Nyerere azidi kumkaba Mkapa ataka kiongozi huyo aondolewe pensheni yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere azidi kumkaba Mkapa ataka kiongozi huyo aondolewe pensheni yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 9, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Sitta Tumma, Mwanza

  MBUNGE wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (CHADEMA), amezidi kumkaba koo Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, safari hii akitaka kiongozi huyo aondolewe pensheni yake, akidai kuwa anaitumia kwa maslahi ya chama chake cha CCM.

  Nyerere aliingia kwenye mabishano na Mkapa wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki baada ya Rais huyo kudai kuwa mwanasiasa huyo si mmoja kati ya wanafamilia wa Julius Nyerere.


  Hata hivyo, siku moja baada ya Mkapa kutoa kauli hiyo, familia ya Nyerere kupitia kwa mwanaye Madaraka Nyerere, ilijitokeza na kusema Vicent ni mwanafamilia wao kwa vile ni mtoto wa baba mdogo wao, Kiboko Nyerere.  Toka wakati huo, Vicent amekuwa akimwandama Mkapa, akidai kuwa anatumia nafasi yake vibaya kama Rais mstaafu kwani anagharamiwa mafao yake ya uzeeni (pensheni) kutokana na kodi ya Watanzania wote.  Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Mara baada ya kurejea kutoka Arumeru ambako chama chake kilitwaa kiti cha ubunge na yeye akiwa meneja kampeni msaidizi, Nyerere aliwaambia wananchi kuwa mpaka anapaswa kuiga mfano wa marais wenzake wastaafu.  "Mkapa anapaswa kuachana kabisa na ushabiki wa kisiasa Wakati wa chaguzi ndogo ikiwa ni pamoja na kukumbatia chama kimoja, wakati maisha yake anahudumiwa kwa fedha zetu wote, vinginevyo aondolewe pensheni ili abakie ‘mpiga debe' wa CCM," alisema.  Katika mkutano huo uliyohudhuriwa na mamia ya wananchi ukilenga kuzungumzia maendeleo ya jimbo na kujipongeza kwa ushindi wa Arumeru Mashariki, Nyerere alisema kuwa Mkapa kwa nafasi yake hiyo anapaswa awe mshauri wa vyama vyote na si kuipigia debe CCM.  "Akumbuke kwamba maisha yake yanaendeshwa na fedha za walipakodi wa Kitanzania hadi sasa, aache kabisa ubaguzi huo; atajenga chuki kubwa kwa wananchi," aliongeza.  Nyerere alilazimika kuzungumzia sakata lake na Mkapa baada ya wananchi kumwomba aelezee kidogo kauli ya kiongozi huyo ya kudai kuwa yeye si mwana familia wa hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.  Kuhsu miradi ya maendeleo jimboni kwake humo, Nyerere aliuagiza uongozi wa manispaa ya Musoma mjini kuhakikisha unamfungulia mashtaka mahakamani mmiliki wa kampuni moja ya Ngeja iliyopewa tenda ya kusambaza umeme katika soko la Kamunyonge, iwapo itafika kesho pasipo kuanza kusambaza nishati hiyo sokoni humo.  Alisema tayari manispaa ilimpa hundi ya fedha za malipo ya kazi hiyo na kwamba ameonekana kutaka kutapeli fedha hizo.


   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Suluhisho ni katiba mpya,kama pension walipwe na nssf/ppf na sio sirikali kama mbwai mbwai bwana!
   
 3. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,949
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  wacha kiroho kimuume muuaji mkubwa huyo, mkwapa
   
 4. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Walipwe na vyama vyao kwa maana ya mshahara na marupurupu mengine. Pension huwezi kumuondelea au useme alipwe na chama hiyo itakuwa ni kumuonea.
   
 5. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Baba yake alikuwa campaigner mkubwa wa CCM toka alipostaafu mwaka 1985 na 1990
   
 6. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Wenzetu wa Malawi waliweza kumuondolea pensheni rais mstaafu kwa kushiriki siasa akiwa mstaafu.
  Watanzania bana!
   
 7. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  atleast alikuwa anajitokeza kwenye urais na ubunge tena chaguz ndogo?
   
 8. S

  STIDE JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  "HIVI MKAPA KWANINI ULIMUUA BABA WA TAIFA!!?"
  Huyu dogo hatokuacha kamwe hadi useme ukweli toka rohoni mwako na UTUBU!! Ole wako ujifanye kumjibu........!!!
  Ulidhani yameisha!!? Dogo ana sapoti kubwa ya ukweli, na familia inamtumia kama chambo, sasa ropoka uone!!
   
 9. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  vicent kampiga knock nut mkapa!hatokuja shiriki kampeni yoyote tena,i believe
   
 10. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hili liwe fundisho kwa viongozi wetu wastaafu kuacha kubagua watz kwa misingi ya itikadi na kushiriki kampeni za vyama. Nilipigwa na butwaa pale mauaji ya wakereketwa wa Chadema yalipokuwa yanatokea kule Igunga yeye(Mkapa) aliendelea na kampeni. Sasa tufike mwisho tujali utanzania wetu na sio tofauti zetu.
   
 11. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #11
  Apr 9, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,996
  Likes Received: 2,651
  Trophy Points: 280
  Kumuonea?yeye ndio anatuonea.
   
 12. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #12
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Siku zote mi huwa nasema kwamba hili lijibwa mkapa ni lichawi sana na jambazi kubwa la rasilamali zetu so tuliache tu lipate vidonge vyake hadi life kwa pressure na ikidi baada ya hapo twende over-politics tufanye uchaguzi mdogo wa Rais mstaafu ili tumchague hata wasira kuliko hili jambazi undertaker.
  BIGUP NYERERE.
   
 13. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #13
  Apr 9, 2012
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,421
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Namchukia Mkapa, ni msaliti mkubwa sana wa nchi yetu.Ni jitu kuburi lisilo dhamini utanzania hata kidogo. Nani alishaona rais anawasemea mbovu wananchi kama alivyofanya Mkapa? Mwalimu alikosea kweli kuliona ndio linafaa kura rais.
  Huyu mtu katukosesha fursa kubwa, madini hasa dhahabu. aliwapa wazungu bureee! sisi tukaishia kukandiwa kuwa tuna wivu wa kike, wavivu wa kufikiri nk...tena kweny hotuba ya kufungua mgodi mpya (Tulawaka). siamini mpaka leo kama Mkapa ni kweli mtanzania au Mmsumbiji kama walivyosema watu...hata hivyo niliona mtu kwenye Tim tv ya msumbiji anafanana na Mkapa kweli!
  Conclusively, Mkapa si mzalendo hata kidogo...huwezi fananisha na Mwinyi aum Kikwete, hawa jamaa unaona kabisa ni watz halisi na wanadhamini wananchi...achana na madhaifu yao kama binadamu.

  I HATE YOU MKAPA.
   
 14. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #14
  Apr 9, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Usibwatuke..
  By then kulikuwa na vyama vingapi kisheria?
   
 15. josefast

  josefast JF-Expert Member

  #15
  Apr 9, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  mkapa aibuuu! M4C kushoto-kulia, hapa-kule!
   
 16. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #16
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nakuunga mkono Kabla yakupost fikiri kwanza.
   
 17. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #17
  Apr 9, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh hapa mnataka kummaliza mama Maria Nyerere; maana naye hayo mafungu ya Serikali ndiyo yanamsaidia kuendesha hiyo Familia yake na yeye mwenyewe kwa ujumla"
   
 18. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #18
  Apr 9, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Hawezi kupata ujasiri huo Nkapa. Anajua mahesabu yamekosewa ametumia formula isiyokuwa yenyewe. Kagusa mahali pabaya.
   
 19. N

  NICE LAMECK JF-Expert Member

  #19
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilikuwepo katika mkutano ndivyo alivyotoa ushauri kwa Mkapa asante V.Nyerere.
   
 20. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #20
  Apr 9, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kwani BWM hawezi funguliwa mashtaka kwa hoja hiyo ya mauaji anayohusishwa nayo???
   
Loading...