Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,467
- 40,972
Waliowahi kukutana na Mwalimu Nyerere, hawatakosa kumwelezea Mwalimu jinsi alivyojiona kuwa ni sawa na watu wengine.
Nikiwa shule ya msingi, darasa 4, nilipata nafasi kwa mara ya kwanza kushikana mkono na Mwalimu Nyerere, si pekee yangu bali tulikuwa watoto 8.
Mara ya pili nilikutana na kula naye Mwalimu Nyerere Butiama, akiwa amestaafu, nami nikiwa JKT baada ya kumaliza kidato cha 6, tukiwa tumepelekwa kwenye ujenzi wa nyumba aliyozawadiwa na jeshi baada ya kustaafu.
Maisha ya Mwalimu Nyerere kuanzia kufanya kazi kwa mikono yake, siyo kwaajili ya kupigwa picha bali kupalilia shamba la mahindi na mihogo kule Mwitongo, toka asubuhi mpaka saa 8 mchana (naiona taswira yake katika akili yangu akiwa amebeba jembe begani anarudi toka shambani akiwa amechoka), mpaka ulaji wake wa chakula, ilikuwa vigumu kuamini kuwa huyu tunayekula naye alikuwa Rais wa nchi. Sisi tuliwekewa chakula mezani, yeye akawa anakula na wajukuu zake kwenye sahani moja na bakuli moja.
Mwalimu Nyerere hakuwahi kujiona kuwa yeye ni binadamu zaidi kuliko binadamu wengine.
Mwalimu Nyerere, kuna wajinga fulani walijaribu kumwita MTUKUFU RAIS, aliwakemea na kuwakatalia kuwa hataki kabisa kuitwa MTUKUFU kwa maana mtukufu ni Mungu pekee yake. Baadaye wengine walijaribu kumwita MHESHIMIWA RAIS, Mwalimu alikataa, akawaambia kuwa wa kuheshimiwa ni wananchi. Akawaagiza kuwa aitwe NDUGU RAIS. Na hiyo ilienea kwa viongozi wake wote. Wakaitwa Ndugu Waziri, Ndugu Mkuu wa Mkoa, Ndugu Mbunge, n.k. Lakini Mwalimu pamoja na kuitwa Ndugu, alipata heshima kubwa ndani na nje ya Tanzania. Matendo yake, maadili yale, uzalendo wake na upendo wake wa dhati kwa watu wake vilimpa heshima kubwa.
Leo tuna viongpzi waongo, wanafiki, wapenda sifa, wengine wevi na mafisadi, wala rushwa, wapora kura, wauaji, watekeji, wabambikiaji kesi, wapendelea watu, waonezi wa watu, LAKINI wanataka waitwe WAHESHIMIWA, wakati hawana heshima, na hakuna anayewaheshimu bali wanaoneshwa unafiki wa kuheshimiwa, na wao kwa sababu wana akili ndogo, wanaamini kuwa wanaheshimiwa.
Viongozi, fanyeni yaliyo ya heshima, mtapata heshima. Lakini kwa kujiita WAHESHIMIWA hamtakuwa waheshimiwa kama mnafanya mambo ya hovyo. Uue watu, uteke, ubambikie watu kesi, wewe kweli unajiona unastahili kuheshimiwa?