Nyenzo za thamani kubwa Maishani

Ninja

JF-Expert Member
Feb 5, 2010
348
535
Wanadamu tumekuwa tukihangaika siku zote kupata mambo mema na hasa hasa mambo yanayotafutwa zaidi duniani ni mapenzi, pesa, mali, maisha bora, maisha marefu, maendeleo na amani na utulivu.

Mambo yafuatayo yametamkwa na wengi kama 'ingredients' za dawa ya kupata mahitaji yote kama yalivyotajwa hapo juu.

Hekima, busara, maarifa, elimu, ujuzi, akili, kipaji, ufahamu, mbinu na werevu. Hizi zimetajwa maeneo mbalimbali kuwa ni nyenzo zenye thamani kuliko fedha, mali na mengineyo kwa kuwa ndio chanzo cha fedha, mali na mengineyo.

Je ni kuna ukweli wowote kwenye kauli hizi?

Je maana halisi ya nyenzo hizi ni nini? Kuna tofauti gani baina ya kila moja?

Je ni mchanganyiko upi ni bora zaidi unapochanganya nyenzo hizi ili kuleta matokeo bora zaidi?

Je ni kwa jinsi gani kila moja ya hizo hupatikana? mfano unawezaje kupata busara? au werevu hutokana na nini?

Je unapimaje kuwa mtu fulani, au wewe mwenyewe, au kiongozi fulani ana mchanganyiko ulio bora wa hayo? au pengine 'formula' imekataa kabisa ni 0+0+0?
 
Busara inatokana na kupevuka kimawazo, mara nyingi wanakuwa nayo zaidi watu wazima, ni uwezo wa kujua kipi cha kudharau. It is an ability to know what to ignore. Kipaji anatoa mwenyezi Mungu. Elimu kusoma. Elimu ndiyo ufunguo wa maisha.
 
Nimeipenda hii definition ya busara, lakini ningefurahi zaidi kama ungefafanua zaidi. Kwa mfano suala la umri na busara.
 
Bila busara huwezi kujua hoja gani ya kujibu na hoja gani ya kuipuuza. mfano, umri unasaidia kwenye busara, kuishi kwingi kunaongeza busara.
 
Kuna kitu bado sikielewi. Mfano mtoto mdogo je aweza kuwa na busara?
 
Kwa watoto hii ni bidhaa adimu. Lakini kwa mtoto yatima inawezekana, hawa wanapevuka hata kabla ya wakati kutokana na maisha. Yatima hadeki.
 
Kweli JF ni noma nimekubali, watu mnaandika vitu vizito sana, ebu ngoja nikae moksu nitafakari kwanza nataka nielewe vizuri. kwamba mtoto yatima inakuaje!
 
Kuna kitu bado sikielewi. Mfano mtoto mdogo je aweza kuwa na busara?

watoto nao wanapaswa kuwa na hekima inategemea malezi yako utakayompa busara aijalishi umri inajalisha upeo wa mtu wa kujua nn cha kufanya kwa wakati sahihi biblia inasema mtoto yesu akakuwa kwa hekima,kimo,ufahamu akimpendeza mungu na wanadamu
 
Haswaa, mambo ya Luka 3 hayo.
 
Back
Top Bottom