Nyerere Akabidhi Kontena la Vitabu Musoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere Akabidhi Kontena la Vitabu Musoma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 14, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MBUNGE wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (Chadema), amefanikiwa kupata kontena moja la vitabu vya masomo ya kuanzia shule ya awali hadi Chuo Kikuu na vitabu hivyo vitasambazwa kwa shule zote za sekondari za kata jimboni humo.
  Msaada huo umetolewa na wahisani kutoka nchini Marekani, ambao pia ni marafiki zake na kwamba vitabu ambavyo tayari vimeshawasili mjini Musoma na kuhifadhiwa vikisubiri kusambazwa shuleni, vitapunguza zaidi kama si kuondoa kabisa tatizo la upungufu wa vifaa hivyo.

  Nyerere alisema kuwa uongozi wake unataka kuona sekta zote ikiwemo sekta ya elimu zinapata maendeleo makubwa kwa kuwanufaisha zaidi wananchi wa jimbo
  hilo na kwamba safari ya kusaka mapinduzi makubwa ya maendeleo ya
  kisekta aliyotumwa na wananchi wake imeshaanza.

  “Nimepata msaada wa kontena zima lenye futi 20 limejaa vitabu vya aina
  mbalimbali kuanzia wanafunzi wa chekechea hadi chuo kikuu. Msaada huu
  nimeupata kutoka kwa marafiki zangu huko Marekani.

  “Vitabu hivi vitasaidia sana kupunguza tatizo kubwa la uhaba wa vitabu
  kwa wanafunzi wetu mashuleni,” alisema.

  Kwa mujibu wa mbunge huyo wa Musoma Mjini, vitabu hivyo vitakabidhiwa
  mbele ya madiwani wote wa jimbo hilo siku yoyote wiki hii kwa sekondari zote za kata na shule za msingi na kwamba vitabu vya chuo kikuu vitawekwa katika maktaba ya mkoa wa Mara, kwani jimbo wala
   
 2. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Nampongeza sana Mh:Mbunge kwakutumbau umuhimu wa Elimu.
  Lengo la Mbunge ni zuri sana ila Tatizo ni Watendaji ushauri wangu kwake ni Kwamba ivyo vitabu kabla yakuvigawa avipige Chata ambayo haifutiki kisha awatangazie Wananchi pa1 na Wanafunzi ili wao ndo watumike kulinda vitabu vyao kwa Manufaa vyao lasivyo havitawasaidia atavikabidhi kisha baada ya wiki atavikuta Kariakoo na kwenye Bookshop tofauti tofauti vikiuzwa.
   
 3. s

  seniorita JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Education is key to liberation, hongera mbunge Nyerere
   
Loading...