William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,375
Ndugu zangu wananchi tunaoishi New York City, na vitongoji vyake, kwa niaba ya kamati maalum ya wananchi kwa kushirikiana na wenzetu wa Ofisi ya Ubalozi wetu wa kudumu UN,
- Ninaomba kuwafahamisha na pia kuwakumbusha kwamba Jumamosi hii yaani Tarehe 6, March 2010, kuanzia saa Nane Mchana tutakutana nyumbani kwa Balozi wetu wa kudumu UN, Address # 30 Overhill road, Mt. Vernon NY kwa ajili ya sala, maelezo na makumbusho yanayomuhusu Marehemu Balozi Mwakawago, ambaye siku za nyuma aliwahi kuwa mkazi mwenzetu hapa New York, akiwakilisha taifa letu UN.
- Ni muhimu sana kwetu wananchi kufika mapema katika shuguli hii ambayo pia tunategemea kujumuika na watoto wa marehemu, pamoja na viongozi wengi wakuu wa taifa na wa Jumuiya za kimataifa. Na pia muhimu sana tukajitahidi sana ndugu zangu kuja na sadaka kulingana na uwezo wetu kwa ajili ya kumuombea marehemu. Wananchi wote mnakaribishwa kuhudhuria bila kukosa.
- Ninaomba niwape heshima za pekee na nzito sana, wenzetu yaani Balozi Dr. Mahiga, Maofisa wote na Ofisi nzima ya ubalozi wetu wa kudumu UN kwa juhudi zenu nzito na za ajabu sana, za kujitoa kwa hali na mali katika uchache wenu, hasa wa nafasi na mali pia ili kujumuika nasi katika kuhakikisha kuwepo kwa hii shughuli Jumamosi.
Mungu Ibariki Tanzania, Aibariki Africa na Umuweke Mahali Pema mwenzetu Marehemu Balozi Daudi Mwakawago, Amen.
Ahsanteni Wananchi wote.
William Malecela.
Mjumbe Kamati Maalum.