Nyerere alikosea kuhusu mpango wa Muungano wa Afrika?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Nilisoma kwenye Raia mwema kuwa baada ya uhuru kulikuwa na mpango wa kuunda shirikisho la Africa. Ilitokea tofauti kubwa ya mawazo ya jinsi ya kuanza umoja huo.

Kwame wa Ghana alitaka shirikisho lianze mara moja. Nyerere akasema hapana, tuanzishe kwanza mashirikisho ya kikanda na yakikua na kukomaa ndiyo tuanze kuungana pamoja kufikia muungano wa Africa.

Njia ya Nyerere ikaonekana kuungwa mkono. Mwandishi anasema leo zaidi ya nusu karne umoja wa Afrika bado uko mbali sana, na yale mashirikisho ya kikanda yamekufa.

Je, Nyerere alukuwa sahihi kwa mawazo yake kuhusu umoja wa Africa?
 
Nkwame alikuwa sahihi

Sent from my 5023F using JamiiForums mobile app
 
Huenda mwl hakujua hatima yake ndani ya muungano ndiyo akaja na hoja yake hiyo,kimsingi Nkuruma alikuwa sawa, leo mtu kama mseveni unaweza kumwambia habari za muungano wa afrika?
 
Back
Top Bottom