nyerere atajwa uuzaji wanyamapori nje ya nchi-dira ya mtanzania

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
15,515
20,005
mwandishi charles mullinda wa gazeti la dira ya mtanzania la 6/10/2011 anaripoti kuhusishwa kwa baba wa taifa na uuzaji wa wanyamapori,
hawa mang'unyuka ndiye anayetajwa kuombewa kibali na baba wa taifa ili apate pesa ya kuwasomesha watoto wake,..marehemu baba yake(hawa)alikuwa mzee wa ccm na alikuwa karibu sana na baba wa taifa...
hakuna barua ya maombi ya kuwinda ya hawa mang'unyuka au ya baba wa taifa ya kumuombea kibali iliyoambatanishwa kwenye habari
ps..
kampuni ya hawa mang'unyuka ya ham marketing company ltd ndio inayohusishwa na utoroshaji wa wanyamapori hai 116 nje ya nchi mwaka jana...
nawasilsha
 
Kwa habari kama hii mtawadanganya watoto wadogo waliozaliwa miaka ya 90 ambao hawakupata kuona uongozi na kumsikia Nyerere kwa uongozi wk.
 
jamani msiumize kichwa kujadili mambo yaliyoandikwa kwenye gazeti la dira
 
ni nyerere yupi???baba wa taifa!!jamani hii laana itawamaliza magamba.kwahiyo wanatafuta wakumtupia zigo lao la mavi??
 
ha ha ha ha kweli zigo zito mtwishe mnyamwezi yaana wameona sasa wamsingizie baba wa taifa?ha ha ha hawana ishu hao haiwezekaniki kama kutuibia wanyama tumekugundua kwao waeleze yanayowahusu na sio kufufua walioshalala mautini.
 
wameshaaanza kufoji sahihi za mwalimu, ngoja tuone mzimu wake utakavyowarudi.
 
cha kusikitisha nao ni watanzania na kuna wanunuaji wa gazeti husika. Pia kumbuka hapao zimetumika nguvu, karatasi, wino na rasirimali nyingine ili gazeti lifike mtaani.
Nchi maskini kama yetu inasikitisha kuona wengine wameridhika na hawaoni haja ya kwenda zaidi ya hapa tulipo!
jamani msiumize kichwa kujadili mambo yaliyoandikwa kwenye gazeti la dira
 
magazeti mengine fungieni vitumbua tu msipate tabu,au kwa wazee wa kule kijijini vutieni sonyo(tumbaku la kienyeji).waandishi makanjanja!
 
Back
Top Bottom