Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,794
- 71,214
Wakati Watanzania wakikumbuka miaka 20 ya uwepo wa CCM bila ya mwanzilishi wake Mwl J.K.Nyerere chama hicho kikongwe kilipaswa kukaa chini na kujipima mbona kimeondoka mioyoni mwa Watanzania na kutoka kuwa chama cha siasa (maridhiano) na kubakia kuwa Chama dola (mabavu)?
Mfano mwepesi kabisa ni hili zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa, imekuwaje watu hawataki kujiandikisha mpaka imebidi vitumike vitisho kwa watumishi mfano waalimu wakajiandikishe?
Hivi imefikia hali ya kulazimishana kujiandikisha kupiga kura wakati zamani siku zilionekana hazitoshi kwa wingi wa wanaojiandikisha?
Hii inaonyesha kuwa watu wenye mapenzi na CCM wanaweza kuwa chini ya 20% kulingana na turn up ya hiari ya uchaguzi.
Sasa jee wale mamia na maelfu wanaojitokeza kuonyesha ni wanaccm ni "wajasiriamali wa kisiasa?"
Wakati tukielekea 2020 kwenye uchaguzi mkuu, huu wa serikali za mitaa upinzani ilikuwa kete muhimu kwao kuamua kutangaza kutoshiriki kwa kutaja sababu zao ili zitekelezwe haraka. Lakini tumeona wapinzani kadhaa ndio wanapiga kampeni ili watu wajiandikishe wasidharau na kesho wanalia wao.
CCM ya Magufuli iangalie inaangukia wapi? Ubabe na kujimwambafai havita wapeleka kokote zaidi ya kujipoteza kwenye ramani ya kisiasa na kubaki kuwa chama cha polisi na TISS.