Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,671
- 149,843
Hotuba za Nyerere zilikuwa zinasisitiza viongozi waheshimu Katiba na pia aliwahi sema katika moja ya hotuba zake kuwa kiongozi asieheshimu katiba hatufai kabisa.
Vile vile Mwalimu Nyerere aliwahi sema CCM si mama yake na ikifikia hatu CCM ikakiuka misingi ya kuanzishwa kwake basi angeweza kujitoa katika chama hicho.
Sasa kwa yanayoendelea leo hii hapa nchini, Nyerere angeacha kukemea na pengine kurudisha/kutishia kurudisha kadi ya Chama cha Mapinduzi?
Sometimes huwa najiuliza ni nini umuhimu wa viongozi wakubwa wastaafu wa nchi hii na kwakweli huwa sipati majibu.
Niwaambie tu ingawa wakubwa hawa kwa sasa wako kimya kavile hawaoni kinachoendelea, Bunge likiamua kutumia madaraka yake na kutaka kumuwajibisha Mkulu,msishangae wakubwa hawa wakakodi ndege kutoka huko waliko jichimbia, hata kama ni Ughaibuni, kuja kuokoa jahazi.
Hili likitokea ndio mtapaswa kujiuliza wao kitu muhimu kwao ni wananchi na nchi kwa ujumla au ni fulani kubaki ofisini.