Nyerere asema walimu wa chuo kikuu wanatakiwa kiukosoa serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere asema walimu wa chuo kikuu wanatakiwa kiukosoa serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurudumu, Dec 23, 2010.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Akihutubia walimu na wanacho kikuu cha dsm leo, kupitia wosia wa baba tbc1, amewakosoa walimu wa chuo kikuu wanaosema hewala bwana kwa kila kisemwacho na serikali.

  Amesema kuna wachache wanaochambua mipango na utendaji wa serikali na wanaandika vitabu. Akasema kwamba yeye hujitahidi kuvisoma hivyo vitabu. Kwamba kuna vile vitabu vinakosoa kwa mantiki na vinasaidia serikali kujitathmini.

  Lakini kuna vingine vinapiga kelele tu na kuna vichache vinaipamba serkali. Lakini huwa anavisoma vyote.

  Amesisitiza kwamba jamii na serikali vinajitaji sana chuo kikuu (kwa wakati ule chuo kikuu kulikuwa kimoja tu)

  -------------------------

  je, serkali na jamii ya tz leo wana mtazamo huu wa Nyerere kuhusu vyuo vikiunganishwa?
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Sasa ndio hivyo walimu hao hao na wasomi wengi tu wakija na mawazo mazuri ya kufanyiwa utafiti lakini ikitokea tu kwamba yamepingana na yale ya watawala wanavyotaka ndio kesho yake unasikia Mwalimu huyo huyo mara kapigwa risasi na watu wasiojulikana getini kwake.

  Acha taifa letu liendelee kudumaa na mawazo mgando. Maendeleo kamwe hayawezi kupatikana kama Wa-Tanzania wote tunamawazo wanayofanana.

  Ukweli huu hata Mzee wetu na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Warioba aliwahi kunukuliwa akisema kwamba ukiona katika kijiji fulani Vijana wanazo mawazo yanayofanana na yale ya wazee wao kwa kila njia na kwamba muda wote hushinda pamoja tu wakipiga gumzo basi wala usijisumbue kuuliza kiwango gani kijiji hicho kitakua kimejiweka kimaendeleo. Tanzania kama taifa hatuko mbali sana na ukweli huu.

  Lakini kubwa zaidi, kuna mwana-JF mmoja humu ndani anaitwa Ndg Ng'wanangwa ameliweka vizuri zaidi hali tulio nayo sasa hivi nchini mwetu akisema kwamba 'NI AHERI KWA SERIKALI KUPAMBANA NA WAASI WANAOPIGANA HUKO MAPORINI KULIKO KUPAMBANA NA WAASI WA KI-FIKRA' jinsihali ilvyo sasa. Hii ni kauli nzitu sana, sana, sana!!!

  Ni taathmini wa hali ya juu. Na maana yake ni kwamba wasomi kwa kuwa wamefika mahala mawazo yao hayasikilizwi, hayathaminiwi wala kuzingatiwa huku taifa likiendelea kuporomoka kana kwamba hakuna hata msomi mmoja tu basi ndio chanzo cha haya yote.

  Na wasomi vijana, hii ndio maana hasa kwetu kung'angania kutaka KUFA NA MAFISADI NA NDUGU ZAO ambao wengi wao ni mbumbumbu tu.Huu ni wakati mzuri sana ndugu, jamaa na marafiki wa MAFISADI kuwambia watu hawa kujitokeza waziwazi na kutuomba msamaha kama taifa laa sivyo na wao gharili itawakumba.

  Mwisho, ni rahisi sana kuua mwili wa watu kibao tu lakini KAMWA HAKUNA ALIEWAHI KUSHINDA VITA DHIDI YA'WAZO'. Kwa mfano tu, hata Prof Haroub Othman aliondoka lakina swala la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio hii hapa imekodoa macho. Prof Mwaikusa katuacha kaondoka zake lakini swala la Mgombea Binafsi ndio hiyo Wa-Tanzania pamoja na EU tumelivalia njuga mwili mzima!!!!
   
Loading...