzi zile kila shirika la umma lilkuwa na chuo chake ukitoka shule ukaajiriwa na shirika hilo unaenda kwanza kusomea mambo ya hilo shirika, mfano chuo cha bandari, chuo cha reli, chuo cha posta na simu nk. huu ulikuwa utaratibu mzuri sana na haishangazi kuona makampuni ya migodi yamekuja tena na huu utaratibu. Sasa je vijana wanaoajiriwa siku hizi huku kukiwa na wababishaji lukuki kwenye makampuni na mashirika ya umma wanajifunza wapi?

3. Sijui kama kuna watu wanakumbuka enzi zile kwamba ATC ilishawahi kuwa mpaka na Boeing 767, leo watu wanajisifia kuleta nembo halafu wanajilinganisha na wakati ule.

4. Shule bure afya bure pamoja na uchache lakini mfano shule ilikuwa ni uwezo wako tu wa darasa utasoma mpaka ukimbie mwenyewe.

5. Vijana wengi sana hawafahamu kwamba miaka ile ya mchonga karibu makao makuu ya mikoa yote ile ya zamani kulikuwa na lami na taa za barabarani ambazo siku hizi mnasubiri A1 outdoor wawawekee na kuchafua mandhari ya miji kwa matangazo kibaoo!

Na yote niliyotaja hao yalianzia almost sifuri, from the humble beginnings. Zamani ukiambiwa serikali haina hela u could tell it from magari, ofisi, fenicha zote zilikuwa ni average joe style. Sasa siku hizi mtu ana olympic size swimming pool nyumbani kwake, na hiyo migari wanayolanguliwa kwa zaidi ya milioni 200 halafu ofisini kuna computer mbili wafanyakazi 200.

Hivyo basi pamoja na mapungufu yote aliyokuwa nayo Nyerere na utawala wake siyo justification ya Kikwete kuwawashia giza watanzania, wala kuzembea kuhusu ajali za kizembe barabarani au kukosekana wauguzi na madawa kwenye zahanati. Times have changed na kama viongozi wa leo wanavyotuthibitishia kwa suti za bei mbaya, magari ya kifahari na mahekalu ya kimtoni mtoni they need to do the same on our roads, our power situations, our clasrooms etc.
 
KUNA WATU WAMEZALIWA NA KUKULIA CANADA NDANI YA TANZANIA
Kuna baadhi ya Watanzania wenzetu wamezaliwa na kukulia Canada ndani ya Tanzania,mmoja wa watu hao ni rafiki yangu mimi.Yeye anahaya ya kusema kuhusu Mwalimu.
1:Rais mwenye maono [Vision],kuunda Taifa lenye muonekana wa aina yake,yani ni moja ya marais waliongoza kwa falsafa [Philosophy] na sio bora kutawala.

2: Rais mwenye Ubinadamu [Ndio maana hakusita kumpa mtu second chance],nae aliyepewa kuonyesha kuwa naye yu binadmu kuna majaribu.

3: Mpenda amani,ukitaka kujua ni mpenda amani,ni pale alipoacha madaraka mikononi mwa Rashid Mfaume Kawawa [Simba wa Vita]

4: Mwenye kiu ya kuona Waafrika na Wanyonge wakiwa huru,alisaidia ukombozi,Afrika na kuwaondoa wazungu Tanzania,pasipo kuwafukuza kwa kuwambia nendeni zenu,bali kwa mikakati [Strategy]

5: Alipoteza nusu ya umri wake kufikilia kuhusu maisha yako na yangu miaka ijayo yaweje wakati wake wa uongozi ndio maana kwa kujua hilo akaacha vitabu kama Mwalimu na Ujamaa, Binadamu na Maendeleo [Man and Developmemt].

6: Aliyeamini kwenye umoja [Zanzibar na East African]

7: Asiyeyumba kusimamia maslahi ya wengi hasa maskini wasio na uwezo na hivyo kuwapa uwezo kwa kuwasomeshea watoto wao,ndio maana leo hii, wasomi na watwala wetu wengi wao ni watoto wa wakulima.Kama nchi hii ingeangalia kusoma kwa mujibu wa koo na familia wtu wengi sana Tanzania wangekuwa ni watumwa wa wachache.Inamaana ambao wangeenda shule ni wale wenye nasaba ya kichifu na wageni wafanya biashara.

8: Mlinzi wa Mali asilia ya Taifa kiasi kuwa hakufukua madini yoyote yale akiamini kizazi kijacho kitapata elimu kifukue chenyewe,nenda kwenye migodi waliok huko kwenye kuchapa kazi ni wabongo ,wazungu kazi yao ni kusimamia na kuachukua chao.

9: Wakati anachukua Nchi Mgodi wa Williamson ulikuwa unamilikiwa na wageni asilimia mia [100%] mgodi huu ni mgodi mama Tanzania.Kisha kwa busara zake kapigania kuchukua mgodi ule toka kwa wakoloni mpaka akafika asilimia hamsini [50%] kusudio likiwa afike asilimia mia [100%] matokeo yake,kaondoka akiwa ana asilimia hamsini mameneja wakiwa waswahili,miaka michache baada ya kutoka kwake madarakani,wazungu wameludi Nchini na chini ya Utawala wa Rais Mwinyi na Waziri ya Mkuu Marecela Serikali imewapa wazunguMgodi ule leo hii Serikali yako inamilki asilimia 27% tu ya share na Mamenaja wakiwa Wazungu.Wengi hawajui kisa na hasira ya Mwalimu kwa Mtu mzima huyo ilianzia wapi kisa ni kikubwa sana.Ndio maana nikasema Mwalimu alikuwa mlinzi mkubwa ajapata kutokea wa mali asili yetu.

11: Rais aliyeangaika usiku na mchana watoto wa Tanzania waende shule mpaka elimu ya chuo kikuu bure,bila kuchimba madini wala kuuza mali ya asili.

12: Rais alieamini kuunganisha makabila mia na kumi na mbili [112] kwa kuishi na kuoleana,nikiwemo mimi leo ni zao la aina yake ya kufikilia.Pamoja na wewe kusema hayo kumbuka Nchi ilikua inaongozwa na machifu.Utawala wa kichifu ulivyotoka na kuiachia Serikali mamlaka ya kuongoza watu leo watu wameingiliana kinasaba kati ya wasukuma na wachaga,wakurya na wagogo,wahaya na wangoni.

13: Rais aliekuwa jasiri alipochokozwa hakusita kusimama na kuonyesha hasira za kitanzania baada ya mavumilivu ya uchokodhi uliokithiri [Idd Amini] vita ambayo Tanzania ilipigana bila msaada wowote kimataifa,na bado tukashinda huku Uganda ikisaidia na Libya kwa kila aina ya shehena za Silaha.

14: Rais aliyetumia nguvu zake na watu wake kuleta ukombozi kwa Mataifa mengine ambayo yalikuwa mikononi mwa wakoloni.Hakika hii ni sawa na kusema asilimia kalibu alobaini [40%] Tumechangia nguvu,mali na akili za ukombozi wa Msumbiji,Zambia,Zimbabwe,Angola,Namibia,South Africa.

15: Kupitia yeye tumesaidia kuweka sawa baadhi ya mataifa kama Uganda [Idd Amini],Sudani [mafunzo Jonn Garang],Kongo [Kabila]

16: Rais aliyeamini kuwa Rushwa ni adui wa haki,kumbe leo nimejifunza kuwa Rushwa sio kitu cha mzaa kumbe rushwa ni tabia na malezi toka kwenye ngazi ya familia ,umemtetea mwenye na kukili kuwa ALIKUA MSAFI BINAFSI,kumbe basi alipata shida kutawala pamoja na watu ambao wamelelewa kuwa wabinafsi, wachoyo na wezi.Je unapata picha gani mtu ambae ni mjenzi wa kwanza wa Taifa ambalo ni wabinafsi.wachoyo na wezi [wakina Baba Benzi] alifanikiwa kwa kiwango cha kusomesha watu bure na kuwapa madawa hospitalini na vyakula mashuleni na vyuoni tena mayai na siagi.Lakini leo hii na kuchuma [utilize] mali asili yote hiyo bado ni shida na ubinafsi uliokithiri kiwango mara dufu kuliko isivyosemekana katika historia ya Taifa hili.

17: Kama ukubahatisha kuwa na ndugu aliyekuwa kiongozi wakati wa Mwalimu pole ndio maana ujui mengi kuhusu Mwalimu,huo upole wa Mwalimu unaosema katika wazembe ambao walikumbana na Mwalimu,wanakwambia omba usikumbane kwenye kiti moto na huyo mzee,pamoja na kuwa na kamwili kadogo kadogo kwa jinsi alivyokuwa ukikumbana nae umemess up kwenye utendaji basi hakika jua umekutana na simba aliyejeruhiwa [Wengi waliokuwa wanabolonga wakiitwa kwake wanasema walikuwa wanaona kama wamekuatana na simba].Ilifikia kuwa alikuwa anaagiza unakula pingu humo humo ndani ya Ikulu kisha anaagiza upelekwe keko.Ukitoka nje ya geti anawaambia wakuludishe [Huruma ya Baba kwa watoto ambao wanaitaji Muungozo kwa kuwa hawajui wanaenda wapi hasa kwenye Taifa changa kama Tanzania kwa wakati huo likiwa na wasomi wachache,Je ukisema unawafunga utawafunga wangapi.au utumie saikolojia kuwafundisha kuichukia rushwa kwa kuwapa majaribu].

18: Rais ambae hakuwa na uchu kama mwenyewe ulivyosema,kwa wataalumu wa vita wanasema tulivyomuondoa nduli Idd amini Uganda,tungeweza kuwa watemi tukaifanya Uganda ni sehemu ya Taifa letu hili, lakini kwa busara za Mwalimu akawakabidhi waganda Nchi yao.

19:Rais ambae aliishi kwa kuangalia jana, leo na kesho. Kwake yeye hakuwa msikivu wa mipaka ya wazungu na ndio maana kwenye hotuba yake ya kihistoria ya Mbeya anasema hakukupata kuwepo Tanganyika.ila washenzi wakoloni kwa kujua faida za ukoloni wakatutengenezea mipaka ili kutugawa.Ukitaka kujua Mwalimu alimaanisha nini nenda kaangalie watu waote wanaokaa kwenye mipaka yetu,uwa awajijui kama ni watanzania au Nchi tunayopakana nayo.Mimi natoka Tarime nina ndugu zangu wako Kenya,wakiwa Tanzania wanaitwa Wakurya wakiwa Kenya wanitwa Watende.Ukienda namanga wakiwa Tanzania wanaitwa masai wakiwa kenya wanaitwa Masai pia,Ukienda moshi vile vile kuna taita taveta,ukienda Mbeya kuna Tunduma,Ukienda Mtwala Kuna wamakonde wa Tanzania na Msumbiji.Hakika watu hawa wote hawajui mipaka ni nini.Kwa kuwa na Mtu Mwelevu kama Mwalimu alijua jinsi ya kutufanya kuishi ndani ya Taifa moja makabila 112.Nani alikwambia hatukupata kuwa na civil war.Vita za makabila zilikuwepo sema Watanzania waliheshimiana katika kutofautina,hata kama watafikishana kwenye pointi ya juu ya kutofautina.Wakurya utofautina na Masai kwa sababu ya kunyanganyana mifugo,Wafugaji utofautina na wakulima kwa sababu ya ardhi lakini hatimae tatizo uisha.Tumeona juzi CHADEMA wametofautina na vyama vya CCM na CUF kwenye swala la KATIBA,lakini leo CDM wamekubali katika kutofautina huko.Haya yote hayaji hivi hivi yanakuja kwa sababu ya Muasisi wa Taifa,hii ni SPIRIT.

20: Rais aliyeamini hakuzaliwa kutawala maisha yake yote,Rais aliyeamini kuwa Mungu alimpa nafasi ya kutuongoza kwa mujibu wa MAONO [VISION] yake nae akatimiza wajibu wake kama binadamu,na kwa imani yake ya KUNGATUKA akaacha watanzania wajiamulie wenyewe huku akisaidiana nao kama Mtanzania mwenye uzoefu na uongozi.Na mfano halisi ni sasa Taifa linapita kwenye misukosuko milefu japo atuchunani ngozi lakini tunatikisika mpaka kila Mwananchi anakili kweli tumetikisika vilivyo.

Bahati yako Mbaya Mdau Uwezi kuwa na Tanzania bila Nyerere na huwezi kuwa Na Nyerere bila Tanzania.Uwezi kuwa na Marekani bila Ablaham Lincoln au Ablahamu Lincoln bila Marekani.Hayo yote yanatokea kwa kuwa Mungu ana sababu.Hivyo Kama ndio BSS basi wewe ni CHAPA LAPA hatua za AWALI ndani ya Jamiiforum ila umejitahidi kupanga ukikuta watu wako shallow hakika unaweza kuwapotosha.Wakiangalia magolofa na magali kibao wataona haya ndio maendeleo,,kisha watasahau kumbe kuna Mwalimu wa vitendo na ukweli aliyewajenga hao wanaovimiliki hivyo wanavyoviona leo.Yaani ndie aliyewapeleka dalasani kusoma na leo ndio hao wajenzi,wabunifu wa hiyo mikakati ya ujenzi,na wamilki halali au wasivyohalali wa hayo maendeleo ambayo wewe unayaona tu yanaelea.
 
Na yote niliyotaja hao yalianzia almost sifuri, from the humble beginnings. .
Nyerere mwenyewe alishakubali kuwa wemefanya makosa mengi enzi za utawala wake...alisema walipoanza kuongoza ilikuwa ni sawasawa na mtu kutupwa kwenye bwawa la maji wakati hujui hata kuogelea....ila ah ndugu zangu hawa wa 'gerezan'i hawataki kuelewa, wenyewe wanaangalia mabaya tu!
 
Nimeongea na Waislamu wengi, kusema kweli hakuna anayemsema vizuri Nyerere pamoja na mazuri yake mengi na pia hakuna anayemsema vibaya Kikwete pamoja na mabaya yake mengi! Piga, ua, garagaza hapa issue kuu ni UDINI! Kwa upande wa Wakristo wamekuwa critical hata kuwaita akina Mkapa, Lowassa, Chenge, etc MAFISADI! Laiti kama Mkapa, Lowassa, Chenge, etc wangekuwa Waislamu ungeona sarakasi nyiingi za Waislamu za kuwasafisha! Anyway, asikudanganye mtu, major issue hapa ni UDINI, period! Ndio maana Waislamu bila haya wanadiriki kuwatetea mafisadi wa Ikulu MWINYI na SITI MWINYI, simply kwa kuwa alikwapua mafungu ya Ikulu kuwajengea misikiti! Fuatilieni mijadala ya Waislamu humu mtajua ninasema nini, maana mawajua
kwa matendo yao!
Ukweli mtupu100%. Hawa wenzetu wa imani ya mwezi cku zote wamejengewa imani ya kuonewa na kutojiamini. Mara ngapi mihadhara yao imegeuka jukwaa la kumshutumu Nyerere badala ya kuhubiri neno la Mwenyezi Mungu? Lakini pamoja na maovu ya Mwinyi na JK hutasikia wanakemea uovu wao. Wakristo hawaangalii dini ya kiongozi ndio maana Mkapa anachanwa live na wakristo. Ni NADRA sana kupata mwislamu asiyekuwa biased na dini hivo Naz shutuma nyingi za Nyerere ziko kidini zaidi hazina uchambuzi uliofanya wewe ndio maana zinakosa mashiko.
Hatukatai kuwa Nyerere alikuwa na mapungufu na hata wale wanotaka kumpa utakatifu wanakuza mambo. Lakini watu wanaposema alikuwa kiongozi bora ni kuangalia mambo yote kwa ujumla utakuta alikuwa kiongozi mzuri. Angalau dawa zilipatikana kwenye hizo hospitali za mbali, hizo shule chache zilikuwa na huduma za kuridhisha. Ujue pia Nyerere started from scrach. Ajira zilikuwepo za kutosha kwani njia za uzalishaji mali zilikuwepo ikiwa ni pamoja na zana za kilimo tofauti na sasa. Kijijini kwangu kuna ghala iliyokuwa inakusanya mazao enzi hizo, wafanyakazi wa ghala na vifaa. Viwanda vilikuwepo vilivoajiri watu, vyama vya ushirika vilikuwepo cku na viwanda vya mazao. Cku hizi ni magofu. Hivo ukija kupima vyote unaona alifanya vyema.
Huenda sehemu ambayo aliteleza ilikuwa ni kwenye elimu. Ingawa ilitolewa bure na vifaa pamoja walimu walikuwepo wa kutosha lakini kutolewa elimu hiyo bure kulifanya serikali kuwahudumia wachache. Ilipaswa watu wachangie elimu ili wenye uwezo wajilipie na serikali kuwalipia maskini. hiyo ingepanua idadi ya watu walipata elimu.
 
Huenda sehemu ambayo aliteleza ilikuwa ni kwenye elimu. Ingawa ilitolewa bure na vifaa pamoja walimu walikuwepo wa kutosha lakini kutolewa elimu hiyo bure kulifanya serikali kuwahudumia wachache. Ilipaswa watu wachangie elimu ili wenye uwezo wajilipie na serikali kuwalipia maskini. hiyo ingepanua idadi ya watu walipata elimu..
I quite agree with you...!
 
Humu ndani, kuna watu wakiona Hayati Julius Nyerere, the First Preisdent wa URT anasemwa vibaya basi wanakuja juu!! Kinachonikera mimi, ni wengi wao kuhusisha na imani za dini! Kwamba, mtu akisema ubaya wa Nyerere, na hasa mtu huyo akihisiwa ni Mwislamu, basi hoja ya wapofu wa hoja watachukulia ukosoaji huo ni chuki ya waislamu dhidi ya Nyerere!! Hivi ni lini Waislamu wamepata kuwa na chuki na mwalimu?! Sasa haya mambo kwamba mtu akitaja mabovu ya Mwalimu basi ni chuki za waislamu dhidi ya mwalimu yanatoka wapi?! Binafsi, am muslim, na kama utaniambia nikutajie my favorite president sitasita kumtaja Julius Nyerere. lakini pamoja na yote hayo, kama nitaambiwa nitaje top two poorest presidents ever happaned in our history, basi Nyerere ni mmoja wapo, akiwa sambamba na mwinyi! Binafsi, nikimwangalia Nyerere, ni eneo moja peke yake ambalo linaweza kumweka kama best leader! hakuwa corrupt leader ingawaje serikali yake ilikuwa very corrupt government!! Na wala si kweli kwamba Nyerere alikuwa mkali kwa corrupt leaders, vinginevyo nchi hii Mwinyi asingeikuta alipoikuta! Sana sana ki2 ambacho labda Nyerere aliweza kuzuia ni kutokuwa na State House corrupt leaders...lakini ukitoka hapo, wengi walikuwa corrupts!

Serikali ya Nyerere ilijaa watendaji ambao walikosa kabisa uwajibikaji na ndio maana Mwinyi alikuja na kitu kilichojulikana kama Fagio La Chuma! Kwanini awe na fagi la chuma wakati uwajibikaji ulikuwapo?! Serikali isiyo corrupt, haiwezi kuwa na irresponsible leaders. Ni kweli, Nyerere hakuwa corrupt leader, lakini aliendesha corrupt government na anayebisha aniambie kwanini viwanda vyote vilifia mikononi mwake!!

Ni kweli JK ni goi goi! hata Nyerere alikuwa ni goi goi kupita kiasi!! hakuwa mkali kama tunavyoaminishwa watu ambao hatukuwa na ufahamu wakati wa utawala wake. Nyerer alikuwa mkali kwa wapinzani wake wa kisiasa, and not otherwise!! Kama alikuwa mkali kweli, umasikini tulionao ulitokea wapi?! Aliwafanya nini waliokuwa wanaharibu mali za umma zaidi ya kuwahamisha?! kama sio ugoi goi tuite nini hii?!

Kulikuwa na miradi kadhaa ambayo ilianzishwa wakati wa utawala wake, na vilevile ilikufa hata kabla haijafika kokote....sasa kama sio ubadhirifu huo tuite nini?! Siwezi kumsifia kiongozi aliye msafi yeye pekee na familia yake wakati serikali yake imejaa watu irresponsible!!

Amekaa Ikulu more than 20 years lakini ametoka akiwa ameachwa barabara zimejaa mahandaki kila mahali!! Bahati mbaya sana, sehemu ambazo zilikuwa na corrupt leaders toka kwenye serikali yake ndio sehemu pekee ambazo angalau zilikuwa na barabara nzuri kidogo! Sehemu ambazo walitoka honest leaders kama yeye, ndizo zikabaki balaa tupu!!! Hiyo ndio sababu kuu iliyofanya mikoa ya kusini kuwa hoe hae zaidi kwani viongozi wake wengi walikuwa honest kama yeye...hawa ni pamoja na akina Kawawa na Nnauye! Hivyo, umaskini wa kusini haukusababishwa na Nyerere kama Nyerere, bali ulisababishwa na irresponsible central government ambayo ugawaji wa keki ya taifa haukuwa the same! ilitegemea sana sehemu husika ana power gani serikalini and how corrupt s/he is!!!

Nyerere ameondoka akiwa ameacha vyuo vikuu viwili tu, UDSM na SUA na kuishia tu ktk kujenga vyuo vya kati ambavyo hata hivyo navyo productivity yake ilikuwa chini. Chuo pekee cha kati ambacho kilikuwa kinatoa elimu ya maana labda ni Mzumbe peke yake....na sababu kuu ni kwavile kilikuwa more political! Tena hata nina mashaka kama kweli kilikuwa kinatoa elimu ya maana!! tangu lini katibu wa nini sijui mwenye miaka 45++ akaweza kuhimili mikiki mikiki ya elimu ya juu?! Tunaambiwa enzi zake elimu ilikuwa na ubora kuliko sasa!! na hii ndio tabia ya wazee....kwamba kila ki2 chao kilikuwa bora!!! Huo ubora ulisaidia nini basi katika kutatua matatizo ya uchumi wa nchi hii?! Sana sana hao tunaoambiwa walikuwa wasomi wakati wa elimu bora ndio hao hao waliogeuka kuwa corrupts wasio na haya wakati wa Mwinyi.....bisheni!!! Kama ni kweli wakati huo elimu ilikuwa bora basi vilevile ilisaidia kuzalisha BEST CORRUPT LEADERS!!! Serkali corrupt haiwezi kuwa na jeuri ya kujenga vyuo vikuu vya kutiosha kwavile haina fedha.....kutokuwa na fedha ni dalili ya serikali corrupt!!!
MATATIZO ya umeme tuliyonayo hivi sasa source yake ilikuwa enzi za mwalimu!!! Serikali ya Mwalimu haiku-forecast mahitaji ya umeme over the next 50 years!! Ni kweli, wakati wa Nyerere, haukuwa wa mgao! Sasa mgao ungetoka wapi wakati nyumba zenyewe za umeme zilikuwa chache?! Mgao ungetoka wapi wakati hakukuwa na uzalishaji mkubwa wa kuhitaji matumizi ya umeme?! Mgao ungetoka wapi wakati hata kumiliki radio ilikuwa ni anasa?! Kwahiyo, si kwamba ni uongozi bora wa Nyerere ambao ulifanya nchi isiwe na mgao/upungufu wa umeme, bali hiyo ilikuwa ni matokeo ya serikali mbovu!

Tunaambiwa huduma za jamii zilikuwa bure! Huduma gani za jamii?! hizo za kufuata zahanati kilometa 50 na shule ya msingi kilometa 10?! Dar es salaam yote hii aliacha shule saba tu za sekondari (za serikali, ambazo hata hivyo hakujenga yeye)-Jangwani, Azania, Tambaza, Forodhani, Kisutu na Kibasila!!! Nani atakayethubutu kusema kwamba shule hizo zilikuwa zinakidhi mahitaji ya elimu ya sekondari jijini? Huko mikoani ndo ilikuwa balaa tupu, unaweza kukuta mkoa mzima una shule moja au mbili za serkali.....bado tunaambiwa huduma za jamii zilikuwa bure! Ni serikali gani ingeshindwa kuhudumia shule chache kama hizo?!

Ubovu wa serikali ya Nyerere ni mwingi kuliko uzuri wake, otherwise, wale wanaoona kwamba mgtu akisema basi ana chuki za kidini (styupid thinking) basi anitajie hapa mazuri yaliyofanywa na serikali yake ambayo natarajia yawe mengi kuliko mabovu!

wapo watakaosema kwamba Nyerere amewezesha nchi hii kuwa na amani! Kwani aliichukuwa wakati nchi haina amani?! Sifa kama hizo anatastahili kupewa Kagame aliyechukua nchi baada ya mauaji ya kutisha nchini mwake! Anyway, waliosoma historia wanisaidie kunitajia ni vita gani vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimepata kupiganwa Tanganyika katika karne ya 19! Kama hakuna au zilikuwa si za kutisha sana, basi inawezekana Watanganyika hatuna silika ya kupigana tangu zama hizo!!

Hivyo basi, mtu anavyotaja ubovu wa Nyerere inakuwa ni ujinga uliepitiliza kusema kwamba ni chuki binafsi...Na inakuwa sio ujinga, bali ni upumbavu mtu akisema ni chuki za kidini! Nyerere kama Nyerere alikuwa was a very good person BUT NOT A GOOD LEADER! He was a good person who was a poor leader! Kutokana na hayo, sipati kigumumizi hata chembe kusema wazi kwamba SI KWAMBA NYERERE ALIKUWA NA MAPUNGUFU, BALI ALIKUWA KIONGOZI MBOVU! Ukweli wenyewe ndio huo, ukiona mgumu kuumeza, chukua maji ushushie!

Anayekataa, atoe data za mazuri yake kama kiongozi yenyewe manufaa kwa Tanzania!

unatumia nguvu nyingi na msuli kuuaminisha umma upupu wako, si kosa lako sema ulitumia mda mwingi madrasa ukashindwa kwenda shule ndo maana uwezo wako wa kuanalyse issuez ni mdogo, nadhani ungefanya uchambuzi kwanza miaka ya 50-60 nchi ilikuwaje, ni misingi ipi iliwekwa na nyerere hadi anangatuka 1985, na nchi aliiacha katika hali gani na nnchi ngapi tulikuwa tunawawasaidia by then ambao wametuacha na wametuacha miaka gani kwa sababu gani, ni mawazo mamngapi ya mwalimu yanafanuya kazi dunia nzima na kwa nini hapa hayafanyiwi kazi, ni viwanda vingapi mwalimu kaacha na sasas havifanyi kazi, misingi ya elimu aliyoacha, kiwango cha rushwa nchi na ufisadi kilikuwaje na sasa kikoje na kwa nini?nadhani ungeenda mbali ukajiuliza ni kwanini nyerere alipenda ujamaa na kwamanufaa ya nani? ni mambo mengi ungeyaangalia kuliko kuamua kuwa mdini wa waziwazi kurisha uma najisi zako, nyerere simungu wala malaika, anayo mabaya ila sio ka unavojitahidi kutunajisi, we ni mtu mbaya sana, mchonganishi, mnafiki na mdini!

tafuta ujue mwalimu alitaka tanzania ipi?soma uongozi na hatima ya tanzania ujue mwalimu alitaka nini na alilenga nini, soma makala zake, soma mapendekezo yake hata baada ya kuachia ngazi, soma kilio chake juu ya kilimo, afya, umeme, na ujiulize ni kwanini haya hayakufanyika kama sio kuaharibiwa na mdini mwenzako? tangu 85 mambo yalianza kumomonyoka na hatimaye unaiona tanzania tusiyoitaka, tanzania siyoiyataka mwalimu,tanzania chovu kuanzia kichwani hadi miguuni, na hii ni kutokana na ufinyu wa mawazo wa viongozi wenye akili sawa na zako!
 
Ndugu NasDaz,
Maoni uliyotoa ni yako, lakini yana walakini mkubwa kudai kwamba kwa sababu Mwalimu alikuwa Mkuu wa nchi kati ya 1962 na 1985, basi yeye ndiyo shina la dimbwi la matatizo tuliyonayo, nasema hapana. Sina haja ya kuchambua hoja zako moja moja, mimi nitajumuisha kwa kukuonyesha tu kwamba, kama ni kwel Mwalimu hakufanya mengi mazuri na matatizo tuliyonayo yalipikwa na yeye, waliopo wameshinda nini kuipaisha nchi na imekuwa tegemezi zaidi, umasikini umezidi (kama hujui kwa sababu unaangalia magari na maorofa ya Dar, nenda kijiji chochote kisarawe, rufuji, kilwa, bagamoyo et al ujionee uduni wa maisha) na ujinga unazidi licha ya wewe kudai kisahihi kibisa kwamba Mwalimu alicha vyuo viku viwilina sasa ni utitili!
Kagame alishika Rwanda 1994, miaka kumi baada ya Mwalimu kung'atuka, wenzetu wana dira, wanapaa!!!!!! Sasa hivi ni mika 16 tangu Mwalimu kuachia madaraka, ndugu yangu, mtoto aliyezaliwa mwaka huo yuko Form three/four, bado tunajificha kwenya kwapa za mwalimu!!!!!!!!!!!
Mwisho, Mwalimu alikuwa na filosofia tofauti ya maendeleo; aliona tertiary education katika maeneo ya ufundi, biashara, kilimo, ufugaji, uganga na afya, uongozi n.k kama kiungo muhimu cha kuwakomboa Watanzania badala ya kuwa na utitili wa vyuo vikuu vinavyota vihiyo wengi wasio na ujuzi wa kubadili maisha yao wenyewe na watanzania masikini kwa ujumla.
 
Kaazi kweli kweli. Asiyejua maana hawezi kuambiwa maana. Nyerere is gone. What we have now is ours, whether ni njaa, kipato kidogo etc. Kama mpaka leo hii hatujaweza kurekebisha Nyerere alipokosea, zaidi ya kuendelea kuharibu, why do we attack him? Nini cha maana tulichofanya ambacho ni tofauti na Nyerere? Huku kuwa omba omba wa kimataifa na kumleta George Bush Tanzania?
 
Ndugu NasDaz,
Maoni uliyotoa ni yako, lakini yana walakini mkubwa kudai kwamba kwa sababu Mwalimu alikuwa Mkuu wa nchi kati ya 1962 na 1985, basi yeye ndiyo shina la dimbwi la matatizo tuliyonayo, nasema hapana. Sina haja ya kuchambua hoja zako moja moja, mimi nitajumuisha kwa kukuonyesha tu kwamba, kama ni kwel Mwalimu hakufanya mengi mazuri na matatizo tuliyonayo yalipikwa na yeye, waliopo wameshinda nini kuipaisha nchi na imekuwa tegemezi zaidi, umasikini umezidi (kama hujui kwa sababu unaangalia magari na maorofa ya Dar, nenda kijiji chochote kisarawe, rufuji, kilwa, bagamoyo et al ujionee uduni wa maisha) na ujinga unazidi licha ya wewe kudai kisahihi kibisa kwamba Mwalimu alicha vyuo viku viwilina sasa ni utitili!
Kagame alishika Rwanda 1994, miaka kumi baada ya Mwalimu kung'atuka, wenzetu wana dira, wanapaa!!!!!! Sasa hivi ni mika 16 tangu Mwalimu kuachia madaraka, ndugu yangu, mtoto aliyezaliwa mwaka huo yuko Form three/four, bado tunajificha kwenya kwapa za mwalimu!!!!!!!!!!!
Mwisho, Mwalimu alikuwa na filosofia tofauti ya maendeleo; aliona tertiary education katika maeneo ya ufundi, biashara, kilimo, ufugaji, uganga na afya, uongozi n.k kama kiungo muhimu cha kuwakomboa Watanzania badala ya kuwa na utitili wa vyuo vikuu vinavyota vihiyo wengi wasio na ujuzi wa kubadili maisha yao wenyewe na watanzania masikini kwa ujumla.

kaka Kesesela ni miaka 26 (1985-2011) watwambie ndani ya miaka hii yote wamerekebisha nini???umetolea mfano wa rwanda ambao tunajua genocide 1994 na sasa wako wapi?lazima tukubali maovu yetu kuwa hatuna viongozi, we are totally failed,na kukubali makosa ni sehem mojawapo ya kupiga hatua mbele!
 
Wanaochangia mada inayomhusu Nyerere mara nyingi wanaingia kwenye mtego aidha wa kumchukia au kumtetea bila sababu za msingi. Wengine wanaishiwa cha kusema ispokuwa kuleta udini. Wamefilisika. Nyerere alikuwa ni binadamu. Katika vitu ninavyomsifu Nyerere mpaka leo ni kuwa alikuwa na akili nyingi na mwerevu, na alikuweza kusimamia kitu alichokiamua. Nyerere alikuwa na mapungufu yake, japokuwa wakti mwingine yalikuwa na ncha kali kabisa. Nami nitatoa maoni yangu kuhusu Nyerere. Mimi ni Mkatoliki. Nimesoma shule ya msingi ya misionari amabapo baba yangu alinilipia ada mpaka namaliza darasa la saba halafu nikaingia shule ya Saint Benedict Secondary School Kingonsera. Hii ni kati ya shule zilizochukuwa na Serikali mwaka 1970 na kuitwa Kigonsera Secondary School.

Elimu
Kwa upande wa elimu tusimsifie sana Nyerere. Shule alizoziacha mkoloni ndizo Nyerere alizobakia nazo. Alijenga chache sana. Alifanya elimu ni ya bure kutoka shule ya msingi mpaka chuo kikuu. Alitaifisha shule za dini, nyingi zikiwa za Kikristu ili waislamu nao wapate elimu ya bure.
Nyerere alikuwa na msimamo wa kutopanua shule za sekondari. Sera ilikuwa watu wote angalau wapate elimu ya msingi, wachache waingie sekondari ili wawe wafanyakazi wa serikali, na wachache zaidi waende vyuo vikuu.
Leo wengi wanamlilia Nyerere kwa vile alitoa elimu bure. Lakini Watanzania lazima wakumbuke kuwa elimu ya bure ina madhara kwenye uchumi wa taifa na elimu yenyewe vile vile. Wananchi lazima wajifunze kuwa wakizaa watoto ni wa kwao siyo wa serikali. Serikali isaidie lakini isitwishwe mzigo wote. Serikali ya Nyerere ilifanya afya, elimu bure kwa wananchi wake lakini ikashindwa kusomesha watu wengi kutokana na kukosa pesa ya kutosha. Nakumbuka mwaka 1969 wanafunzi 13,000 tu ndiyo walichaguliwa kuingia sekondari kwa nchi nzima! Serikali ilijitahidi kudidimiza bei za mazao ya wakulima ili ipate pesa za kuendeshea elimu na afya mpaka wakulima wakaacha kulima na kufanya hali ya uchumi kuwa mbaya zaidi. Hizi ni kati ya sababu inazofanya Tanzania iwe kati ya nchi za mwisho kwa elimu barani Afrika.
Uchumi.
Hakuna nyanja ambayo Nyerere alifanya vibaya zaidi kuliko swala la uchumi. Nyerere alichukia ubepari na ukabila. He was a Fabianist. Hicho ndicho kilichomfanya ataifishe mali za makampuni ya binafsi na kuziita ni za umma. Lakini kitu kingine kilichomfanya ataifishe mali za binafsi ni kuwa alikuwa anaogopa matajiri asingeweza kuwatawala kirahisi. Hiyo ndiyo sababu vilevile iliyomfanya ataifishe vyama vikuu vya ushirika kama KNCU. BCU, NgoMat, n.k. Wakuu wake kama akina Kahama, Bomani, Ngwilulupi, Kapinga, etc.walipewa kazi serikalini au mashirika yaliyotaifishwa.
Mashirika mengi ya Umma yalikufa siyo kwa sababu ya rushwa au wizi bali sababu ya uongozi mbaya. Kwa kweli tulikuwa na mameneja ambao hawakuwa na sifa za kuendesha mashirika makubwa kama yale. Masihirika yote aliyoanzisha Nyerere yalikuwa ni kama yamekufa wakati anaondoka tukabakia na mizoga tu.
Kitu kingine kilichoharibu uchumi wa Tanzania ni uanzishwaji wa vijiji vya ujamaa. Vijiji vingi vilipewa misaaada kama matrekta na malori ya gharama kubwa kwa serikali lakini walishindwa kuyatumia. Kulikuwa hakuna technicians wa kuyahudumia na yakafa.
Kuna watu wanaamini kuwa Nyerere alijenga uchumi imara. Nyerere alitoka Ikulu akiacha nchi ina dola laki tano tu (USD500,000). Sijui wangapi mnakumbuka wakati Nyerere alipokuwa anazunguka duniani kuaga rafiki zake nchi ilishindwa kabisa kununua mafuta. Ilibidi Rais Mwinyi aseme mapato yote ya mauzo ya kahawa yasiguswe bali yalipie mafuta. Kwa kweli Rais aliyekuja kuiokoa hii nchi kiuchumi ni Mkapa, pamoja na mapungufu yake. Ametoka ikulu wakati nchi ikiwa Dola Billion tatu na kidogo.
Rushwa.
Nyerere alichukia sana rushwa. Japokuwa hata wakati wake rushwa ilikuwepo lakini ilikuwa si kama tunavyoona leo. Ilikuwa ni nadra sana kusikia mtu ameshukiwa kwa rushwa. Waliokwapua waliwajibishwa. Njagu (intelligence) walimwagwa kila mahali kunusa rushwa na kujua yupi anamsema vibaya Nyerere na serikali yake.
Hata hivyo naweza kusema Nyerere alikuwa ni chanzo cha rushwa iliyotapakaaTanzania ya leo bila ya yeye kukusudia(Unintended consequences). Nazungumzia rushwa iliyotapakaa kwenye maofisi yote ya serikali, yaani ile ya kudaiwa kitu kidogo ili uhudumiwe. Rushwa hii vilevile inadidimiza uchumi wa Tanznaia. Sizungumzii rushwa ya ulafi wa wakubwa wanaokwapua mabilioni, hii ni ya hawa makuu wa siku hizi.
Rushwa ndogo ndogo, ambayo inakera kweli kweli ilianzia enzi za Nyerere kutokana na vitu viwili. Kwanza mwaka 1966 baada ya mgomo wa wanafunzi wa UDSM Nyerere alisema kiwango cha juu kabisa cha mshahara kitakuwa Shs. 5,000 ambao alisema ndiyo utakuwa mshahara wake kwa mwezi. Kiwango kile hakikubadilika labda mpaka anatoka urais licha ya gharama za maisha kupanda sana sana. Cha kushangaza, alipostaafu mwaka 1985 ilitangazwa kuwa posho yake kwa mwezi itakuwa Shs 74,000 (bila kodi) wakati alikuwa anapata Shs 5,000 kwa mwezi. Kwa kweli alikuwa hana uchungu na matatizo ya wafanyakazi. Kitu cha pili kilicholeta makali sana kwa wafanyakazi ni ile Sheria ya Kodi ya mapato ya mwaka 1973. Kodi ile dhidi ya wafanyakazi ilikuwa ni ya kiroho mbaya sana.
Utawala
Nyere alikuwa havumilii kabisa mtu kumsema yeye au serikali yake. Wote waliojaribu kufanya hivyo waiishia pabaya. Mifano ipo mingi tu kama akina Tuntemeke Sanga na Kambona. Nyerere alikuwa akikuchukia alikuchukia kweli kweli, na akikupenda alikupenda sana na alikuwa radhi kukufumbia macho. Wale wenye archives fuatilieni hotuba ya Nyerere mwaka 1977 ambapo alisema hawezi kukosa usingizi mtu akimwambia mkewe chumabi kwake kuwa hampendi lakini hatavumilia kama ataitisha mkutano na kusema hayo.
Nje ya Tanzania
Nyerere alijijengea sifa kubwa nje ya mipaka yetu. Alituletea sifa nyingi sana. Hata ulikuwa ukitembelea nchi za nje walikuwa wanatuheshimu. Akisimama kuzungumza walikuwa wanamsikiliza. Nchi nyingi tulikuwa hatuhitaji visa. Sifa za Nyerere mpaka leo hii bado ni nyingi sana huko nje, kama zilivyo nchini.
Hitimisho
Nyerere alikuwa binadamu kama binadamu wengine wote. Alikuwa na mazuri na mabaya. Tusimjadili kutumia udini. Udini utaiumiza Tanzania ya leo na kesho siyo Nyerere ambaye tumemzika.
 
Nyerere alikuwa ni rais bora kwa mambo yafuatayo.
  1. Aliweka misingi ya umoja miongoni mwa Tanzania kwa kuhakikisha kuwa makabila 120 ya Tanzania yote yanaweza kuunganishwa na lugha moja ya Taifa-Kiswahili. Alihakikisha kuwa watanzania wanakuwa ni wamoja kwa kuanza na utoaji wa elimu wa kuwachanganya watanzania wa sehemu mbalimbali, mfano Mtu anatoka Mtwara kwenda kusoma sekondari ya Mara na kunyume chake. Hapo aliweza kujenga umoja miongoni mwetu
Umeandika mengi sana, naona ni itakuwa vyema tukichambuwa mojamoja, tunaanza kwa mlolongo wako:

Hilo la kwanza si kweli, Nyerere alikuja Dar ambayo ni pwani na ndio chimbuko la Kiswahili, alikuja tayari anajuwa Kiswahili, Jee, alikifikisha yeye huko kwao halafu ndio akajifundisha?

Kiswahili kilishaenea Afrika Mashariki na zaidi kwa karne kadhaa kabla ya Nyerere. soma:

For centuries, Swahili remained as the language for the people of the East African coast. Long-time interactions with other people bordering the Indian Ocean spread the Swahili language to distant places such as on the islands of Comoro and Madagascar and even far beyond to South Africa, Oman and United Arab Emirates. Trade and migration from the Swahili coast during the nineteenth-century helped spread the language to the interior of particularly Tanzania. It also reached Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, Central African Rebublic, and Mozambique.

Hata hilo la kuwachanganya kwa kusoma si kweli kuwa alifanya hivyo kwa ajili ya kuwachanganya watu, hayo yalianza kufanyika kabla ya Nyerere na yeye mwenyewe Nyerere ni kielelezo tosha kwa hilo, kazaliwa wapi? kasoma wapi? akafundisha wapi? Ingekuwa kabla ya yeye kuchukuwa madaraka hakuna muingiliano, kuchanganyika, mawasiliano na amani angefika huko shule alizosoma na kazini?

Nyerere aliwahamisha watu kwa nguvu kutimiza siasa yake ya ujamaa iliyoshindwa na ilikuwa ni moja ya njia za kulitumikia kanisa (hili lina ushahidi).
 
Back
Top Bottom