Nyerere Day: Kutoka Ukumbi wa Arnautoglo 1963 hadi Ukumbi wa Diamond 1985

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,786
30,079
NYERERE DAY KUTOKA UKUMBI WA ARNAUTOGLO 1953 HADI UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE 1985

Julius Kambarage Nyerere aliunyanyua mguu wake kuanza safari ya uongozi wa Tanganyika tarehe 17 April 1953 katika uchaguzi wa kugombea urais TAA.

Julius Nyerere sasa akijulikana kama Baba wa Taifa aliliaga taifa la Tanzania tarehe 5 Novemba 1985 akiondoka madarakani.

Mtangazaji Khalid Gangana amenihoji kuhusu Mwalimu Nyerere na wazalendo wengine aliokuwanao katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Pamoja na hayo alitaka kujua pia hotuba gani za Mwalimu ambazo mimi binafsi zimenigusa na kunifikirisha.

Nilimtandikia hotuba kadhaa katika kitanga chake.

Mbili ndani ya Parish Hall, Tabora wakati wa Kura Tatu na siku ya pili baada ya kupita Kura Tatu hotuba aliyotoa Nyerere sokoni Tabora.

Katika hotuba hii Mwalimu aliangua kilio ba hali kadhalika wananchi waliokuwa wanamsikiliza.

Kuna mambo hadi leo mimi bado yananitatanisha sijui kwa nini yamekuja kuwa hivi.

Mtangazaji Khalid amepata hamu ya kunihoji baada ya kusoma makala yangu ya wazalendo saba waliolala usingizi fofofo kwa miaka.

Nilimweleza kuwa ile sefu ya Ally Sykes kwangu mimi ilikuwa mfano wa kisiwa chenye hazina katika kitabu cha R L Stevenson, "Treasure Island," nami nikabahatika kuigundua hazina hii kisiwani ilipofichwa.

Moja ya hazina nilizopata ni kuiona saini halisi ya Julius Nyerere kwenye karatasi ya kawaida katika barua za TAA.

Nikakuta mengi.

Nashangazwa sana na vitabu viwili vya maisha ya Rashid Kawawa.

Historia ya Mzee Rashid Kawawa haioani na yale niliyosoma kuhusu yeye katika Nyaraka za Sykes nilizosoma.

Dome Okochi Budohi na Rashid Kawawa wakifahamiana vyema na walipata kucheza filamu moja pamoja, "Mgeni Mwema."

Dome Budohi kadi yake ya TANU No. 6 na alikamatwa na Special Branch 1955 kwa shutuma za kuwa Mau Mau.

Aliwekwa kwenye Kambi ya Mau Mau Handeni ambako Kawawa alikuwa mmoja wa wafanyakazi wanaoshughulika na hawa wafungwa Dome akiwa mmojawapo.

Kawawa hajaeleza chochote katika vitabu vyote viwili kuhusu Dome Budohi.

Kama vile Dome mwenye kadi ya TANU No. 6 na kiongozi katika TAA pamoja na Nyerere, Abdul Sykes, Ally Sykes John Rupia, Kasella Bantu kwa kuwataja wachache, hakuwapo au hakupata kumjua.

Haya ni baadhi ya mambo niliyoeleza.

Kipindi hiki kitakuwa hewani hivi karibuni.

Picha ya nne wa pili kutoka kushoto ni Rashid Kawawa wakati wa ujana wake akiwa mcheza filamu maarufu.

Screenshot_20211006-231221_Facebook.jpg
 
Hizi picha zilipigwa kabla ya kupata uhuru wa Tanganyika? Je kipindi hicho laptop zilishaingia Tanzania?
 
Hizi picha zilipigwa kabla ya kupata uhuru wa Tanganyika? Je kipindi hicho laptop zilishaingia Tanzania?
Dumu,
Ni picha zipi?

Hizo za Black and White ni za zamani computer bado.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom