Nyerere Hakuwa na mapungufu, alikuwa Kiongozi Mbovu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere Hakuwa na mapungufu, alikuwa Kiongozi Mbovu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NasDaz, Dec 4, 2011.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Humu ndani, kuna watu wakiona Hayati Julius Nyerere, the First Preisdent wa URT anasemwa vibaya basi wanakuja juu!! Kinachonikera mimi, ni wengi wao kuhusisha na imani za dini!

  Kwamba, mtu akisema ubaya wa Nyerere, na hasa mtu huyo akihisiwa ni Mwislamu, basi hoja ya wapofu wa hoja watachukulia ukosoaji huo ni chuki ya waislamu dhidi ya Nyerere!! Hivi ni lini Waislamu wamepata kuwa na chuki na mwalimu?! Sasa haya mambo kwamba mtu akitaja mabovu ya Mwalimu basi ni chuki za waislamu dhidi ya mwalimu yanatoka wapi?! Binafsi, am muslim, na kama utaniambia nikutajie my favorite president sitasita kumtaja Julius Nyerere. lakini pamoja na yote hayo, kama nitaambiwa nitaje top two poorest presidents ever happaned in our history, basi Nyerere ni mmoja wapo, akiwa sambamba na mwinyi!

  Binafsi, nikimwangalia Nyerere, ni eneo moja peke yake ambalo linaweza kumweka kama best leader! hakuwa corrupt leader ingawaje serikali yake ilikuwa very corrupt government!! Na wala si kweli kwamba Nyerere alikuwa mkali kwa corrupt leaders, vinginevyo nchi hii Mwinyi asingeikuta alipoikuta! Sana sana ki2 ambacho labda Nyerere aliweza kuzuia ni kutokuwa na State House corrupt leaders...lakini ukitoka hapo, wengi walikuwa corrupts!

  Serikali ya Nyerere ilijaa watendaji ambao walikosa kabisa uwajibikaji na ndio maana Mwinyi alikuja na kitu kilichojulikana kama Fagio La Chuma! Kwanini awe na fagi la chuma wakati uwajibikaji ulikuwapo?! Serikali isiyo corrupt, haiwezi kuwa na irresponsible leaders. Ni kweli, Nyerere hakuwa corrupt leader, lakini aliendesha corrupt government na anayebisha aniambie kwanini viwanda vyote vilifia mikononi mwake!!

  Ni kweli JK ni goi goi! hata Nyerere alikuwa ni goi goi kupita kiasi!! hakuwa mkali kama tunavyoaminishwa watu ambao hatukuwa na ufahamu wakati wa utawala wake. Nyerer alikuwa mkali kwa wapinzani wake wa kisiasa, and not otherwise!! Kama alikuwa mkali kweli, umasikini tulionao ulitokea wapi?! Aliwafanya nini waliokuwa wanaharibu mali za umma zaidi ya kuwahamisha?! kama sio ugoi goi tuite nini hii?!

  Kulikuwa na miradi kadhaa ambayo ilianzishwa wakati wa utawala wake, na vilevile ilikufa hata kabla haijafika kokote....sasa kama sio ubadhirifu huo tuite nini?! Siwezi kumsifia kiongozi aliye msafi yeye pekee na familia yake wakati serikali yake imejaa watu irresponsible!!

  Amekaa Ikulu more than 20 years lakini ametoka akiwa ameachwa barabara zimejaa mahandaki kila mahali!! Bahati mbaya sana, sehemu ambazo zilikuwa na corrupt leaders toka kwenye serikali yake ndio sehemu pekee ambazo angalau zilikuwa na barabara nzuri kidogo! Sehemu ambazo walitoka honest leaders kama yeye, ndizo zikabaki balaa tupu!!! Hiyo ndio sababu kuu iliyofanya mikoa ya kusini kuwa hoe hae zaidi kwani viongozi wake wengi walikuwa honest kama yeye...hawa ni pamoja na akina Kawawa na Nnauye!

  Hivyo, umaskini wa kusini haukusababishwa na Nyerere kama Nyerere, bali ulisababishwa na irresponsible central government ambayo ugawaji wa keki ya taifa haukuwa the same! ilitegemea sana sehemu husika ana power gani serikalini and how corrupt s/he is!!!

  Nyerere ameondoka akiwa ameacha vyuo vikuu viwili tu, UDSM na SUA na kuishia tu ktk kujenga vyuo vya kati ambavyo hata hivyo navyo productivity yake ilikuwa chini. Chuo pekee cha kati ambacho kilikuwa kinatoa elimu ya maana labda ni Mzumbe peke yake....na sababu kuu ni kwavile kilikuwa more political! Tena hata nina mashaka kama kweli kilikuwa kinatoa elimu ya maana!! tangu lini katibu wa nini sijui mwenye miaka 45++ akaweza kuhimili mikiki mikiki ya elimu ya juu?!

  Tunaambiwa enzi zake elimu ilikuwa na ubora kuliko sasa!! na hii ndio tabia ya wazee....kwamba kila kitu chao kilikuwa bora!!! Huo ubora ulisaidia nini basi katika kutatua matatizo ya uchumi wa nchi hii?! Sana sana hao tunaoambiwa walikuwa wasomi wakati wa elimu bora ndio hao hao waliogeuka kuwa corrupts wasio na haya wakati wa Mwinyi.....bisheni!!! Kama ni kweli wakati huo elimu ilikuwa bora basi vilevile ilisaidia kuzalisha BEST CORRUPT LEADERS!!! Serkali corrupt haiwezi kuwa na jeuri ya kujenga vyuo vikuu vya kutiosha kwavile haina fedha.....kutokuwa na fedha ni dalili ya serikali corrupt!!!

  MATATIZO ya umeme tuliyonayo hivi sasa source yake ilikuwa enzi za mwalimu!!! Serikali ya Mwalimu haiku-forecast mahitaji ya umeme over the next 50 years!! Ni kweli, wakati wa Nyerere, haukuwa wa mgao! Sasa mgao ungetoka wapi wakati nyumba zenyewe za umeme zilikuwa chache?! Mgao ungetoka wapi wakati hakukuwa na uzalishaji mkubwa wa kuhitaji matumizi ya umeme?! Mgao ungetoka wapi wakati hata kumiliki radio ilikuwa ni anasa?! Kwahiyo, si kwamba ni uongozi bora wa Nyerere ambao ulifanya nchi isiwe na mgao/upungufu wa umeme, bali hiyo ilikuwa ni matokeo ya serikali mbovu!

  Tunaambiwa huduma za jamii zilikuwa bure! Huduma gani za jamii?! hizo za kufuata zahanati kilometa 50 na shule ya msingi kilometa 10?! Dar es salaam yote hii aliacha shule saba tu za sekondari (za serikali, ambazo hata hivyo hakujenga yeye)-Jangwani, Azania, Tambaza, Forodhani, Kisutu na Kibasila!!! Nani atakayethubutu kusema kwamba shule hizo zilikuwa zinakidhi mahitaji ya elimu ya sekondari jijini? Huko mikoani ndo ilikuwa balaa tupu, unaweza kukuta mkoa mzima una shule moja au mbili za serkali.....bado tunaambiwa huduma za jamii zilikuwa bure! Ni serikali gani ingeshindwa kuhudumia shule chache kama hizo?!

  Ubovu wa serikali ya Nyerere ni mwingi kuliko uzuri wake, otherwise, wale wanaoona kwamba mgtu akisema basi ana chuki za kidini (styupid thinking) basi anitajie hapa mazuri yaliyofanywa na serikali yake ambayo natarajia yawe mengi kuliko mabovu!

  wapo watakaosema kwamba Nyerere amewezesha nchi hii kuwa na amani! Kwani aliichukuwa wakati nchi haina amani?! Sifa kama hizo anatastahili kupewa Kagame aliyechukua nchi baada ya mauaji ya kutisha nchini mwake! Anyway, waliosoma historia wanisaidie kunitajia ni vita gani vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimepata kupiganwa Tanganyika katika karne ya 19! Kama hakuna au zilikuwa si za kutisha sana, basi inawezekana Watanganyika hatuna silika ya kupigana tangu zama hizo!!

  Hivyo basi, mtu anavyotaja ubovu wa Nyerere inakuwa ni ujinga uliepitiliza kusema kwamba ni chuki binafsi...Na inakuwa sio ujinga, bali ni upumbavu mtu akisema ni chuki za kidini! Nyerere kama Nyerere alikuwa was a very good person BUT NOT A GOOD LEADER! He was a good person who was a poor leader! Kutokana na hayo, sipati kigumumizi hata chembe kusema wazi kwamba SI KWAMBA NYERERE ALIKUWA NA MAPUNGUFU, BALI ALIKUWA KIONGOZI MBOVU! Ukweli wenyewe ndio huo, ukiona mgumu kuumeza, chukua maji ushushie!

  Anayekataa, atoe data za mazuri yake kama kiongozi yenyewe manufaa kwa Tanzania!
   
 2. T

  Topical JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  oh my god.

  st. Nyerere...

  mtakatifu hana dhambi wewe hujaenda shule nini?
   
 3. S

  Seacliff Senior Member

  #3
  Dec 4, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  NasDaz, unashindwa kuelewa kwamba ukitafuta ubaya wa kiongozi yeyote duniani utaupata. Sitawatetea wale wanaodai kuwa Waislamu wana chuki na Nyerere kwa sababu huo ni ufinyu wa mawazo, ila nafikiri wale wote wanaomsifia Nyerere ni watu ambao wameangalia kwa makini yale aliyofanya kwenye kipindi cha uongozi wake.

  Mimi ni mmoja wao. Nimeona first hand umuhimu wa elimu ya bure na afya ya bure kwa sababu nimeifaidi. Nimekwenda darasani ambapo nimekuta textbooks kabatini pale darasani na kila mara daftari langu linavyomalizika nakwenda kwa mwalimu ananigawia lingine jipya naendelea na kazi yangu kama mwanafunzi.

  Wanaomsifia Mwalimu hawaangalii ni kiasi gani ameijaza mifuko ya watu bali wanaangalia kuwa nchi as a whole imesonga mbele kiasi gani wakati yupo. True, kuna policy zake nyingine zilitunyima maendeleo kiasi fulani lakini nitashangaa kama utamlinganisha Mwalimu na kiongozi kama Mheshimiwa wetu wa sasa ambaye anakaa kimya wakati amezungukwa na wezi wa wazi wazi. Hata watu wake kwenye chama chake mwenyewe wanamlaumu kwa mambo yanayoendelea.

  Usiwe na chuki kwa sababu ya wajinga wachache wanaotaka kuendeleza chuki za kidini na za kikabila. Wakati wa Nyerere usingeweza ukasikia mtu anasema wazi wazi kuwa mtu fulani hafai kwa sababu ya dini yake au kabila lake na siyo kwa sababu watu walikuwa wanapendana kuliko sasa hivi ila ni kwa kuwa viongozi waliokuweko wakati huo walikuwa wanatuonyesha kuwa taifa haliwezi kuendelea bila waTanzania kushirikiana kama wamoja. Chukia wanaomtetea kwa kutumia mbinu mbaya lakini mpe Mwalimu heshima anayostahili, please.
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  huwezi sema eti baada ya miaka 50 nchi ya tatu duniani kwa kuomba omba na umasikini
  na yeye Nyerere alitawala nusu ya miaka hiyo 50 halafu useme Nyerere was the best leader Afrika

  that is insult to people with brain........
   
 5. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,994
  Trophy Points: 280
  Mbovu tu au mbovu zaidi ya wote?
   
 6. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimeisoma hii habari yako ndefuuuu mpaka nimefika mwisho ila sijaelewa hasa ni nini unachotaka kusema au ni nini hasa mchango wa hiki ulichokiandika katika maendeleo ya Tanzania yetu hii ya sasa.

  Unataka kutuambia kwamba kwa vile kipindi cha Nyerere kulikuwa na viongozi corrupt kwa hiyo ni halali na sasa tuwe na viongozi corrupt? Embu tupe link kati ya hicho ulichokiandika na hali ya Tanzania kwa sasa mkuu...

  Tusijadili historia tuuuu bila kujua inatusaidia nini katika maisha yetu kama watanzania wa leo.
   
 7. T

  Topical JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  everybody

  Nilikuwa nafikiri anataka kusema nyerere alikuwa kiongozi mbovu bahati aka over stay 24 yrs

  Viongozi waliofuata ilibidi wasafishe uchafu mwingi uliolundikana, ikiwemo tabia chafu (kutowajibika, rushwa ) iliyojengeka miaka 24yrs kwa civil servants wa taifa..wakajikuta wanamaliza miaka 20yrs kufanya hivyo..

  Kwa hiyo 24-20 =4 inafact sisi kama nchi nafikiri tumefanya kazi miaka minne kutokana na historia hii..

  Nafikiri hiyo ndio LINK
   
 8. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #8
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,994
  Trophy Points: 280
  Tatizo lililokuwepo chini ya mwalimu la kuwahamisha viongozi wabovu na wala rushwa kama punishment badala ya kuwavua madaraka na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria, kusema kweli limetu cost na bado linaendelea kufanya hivyo...Ni culture mbovu ambayo mizizi yake ni CCM.
   
 9. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #9
  Dec 5, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  everybody,

  Kumbuka kuwa kinga ni bora kuliko tiba. Tunasoma historia ili kujuwa vikwazo na mafanikio ya wazee wetu akiwemo Mwalimu. Kujua walipatia wapi na/au walikosea wapi, inasaidia sana kuepuka kurudia makosa waliyofanya wazee waliotutangulia.

  Kwa mantiki hiyo basi, wazee wetu wote wanajadilika. Kuna baadhi ya watz hawapendi kuona au kusikia Mwalimu akitajwa vibaya. Kibaya sasa, badala ya kujibu hoja za msingi, wanakimbilia matusi na kejeli au hoja ya udini ama husema 'Mwalimu alishakufa, haifai kumjadili kwa kuwa hawezi kujibu tuhuma dhidi yake'. Majibu hayo yanaashiria kukosa majibu kwenye hoja za msingi.

  Kila binadam ana mazuri na mabaya yake. Tafakari.
   
 10. M

  Mchomamoto Senior Member

  #10
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimesoma michango yenu wana JF wenzangu!!wengi wenu mnahitaji shule kubwa sana juu ya L. Nyerere na kipindi cha uongozi wake, ni shule ndefu kidogo na inayohitaji uwe tayari kuisikiliza nakuielewa la sivyo utakurupuka tu juu ya L.Nyerere!!!
   
 11. M

  Mchomamoto Senior Member

  #11
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimesoma comments zenu wana JF wenzangu lakini wengi nimeona mnahitaji darasa la kutosha juu ya Late Nyerere na kipindi cha uongozi wake, la sivyo unaweza kukurupuka kuongea juu ya uongozi wake maana wengi hawana ufahamu kwenye hilo!!!!
   
 12. T

  Topical JF-Expert Member

  #12
  Dec 5, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Usitishe watu kwamba kuna kitu kikubwa sana kwenye uongozi wa nyerere..

  embu eleza moja moja basi tuelewe kuliko maneno matupu..
   
 13. JS

  JS JF-Expert Member

  #13
  Dec 5, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tupatie basi hiyo shule Mchomamoto maana wengine ndo tunajifunzia hapa hapa kiundani zaidi. Itakuwa vizuri zaidi.
   
 14. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #14
  Dec 5, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  Haya wa dunia leteni mazuri ya Nyerere maana mimi nikisema hakuna, mtabisha lakini kuonesha zuri lake hamuwezi.
   
 15. K

  KISUKALI Member

  #15
  Dec 5, 2011
  Joined: Feb 28, 2010
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fungua Darasa mkuu kuna Wanafunzi wengi tu, tayari kupokea Elimu juu ya somo husika.
   
 16. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #16
  Dec 5, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Solution mojawapo ni kuangalia balance of payments....
  Ni kitu gani kinachotuingizia fedha taifa letu..?
  Fedha kutokana na jasho letu ni kiasi gani?
  Pili ni kitu gani kinachotumalizia fedha yetu?.... social services?... oil?
  Halafu ndiyo tufananishe ni rais yupi ali manage uchumi wetu vizuri kuliko mwingine yeyote.
  Maneno bila figures ni sawa na jibwa linalobwakia mti ambao wala hauna masikio na hauwezi kuhama.
   
 17. I

  IWILL JF-Expert Member

  #17
  Dec 5, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Dhambi kubwa ya nyerere ilikuwa ni kumuteua Mwinyi kuwa rais, kumpendekeza Mkapa kama mgombea wa chama chake na pia kumfanyia kampeni kama zuzu, naye Mkapa akampa urais pungu1 kuongoza nchi.....here we are!!!!
   
 18. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #18
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,994
  Trophy Points: 280
  Kwani ni yapi tunayafanya ya tofauti hadi tuwe na nguvu ya kumnyoshea mwalimu kidole?

   
 19. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #19
  Dec 5, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nyerere alikuwa ni rais bora kwa mambo yafuatayo.
  1. Aliweka misingi ya umoja miongoni mwa Tanzania kwa kuhakikisha kuwa makabila 120 ya Tanzania yote yanaweza kuunganishwa na lugha moja ya Taifa-Kiswahili. Alihakikisha kuwa watanzania wanakuwa ni wamoja kwa kuanza na utoaji wa elimu wa kuwachanganya watanzania wa sehemu mbalimbali, mfano Mtu anatoka Mtwara kwenda kusoma sekondari ya Mara na kunyume chake. Hapo aliweza kujenga umoja miongoni mwetu
  2. Alikuwa akijali zaidi masilahi ya watu masikini na hivyo kufuata siasa ya ujamaa na kujitegemea, elimu bure, matibabu bure
  3. Nyerere aliweza kusimamia kile alichoamini, hata kama huko mbeleni kilikuwa kinamfanya aonekane wa ajabu. Alikuwa na msemo kuwa 'Ukigeuka nyuma utakuwa jiwe'. Msimamo ambao ulimfanya aachie madaraka kwa amani baada ya kuona kuwa hakuwa na uwezo wa kuendelea kuyasimamia yale aliyoyaamini tena baada ya kubanwa mbavu na nchi za kibepari.
  4. Nyerere aliweza kuzuia uvunaji wa maliasili zetu kwa kigezo kuwa 'Watanzania bado hawajawa na uwezo wa kuvuna rasilimali zetu kwa faida yetu'. Akazuia uchimbaji wa madini mpaka tutakapopata Technology yetu, huo ulikuwa ni mtazamo wa kiongozi anayeangalia Future generation zaidi ya kuangalia masilahi binafsi ya wakati uliopo.

  Ubovu wa Nyerere akiwa rais
  1. Serikali yake ilijengeka katika misingi ya hofu na kutoaminiana miongoni mwa wananchi hasa kuhusu kuisema serikali vibaya, kuna watu waliteswa na kuwekwa kizuizini na mpaka leo hii wengine hawajulikani walipo - Huu ulikuwa ni udikteta baridi.
  2. Nyerere alikuwa ni mbovu sana katika uchumi kiasi kwamba nchi ilikuwa hoi bin taaban kwenye uchumi. Kitendo cha kuwakabidhi nyadhifa za U-GM watu waliokuwa wanaonekana kumtii zaidi na kuwa watiifu kwa Chama bila kujali uwezo wao kitaaluma kiliua makampuni mengi ya umma. Mtu anaiba Mwanza anahamishiwa Mtwara.
  3. Kuna wakati aliitwa 'HAAMBILIKI' kwa kutokuwa tayari kusikiliza ushauri wa kitaalam kuhusu uchumi na kujikuta analiingiza Taifa katika mporomoko mkubwa sana wa kiuchumi. Watu walivaa kaniki na mifuko ya mbolea iliyokuwa ikijulikana kama 'visalfeti'.
  4. Alikuwa ni rais ambaye aliyewalea mafisadi na kuwalinda ili mradi tu ni makada wazuri wa TANU and later CCM, mfumo ambao mpaka leo hii unaendelea kuliangamiza taifa, mfumo wa kulindana. Unaiba ATC unahamishiwa NIC ila ni sharti uoneshe kweli wewe ni kada mzuri.
  5. Azimio la Arusha ilikuwa ni worse decision than ever, huwezi kuwainua masikini kwa kuwanyang'anya matajiri bali kwa kuwawezesha nao wafikie huo utajiri, utaifishaji uliirudisha nyuma nchi kimaendeleo, mifumo ya kiuchumi dunia ilikuwa katika mtiririko huu 'Communism -> Slavery -> Feudalism -> Capitalism - > Socialism' Kitendo cha Nyerere kuruka mfumo mmoja muhimu zaidi wa Capitalism, na kurukia mfumo wa mwisho ambao mataifa mengi yalioendelea bado hayaufikia wa Socialim, ilikuwa ni makosa, hamuwezi kugawana umasikini halafu mkabakia salama. Matokeo yake sehemu zote zilizotaifishwa zikawa failure.
  6. Uanzishwaji wa vijiji vya ujamaa ni another nightmare ya Nyerere. Bila kujua au kwa kujua watendaji wake walikuwa wakihamisha watu kwenye makazi yao ya kudumu kwa nguvu na kuwahamishia sehemu nyingine waanzishe vijiji. Kuna baadhi ya watanzania waliliwa na Simba kwa kuachwa porini waanzishe vijiji.

  Mazuri baada ya kustaafu:
  1. Alikuwa active katika kuifanya serikali kumfikiria reaction yake itakuwaje katika maamuzi mengi na hivyo kuwa kama watch dog na kuiwajibisha serikali kiasi fulani.
  2. Hakuogopa mtu alikuwa kisema yale anayoamini kuwa ni ya kweli na hivyo kujenga nidhamu fulani miongoni mwa watendaji wa serikali na viongozi.
  3. Kumkataa Malecela (Jumanne) kugombea urais, alituepusha na kutawaliwa na muhuni. Kwani aliwahi kumuweka kwenye kundi la wahuni, hatujui nini kingetokea kama huyu bwana angeachwa ili apigiwe kura na mkutano mkuu maalum.
  4. Kitendo cha kumuwekea Mizengwe Jakaya kwenye uteuzi wa mgombea urais 1995, ilikuwa ni good movie ilituepusha mapema na uatwala wa kiswahiba.

  Mabaya baada ya kustaafu
  1. Kitendo cha kumpigia chepuo Mkapa na kupitishwa kuwa mgombea wa CCM mwaka 1995 na baadae kuja kugeuka mjasiliamali Ikulu ilikuwa ni kutuuzia mbuzi kwenye gunia. Leo hii angekuwa hai hakuna ambaye angemsikiliza tena kwenye kutuwekea viongozi.
  2. Nyarere ni MUANZILISHI WA UCHAKACHUAJI WA KURA. Mwaka 1995 Baada ya Seif kumshinda Salmini na DTV kutangaza wiki moja kabla ya uchaguzi wa Tanzania bara, na yeye kwenda kulazimisha Salmini atangazwe ni dhambi na precedence ambayo itaendelea kumuandama hasa pale watanzania watakapokuwa wanatoana ngeu kwa wizi wa Kura uliozoeleka ambao muasisi wake ni Nyerere.

  Note:
  Japo nyerere anaingia kwenye kundi la marais waliofanya vibaya zaidi, ila historia inamuweka pazuri kwa kumtetea kuwa Baada ya harakati za kudai Uhuru ambazo alikuwa ni moja ya sehemu muhimu. Tanzania ya baada ya uhuru ilikuwa na wasomi wachache na hivyo kujikuta katika wakati mgumu wa kupata watendaji walifuzu. Matokeo yake akawaweka makada wa Chama kuendesha uchumi kisiasa zaidi ya kitaalam. Dhambi ambayo mpaka leo inawaandama viongozi wengi kwa kujiona wao ni kila kitu, na kukubali kuwa hujui ni kushindwa uongozi. Matokeo yake tuna viongozi ambao wao kila taaluma wanaijua, Udaktari, Uhandisi, Uhasibu na kila kitu.
   
 20. kashengo

  kashengo JF-Expert Member

  #20
  Dec 5, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 2,651
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 180
  Umejitahidi kuyabainisha...ILA KUIBA KURA kwa kweli ni jambo la kishenzi kabisa yeye kama muasisi uchaguzi wa zanzibar 1995
   
Loading...