Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Mwalimu Nyerere alifariki mwaka 1999. Mzee huyu alikuwa mzalendo sana, alipigania maslahi ya nchi kwa nguvu zake zote. Mwaka 2000 mchanga wa dhahabu (gold ore and copper concentrates), ukaanza kusafirishwa kupelekwa Japan na China. Nchi hii ni tajiri kweli kweli, shipment moja ya kontena zinazokwenda Japan inaweza kuwa na makontena 66 mpaka 88, kwa mwezi zinaweza kusafirishwa hata shipments nne.
Mzigo ulipitia bandari ya Tanga kuanzia mwaka 2000 mpaka 2007, kutokana na matatizo mbalimbali ya mzigo kuchelewa ukiwa relini kati ya Isaka mpaka Tanga, matajiri wakachukizwa na ucheleweshwaji wa mali, hivyo uamuzi wa mzigo kupitia bandari ya Dar ukaonekana ni wa busara ili kuepuka muda wa njiani. Ni hivi karibuni ndipo Rais Magufuli aliizungumzia biashara hii ya mchanga wa dhahabu wakati akiongea na wafanyabiashara. Lakini ni baada ya biashara yenyewe kufanyika kwa kipindi cha miaka 16!, yaani tumepigwa kwa muda mrefu tu.
Leo hii yanazuka maongezi ya Olduvai Gorge pamoja na ndege ya Kenya kuandikwa Mlima Kilimanjaro. Mambo mazito na ya msingi hayaongelewi, tunapoteza muda kwenye udaku na light stories zisizo na mguso wa moja kwa moja kwenye maisha yetu. Hii nchi ni tajiri sana, maelfu ya makontena ya mchanga yameshakwenda Japan na China, sisi tunatoka povu kuongelea habari za mimba ya Wema Sepetu, na mambo mengine mepesi sana.
Rais ametoa changamoto ya ule mchanga kufanyiwa process zote humu humu nchini. Bado sijawasikia wasomi wetu wakiongelea ni namna gani wamejiandaa kutengeneza fedha kutokana na furnace itakayofungwa nchini na ajira mbalimbali zinazoweza kupatikana. Waungwana haya ambo ya olduvai gorge na mlima kilimanjaro ni sehemu ndogo sana ya masuala yenye kuhitaji mijadala makini.