Nyerere alihusika na siasa za Zanzibar kabla ya Mapinduzi?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere alihusika na siasa za Zanzibar kabla ya Mapinduzi?!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gaijin, Jul 18, 2010.

 1. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  katika pita pita zangu kutafuta vitabu vinavyohusiana na harakati za kutafuta uhuru Tanzania nimekutana na kitabu hiki UKWELI NI HUU (KUUSUTA UONGO) kilichoandikwa na Amani Thani ambae alikuwa muasisi wa chama cha Zanzibar Nationalist Party. Kitabu hicho amekiandika 1994 akiwa ukimbizi Dubai

  kwenye kitabu hicho ambacho kinahusiana zaidi na Zanzibar, magogeni wote wa siasa kuanzia kina Karume, Ali Muhsin, Babu na Nyerere wanatajwa. Sijakimaliza kukisoma lakini muandishi anasema haya ambayo yamenivutia hadi sasa

  1) Babu alisomeshwa (short course) na ZNP lakini alikigeuka chama na akataka kishindwe katika uchaguzi.

  2) Nyerere alihusika moja kwa moja na maamuzi yaliyokuwa yakifanywa na chama cha Afro Shiraz Party Kabla ya Uhuru (ambayo yalirudisha nyuma upatikanaji wa uhuru wa Zanzibar) na alikuwa miongoni mwa waliokianzisha chama hicho (behind the scenes).

  3) Pia amezungumzia suala watu waliokimbia Zanzibar baada ya mapinduzi, kurudishwa kwa nguvu na Nyerere huku akijua kuwa wanaenda kuuwawa.

  Kinazungumzia kuhusu mateso ya jela alizokaa muandishi na mambo mengine ....

  Sasa najiuliza hivi...............

  1. hivi Nyerere alihusika kweli au Amezuliwa?

  2. Kwa Asilimia ngapi yaliyoandikwa humo yana ukweli wowote?

  Hebu nijuzeni kidogo manake wengine historia ya nchi yetu inatupiga chenga


  Kitabu hicho kwa kiingereza bofya chini
  The Nobility of Zanzibar
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  This is a known fact, mfano mmoja ni Kassim Hanga ambaye Nyerere alimrudish Zanzibar huku akijua wazi kabisa kwamba Karume atamfanyia summary execution.
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kiranga,
  Hanga alijichimbia kaburi lake mwenyewe alipoamua kumwuunga mkono Kambona katika njama za kupindua serikali. Ilikuwa yeye ndiye achukue nafasi ya Karume Zanzibar.
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Jul 18, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Discussion hii nilishaichoka sasa; watu wa Zanzibar wanaipenda sana. Tukifunga thread moja wanaazisha thread nyingine. Wanapenda sana kumzungumza Nyerere kuliko hata viongozi halisi waliowaletea mapinduzi yale na kuingiza visiwa hivyo kwenye muungano. Sijaona mtu anaandika lolote kuhusu uongozi wa Karume, Babu, Natepe, Okelo, Thabit Kombo, na viongozi wengine wa zanzibar wakati huo. Historia ya Zanzibar yote imekuwa ni ya Nyerere tu.

  Mkuu Gaijin:

  Kitabu hicho unachosema, tulishakijadili sana hapa, na niliwahi kuleta PDF version yake ya Kiswahili. Ukisaka thread za mwaka 2007 utapata majibu mengi sana.
   
 5. N

  Ngala Senior Member

  #5
  Jul 18, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ebu tembelea hapa napo wshao.blogspot.com. pengine utaongeza uelewa.ni habari ambazo hazijawahi kukanushwa maana mii nawe hatukuwepo enzi hizo japo yote kwa yote hayasaidii chochote zaidi ya kukumbusha machungu ingawa ni muhimu kwa kumbukizi" ni wetu sote mungu ni wetu sote
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kichunguu samahani kwa kuwakwaza....

  Sikujua Kama kimeshajadiliwa humu nitakisaka..... Maana upsnde wangu muandishi kaniachia shock. Kaandika with too much emotions za ukweli au uongo nitaweza pata msaada labda nikisoma hiyo thread uliyosema
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Jul 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Gaijin,
  Watu kama hawa huna haja ya kuwanukuu kwa sababu ni vichaa kama wale Makaburu wanaodai kwamba hapakuwepo na Ubaguzi South. Historia ya Zanzibar pekee ndiyo inayoweza kukupa picha kamili..Nimemsoma jamaa kwa kiasi kidogo sana nikamjua kwamba ni mzushi na mwarabu ambaye anajaribu kuonyesha Uzuri wa utawala wa Sultan. Kama kweli kulikuwa hakuna Ubaguzi Zanzibar ilikuwaje vyama vyote cvilivyoanzishwa vilikuwa ktk makundi ya RANGI na sio imani ya kiitikadi au vinginevyo?.

  hakua asiyejua kwamba ZNP kilikuwa chama cha pro Arabs ambacho kiliungana na kile cha Pemba kuwashinda Afro Shiraz. Huyu jamaa pia anadai kwamba Nyerere ndiye alisaidia kuanzishwa kwa Afro Shiraz party - Muulizeni Afro Shiraz ilianzishwa mwaka gani na kina nani kwa ujumla walikuwa waasisi?

  Kazungumzia pia kuhusu Abdulrahman Babu alishomeshwa na ZNP? iliwezekana vipi ikiwa chama hicho kilianzishwa mwaka 1955 wakati Babu mwaka 1951 alikwenda UK kusomea Philosophy na English Literature na aliporudi toka masomoni mwaka 1957 alijiunga na ZNP na kuwa Secretary General.. babu aliondoka ZNP kwa sababu chjama hiki kiliendeshwa kwa misingi ya rangi naye akiwa na imani ya itikadi ya kushoto (maxisim)..Umma party ndio chama pekee kilichokuwa kikifuata mrengo wa kushoto (A left wing movement) wengine woote RACE played a role big time.

  Maswala ya watu kurudishwa Zanzibar na kuuawa ni maswala ya Wazazibar wenyewe.. Huu ni Unafiki mkubwa sana ambao sielewi umetokea wapi na hasa ndugu zangu Waislaam ambao kwa kila hila wanajaribu kumpaka mwalimu kwa kila baya hali ni wao wenyewe walijimaliza. Ebu semeni ukweli namtu ajitokeze kukana haya..

  Sii kina Chaulembo, Adam Nassib na masheikh wengine makada wa TANU waliopiga vita Uislaam hadi kuvunjika kwa EAMWS. Hivi sii kweli Waislaam waliokuwa wanachama wa TANU wakati wa Nyerere ndio walikuwa wakipiga vita vikali Uislaam kwa sababu na kulilia madaraka na nyadhifa serikalini?. Na ndio wao waliopendekeza kuundwa kwa Bakwata badala ya EAMWS..Marehemu Karume hata kudiriki kusema Kufunga Ramadhan haikuwa swala la Faradh (lazima)..

  Lakini maajabu ya Mussa waislaam wako radhi kusamehe wabaya wao wenyewe na kutafuta mchawi, kama hawa jamaa wa ZNP wanavyozidi kuweka mashaka (brain wash) ktk vichwa vya Wazanzibar.. Sina hakika kama walikuwepo uchaguzi wa mwaka 1959 au 1961 au hata kujua vurugu na uhasama uliokuwepo baina ya Afro Shiraz na ZNP. Mkimbizi gani atakimbilia Oman hali yeye asili yake ni Oman!..aseme karudi kwao.
  Ujinga mwingine haufai kuzungumziwa mwacheni mzee wetu Marehemu Nyerere apumzike mahala pema peponi..
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Speak for yourself. Mimi nilikuwepo enzi hizo. Nilimfahamu Hanga, nilimfahamu Kambona na nilimfahamu Nyerere. Hata Karume niliwahi kumwona kwa mbali.
   
 9. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Mkandara ........ Huu utandawazi una madhara makubwa sana. Unaweza hata usitie nie ya kukutana na kina Amani Thani lkn ukakwaana nao Kama hivyo na ukajikuta unaingiwa na Shaka moyoni mwako

  tatizo linakuja Mimi Kama gaijin nna amini maneno yaliyokuwemo kwenye karatasi. Watu wengi pia nafikiri wanaamini Hilo pia.
  Uhaba wa vitabu vya historia ya Tanzania linatuchanganya. Labda pia vitabu vipo Ila raia hatulazishwi au kupendekezwa kuvisoma.
  Tunapoona jambo lipo hush-hush sana na conspiracy theories kibao kuibuka tunaanza kuamini vitabu/maneno ya extremists tu. Wanaoipamba sana historia na wanao ikashifu.

  Hebu tupeni list ya vitabu vya neutralists tupate kujifunza cha ukweli. Vijana tunapotea
   
 10. jambotemuv

  jambotemuv JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Hapo uone wadhalimu walivyokosa aibu na kiu ya kuwanyanyasa na kuwanyonya wanyonge haiishagi.
  Iweje zanziba ambako hata utumwa ulishamiri leo uniambie hakukuwa na ubaguzi? Ndo Zanziba ileile mwarabu alikuwa anamwamrisha mweusi kukwea mnazi ili amtungue kwa kujaribu uwezo wa bunduki yake? Ndo waarabu walewale walokusanya watumwa toka kigoma Tabora tunaambiwa huko Zanz walikuwa malaika kiasi huwezi kujua nani mweusi na yupi mweupe kwenye jamii?
  Wliofanya mapinduzi walikuwa wote wakazi wa Zanzibar. Inaingiaje akilini kuwa watapindua serikali ili wajitese?
  Huyu na wapambe wake wote waendelee kuteseka waliko kwa kukosa nafasi ya kuwatesa na kuwanyanyasa wenye nchi yao. Kama hiki nacho chaitwa kitabu basi kazi tunayo!
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Jul 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu mara nyingi unaposoma kjitabu mara nyingi unaituma akili yako kuelewa mwandihsi alikuwa na lengo gani kama kuelilisha au kukuza Fitna na mara zote mimi naposoma kitabu au historia inayoegemea upande mmoja huiacha kama ilivyo kwani mara zote kila story ina pande mbili..na kumbuka tu kwamba maneno yaliyopo ktk karatasi sii utafiti wa kisayansi isipokuwa mtazamo wa mhusika kulingana na upande gani wa senyenge alisimama.

  Na hakika kukosa kuweka kumbukumbu ndilo tatizo la nchi zetu kwa sababu imekuwa ni aibu kuzungumzia Utumwa au kutawaliwa. Hakuna Mtanzania anayeweza kukueleza kwa undani Utawala wa Mreno, Mjarumani au Muingereza kwa fikra huru za Watanzania isipokuwa hisia zake mwenyewe. Sawa kabisa na leo ukisoma vitabu vya Marekani kuhusu Iraq na ukisoma wapambe wa Saadam utakuta historia mbili tofauti. Kisha napo kuna Kudish, Sunni na Shiah woote wataandika sii kwa fikra huru zisizofungamana ila historia inayohusu machungu yao..

  Na binadamu tuna desturi ya kupenda kuuza vitabu hivyo kama magazeti habari za uongo hununulika zaidi ya ukweli kwani ukweli wa historia yetu unauma sana kuusikia na hakika wazee wetu wameshiriki kwa aina fulani kuneemesha yote yaliyotukia. Na hata haya yanayotokea wakati huu wa JK tutakuja yapamba sifa/kashfa za kinafiki hali sisi wenyewe ni part ya Utawala huu toka mwalimu Nyerere,Mwinyi na Mkapa. Na trust me, historia yetu itaelezwa zaidi mabaya wa hao viongozi na watu waliokuwa against them kuliko kujieleza wao wenyewe ktk nafasi zao waliweza kufanya mabaya yapi.

  Kuna documents nyingi tu unaweza kuzipata kupitia vyombo vya habari kama Zanzinet na fanya kufuatilia links zao na kusoma mchanganuo mbalimbali wa mawazo. Najua wewe mtu mzima unaweza kuchambua mchele na kutupa pumba..
   
 12. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #12
  Jul 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Naomba ukiweke tena ndugu yangu hiyo PDF maana wengine tulikuwa hatujaingia JF mwaka 2007, please!
   
 13. Dx and Rx

  Dx and Rx JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2017
  Joined: Jul 16, 2017
  Messages: 873
  Likes Received: 2,309
  Trophy Points: 180

  Nyerere
   
Loading...