Nyerere alivyoulemaza ukoo wake kwa kuuzoesha kutegemea ufadhili

SuperNgekewa

Member
May 10, 2010
49
3
Ukoo wa Mwalimu Nyerere sasa taabani

*Yatima, vitegemezi wake wakosa msaada
*Dada yake afariki kwa kukosa nauli ya kwenda Dar
*Kikwete,Museveni wafichwa ukweli wa mambo

Majira,

Na Waandishi wetu Dar na Butiama.

AKIZUNGUMZA kwa hisia huku wakati fulani akionekana dhahiri kulazimika kusita na kuvuta pumzi nzito, mpwa wa Mwalimu, Bw. Anhthony Nyerere, amelithibitishia Majira Jumapili na Watanzania kwa ujumla kuwa pamoja na wanasiasa wengi kujisifu hadharani kuwa wanamuenzi Mwalimu Nyerere, halisi halisi ya ukoo wake ni taabani na inasikitisha.

Akizungumza katika mahojiano maalum na gazeti hili nyumbani kwake, Dar es Salaam juzi, Bw. Anthony ambaye pia kwa mujibu wa mila za Kizanaki ndiye mrithi wa mali za mjomba wake (Mwalimu Nyerere), anasema miaka nane sasa ndugu wa Mwalimu walioko Butiama, yatima aliokuwa amewachukua na kuwalea, jamaa wengine na watu wengi waliokuwa wakimtegemea Mwalimu wana hali mbaya kuliko ambavyo jamii inaweza kuamini.

"Nimeamua kuvunja ukimya na kuyaeleza haya kwa Watanzania si kwa nia mbaya bali kuielewesha jamii kuwa tofauti na hisia zao, tangu Mwalimu alipofariki ukiondoa wanafamilia chini ya Mama Maria, wana ukoo wengine ambao walikuwa wakilelewa na Mwalimu na ambao hakuwaachia mali zozote, wako taabani, hali zao kimaisha zinatisha," alisema Anthony ambaye ni mtoto wa (mama) Nyakigi Nyerere, mdogo wa Mwalimu.

Akifafanua hali ilivyo sasa Bw. Anthony alisema kwa ujumla ukoo wa Mwalimu hata mwenyewe alipokuwa hai haukuwa na maisha ya kifahari kwa sababu Mwalimu alikuwa si tajiri, lakini alikuwa akijitahidi kuwasaidia shida ndogondogo huku akilea yatima kadhaa.

"Mwalimu aliweza kutoa vjifedha kila alipopata kuhakikisha kuwa anawatunza watoto wengi yatima aliowachukua sehemu mbalimbali, kuwasaidia ndugu zake wengine ambao wana umasikini mkubwa kwa kusaidia gharama kama vile za maji, umeme na chakula.

"Kwa mfano Mwalimu alikuwa akilipa ankara za maji na umeme kwenye nyumba ya Mama Nyakigi lakini tangu alipofariki,huduma hizo zimesitishwa katika nyumba hiyo na hakuna aliyeweza kujitolea kusaidia," alisema.

Akasisitiza: "Huyu Nyakigi ambaye ndiye mama yangu yeye ni wa tano wakati Mwalimu ni wa nne kuzaliwa. Ni mmoja wa ndugu waliokuwa wakipendana sana na Mwalimu kiasi kwamba Mwalimu alikuwa siku zote akimwita dada yake huyu kwa jina la shangazi.

"Lakini tazama Mama Nyakigi aliyekuwa akilipiwa gharama hizo na kupewa fedha za kujikimu na Mwalimu mwenyewe, aliishi kizani kuanzia Mwalimu alipofariki akiwa hana maji pia hadi mwaka 2002 alipofariki."

Akizungumzia kifo cha Nyakigi, Bw. Anthony kwa masikitiko alisema mama huyo alikosa japo nauli ya kusafirishwa kwenda hospitali ya Muhimbili kwa matibabu.

"Tulikosa fedha za kumsafirisha kwenda Muhimbili na akafariki mwaka 2002. Hata kwenye maziko yake, hatukupata hata senti ya mtu," alisisitiza.

Kuhusu yatima waliokuwa wakilelewa na Mwalimu, Anthony alisema kwa sasa wengi wamesambaratika, huku waliopo wakiendelea kuishi katika nyumba ya mama yake Mwalimu ambayo hata hivyo ni chakavu na haina umeme.

"Sina pesa kwa sasa, mimi kama mkuu wa ukoo inanilazimu kuikarabati lakini siwezi, hata nyumba ya mama Nyakigi imebaki ina nyufa na jiko lake la nyuma limebomoka. Aliishi maisha ya shida sana,"alisema.

Bw. Anthony alisema kuna watoto wa mjomba wa Mwalimu aitwae Salim Nyakomge, mtu ambaye ndiye Mwalimu alitumia ngo'mbe wake kupata fedha za kwenda Chuo Kikuu Makerere, hao nao maisha yao ni taabani na sasa wanaishi kwenye vibanda vya tope vilivyoezekwa kwa nyasi.

Alimtaja mtu mwingine ambaye anataabika kuwa ni mpishi wa Mwalimu, Mzee Mohammed Sheikh ambaye amekuwa na Mwalimu tangu alipokuwa Waziri Mkuu mwaka 1960 hadi na kuendelea na kazi hiyo hadi alipostaafu mwaka 1983.

"Huyu Mzee ana matatizo makubwa. Ameunguliwa na nyumba yake huko Tanga na yuko hapa Dar es Salaam kwa wajukuu zake nako anapata shida tu. Hana pa kuishi, hana pa kwenda, hana pa kujishikiza," aliongeza.

Kielelezo kingine cha matatizo yanayoukabili ukoo wa Mwalimu kwa sasa ni hali ya sasa ya Kiboko Nyerere, mdogo wa mwisho na mmoja wa vipenzi wake.

Kiboko kwa mujibu wa Bw. Anthony hivi sasa yuko kitandani akiwa mgonjwa, msaada pekee alionao ni kijana wake mmoja wa kiume anayemsaidia na pia kipato chake cha sh. 15,000 anachokipata kwa mwezi kutokana na wapangaji wa nyumba yake.

"Tumejitahidi kuchanga fedha wakati fulani tukampeleka Mwanza kupata matibabu, lakini hivi sasa amerudishwa nyumbani hatuna fedha. Bahati nzuri ana nyumba aliyojengewa na marehemu Sokoine, ina vyumba vinne. Kwa sasa amepangisha vyumba vitatu kila kimoja sh. 5,000 kwa mwezi hivyo anashukuru Mungu kuwa na sh. 15,000 kwa mwezi lakini hali ya afya yake ni mbaya,"alisema.

Bw. Anthony alisema kitu kinachomuuma zaidi kuliko umasikini huo ambao yeye anasema "tumeuzoea na Mwalimu alishatuandaa kuishi hivyo," ni kubaini kuwa kuna viongozi ambao hufika na kuahidi kuwasaidia wanaukoo hao lakini wanakwazwa na watu aliowataja kuwa ni warasimu.

"Mama Nyakigi aliwahi kuomba msaada kwa Rais (mstaafu) Benjamin Mkapa ambaye alikuwa tayari kusaidia lakini akaambiwa 'Mzee fedha za kuwatunza hawa mbona zipo.' lakini hazikuonekana,'," alisena na kuongeza:

"Kuna wakati alikuja Rais (Joseph) Kabila wa DRC, akakutana na Mama Nyakigi akaliliwa shida naye akaahidi kuleta fedha. Najua alileta fedha nyingi sana, lakini zilikokwenda hazikuwafikia wanaukoo wa Mwalimu."

Bw. Anthony pia alisema alikasirishwa na kitendo cha hivi karibuni, Rais Yoweri Museven wa Uganda na Jakaya Kikwete walipokuwa Butiama, ambapo watu aliowaita 'vimbelembele' hawakudirika hata kuwafahamisha viongozi hao kuwa mmoja wa vipenzi vya Mwalimu; Kiboko, alikuwa mahututi kitandani.

"Hili jambo mimi lilinikera sana na kila ninapolitafakari naona ulikuwa ni unyama mkubwa sana. Kama Museveni na Kikwete wangefahamishwa kuwa kuna kipenzi cha Mwalimu alikuwa kitandani mahututi sijui ingewapunguzia nini hao waliokuwa na viongozi hao," alionesha kukerwa.

Kutokana na shida hizo, baadhi ya vijana, waliokuwa wakiishi na Mwalimu kwa muda mrefu na kusaidiana naye kazi za shamba kule Butiama, sasa wamekimbia kutokana na hali hiyo, kama anavyothibitisha mmoja wao, Bw. Hamis James Kiberiti, alipofanya mahojiano na Mwandishi Gladness Mboma, jijini Dar es Salaam wiki hii.

"Najua watanzania wengi hawataamini, lakini naomba waamini kuwa toka alipofariki Mwalimu Nyerere ukoo wake kwa sasa uko taabani ukiishi katika mazingira magumu kimaisha," alisema Bw. Kiberiti.

Alisema ukoo wa Mwalimu Nyerere umekumbwa na hali ngumu ya maisha na hata kufarakana kutokana na kumtegemea Mwalimu Nyerere enzi za uhai wake kwa kila jambo.

"Sikufichi Mwalimu alikuwa akilima na kisha mazao anayopata anayagawa kwa ndugu zake yaani kaka, dada zake na wengineo pamoja na kuwasaidia pia kwa mahitaji mengine ya muhimu.

"Lakini baada ya kifo chake, vitu hivyo vyote vilikosekana,hivyo baadhi ya vijana walikimbilia mijini na maisha yao bado yanatisha kama unavyoniona mimi, huwa naona aibu kumweleza mtu kuwa mimi niliishi karibu na Nyerere," alisema kijana huyo ambaye anafanya kazi za 'deiwaka' na pia kulinda kiwanja cha mtu eneo la Kimara, Dar es Salaam huku akiishi kwenye kibanda kilichojengwa kwa mabati chakavu.

"Kama mnataka kuamini hilo ninaomba Watanzania wenye uchungu na ukoo wa Mwalimu siku moja waende kutembelea Butiama wajionee wenyewe.

"Mkifika ombeni kuonana na ndugu zake Mwalimu Nyerere aliozaliwa nao tumbo moja mjionee maisha wanayoishi, nyumba zimechoka wao wenyewe wamechoka wako hoi taabani, mimi ni kijana nina nguvu lakini nina waonea huruma wazee wangu hao," alisema.

Alitoa mfano wa mdogo wa Mwalimu, Bw. Kiboko kuwa sasa yupo hoi kitandani, anaumwa ni wa kugeuzwa na hana msaada wowote anaoupata.

Kijana huyo anakiri kuwa aliamua kukimbilia mjini kutafuta maisha kutokana na ugumu ulioibuka kijijini.

Majira Jumapili pia lilizungumza na wakazi wa Butiama ambako mwandishi wetu, Joyce Mabiti, anathibitisha kuwa wazee waliokuwa marafiki wa Mwalimu, nao 'wanalia njaa.'

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hilo kijijini hapo wiki hii umeonesha kuwa pamoja na hali inayowakabili wanaukoo wengi wa Mwalimu kuwa tata, wazee waliokuwa marafiki wakubwa wa Mwalimu, walisema shida zimeongezeka.

Akiongea kwa niaba ya wazee wenzake, Bw Marwa Ihunyo (82) alidai kuwa enzi za uhai wa Mwalimu, walikuwa wakipata misaada mbalimbali ikiwemo pesa kwa ajili ya kujikimu jambo ambalo amedai kuwa hivi sasa halipo kabisa.

Mzee Ihunyo ambaye alisoma na Mwalimu mwaka 1933 katika Shule ya Msingi Mwisenge iliyoko mjini Musoma pamoja na misaada hiyo waliokuwa wakipata kutoka kwake alikiri pia kuwa Mwalimu alikuwa akiwaelimisha mambo mbalimbali ya kisiasa, kilimo na maendeleo kwa ujumla.

Alisema kuwa inasikitisha kuona viongozi wa Serikali wamewasahau wazee hao na badala yake wamekuwa wakiwakumbuka katika kipindi cha maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Nyerere pekee.

Aliwashauri viongozi wa Serikali kuwa na tabia ya kuwatembelea wazee hao mara kwa mara ili kujua matatizo yao na kuweza kuwasaidia.

"Unajua Mwalimu alipenda sana mshikamano kati ya viongozi na wananchi hivyo nawashauri viongozi wa serikali kuendeleza tabia hiyo ili kuweza kuondoa matatizo yanayowakabili wananchi hasa sisi wazee," alisisitiza.

Akihitimisha kuhusu hali iliyoukumba ukoo wa Mwalimu miaka nane baada ya kifo chake, Bw. Anthony amewataka Watanzania kujua kuwa wanaukoo hao hawalilii kuwa na maisha ya gharama, wanajua Mwalimu aliwafundisha uvumilivu lakini wameamua kuweka bayana ili jamii na hasa wahisani wanaotoa fedha zao nyingi pia wajue haziwafikii walengwa.


Posted by Chama Cha Watanzania Oslo - CCW Oslo at
Links to this post
 
Walishindwa kujiandaa kuishi peke yao bila Nyerere kwa miaka mingi namna hiyo?

Walishindwa kujiwekea vimiradi ili viwasaidie pindi Nyerere akikosekana?

Walishindwa kusoma na kujiendelea (hata watoto wao) wakati Nyerere akiwa hai?

Nyerere anafahamika kuwa alikuwa akisomesha sana ndugu zake zaidi ya watoto wake.

Mfano hai ni Dr. Hussein kama sikosei aliyekwenda kumuowa mtoto wa Mwinyi.

Nikiwa Interchick nilipambana na jamaa akiitwa Makongoro aliyekuwa Mkurugenzi wa Interchick na Interfreight na shule yake akiwa kamalizia USA. Pia palepale Interchick alikuwepo kijana akiitwa Joseph Matare akiwa kama Stores Officer akiishi kwa mshahara wake.

Kama walifikiri Nyerere ataishi milele, basi wataula wa chuya. Inauma ila ndiyo ukweli wenyewe.

Kama ilivyo neno CCM, walitakiwa wachukue chao mapema. Ila Wazanani/Wakurya kwa uvivu ni kama Wanyamwezi.

Walifikiri Ng'ombe wa Kukamua ataishi milele. Too sad for them.
 
Mtu mmoja ataulemaza vipi ukoo mzima? Hivi mlitaka Nyerere aubebe ukoo mzima mgongoni?

Angewabeba mgongoni napo mngemuita fisadi, damned if you do, damned if you don't.

Mimi kwa hili namsifu Nyerere kwamba hakupendelea ukoo wake, na kama mtu hauko industrious mwenyewe natural economic laws zinakuangusha, wala si Nyerere.

Kama taifa letu lingekuwa la matajiri, Nyerere angekuwa na mihela kibao ningemuona mchoyo.Lakini hatuna rekodi ya mifedha ya Nyerere, kwa hiyo siwezi kusema kwamba Nyerere alikuwa mchoyo.

Tatizo watu wanakuwa kkama hawamuelewi Nyerere kwamba alikuwa kama ascetic monk.Kuna watu washaenda Msasani kwa Nyerere wakati Nyerere rais wakala mlo wa viazi kwa karanga, wakashangaa hivi hapa ndipo kwa rais kweli?

Alivyofariki Nyerere Mama Gracias Machel, mke wa Mandela, alikuja haraka sana Msasani kumpa company Mama Maria Nyerere pamoja na kuweka mambo fulani sawa, alipofikishwa `chumbani kwa Nyerere hakuelewa, aliomba tena na kusema jamani nipelekeni chumbani kwa Nyerere nihakikishe vitu viko orderly, akaambiwa chumba ndicho hiki, Gracia hakuamini kwamba huyu rais Nyerere tuliyemsikia tangu tuko msituni tunapigania uhuru wa Mozambique, aliyetusaidia sana, rais wa nchi influential kama Tanzania ndio alikuwa analala chumba hiki? Chumba kialikuwa simple sana.

Sasa mtu ambaye hakuwa na makuu katika maisha yake mwenyewe utategemeaje awe na ukoo wenye mambo ya ajabu?

Andrew (where is Ganesh when you need him ?) mwanaye anasema wazi hapa kwaamba hata nauli huwa anagongea.

Nyerere ni intellectual aliyelewa usomi power na dini, mambo ya pesa na maendeleo ya kiuchumi hakuhusudu sana, ndiyo maana mpaka leo Tanzania uchumi wetu matatani, sasa utategemeaje ukoo wake uwe katika hali nzuri kiuchumi ?
 
Lakini niulize si kuna sheria ya kuwaenzi viongozi wastaafu wakuu na bila shaka kwa sheria hiyo serikali inawajibika kwa ustawi wa viongozi hao na aila zao, sasa hii inatumikaje?

Upande wa kimaadili wa malezi ya kiafrika, watoto anapofariki baba yao wanashika pale alipoachia katika kusimamia mambo ya kiukoo (inategemea na mila za pahala najuwa) sasa vipa kwa akina Makongoro, Madaraka na Ros-Mary Nyerere, watoto wa Nyerere, hawajuwi kuwa Butiama kuna wajomba na shangazi zao wanakufa njaa, wakati wao wanatumia fahari za baba yao. Ikumbukwe at one time baadhi yao walishakuwa hata wabunge!
 
Junius,
Utawasaidia wangapi? Na for how long? Watoto aliowazaa Mwalimu, alhamdullilah, pamoja na mkewe, Mama Maria, wanaishi vizuri. Hata mimi ninao wajomba na shangazi pale kijijini, lakini ukianza kusema uwasaidie kila mtu hautaweza. Where does personal responsibility begin within one's own life?
 
Huyu jamaa Anthony naona nia yake ni kumdhalilisha Mwalimu na familia yake ya karibu (Mkewe na wanawe) ambao wala hawajamlalamikia marehemu baba yao Mwalimu kwa maisha wanayoishi. Naamini kila mmoja anahangaika kivyake kama Mtanzania mwingine yeyote na ndivyo Mwalimu alivyowalea na kuwajenga wawe hivyo - wawe sawa na Watanzania wengine.

Jamaa analeta mambo ya extended family wasaidiwe! Kama Mwalimu alikuwa akiwasaidia ni kwa roho yake nzuri tu haikuwa haki yao. Yaelekea jamaa hao wanaolalamika na kutaka misaada ni wavivu tangu zamani na walikuwa hawataki kujituma. Mwalimu alikuwa na mashamba makubwa ya mfano lakini hawakutaka kuiga pamoja na ukweli kwamba angeliweza kabisa kuwasaidia kwa kuwapa matrekta yake walimie tena bure. Wangejifunza na kuiga kwa Mwalimu wangelikuwa mbali, wala wasingelikuwa wanalialia mpaka leo.

Kuna jamaa wa Butiama aliyewahi kunieleza kwamba hawa jamaa wakati Mwalimu akienda shambani wao walikuwa wakimuangalia tu. Jioni akirudi kutoka shamba wanamfuata nyumbani kwake kucheza naye bao na baada ya bao kula naye chakula cha jioni, ndio ulikuwa mtindo wa kila siku. Ikifika wakati wa mavuno hata kumsaidia kuvuna hawaendi, lakini chakula kikifika kwenye maghala wanakuja kuomba na Mwalimu anawapa!

Kuwalalamikia marais eti kwa nini hawaisaidii hiyo extended family ni kujidhalilisha na kudhalilisha jina la Mwalimu bure tu.
 
Mkuu Jasusi,
Ni kweli lakini kuna zile shida ndogo ndogo unazoweza kumwachia mtu mwenyewe apambane na maisha, lakini yale mambo yanahitaji msaada wa kiukoo au kifamilia wanapaswa kabisa kutoa mchango wao. Hebu tazama shangazi yao kakosa nauli ya kuja Muhimbili kwa matibabu au mjomba yao yupo mahututi kitandani pengine anaumwa ugonjwa unaotibika tu msaada hana.
 
Lakini niulize si kuna sheria ya kuwaenzi viongozi wastaafu wakuu na bila shaka kwa sheria hiyo serikali inawajibika kwa ustawi wa viongozi hao na aila zao, sasa hii inatumikaje?

Upande wa kimaadili wa malezi ya kiafrika, watoto anapofariki baba yao wanashika pale alipoachia katika kusimamia mambo ya kiukoo (inategemea na mila za pahala najuwa) sasa vipa kwa akina Makongoro, Madaraka na Ros-Mary Nyerere, watoto wa Nyerere, hawajuwi kuwa Butiama kuna wajomba na shangazi zao wanakufa njaa, wakati wao wanatumia fahari za baba yao. Ikumbukwe at one time baadhi yao walishakuwa hata wabunge!

"Ukibadilika wewe (kifikra) kama raia unaepata tabu pale ulipo, ndipo mabadiliko yatatokea katika vyombo vyengine, kwahiyo Ohaaa...Zinduka....!!!" BABU JUMA DUNI HAJI

sasa babu Juma vyengine ndio nini sasa??? hebu parekebishe hapo
 
Alivyofariki Nyerere Mama Gracias Machel, mke wa Mandela, alikuja haraka sana Msasani kumpa company Mama Maria Nyerere pamoja na kuweka mambo fulani sawa, alipofikishwa `chumbani kwa Nyerere hakuelewa, aliomba tena na kusema jamani nipelekeni chumbani kwa Nyerere nihakikishe vitu viko orderly, akaambiwa chumba ndicho hiki, Gracia hakuamini kwamba huyu rais Nyerere tuliyemsikia tangu tuko msituni tunapigania uhuru wa Mozambique, aliyetusaidia sana, rais wa nchi influential kama Tanzania ndio alikuwa analala chumba hiki? Chumba kialikuwa simple sana.?[/QUOTE]

Mkuu, Maisha hayo ya Mwalimu Nyerere yanazidiwa kwasasa hata na karani wa Halmashauri/Mji/Manispaa au Jiji, na ndio maana hata Mama Machel alaishangaa. Hakuwa mbinafsi na ndo maana hata familia yake aliiona ni sawa na mtanzania yeyote hata yule wa kutoka, Iseke huko Manyoni!!!

Pengine hali hii ndo inawafanya viongozi wa sasa (MARAHISI) waibe na kujilimbikizia kupindukia.!!!
 
hawa wasilete kutofikiri, kuumwa kwa huyo mdogo wa Nyerere na kukosa matunzo ni failed policies za serikali wanayoiabudu kama kweli wanataka mabadiliko wajaribu kufikiria kubadili serikali iliyo madarakani! Kwa vile kwanye nchi hii kuna karibia watu 40 milioni wanaoishi kwenye mazingira hayo hayo! Hiyo picha si ngeni! Huduma kama za afya inapaswa zitolewe na serikali bure kwa wazee! Pigia upinzani utaona mabadiliko
 
Watoto na wajukuu halisi wa Nyerere hawako taabani ingawa siyo matajiri. Wanaishi maisha ya kwaiada yasiyo na dhiki yoyote. Ingawa alikuwa akiishi maisha simple na wala hakuwa na upendeleo kwa watoto wake, siyo kweli kuwa watoto wale walilemaa na kuwa wategemezi; in fact walianza kujitegemea hata kisiasa hata wakati baba yao angali hai. Makongoro aliwahi kuwa mbunge kwa tiketi ya NCCR Mageuzi akipingana na CCM ya baba yake. Kwa jumla watoto wake wote wana elimu za kutosha sana na wana shughuli zao wakiishi maisha mazuri tu.

Kosa alilofanya Nyerere ni lile la kutowafukuza watu wote waliokuwa wakijiunga na ukoo wake pale Butiama kwa nia ya kumtegemea yeye. Katika hao wanaolalamika utashangaa kuwa kuna Wasizaki, Washashi, Waikizu, Wangurimi na makabila mengine yanayozunguka hapo Butiama, na hata Wazanaki ambao hawana ukoo kabisa na Nyerere, ila basi tu.
 
As much as i sympathize with the clans situation I also feel as a person and know that under the constitution the government is not obliged and neither is it fiscally capable of supporting the extended family of a former leader. The government was obliged to take care of Nyerere as an ex president and they did. The government is also obliged to offer some assistance to the former first lady and it seems they are and that it enough. Not even Nyereres children can and should receive any support from the government. If you support the extended family of every ex national leader how many people are you going to support?

Mr. Anthony Nyerere claiming that the late leader crippled them is nonsense. By the way Nyerere supported them as a personal responsibility so I don't know why now they feel it is the governments responsibility. Second, when Nyerere was alive they chose not to use the opportunity to advance themselves, that is up to them. And third, it is sad that an adult would want to live off a legacy of a deceased man, sad in deed.

By the way why is this man called Anthony Nyerere when the man himself was related to his mother?
 
Nadhani hao wakina Nyerere wamweke sawa huyu jamaa. Anawaadhiri mno. Mtu ambae anamwachia mama yake mzazi aadhirike akitegemea watu baki ndio wamsaidie hastahili heshima. Mbaya zaidi ni anavyoshindwa kuona udhaifu wake na kubaki kuwalalamikia wengine. Naamini kosa walifanya hao waliomfuata Mwalimu kwa kuimba ngojera ambazo zilifanya wadandiaji wote waone watatelezea hapo. Ukoo huo unajulikana na sio wote ambao ni loosers kama inavyoelekea alivyo huyu jamaa.

Amandla......
 
...sasa vipa kwa akina Makongoro, Madaraka na Ros-Mary Nyerere, watoto wa Nyerere, hawajuwi kuwa Butiama kuna wajomba na shangazi zao wanakufa njaa, wakati wao wanatumia fahari za baba yao. Ikumbukwe at one time baadhi yao walishakuwa hata wabunge!

Ukishasoma majibu ya Kiranga hapo juu, utakubaliana na mimi kuwa unasema utumbo mtupu hapa.
 
Mtegemea cha nduguye...................(mambo ya Darasa la III,Shule ya Msingi Mtakuja)
 
mpwa wa Mwalimu, Bw. Anhthony Nyerere ...alisema Anthony ambaye ni mtoto wa (mama) Nyakigi Nyerere, mdogo wa Mwalimu.
how does he get his last name?
 
Sijui kwanini naamini hii habari imekuwa recyled.. ni kana kwamba nimewahi kuipitia huko nyuma karibu mwaka mmoja uliopita.. au ndiyo uzee wenyewe
 
Nadhani hao wakina Nyerere wamweke sawa huyu jamaa. Anawaadhiri mno. Mtu ambae anamwachia mama yake mzazi aadhirike akitegemea watu baki ndio wamsaidie hastahili heshima. Mbaya zaidi ni anavyoshindwa kuona udhaifu wake na kubaki kuwalalamikia wengine. Naamini kosa walifanya hao waliomfuata Mwalimu kwa kuimba ngojera ambazo zilifanya wadandiaji wote waone watatelezea hapo. Ukoo huo unajulikana na sio wote ambao ni loosers kama inavyoelekea alivyo huyu jamaa.

Amandla......

Fundi,

Bahati mbaya hii mentality haijaishia katika ukoo wa Nyerere. Mpaka leo utasikia kuna Watanzania kibao wanalialia Nyerere arudi ili amalize matatizo yetu, kama Nyerere ana miguu mitatu na macho manne vile.

Personal responsibility ndogo sana.
 
Back
Top Bottom