Nyerere Day: tuwakumbuke mashujaa hawa wawili kwa pamoja

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,841
30,168
NYERERE DAY: TUWAKUMBUKE MASHUJAA HAWA WAWILI KWA PAMOJA ABDULWAHID KLEIST SYKES NA JULIUS KAMBARAGE NYERERE

Leo tarehe 13 Oktoba ndiyo siku aliyozikwa Abdul Sykes siku ya Jumapili mwaka wa 1968.

Fumba macho yako na lete picha ya Mtaa wa Lindi, Gerezani mwaka wa 1968 umma mkubwa umefurika nyumbani kwa Bi. Mruguru bint Mussa watu wako kwenye msiba Abdul Sykes amefariki na maziko yake ndiyo yanasubiriwa.

Dar es Salaam ilikuwa haijapata kushuhudia mazishi makubwa kama haya.

Watu wamefurika mtaa mzima na mitaa ya jirani wanasubiri maiti ipelekwe msikiti wa Kitumbini kwa ajili ya sala ya jeneza kisha mwili ukazikwe makaburi ya Kisutu.

Julius Kambarage Nyerere amekaa barazani nyumbani kwa Bi. Mruguru katika jamvi yuko na Ahmed Rashad Ali na watu wengine maarufu katika mji wa Dar es Salaam.

Katika hawa watu maarufu ni Chief Abdallah Said Fundikira.

Yeye ametokea Nairobi Makao Makuu ya East African Airways ambayo yeye alikuwa Mwenyekiti wa shirika hilo.

Chief Fundikira amekuja kumzika rafiki yake.

Katika baraza hiyo yuko Zuberi Mtemvu, Shariff Abdulkadir Juneid, Rashid Mfaume Kawawa, Ali Mwinyi Tambwe kwa kuwataja wachache.

Mwezi Oktoba jua ni kali sana Dar es Salaam na joto lake linakithiri.

Mwalimu Nyerere ametulia tuli jamvini anasubiri maziko.

Mwili uko tayari waliokuwa wanashughulika ndani walikuwa masheikh wawili maarufu mjini Dar es Salaam, Maalim Mohamed Matar na Sheikh Kassim bin Juma siku hizo anafahamika zaidi kwa jina la Darwesh.

Kabla jeneza alijatoka Mwalimu Nyerere ameomba aruhusiwe kumwaga rafiki yake Abdul Sykes.

Nyerere ameomba auone uso wa Abdul Sykes kwa mara ya mwisho.

Mwalimu akafahamishwa kuwa Waislam hawafunui maiti hivyo akasimama kwa dakika chache kisha akatoka nje.

Usifumbue macho yako bakia hivyo hivyo vuta picha jeneza limetoka na likagombewa kupokelewa Mwalimu Nyerere wasaidizi wake wamemweke nyuma ya jeneza katikati analiangalia jeneza.

Siku ile ulinzi ulikuwa umeimarishwa pakubwa kwa sababu kulikuwa na mgogoro mkubwa wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) mgogoro ambao haujapata kutokea.

Taarifa za kijintelijensia zilikuwa zinasema kuwa Waislam wamekasirishwa na msimamo wa serikali na kuna hofu huenda kuwepo kwa Nyerere mazikoni pale kunaweza kuzua vurugu.

Paul London alikuwa rafiki ya baba yangu na watu wakifanyakazi Exchange, moja ya Idara za Posta ikishughuika na mawasiliano ya simu.

Paul London alikuwa rafiki ya Abdul Sykes.

Katika uimarishajiwa ulinzi siku ile kwa bahati mbaya bila kukusudia kwa jinsi watu walivyoshonana, Paul London alikatiza mbele ya Nyerere.

Watu wa usalama wakambana huku na huku wakaendanae pembeni wakamchuua hadi Central Police.

Baada ya maziko walimwachia baada ya Pau London kueleza vyema uhusiano wake na marehemu.

Mwalimu alitembea kwa miguu kutoka nyumbani kwa Bi. Mruguru hadi Msikiti wa Kitumbini akasimama nje kusubiri sala ya jeneza.

Nje ya msikiti kulikuwa na umma mkubwa.

Siku zile maduka ya jirani na msikiti mengi yalikuwa ni maduka ya Wahindi washoni wa nguo.

Muhindi mmoja kuona Mwalimu kasimama akachuua kiti kumpelekea akae.

Mwalimu akakataa kukaa akabakia kasimama.

Maiti ilipotoka Mwalimu akawa bado yuko nyuma ya jeneza Abdul Sykes anamsindikiza rafiki yake hadi Makaburi ya Kisutu alipozikwa.

Mwalimu hakupata baada ya siku hii kushiriki katika maziko yoyote yale kwa nama hii.

Msomaji wangu naamini unajiuliza nini sababu ya Mwalimu Nyerere kufanya hivi?

Imesadifu kuwa vifo vya marafiki hawa wawili wazalendo, Abdul Sykes na Julius Nyerere vimefuatana tarehe zao katika mwezi huu wa Oktoba kama kadi zao za TANU zilivyofatana.

Huwezi kuandika historia ya Nyerere ukamwacha Abdul Sykes nje ya kurasa zako kwani utakuwa umeidhulumu historia ya Tanzania na umejidhulumu mwenyewe katika utafiti wako.

PICHA: Kulia ni Nangwanda Lawi Sijaona, Abdul Sykes, Julius Nyerere na Dossa Aziz kwenye hafla ya kumuaga Nyerere safari ya pili UNO mwaka wa 1957.

Msikiti wa Kitumbini kama ulivyo sasa.

Msikiti unafanyiwa ukarabati mkubwa.

Screenshot_20211013-194336_Facebook.jpg
 
Nyerere wakati anaenda kucheck Afya London aliondoka akiwa mzima na furaha tele baada ya kufika hospital mambo yakabadilika.
 
Kumbe Nangwanda Sijaona alikuwa Kiongozi?
Alikuwa nani? Ilikuwaje Hadi akapewa jina la uwanja wa mpira?
 
Siku ile ulinzi ulikuwa umeimarishwa pakubwa kwa sababu kulikuwa na mgogoro mkubwa wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) mgogoro ambao haujapata kutokea.

Taarifa za kijintelijensia zilikuwa zinasema kuwa Waislam wamekasirishwa na msimamo wa serikali na kuna hofu huenda kuwepo kwa Nyerere mazikoni pale kunaweza kuzua vurugu.

Mzee Mohamed

Kuna ulazima upi kuunganisha sehemu hiyo hapo juu kwenye bandiko lako?

Kuna uhusiano wowote ule na Kichwa cha habari?
 
Siku ile ulinzi ulikuwa umeimarishwa pakubwa kwa sababu kulikuwa na mgogoro mkubwa wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) mgogoro ambao haujapata kutokea.

Taarifa za kijintelijensia zilikuwa zinasema kuwa Waislam wamekasirishwa na msimamo wa serikali na kuna hofu huenda kuwepo kwa Nyerere mazikoni pale kunaweza kuzua vurugu.

Mzee Mohamed

Kuna ulazima upi kuunganisha sehemu hiyo hapo juu kwenye bandiko lako?

Kuna uhusiano wowote ule na Kichwa cha habari?
Uzalendo...
Hayo ni sehemu ya mambo muhimu yaliyotokea katika maziko ya Abdul Sykes.

Labda nikueleze yaliyopitikana asubuhi siku ile ya mazishi.

Watu wa usalama walishauri Nyerere asihudhurie maziko.

Rashid Kawawa alipinga ushauri ule.

Kawawa alimwambia Nyerere kuwa watu wa Dar es Salaam wasingemjua kama si Abdul Sykes kumpokea kwake na kwenye TAA nakufanya yote aliyofanya hadi Nyerere akachukua uongozi wa TAA na kisha TANU.

Abdul na Nyerere walikuwa rafiki ndugu na Nyerere aliishi nyumbani kwa Abdul baada ya kuacha kazi ya ualimu na ikiwa hatahudhuria maziko yake watu watamfikiria vibaya sana.

Kawawa akamwambia kuwa Chief Abdallah Said Fundikira amewasili kutoka Nairobi kuja mazikoni.

Ikawa hoja ya Kawawa imeshinda na kilichotakiwa kufanywa ni kuimarisha ulinzi ii Nyerere ahudhuriie maziko ya Abdul Sykes.

Nyerere aliagiza ng'ombe mmoja apelekwe nyumbani kwa Bi. Mruguru bint Mussa kama kitoweo kwa watu watakokuja mazikoni.
 
Kumbe Nangwanda Sijaona alikuwa Kiongozi?
Alikuwa nani? Ilikuwaje Hadi akapewa jina la uwanja wa mpira?
The Boss,
Nmekunyambulia hayo hapo chini kutoka kitabu cha Abdul Sykes:

''TAA mjini Lindi ilikuwa chini ya uongozi wa Suleiman Masudi Mnonji aliyekuwa Rais na Katibu wake alikuwa Mohamed Waziri.

Mnonji alikuwa fundi cherahani na Waziri alikuwa mchoraji wa ramani za nyumba.

TAA ilichelewa kuanza mjini Lindi. TAA ilianzishwa Lindi mwaka 1953 wakati uongozi wa TAA mjini Dar es Salaam si tu ulikuwa unaigeuza TAA kuwa chama cha siasa bali ulikuwa ukifanya mipango kumpeleka mjumbe wake Umoja wa Mataifa kudai uhuru.

Masudi Mnonji alikuwa na uzoefu wa kutosha katika siasa.

Baada ya Vita Kuu ya Pili alikuwa amejaribu kuanzisha vyama vya wafanyakazi katika mashamba mbalimbali ya mkonge kusini mwa Tanganyika.

Vilevile aliwakusanya wapishi na madobi mjini Lindi waanzishe umoja wao.

Ilikuwa kupitia juhudi zake binafsi TAA ijapokuwa ilichelewa, ilikuja kuanzishwa mjini Lindi na Mnonji alijitolea nyumba yake katika mtaa wa Makonde kama ofisi ya chama.

Mnonji kwa kutambua umuhimu wa kuwa na uongozi ulioelimika vizuri, alimleta Lawi Nangwanda Sijaona kutoka Nachingwea aje Lindi aishauri TAA jinsi ya kufanya mambo kwa utaalamu.''

Suleiman Masudi Mnonji nyumba yake ndiyo ilikujakuwa ofisi ya kwanza ya TANU Jimbo la Kusini siku zile likijulikana kama Southern Province.

Mwaka wa 1958 baada ya TANU kuamua kushiriki katika Uchaguzi wa Kura Tatu ndipo Lawi Sijaona akaingia katika Baraza la Kutunga Sheria.

Nakurejesha tena kwenye kitabu cha Abdul Sykes:

''Kwa sababu ya yale masharti magumu ya uchaguzi, TANU ilibidi itazame nje ya uongozi wake ili kupata wagombea uchaguzi wenye sifa zilizohitajika kugombea uchaguzi dhidi ya UTP.

TANU iliwachagua Julius Nyerere, Chief Abdallah Said Fundikira, John Ketto, Nesmo Eliufoo, John Mwakangale, Lawi Sijaona, Paul Bomani na George Kahama kusimama kama wagombea wa TANU.''

Lawi Sijaona hakupata kumsahau Masudi Mnonji na hata pale alipowekwa kizuizini Lawi Sijaona akiwa waziri katika serikali ya Nyerere alikuwa akimtembelea kumfariji na walibakia marafiki hadi Mnonji alipofariki dunia.
 
Maelezo yanataja watu wanne lakini picha uliyoweka ina watu wawili! Je, huyo aliyesimama katika picha ya watu wawili ndiye Abdul Sykes au?
F...
Picha ina watu wannr ikiwa hao wengine hawaonekani ni tatizo la mtandao.

Aliyesimama ndiye Abdulwahid Kleist Sykes.
 
Back
Top Bottom