Nyerere Day; Siku ya wapinzani wa CCM ?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,702
71,013
Tarehe 14 ya mwezi October kila mwaka Watanzania wameifanya siku ya kumbukumbu ya kifo cha Mwl J.K.Nyerere (RIP) kutokana na mchango wake kwa taifa hili ambao kila mtu anautambua.
Pamoja na yote,Mwalimu alipiga vita kwa nguvu zake zote ufisadi,ubinafsi,unyonyaji,ubadhilifu wa mali ya umma,ujinga,maradhi na vyote vyenye majina mabaya.
Tokea kifo chake,CCM imeamua kuyakumbatia na kuyaenzi yale yote aliyoyakataa kwa nguvu mpya na kasi ya ajabu.
Kwa kuwa Wapinzani sasa wanazungumza kile alichokuwa anasema Mwalimu,kwa nini tusiipitishe siku ya kumbukumbu yake kuwa siku ya upinzani dhidi ya CCM kwa viongozi kuandaa maandamano na hotuba zenye hamasa ya kufahamu kinachoendelea ili kila raia mwema wa nchi hii afahamu na kuunga mkono juhudi hizo.
.
 
Enzi hizo ilikuwa kwenye Kigoda Cha Mwalimu Ni wiki ya kumsakama na kumsimanga Jakaya lakin tangu Chuma kishike mpini wamepoteana
 
Sio kwamba watu hawana hoja bali wengi wanaogopa kupimwa mkojo. Hasara za kuzuia watu kuongea tutaziona vizuri baada ya awamu hii ya kwanza kuisha.
 
Kumbe enzi zile wanajiachia ilitokana Na ujasiri wa Rais wa wakati huo kuruhusu kutukanwa Sio ujasiri WA watukanaji kutoogopa chochote maana Sasa hivi wameufyata hakuna Cha Warioba, Butiku wala Shivji
 
Alitukanwa au alikuwa anaambiwa ukweli? Huyu wa sasa hana kifua kipana cha kuvumilia kusikia ukweli na wala sio ubora. Ukiwa na matumizi mabaya ya madaraka huwezi kuruhusu kusikia ukweli, lakini ukimudu kusikia ukweli utakuwa bora na nafasi ya makosa yanayoweza kuepukika huondoka.
 
Kumbe enzi zile wanajiachia ilitokana Na ujasiri wa Rais wa wakati huo kuruhusu kutukanwa Sio ujasiri WA watukanaji kutoogopa chochote maana Sasa hivi wameufyata hakuna Cha Warioba, Butiku wala Shivji
Hivi kwa akili yako yule na huyu nani anatukanwa sana kwa maana ya kutukanwa? Mkwere analikuwa anapewa vijembe vya kisiasa na alivikubali na yeye alikuwa anajibu pia bila hasira.
Jamaa yangu ndiye amejitafutia matusi mwenyewe na majina ya ajabu ajabu hajawahi kuitwa yeyote aliyepata kuingia ofisi ile
 
Tarehe 14 ya mwezi October kila mwaka Watanzania wameifanya siku ya kumbukumbu ya kifo cha Mwl J.K.Nyerere (RIP) kutokana na mchango wake kwa taifa hili ambao kila mtu anautambua.
Pamoja na yote,Mwalimu alipiga vita kwa nguvu zake zote ufisadi,ubinafsi,unyonyaji,ubadhilifu wa mali ya umma,ujinga,maradhi na vyote vyenye majina mabaya.
Tokea kifo chake,CCM imeamua kuyakumbatia na kuyaenzi yale yote aliyoyakataa kwa nguvu mpya na kasi ya ajabu.
Kwa kuwa Wapinzani sasa wanazungumza kile alichokuwa anasema Mwalimu,kwa nini tusiipitishe siku ya kumbukumbu yake kuwa siku ya upinzani dhidi ya CCM kwa viongozi kuandaa maandamano na hotuba zenye hamasa ya kufahamu kinachoendelea ili kila raia mwema wa nchi hii afahamu na kuunga mkono juhudi hizo.
.
wapinzani wanaompa fisadi fursa?
 
Acheni utani na usanii nyie. Kwa upinzani huu Wa njaa na utapeli?
 
Kumbe enzi zile wanajiachia ilitokana Na ujasiri wa Rais wa wakati huo kuruhusu kutukanwa Sio ujasiri WA watukanaji kutoogopa chochote maana Sasa hivi wameufyata hakuna Cha Warioba, Butiku wala Shivji
kwa upeo wa akili yako unadhani kuogopwa na kuwaziba watu midomo ndio jambo la.kupelekea nchi kuendlea ? unaikumbuka G55? hii ilitokea wakati huyo mwalimu akiwa hai. sema na wanaokutuma na kukulipa hakuna maendeleo bila watu kukinzana mawazo. madhara yatakayopatikana kwa kuwaziba watu midomo ni makubwa kuliko ujenzi wa reli na madege
 
wapinzani wanaompa fisadi fursa?
fisadi ni nani? serikali inayopiga vita ufisadi inaruhusuje kiongozi wake kuingiza makontena yote yale bila kulipa ushuru na au kuchukuliwa hatua yyete? ati nawe ni Chizi chizi?
 
kwa upeo wa akili yako unadhani kuogopwa na kuwaziba watu midomo ndio jambo la.kupelekea nchi kuendlea ? unaikumbuka G55? hii ilitokea wakati huyo mwalimu akiwa hai. sema na wanaokutuma na kukulipa hakuna maendeleo bila watu kukinzana mawazo. madhara yatakayopatikana kwa kuwaziba watu midomo ni makubwa kuliko ujenzi wa reli na madege

G55 ilitokea wakati wa Mzee Ally Hassan Mwinyi

Wakati wa Nyerere ulikuwa Ni kupiga Makofi ya zidumu fikra sahihi Za Mwenyekiti

Kwa taarifa yako Pengine ulikuwa Mdogo Au hujazaliwa

Magu hajafikia umafia wa Julius Nyerere
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom