inamankusweke
JF-Expert Member
- Apr 24, 2014
- 17,944
- 18,211
Alibinua royce rolls la Bei Kali katikati ya umasikini,lipo makumbushoWewe ndiyo unawadanganya watu.
Mambo ya kusema mtu sijui amekuja lini Dar, hayana msingi, na hayana uhusiano.
Mwalimu wakati wa uhuru mwaka 1961 (sikuwepo) akitangazwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza, alifika Mnazi mmoja akiwa kwenye benz. Benz hiyo ilinunuliwa na serikali ya Mwingereza. Miaka kadhaa iliyofuata alitumia benz.
Nikiwa na akili timamu, nipo shule ya msingi, nilimwona Mwalimu mwaka 1978 akiwa kwenye 110 landrover Mkoani Iringa. Mwaka 1979 nilikuwa eneo moja linaitwa Madaba, huko Ruvuma, nilimwona mwalimu akiwa kwenye 110. Watu wakawa wanaiongelea sana hiyo gari kwa sababu walikuwa hawajaona toleo hilo la landrover. Landrover zilizozoeleka zilikuwa ni 109.
Mwaka 1989, nimemwona Mwalimu akiwa kwenye landrover kijijini Butiama.
Kwa umri wako, haipendezi kuwahadaa watu.
Mwalimu alitumia benz, na huenda hata magari mengine lakini siyo eti kwa sababu ya kupenda anasa. Kwa ujumla Mwalimu aliyaishi maisha ya chini sana, maisha ya kawaida, nadiriki kusema ya chini kuliko hata tuliyokuwa tukiishi sisi.
Wanaotoka karibu na Butiama, wakaangalie pale kwenye jumba la makumbusho yake wakaone vitu alivyokuwa akivitumia, pamoja na mavazi yake. Nilipokuwa pale nilishangaa kuona hata saa alizokuwa akizivaa, kwa miaka ile ya 1980, ni zile ambazo zilikuwa zikiuzwa kule Kariakoo sh 5,000.