Nyerere aliamini mke wa kaisari hatuhumiwi lakini JK apinga! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere aliamini mke wa kaisari hatuhumiwi lakini JK apinga!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Oct 8, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Nyerere siku zote aliufananisha utumishi wa Umma na mke wa kaisari ambaye aliachika kwa sababu alituhumiwa tu. Kaisari wala hakupoteza sekunde kuchunguza tuhuma dhidi ya mkewe bali alimpa talaka stahiki. JK kwa kuwakumbatia mafisadi na kudai bado tuhuma zao hazijathibitishwa na mahakama ni dhahiri anambeza Baba wa Taifa yaani hakuwa na busara hata chembe.

  Na anayembeza Baba wa Taifa ni lazima tumkatae Oktoba 31 kwa kuwa ni mbabaishaji mahiri tu kwenye sura nzima ya utawala bora.
   
 2. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hizi propaganda nyingine muwe mnazichuja kwanza ili zisije zikawarudia.......................
   
 3. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Siju kama jk anafahamu hata maana ya utawala bora. Yeye anaendesha nchi kiuswahili swahili tu. Uwezo wake ni mdogo sana. Isitoshe jk hawezi kuenzi mazuri ya Baba wa Taifa kwani anamchukulia kama adui yake aliyempokonya tonge mdomoni mwaka 1995 pale Dom. Yeye anaendeleza libeneke na mafisadi waliomweka madarakani.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kumfananisha Nyerere na JK ni kama kufananisha mWANGA NA GIZA, JOTO NA BARIDI, mbingu na nchi!...Hakuna alichomwiga baba wa taifa huyu JK!...NOTHING!
   
Loading...