Nyerere Aponda Safari za nje Za Rais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere Aponda Safari za nje Za Rais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ibange, Jan 27, 2012.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mtu anaweza kukishangaa sana kichwa cha habari hapo juu. Lakini niliguswa sana na hotuba ya Nyerere jana kipindi cha Wosia wa baba utadhani alikuwa anamponda JK. Nilitokwa na machozi baada ya hotuba kwani niliona fikra nzuri sana za wazee wetu zinapuuzwa kwa sasa na zinaonekana hazina maana. Alisema mambo yafuatayo:

  (i) Ni aibu rais na mawaziri wake kusafiri sana kwenda US, China, Russia nk kwa ajili ya kuomba
  (ii) Si ushujaa kufanikiwa kupata misaada kutoka nje
  (iii) Hatima ya kuombaomba nje ni kupuuzwa na mataifa yanayotoa misaada
  (iv) Ni aibu nchi kutokusanya kodi na kuwategemea nchi nyingine wakusanye kodi kwao waje watusaidie
  (v) Misaada hata siku moja haitapunguza umaskini. Alitoa mfano wa makanisa na misikiti kila siku tunatoa sadaka lakini hawajawahi kutosheka
  (vi) Alisisitiza swala la uwajibikaji, matumizi mazuri ya rasilimali na kutoza matajiri kodi bila ya mzaha ili tuweze kujiendesha wenyewe kama nchi

  Baada ya kusikiliza hotuba hii nimezikumbuka safari za JK nje kila mara kwa kisingizio cha kwenda kuomba na hata wakati wa kampeni alisema asiposafiri watanzania tutakufa njaa.

  My take. Viongozi wa leo wamekosa fikra sahihi za kukomboa wananchi wanaona ni rahisi kuomba nje kuliko kujenga na kutekeleza mipango ya kujitegemea. Nashauri Mod aanzishe mijadala kati ya wana JF na viongozi wa siasa kuhusu sera za vyama katika mambo ya msingi kama kujitegemea, maendeleo, ajira, mambo ya nje nk. Tukifika hapo JF tutaacha kushabikia vyama "blindly" na badala yake tutajiunga na vyama kutokana na sera zake zinazozingatia uhuru na maendeleo ya Tz ya leo. Ijumaa Karim!
   
 2. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  sawa kauli ya mwalimu haipaswi kupuuzwa lakini kila zama na kitabu chake...kuna mambo ya Nyerere ukiyafanya leo wakati wa utandawazi kwa kujifungia ndani ya nchi eti unatuma tu wawakilishi hakika unaowatuma watakudanganya siku moja. Enzi za mwalimu hata viongozi wa chini walikuwa hawasafiri sana hivyo ilikuwa sio rahisi kumdanganya. hivi sasa ni utandawazi ni ama kuchagua kuwapa ruksa wasaidizi wako waende nje na kuja kukushauri Rais ukiwa ndani au kuchagua kupewa majibu ya uongo na wasaidizi katika masuala ya msingi.
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Ili kuongoza kizazi cha utandawazi ni lazima Rais aujue na kuuelewa utandawazi. kwa kukaa ndani ya nchi ni kupitwa na wakati kwani utandawazi unakimbia kwa kasi ya ajabu
   
 4. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Nilidhani Nyerere wa Musoma au Makongoro
   
 5. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Mama Porojo again!!!
  Kwa hiyo ili rais aijue dunia inaidi azunguke weee!!!!!
  Kazi ya wasaidizi wengine ninini?
  Teknolojia ya kompyuta ni mapambo?
  Ooh,,...niwie radhi mama...kumbe JK huwa anakesha tu feis buku!!!,nilisahau
   
 6. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Kila kitabu na dhana zake..... sio kweli hoja ya msingi iko palepale, tuanatakiwa kujitegemea kwa rasilimali tulizo nazo
   
 7. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #7
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Huyu mzee alikuwa na maono ya mbali sana ...
   
 8. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #8
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mama porojo kwa porojo aah, kazi ipo, yaani watu wanaamua kufumba macho na kuziba masikio ili tu wamtetee father house, mmh eti utandawazi unakimbia, jamani!!!!!
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Jan 27, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kuombaomba ni kero kwa waombwaji!

  Hata katika level ya individual, mtu aneyependa kuombaomba kila mkikutana huwa anakera....na hasa kama akiwa anaomba wakati uwezo wa kutatua matatizo yake anao tena bila ya kuomba!
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Jan 27, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  JK ni balaa mie nimemuona anaongea kwenye forum kubwa ile akawa anaongea kama anaongea na wazee wa Darisalama nimeshangaa sana .Yaani haongei point anatoa historia utadhani anaongelea Temeke na wazee wa CCM
   
 11. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #11
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  JK ni JANGA!!!
   
 12. y

  yaya JF-Expert Member

  #12
  Jan 27, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mama Porojo naomba nikuulize.
  Jina lako ni kiashiria cha mawazo yako?
  Hii uliyoieleza hapo ndiyo tafsiri yako ya utandawazi??? Kusafiri sana ili usidanganywe??? Pole sana.
  Kumbe wapo wengi wanaokubaliana na porojo za bila kusafiri wa-Tz watakufa kwa njaa!!!
  Kama unafikiri maneno hayo ya Baba wa Taifa ni ya zama za kale basi umekosea. Aliyazungumza kama nabii akitabiri jinsi nchi ya Tz itakavyoendeshwa pindi akija kiongozi anayefikiri wa-Tz hawana uwezo kwa lolote zaidi ya kuombewa misaada.
   
 13. i

  ibange JF-Expert Member

  #13
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ndivyo Nyerere alivyosema. Akasema heshima ya mtu inatokana na kujitegemea. Kama hana ulemavu na anaombaomba atapuuzwa na hata watu watakuwa wanamkimbia
   
 14. k

  kwamagombe Senior Member

  #14
  Jan 27, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Marehemu Baba wa Taifa alikuwa anaona mbali saana, ardhi imejaa tele, rasilimali za kumwaga lakini leo hii nchi inakuwa omba omba ni aibu sana, kwakweli hatujajipanga watanzania wenzangu na hasa viongozi wa Serikali. ni aibu saaaaana kuomba tunajidhalilisha
   
 15. WILLY GAMBA

  WILLY GAMBA JF-Expert Member

  #15
  Jan 27, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 210
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Viongozi makini kusafiri huwa option ya mwisho. Angalia Kim II Sung,Sadam, Gadafi, ninawaheshimu sana kwa kutufunza kuwa safari sio tija ila inaweza kuwa ni udhaifu wako.
   
 16. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #16
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,131
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Ukitaka majibu ya chapchap kutoka kwa JK kuhusiana na hizo hotuba za baba wa taifa kuusiana na hizo safari anazokwenda kuomba misaada basi tegemea jibu kama hili - "Nasafiri sana kwenda nnje kwasababu utawala wa Mwalimu nchi ilikua haina watu wengi kama sasa"
   
 17. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #17
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Marehemu Raisi Nyerere alikuwa Mwl wa Watanzania, kwa kila hatua alijitahidi kufundisha mambo mengi ya msingi na yenye busara kwetu sisi Watanzania, lakini sasa wanafunzi wa Nyerere tunamwangusha!!!!! Aliyotukataza ndiyo yanayofanywa bila hata woga wala kificho, WIZI, RUSHWA , DHURUMA, UFISADI yote haya aliyasema kwa msisitizo kwenye maadili ya viongozi!!!! Sasa kiko wapi watu wanafanya maajabu kabisa, watu kama Lowasa Mwl Nyerere aliwakataa akijua kabisa kuwa ni wezi, sasa wanakumbatiwa!!!! Nchi hii inahitaji ukombozi wa kweli, kuweza kurudisha maadili mema taifa liweze kujikomboa !!!!!!

   
 18. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #18
  Jan 27, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nyerere alipata fursa adimu ya kutuongoza Watanganyika na kisha Watanzania kwa takriban miaka 25. Cha kushangaza ni kwamba hayo yoote uliyoyataja na mengine mengi ambayo hukuyataja Nyerere aliyafanya. Likiwamo hilo la safari nyingi za nje kutembeza bakuli (omba omba) na kama ilivyo kawaida ya omba omba, kuna sehemu alipewa na kwingine aliambulia patupu. Kwa hiyo hoja yako dogo haina msingi.
   
 19. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #19
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nyerere ndio aliotufanya mpaka leo tuwe maskini. Aliwaweka watu kisiasa zaidi kuliko kiutendaji, aliingiza nchi vita vya uganda tukatumia rasilimali zetu zote, aliwafukuza watu wenye akili ili abakie na mazuzu awatawale vizuri, alitumia rasilimali zetu kukomboa nchi zingine ambazo baadae hata shukurani hawana . Hana na nyie endeleeni kuonyesha ubaya wa Nyerere..........................

   
 20. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #20
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  retard!!
   
Loading...