Nyerere alikosea sana alipokumbatia wahindi/warabu na kuwafukuza wazungu

Artifact Collector

JF-Expert Member
Mar 7, 2019
6,539
10,006
Kipindi Cha azimio la Arusha wazungu wengi walifukuzwa Ila Cha ajabu wakabaki wahindi Leo hii wahindi na wakifuatiwa na warabu ndo wamekamata biashara kubwa na Wana ukwasi Mkubwa

Maajabu ya mhindi/mwarabu hata nyumba ajengi Yuko tayari kuishi kwenye nyumba za NHC au kupanga kule kariakoo au upanga na kamwe hawez fanya uwekezaji wa maana hapa Tanzania

Kwa lugha nyingine hakuna faida yeyote ile nchi inayopata kutoka kwa hawa watu yaan wanatumia Tanzania kama shamba la bibi, mhindi au mharabu hata azaliwe Tanzania ataishi kama passenger kwa maisha yake yote

Tunauchumi ambayo walioshika uchumi ni passenger hakuna hela yeyote Ile wanayoipata Tanzania wanawekeza Tanzania mim nimekaa na wahindi na warabu hakuna watu wabinafsi Kama wale

Muhindi/mwarabu/na Sasa mchina hata azaliwe Tanzania ataishi kama passenger muangalie rostam na Manji wameshachuma Tanzania ssa wanaishi dubai

Suluhisho nchi isiwape tender mtu ambaye ni passenger sababu faida yeyote Ile anayoipata anaipeleka abroad hafanyi uwekezaji wowote ule, wapewe tu kama hakuna option

Mfumo wa elimu inabid ufanyiwe overhall kubwa sana, tutrain vijana wetu kwenye mambo ya ufundi na kuoperate Mashine ili machine operator na production managers wasiwe wanatoka India au china
 
Mwalimu Nyerere,hakufukuza mtu,Tanzania,waliondoka wenyewe.Wapo wazungu,waliokuwa mawaziri,waliokuwa watumishi wa serekali, wapo waliokuwa wafanyabiashara wakubwa,wapo waliokuwa wakulima,wapo wahindi walikuwa mawaziri,wapo waliokuwa wafanyakazi wa secta tofauti.

Hakuna aliyefukuzwa,Mwalimu hakuwa mbaguzi,wa aina yoyote,alikuwa akipenda watu wote.

Hizo nyumba unaziona wanaishi wahindi(ndio wengi),za ghorofa na waarabu wachache,zilikuwa zao,zilitaifishwa,lakini Mwalimu,hakuwafukuza,aliwapa wakae.

Mwalimu,aliwapenda raia wake,bila kuwabaguwa,na wapo wahindi,waarabu,wazungu,walishiriki harakati za kudai uhuru,mwalimu hakuwabagua,alikuwa nao bega kwa bega.
 
Kinachokusumbua ni chuki ilichanganyika na umasikini na ushamba,nyerere alimfukuza mzungu yupu?

Kwa tarifa yako waarabu wamekuwepo tnz kabla ya uhuru na waidi pia hiyo dar unayo iyona na bandari yake hao usio wataka ndio waanzilishi

Tambua walipa kodi wakubwa nchi hii ni waidi na waarabu pia hao ndio wameajiri utitili wawatu kwenye viwanda viao mbasi maroli maduka mameli

Mizigo mingi inayo shuka bandalini ya kwao ulitaka wawekezi nini zaidi ya hapo

Na wakionoka ichi inayumba sana tena sana wewe na mimi kazi zetu majungu na roho mbaya na kuwa chukia matajiri utadhani wao ndio walio kufanya uwe masikini hii tabia kaipanikiza jiwe

Jiulize wewe kwenye ukoo wenu mmewekeza nini nchini hapa na mme ajiri watu wangapi?
 
Mwalimu Nyerere,hakufukuza mtu,Tanzania,waliondoka wenyewe.Wapo wazungu,waliokuwa mawaziri,waliokuwa watumishi wa serekali,wapo waliokuwa wafanyabiashara wakubwa,wapo waliokuwa wakulima,wapo wahindi walikuwa mawaziri,wapo waliokuwa wafanyakazi wa secta tofauti.
Hakuna aliyefukuzwa,Mwalimu hakuwa mbaguzi,wa aina yoyote,alikuwa akipenda watu wote.
Hizo nyumba unaziona wanaishi wahindi(ndio wengi),za ghorofa na waarabu wachache,zilikuwa zao,zilitaifishwa,lakini Mwalimu,hakuwafukuza,aliwapa wakae.
Mwalimu,aliwapenda raia wake,bila kuwabaguwa,na wapo wahindi,waarabu,wazungu,walishiriki harakati za kudai uhuru,mwalimu hakuwabagua,alikuwa nao bega kwa bega.
Toka lini nyerere aliwapenda watu wake? Rubbish
 
Idd Amin aliwafukuza Wahindi,je nini kilitokea Uganda?

Wahindi wengi walihamia Uingereza na Canada na huko wakawa vizuri tu kiuchumi,
Utajiri au kufanikiwa ni mind set yako tu,nidhamu na mipango endelevu,utajiri au mafanikio hayaji kwa kumchukia aliyekuzidi bali unatakiwa kujifunza kupitia kwao.
 
Unajenga nyumba ya milioni 60 mnaishii watu wanne, umbali kilometer 30 Ili ufike kazini mafuta ya gari KILA siku elf 50.

Muhindi anapanga town vyumba viwili vya kulala na sebule.

Wanalala kwa jinsia baba atalala chumba kimoja na watoto wa kiume na ndugu wa kiume, mama hivyo hivyo.

Hio milioni 60 kafungua duka la jumla, baba anauza, mama keshia, watoto wanamlinda mfanyakazi mwafrika asiibe. Then ndio uje ulingane nao.

Wao starehe ni weekend tena siku moja.

Mswahili KILA rangi jeupe unataka upitie, club viwanja vyote vyako, chakula hotelini wao duka linafungwa mchana wanaenda kula nyumbani.

Ndio uje ucompete nao kwenye uchumi. Wapi na wapi.
 
Once your star you will be star forever, Wahindi waliofukuzwa east africa Uganda na Tanzania wengi waliondoka masikini mikono mitupu wakaenda pata hifadhi Canada, UK na USA huku wakiacha mali zao, leo ni matajiri nchi hizo. Nilikutana na mhindi mmoja alishukuru kufukuzwa east africa akiwa hana kitu leo ni tajiri
Mkubwa tu canada.
 
Nyerere era yake ilishapita kizazi hiki hakijui kama kuna mtu anaitwa Nyerere na ni who ktk nchi hii. Tuwaige Wahindi na waarabu tuache kulia lia. Resources za dunia ni unlimited na ni free kwa yeyeto mwenye macho.
Mbona wachina wanakuja empty zaidi ya akili zao wanachuma na wanakuwa matajiri. Shida ni sisi sio wao.
 
Watu weupe wanabebwa na uaminifu na connection.
Chukua ndugu YAKO asiye na Kazi mpe bodaboda tu au biashara yeyeto KISHA lete mrejesho. Angalau kwa makabila kama wachaga, wakinga na wapemba tena wao kwa wao thus kiuchumi wanahesabika.
Adui wa mswahili ni mswahili mwenzake.
 
Kitu kingine ndugu yangu FOCUS kwenye mambo yaliyo kuwa Positive katika maisha yako wacha kabisa chuki isiyo kuwa na sababu ktk maisha yako utafika mbali na hii ndio principle ya MAISHA.

Sent from my SM-S901B using JamiiForums mobile app
Hujui kama hili ni jukwaa au forum nilishakuja kukulia shida mpaka unaniambie nifocus kwenye maisha unajua ujinga unakusumbua sana hii ni forum unajua maana ya forum
 
Unajenga nyumba ya milioni 60 mnaishii watu wanne, umbali kilometer 30 Ili ufike kazini mafuta ya gari KILA siku elf 50.
Muhindi anapanga town vyumba viwili vya kulala na sebule.
Wanalala kwa jinsia baba atalala chumba kimoja na watoto wa kiume na ndugu wa kiume, mama hivyo hivyo.
Hio milioni 60 kafungua duka la jumla, baba anauza, mama keshia, watoto wanamlinda mfanyakazi mwafrika asiibe. Then ndio uje ulingane nao.
Wao starehe ni weekend tena siku moja.
Mswahili KILA rangi jeupe unataka upitie, club viwanja vyote vyako, chakula hotelini wao duka linafungwa mchana wanaenda kula nyumbani.
Ndio uje ucompete nao kwenye uchumi. Wapi na wapi.
🤔🤔Ila sisi kukimbilia kujenga ndo habari y mjini eti..Ellon musk hana nyumba hata matajiri wakubwa wamepanga ili kuwa na access na sehemu zao za kazi ila sio kwamba nyumba hawana uwezo wa kujenga mfano Harmonize kapanga, Diamond kapanga..
 
Wakati wewe unapoteza mda miaka 30 upo darasani unaloweka miguu kwenye beseni unasoma upate vyeti Ili ukaajiriwe, mwenzako miaka 30 yupo field anasimamia biashara za familia. Ukitoka shuleni unaenda tuition, mwenzake anarudi kukaa dukani na kufunga mahesabu ya biashara ya familia kugain experience anaenda shuleni kukua na sio akaajiriwe. Akifika form ana msingi wa milioni 50,anajua kuendesha roli, kucheza na spana, nk.

Mimi sijawahi muona msomali chuo kikuu. Wahindi na waarabu utawasaka kwa torch.
Wakati wewe unasaka degree mwenzio ni supervisor au mwajiri.
 
Back
Top Bottom