Nyerere alishiriki Mauaji ya Kassim Hanga? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere alishiriki Mauaji ya Kassim Hanga?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, May 30, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Na Ally Saleh,

  Kuna taarifa nyingi za kuwa Rais wa kwanza Abeid Karume hakuwa mstahamilivu kwa wakosaji wake na wengi wa hao walipotea na hawakujuliana hadi leo. Baadhi ya waliopotea ambao hawkutolewa maelezo ni pamoja na mawaziri wake mwenyewe akiwemo Abdalla Kassim Hanga aliyekuwa Makamo Rais kisha akapelekwa kuwa Balozi nchini Guinea.

  Hanga alishushuliwa uwanjani na Nyerere kwa kutakiwa akiri kuwa alikuwa na mpango wa kumpindua Karume kisha Nyerere akamleta Zanzibar akijua kuwa atakuja kuuliwa…na ndivyo ilivyokua.


  Taarifa za watu waliopotea chini ya utawala wa Karume hazina hakina lakini inaaminika ni karibu ya 400 hivi katika muda wake wa utawala wa mkono wa chuma.


  Nimepata kipusa cha picha ya siku ya Hanga alipowekwa uwanjani huko Dar es salaam na nimeona tuione na kujua siku ya mwisho Hanga kuonekana hai hadharani ilikuwa vipi. Maelezo ya picha yalisema hivi:


  President Julius Nyerere is pictured on January 16th when he addressed an open air rally where the detained former Tanzania Minister and Vice-President of Zanzibar was brought to face the people. Mr. Kassim Hanga (seated between two police officers) is under detention with a number of other top Tanzanians after allegedly boasting that he had been called from voluntary exile in Guinea to lead an army coup on Zanzibar.

  [​IMG]
  IMAGE:© Bettmann/CORBISDATE PHOTOGRAPHED January 16, 1968
  LOCATION Dar-Es-Salaam, Tanzanian

  Nukuu:
  Hanga ni huyo alie chini ya ulinzi wa polisi wawili.


  source: Mzalendo.net
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hapa ndipo ninaposhangaa pale huyu mzee anapoonekana kama nabii na baadhi ya Watanzania na zaidi "wenda wazimu" wa kutaka kumfanya "mtakatifu" wakati mikono yake imejaa damu za watu wasiokuwa na hatia.
   
 3. K

  Kijiweni Member

  #3
  May 30, 2010
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwenda wazimu wewe mwenyewe na hao wazenj wenzako.

  Usafi wa Nyerere unabaki pale pale.
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Nadhani unatakiwa kuchekiwa akili. Wewe mwenyewe umeweka post hapo kwamba Hanga alirejeshwa Unguja kwa Karume, sasa muuaji iweje awe Nyerere?
   
 5. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Mtu akikwambia jambo la kijinga na wewe ukalishududia ............................. Mhhhhhhhhhhhhhhhhh inakuwa kazi.
   
 6. H

  Henry Philip Senior Member

  #6
  May 30, 2010
  Joined: Jul 29, 2008
  Messages: 114
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MImi ninachoamini siku zote, siasa kama siasa ni taaluma kama taaluma nyinginezo lakini bila kukosea ni taaluma iliyojaa kila aina ya uchafu, kwani mtu aliye ndani ya siasa ana malengo yake na siku zote yuko tayari kulinda malengo yake kwa gharama yoyote hata kwa kutoa roho za watu, labda tu kama mtu huyo anamwogopa Mungu na kumwabudu kwa roho na kweli. Tofauti na hapo ni unyama usioelezeka.

  Poleni watanzania wenzangu mnaoteseka kwa uongozi mbaya wa kifisadi.
   
 7. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #7
  May 30, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Uyu mtoto wa mama mdogo, yaani mama wa kambo anahangaika, anahitaji msaada...looks lunatic. Hana jipya.
   
 8. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #8
  May 30, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Ni Nyerere aliyemuhakikishia Sekou Toure kuwa Hanga akirudi Tanzania atahakikisha anakuwa salama, matokeo yake, kama unaona hapo kwenye mkutano amewekwa chini ya ulinzi akidogolewa kwa maneno ya kejeli na baadaye, kwa kujuwa kitakachomfika, Nyerere alimrejesha Zanzibar akauwawa.

  Kama kiongozi wa Jamhuri ya Muungano mwenye dhamana na usalama wa raia wake tena kiongozi wake aliemteua yeye kuwa balozi Guinea, asijuwe kilichomtokea mpaka leo? hii haiwi hoja kuwa kwa kuwa alijuwa ndiyo maana kanyamaza mpaka kufa kwake?

  Usafi wa Nyerere na ubaki pale pale lakini na damu aliyomwaga is haunting him!
   
 9. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #9
  May 30, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hawa wazenji tatizo lao ni muungano, wataongea hadi yasiyokuwepo duniani. kwanini tusiwaruhusu tu waende na zanzibar yao? si unaona walivyo na visa? shida yake achimbue na kumlaani nyerere ili adenounce na muungano kuwa nyerere alifanya kitu kibaya....mimi ningekuwa rais,nakwambia ningeshawaambia muda mrefu kama wanataka kunyoa wanyoe, kama wanataka kusuka wasuke.basi...kwasababu hakuna hata tunachofaidika sisi wabara kutokana na zanzibar, zaidi ya mzingo wa matatizo tu.
   
 10. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #10
  May 30, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Mkuu, Mpe kila mtu 'the benefit of the doubt' Hata mzazi wako. Hiyo doubt ndogo unayompa itakuliwaza siku ukisikia maovu yake.

  Sasa wewe na mwingine anayesema Nyerere atabakia kuwa msafi siku zote ni kama kwamba Nyerere ni Muumba, Mungu.

  Taarifa za siku hiyo zinasema wengi waliamini siku hiyo Nyerere alikuwa kama mulevi.
  Alitukana na kutukana na kutukana! Kwa ujumla maneno yake tu yalitosha kuwaonyesha watu wa usalama kwamba huyo mtu alikuwa hatakiwi tena. Na hicho ndo chanzo cha kumuweka hadharani na baadaye kumpoteza.

  Hata kama alipelekwa Z'bar bado chanzo alikuwa ni Nyerere. Mbona hazungumziwi katika siasa na kueleza sababu za kifo chake?

  Familia ya Hanga iko wapi?
   
 11. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #11
  May 30, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  sasa mnataka mkamfufue ili mmshitaki, mbona mnaongea mambo ambayo hayana kichwa wala mkia, mnachotaka haswa ni nini nyie wazenji? eleza hapa unachotaka kutokana na hii threat...tuwasaidie nini sasa?
   
 12. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #12
  May 30, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Chuki dhidi ya Wayahudi imekuwepo karne na karne hadi imepatiwa jina la "Antisemitism!" Na kwa mwendo huu wa Mzalendo.net na watu wenye vichwa vibovu kama Junius tutakuwa na kitu kinaitwa "AntiNyerereism!"
   
 13. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #13
  May 30, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mkuu huna maelezo mengine...?
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  May 30, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kwa maneno hayo ya rangi ya zambarau Hanga alijichimbia kaburi lake mwenyewe.

  President Julius Nyerere is pictured on January 16th when he addressed an open air rally where the detained former Tanzania Minister and Vice-President of Zanzibar was brought to face the people. Mr. Kassim Hanga (seated between two police officers) is under detention with a number of other top Tanzanians after allegedly boasting that he had been called from voluntary exile in Guinea to lead an army coup on Zanzibar.
   
 15. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #15
  May 30, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu Buchanan,

  Sioni sababu ya kumshambulia Junius kwani ameleta hoja ambayo pengine inaweza kusaidia kuiweka historia ya Tanzania sawa. Kuna watu wengi hapa JF hawamjui hata huyo Hanga ni nani kwani walizaliwa baada ya Hanga kuwa amepotezwa. Nasikia huyu Bwana aliuawawa kinyama sana kwani alifukiwa kaburini akiwa hai na Nyerere kama kiongozi mkuu wa nchi haiwezekani kwamba hakuyajua haya!!! Naogopa kumuhukumu Nyerere wala Karume kwa unyama waliomfanyia Hanga lakini nina imani watajibu mbele ya kiti cha hukumu siku ikifika!!!!

  Tiba
   
 16. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #16
  May 30, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Hii ni kukumbushana kwamba hamukutawaliwa na Muumba. Alikuwa Nyerere, alikuwa binadamu. Alitenda mema mengi na pia maovu rundo. Inabidi tukumbuke sana tena sana pale ambapo uovu wao ulisababisha maisha ya watu kupotea. Kumbuka familia za hao waliouwawa ni wa-Tz wenzetu.

  Vipi kama mzazi wako angekabwa sehemu za siri mpaka akafa na usifahamu alikopelekwa. Leo hii ungezungumza kwa jeuri hiyo na kushukuru wema wa Nyerere.

  Hata hivyo muna tabia ya kurudia hotuba, hebu rudieni hotuba ya siku hiyo tumusikie huyo muumba wa CCM bara.
   
 17. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #17
  May 30, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  kwa hiyo Mkuu ilikuwa uwongo kuwa Nyerere alikuwa muadilifu hivyo mpaka ionekane anastahiki sifa za kiutakatifu, wakati mtuhumiwa anamhukumu kifo hadharani kabla ya kufunguliwa mashtaka yake katika vyombo vya sheria, ndiyo tuamini kuwa Nyerere aliongoza kwa "mkono wa chuma?"
   
 18. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #18
  May 30, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nyerere alifanya mambo mabaya mengi saana huyu jamaa anayelalamika hajapata kuyasikia tu. Watu kibao wamefia mikononi mwake na familia nyingi sana leoo tanzania zinamlalamikia sana nyerere kwa kuzifanyia visa. Kwa mfano kuna wati wengi Tanzania ambao walikuwa wameenda shule na Nyerere aliwanyanganya vyeti wakaishia kuwa walimu tu na wengine kuishia mtaani na kutofanya vitu vya maana. alikuwa anatoa adhabu ambazo ni kubwa na hazina viwango.

  Kwa wanaomjua mwalimu babu sasa hivi ni marehemu alinyanganywa vyeti na nyerere kwa kuchelewa kuunganisha mitambo tu na mzee wa watu kafa akiwa anafundisha tution tambaza pale. Hotuba zake ni nzuri lakini zilikuwa siasa sana kueleza vitu visivyotekelezeka.
   
 19. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #19
  May 30, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Junius,
  Uadilifu wa Nyerere unabaki palepale. Kumbuka kabla ya Hanga kwenda Guinea (kumfuata mkewe) alisetiriwa mainland na Nyerere. Alipofika Guinea akaungana na Kambona katika mipango ya kupindua serikali. Katika mazingira kama hayo Nyerere hakuwa na sababu tena ya kumhifadhi Hanga. Ndio maana nimesema Hanga alijichimbia kaburi lake mwenyewe/
   
 20. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #20
  May 30, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Speech ya Nyerere ya 1985 (sikumbuki mwezi lakini ilikuwa kabla ya uchaguzi) ilieleza mengi kuhusu hayo. Na ni yeye mwenyewe aliyekuwa anasema hayo na ilitoka live kwenye radio kupitia Radio Zanzibar. Alikuwa anahutubia Pemba.

  Kuna ye yote aliyenayo tukumbuke historia?
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...