Nyerere alifanya kosa kubwa japo nia yake ilikuwa nzuri!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere alifanya kosa kubwa japo nia yake ilikuwa nzuri!!

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by KakaKiiza, Sep 16, 2012.

  1. KakaKiiza

    KakaKiiza JF-Expert Member

    #1
    Sep 16, 2012
    Joined: Feb 16, 2010
    Messages: 10,070
    Likes Received: 1,523
    Trophy Points: 280
    Mwalimu Julius K.Nyerere alifanya makosa makubwa sana ambayo hadi sasa yanatugharimu kuhusu swali la Muhungano!
    Nasema kitu kilichokosewa ni Kuwa na Mabunge mawili ndani ya nchi moja!.
    Kuruhusu kuwepo na Maraisi wawili ndani ya nchi moja!
    Kuruhusu katiba mbili katika nchi moja!
    Japo lengo lake lilikuwa zuri lakini akuangalia maswala ya kitaalamu ategemea kuongoza kwatumia mkono wachuma nakudhani watu ni wajinga!
    Leo tunashuhudia matatizo ya Muungano yanavyoisumbua serikali ya Muungano,leo Uhamusho mara Baraza,hivi nibaadhi ya vitu vinavyovuruga muungano!Na hainajinsi yakuendelea kuabudu serikali moja wakati kuna maraisi wawili na mabunge mawili na katiba mbili!Kwa jinsi hiyo ninchi mbili serikali isipepese macho ikubali serikali tatu hakuna cha kuogopa!
     
  2. Kongosho

    Kongosho JF-Expert Member

    #2
    Sep 16, 2012
    Joined: Mar 21, 2011
    Messages: 36,134
    Likes Received: 246
    Trophy Points: 160
    alifanya alichoweza, kazi wa wengine kumalizia.

    Labda kwa wakati huo ilikuwa ndio option kwake ilobaki.

    Tunaweza amua wenyewe tunachotaka.
     
  3. WA-UKENYENGE

    WA-UKENYENGE JF-Expert Member

    #3
    Sep 16, 2012
    Joined: Oct 1, 2011
    Messages: 2,905
    Likes Received: 226
    Trophy Points: 160
    Tatizo naona nii kukosa taarifa sahihi ambazo zinapatikana magogoni tu, taarifa hizo tukiweza kuzipata tuangalie hali ya mambo ilivyokuwa, na je katika hali ya wakati ule option zipi zilikuwapo ambazo zingeweza kusaidia kutokana na hali ilivyokuwa kipindi hicho. Kama siyo taarifa ya kina kutoka magogoni, pengine kitengo cha usalama! basi waje wanaJF watuwekee hali ilivyokuwa na sababu zilizosababbisha kufikia maamuzi hayo!!
     
  4. T

    THOMAS NJUMA New Member

    #4
    Sep 17, 2012
    Joined: Aug 3, 2012
    Messages: 3
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Ni kweli Nyerere alifanya makosa makubwa, lakini wewe unataka kufanya makosa makubwa zaidi japo nia yako ni nzuri. Itakuwa jambo la ajabu kuwa na serikali tatu kwa nchi mbili ambazo hazina uwiano wa kweli wa rasilimali za aina zote! Je, wewe unaogopa nini, kusema kwamba Muungano ufe. Wenzetu wamechochwa na serikali mbili, serikali moja ndo hawataki kusikia kabisa. Hizo serikali tatu ni hatua moja mbele ya kufuta Muungano, wenzetu tunawapenda sana, lakini kwa kuwa hawatuhitaji tena ni kuachana nao tu kuliko kupoteza muda!!
     
  5. Root

    Root JF-Expert Member

    #5
    Sep 17, 2012
    Joined: Jan 23, 2012
    Messages: 22,455
    Likes Received: 7,972
    Trophy Points: 280
    Hili swala lijadiliwe ili ijulikane kama ni.nchi mbili au moja
     
  6. KakaKiiza

    KakaKiiza JF-Expert Member

    #6
    Sep 18, 2012
    Joined: Feb 16, 2010
    Messages: 10,070
    Likes Received: 1,523
    Trophy Points: 280
    Kwangu mimi binafsi ningesema nataka serikali moja inayojitegemea maana mpaka sasa mimi sijui nifaida gani niliyoipata kwakuwa na serikali mbili nikiwa na maana ya Muungano na ya bara kwakuwa mimi nipo bara naona kwangu ni hasara kwakuwa kama niserikali mbili sasa yanini kuwa muungano wa serikali moja??Mimi niliwahi kununua gari zanzibar kufika hapa nikalipa tena ushuru wakati huohuo walikuwa wametangaza Bungeni kuwa ukinunua kitu zanzibar na TRA yazanziba ikahakiki kuwa wewe umelipa ushuru inamaana ukija bara hautakiwikulipa tena ajabu nikalipa tena sasa mimi nina faida gani na muungano wakupendelea sehemu moja??

    Tuwaombe wanabodi wa weke michango yao na kama kuna umuhimu wakuiwekea sticky thread hii!tumuombe Invisible
     
    Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
  7. KakaKiiza

    KakaKiiza JF-Expert Member

    #7
    Sep 18, 2012
    Joined: Feb 16, 2010
    Messages: 10,070
    Likes Received: 1,523
    Trophy Points: 280
    Hayo ndotunataka kwenye katiba yasasa yajadiliwe lakini ajabu CM hawataki kitu kusikia muungano unavunjika!!
     
  8. WA-UKENYENGE

    WA-UKENYENGE JF-Expert Member

    #8
    Sep 18, 2012
    Joined: Oct 1, 2011
    Messages: 2,905
    Likes Received: 226
    Trophy Points: 160
  9. Bilionea Asigwa

    Bilionea Asigwa JF-Expert Member

    #9
    Sep 18, 2012
    Joined: Sep 21, 2011
    Messages: 12,591
    Likes Received: 9,524
    Trophy Points: 280
    shida ilikuwa kwenye kupata viongozi watakaoendeleza kile alichokianza...si kila kitu kinafanywa mara moja .....
     
  10. Kichuguu

    Kichuguu Platinum Member

    #10
    Sep 22, 2012
    Joined: Oct 11, 2006
    Messages: 7,094
    Likes Received: 596
    Trophy Points: 280
    Muundo huu wa muungano tuliwahu kuujadili zamani sana mwaka 1976 kabla ya TANU kuungana na CCM; mgeni rasmi alikuwa mzee Thabit Kombo. Ilivyyonekana ni kuwa ingawa Nyerere aliwasaidia sana katika kuimarisha nchi baada ya mapinduzi, hakuwa ana wazo la kuungana kwa kuwa ni kipindi ambacho alikuwa ameshindana na Nkurumah kuhusu uundwaji wa United States of Africa, na juhudi zake kubwa wakati huo zilikuwa ni kuundwa kwa shirikisho la Afrika ya Mashariki. Wazo la kuungana lilisukumizwa sana na Karume ambaye aitaka tuwe nchi moja tu wakati Nyerere akiwa Rais na yeye mwenyewe akiwa makamu wa Rais. Baada ya majadiliano ya kama wiki tatu hivi, ndipo Nyerere alipokubwali muungano huo ila akawa ameweka masharti ya kutoonyesha kuwa ameivamia na kuimeza Zanzibar; ndipo akaja na huo muundo wa autonomy ya Zanzibar kwa mambo yake ya ndani. Wakati huo, Zanzibar haikuwa na structures zozote za serikali zaidi ya baraza la mapinduzi, kwa hiyo autonomy ya Zanzibar ikawa inasimamiwa na baraza hilo la mapinduzi.

    Muundo huu tunaoona leo wa kuwepo kwa baraza la wawakilishi, bendera ya Zanzibar na wimbo wa Taifa wa Zanzibar ni mambo yaliyokuja baadaye sana na wala hayakuwamo katika makubaliano ya awali ya Muungano.
     
  11. Horseshoe Arch

    Horseshoe Arch JF-Expert Member

    #11
    Jan 27, 2014
    Joined: Aug 10, 2009
    Messages: 9,916
    Likes Received: 3,181
    Trophy Points: 280
    Sijui ni kwanini ila natamani Tanzania moja,ambayo itaongozwa na Rais mmoja, kama ilivyo mikoa mingine kisiwa cha Unguja na Pemba viwe mikoa na kuwa chini ya wakuu wa mikoa ambaye atawajibika moja kwa moja kwa waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa!

    Natamani Tanzania itakayokuwa na mahakama kuu moja,na mahakama ya rufani moja huku mikoa yote including Pemba na Unguja ikifuata mfumo wa mahakama za kata,wilaya,hakimu mkazi na kama itaonekana inafaa kwa sababu ya kurahisisha utendaji kuwe na mahakama kuu za kikanda ili kurahisisha utendaji.

    Natamani nchi ambayo bunge litakuwa moja na kila mbunge akiwa mwakilishi wa wananchi kwenye jimbo lake..Natamani Tanzania ambayo ....ambayo...Ambayo! Still loading
     
  12. J

    Jurist.net Member

    #12
    Feb 19, 2014
    Joined: Jan 23, 2014
    Messages: 6
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Hatutaki muungano mbona hamtuelewi jamani.. mumetudhulumu vyakutosha saiv basii.. kaeni na Tanganyika yenu na sisi tupumueeee..!
     
Loading...